Chadema wachapana makonde Mwanza

Kwa hiyo nchi ibaki kwa "wanaoongoza" kwa bastola? Nyie subirini mziki wenu 2015, mtajua nani atakae kabidhiwa nchi, hata kama ni kwa mtindo wa Ivory Coast! Nyie kura hampati hata kwa dawa.

Tumewazoe hata 2010 mlisema hivyo!
 
matata ni chadema !!!! yaani mtu anavamia vikao vya chama kwa lazima anaona maoni ya kamati kuu ni tope kwa uchu wa madaraka alionao halafu mnasema CHADEMA wachapana makonde
 
hawa akina matata ni aina ya viongozi waliokuwa wanamini chadema iko waazi ni kupata nafasi tu ndio maana hawavumilii hawafai kabisaaa matata na chagulani
 
Cdm mjifunze kwa hili. matata alikuwa mgombea wa ccm .aliposhindwa ktk kura za maoni tu akaingia cdm ndani ya siku chache na kuruhusiwa kupeperusha bendera ya cdm ndani ya kata hiyo hiyo.ktk uchaguzi ujao msirudie kosa hili,sisi wana mwanza tuko nanyi bega kwa bega ingawa ccm hawalali wakipanga mbinu chafu za kuwamaliza lkn hawatafanikiwa
 
[h=2][/h]JUMATANO, SEPTEMBA 26, 2012 10:59 NA JOHN MADUHU, MWANZA

*Makao makuu wachanganyikiwa, wamtuma Kigaila kutuliza upepo
*Mbunge Highnes Kiwia atupiwa lawama
HALI ya mambo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Mwanza ni tete.

Hali hiyo imekuwa tete, baada ya Kamati Kuu ya chama hicho, kutengua matokeo ya ndani ya chama yaliyohusu washindi wa nafasi ya kuwania kiti cha Meya na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilemela.

Pamoja na mambo mengine, matokeo hayo yametenguliwa baada ya Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, kutishia kujiuzulu ubunge, kwa kuwa alikuwa akipinga uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho, Wilaya ya Ilemela, ambayo iliwapitisha Marietha Chenyenge kuwania nafasi ya Meya na Rosemary Brown, kuwania nafasi ya Naibu Meya.

Kutokana na mvutano huo, CHADEMA makao makuu, wamelazimika kumpeleka jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa chama hicho, Benson Kigaila, ili akarejeshe hali ya amani iliyotaka kutoweka ndani ya chama hicho, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilemela, kesho kutwa.

Habari za uhakika kutoka katika kikao cha madiwani wa CHADEMA, waliokutana katika ofisi zao za mkoa zilizopo eneo la Pasiansi, zinaeleza aliyekuwa mgombea nafasi ya Meya, Dan Kahungu ambaye inasemekana alikuwa akiungwa mkono na Mbunge Kiwia, aliamua kukata rufaa kupinga maamuzi ya Kamati ya Utendaji, kuwapitisha Marietha Chenyenge pamoja na Rosemary Brown.

Inadaiwa Marietha na Rosemary, walikuwa na onyo kali kutoka kwa uongozi wa juu, kutokana na mwenendo wao uliosababisha kung'olewa kwa aliyekuwa Meya wa Jiji la Mwanza kupitia chama hicho, Josephat Manyerere.

Taarifa zaidi kutoka katika kikao hicho cha madiwani, zinasema kutokana na rufaa hiyo, uongozi wa CHADEMA uliamua kufanya uamuzi wa kufuta matokeo hayo na kuagiza Kigaila kwenda Mwanza kuwaeleza wanachama wa chama hicho ni kwa nini uongozi wa juu, umeamua kufuta matokeo hayo na kumteua Abubakar Kapera kuwa mgombea nafasi ya Meya wa Manispaa ya Ilemela na Dan Kahungu kwa nafasi ya Naibu Meya.

"Kigaila alipoanza kueleza msimamo wa chama hali ilikuwa tete, kwani madiwani hatukukubaliana na uamuzi huo, kwani yalifikiwa kwa manufaa ya Mbunge Kiwia ambaye ndiye anayekivuruga chama kwa manufaa yake binafsi.

“Madiwani waliweka wazi, kwamba wako tayari kuwapigia kura wagombea wa vyama vingine, ili kuonyesha msimamo wetu kuhusu kutokubaliana na uamuzi huo kwani inavyoonyesha wanawake hawakubaliki ndani ya CHADEMA,” alisema mtoa taarifa wetu.

Taarifa zaidi zinaeleza, idadi kubwa ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya ya Ilemela, wanatarajia kutoa tamko la kuachia ngazi, baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa makao makuu ya chama yaliyoko Kinondoni Dar es Salaam.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, walisema viongozi wa CHADEMA, makao makuu, wamekiuka na kushindwa kuheshimu uamuzi uliofikiwa na kamati hiyo, ambayo iko kwa mujibu wa Katiba ya chama chao.
"Tuko na Kigaila ambaye ametumwa kuleta ujumbe wa makao makuu na kimsingi hatukubaliani na uamuzi wa makao makuu.

“Kitendo walichokifanya ni kuingilia uamuzi wa Kamati ya Utendaji, kwani barua za onyo wanazodaiwa kupewa wahusika kwamba walishiriki kumwondoa madarakani Meya Manyerere, wahusika ndiyo wamezipata leo.

“Kama walikuwa na uamuzi huo tangu mwanzo, basi wangeusema mapema na tusingeweza kupoteza muda wetu bure,” alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Kiwia alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi, hakuweza kupatikana kwa kile kilichoelezwa kuwa, alikuwa katika kikao cha Kamati ya Uendaji ya chama hicho.



[h=4][/h]
 
hii ni trela bado filim!! hakuna cha CDM wala CCM wote hawa ni mafisadi safari yetu ya ukombozi bado ni ndefu!!!
 
Siasa za mwanza ni chafu sana, wameshauwawa sana hapo watu si ccm, nccr, chadema etc.

Mwanza ni mwanza, hata mbunge kukaa vipindi viwili sio rahisi....

Ila CHADEMA kwa mwanza wanachemka, they need to act quickly, nakumbuka hata Slaa alishawahi onja joto ya jiwe hapo

MWanza wanamhitaji Mbowe mwenyewe asimamie chama hata kama ni kwa 10% ni jiji la wanajeshi
 
ukombozi wa kweli tanzania bado sana, wengi wanaojiita wanamapinduzi ni wachumia tumbo.
 
Mgongano wa mawazo ni kawaida kwa chama chenye demokrasia. Tutalumbana tena kwa hoja, mwisho tutakubaliana kimaamuzi na kimsimamo. Na hayo yatakuwa maamuzi na msimamo wa chama. Thats democracy!
 
Kuna tatizo la falsafa hapo kuhusu nafasi ya Makao Makuu kwenye mambo ya mamlaka ya Wilaya na Mkoa. CDM falsafa yake ni kupeleka madaraka kwenye ngazi ya Majimbo na wilaya na mikoa hufanya uratibu. Tatizo ni kutokuipa mikoa mamlaka ya kutoa maamuzi kwenye mambo yanayohusu madiwani walioko kwenye mamlaka zao.
 
Back
Top Bottom