Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Pengo yuko chama gani?
Poor Mwita!
Sijasema CDM kijishushe kwa CCM! No where in my post I have indicated that!
Nimesema kijishushe kwa jamii ile ambayo wanaambiwa hawapo!
Hivi leo hii CDM ikaamua kutumia sh. laki moja tu kusema imetoa msaada wa madaftari shule ya sekondari Al-almain kuna kosa?
Leo hii CDM wakisema wanamtembela Mufti na kuuliza Bakwata inafanyaje kazi na kutoa pongezi kwa kazi nzito ya kuongoza Bakwa ni kosa/
Leo hii sikuu ya Idd ikifika na CDM ikatoa mdaada kwa watoto mayatima ni kosa
Kwa kufanya hayo au yanayofanana na hayo CDM itakuwa kwa kiasi gani imejivua hizi TUHUMA
Mwita, I know you hate me, because you think I hate CDM, I dont hate anybody NINACHOKASIRIKA NI KUFANYA MATENDO YASIYOPELEKA KUIONDOA CCM, ILI HALI MIJIAMINISHA MTAKA KUINDOA CCM! this is a lie and must stop!
Vodaco, zain, tigo wanapata wateja kwa style nyingi, Je haiwezekani CDM ikavuna watu woote kwa style hii
Kama CDM ilianzisha operation SANGARA MWANZA, leo hii HAIWEZI KUANZISHA OPERATIONS KOROSHO MTWARA? au CDM itoiondoa ccm kwa mikoa fulani tu..BULLSHIT!!
Mimi ninayesema haya naonekana mbaya kwa lipi? wakati I believe I am posing challenge to chadema for good!!
Jamani ukweli utasimama na hata sasa watu wanajua nasimamia wapi, Come on, kupeana moyo na kutokosoana ni makosa na kama ni hivyo, I am sorry for you
Heshima kwako Waberoya,
Mkuu nimesoma bandiko lako mara mbili nimekuelewa sana bahati mbaya wapo wanajamvi wengi wenye uelewa mkubwa watakuja hapo na kujifanya hawajaelewa kitu.Umetoa tathmini ya hali halisi ilivyo mitaani [si JF] hakika nimeshuhudia mwenye juhudi zinazofanywa na watu mbali mbali kwa msaada wa mkubwa wa vyombo vya usalama.Rejea maandamano ya CHADEMA Arusha serekali na CCM hawakuwa na majibu ya kuhalalisha mauaji kilichofanyika ni kuwaita masheikh kutoa tamko la kulaani maandamano na kuunga mkono mauaji ya watu wasiokuwa na hatia na kukubali kuacha ukweli ukipotezwa.Ajabu ni CHADEMA yenye badala ya kuwaza na kuwazua ili andaa mpango mzuri wa mazishi ya marehemu wa dini zote mbili ingawa marehemu wa dini ya kiIslamu kulikuwa na patashika nguo kuchanika.Baada ya mazishi nilitegemea CHADEMA waje na plan B hasa kumaliza mbegu ya mgawanyiko wa kupandikizwa [kinga rasmi ya walioshindwa kutimiza wajibu wao] mpaka leo bado sijaona.
CHADEMA wanajua siasa za Tanzania tangu enzi za Mzee wa Kiraracha na Prof Lipumba walipotezwa kwenye ulingo wa siasa kwa kupandikiziwa uzushi wa ajabu,walishindwa kufanyia kazi uzushi matokeo yake sote tunajua,Uzushi unaenezwa na CCM dhidi ya CHADEMA bahati mbaya haufanyiwi kazi na viongozi badala yake wanadhani kufanya maandamano na kurusha mapicha ya wingi wa watu JF wamemaliza kazi!,tutakuja shangaa kama si kushangazwa.Ushauri wa Waberoya ufanyiwe kazi mara moja Tanzania inahitaji kukombolewa CHADEMA haiwezi kuikomboa nchi kama haiwezi kuifanyia kazi changamoto iliyoko mbele yake.
Ngongo,
Tatizo lenu anti-chadema ni kwamba mmekariri mbinu za siasa alizokuwa anatumia lyatonga mrema na lipumba tangu enzi na enzi, sasa hivi ni kipindi kingine na chadema inafanya siasa za kiwango kingine, bongo haijawahi kuwepo hii staili ya chadema.
Huwezi kuizuia ccm kutumia vyombo vyake vya dola kuisaidia kueneza propaganda dhidi ya chadema. Huwezo kuizuia ccm kuvitumia vyombo vya dola kuwaua raia wasiokuwa na hatia kwa kisingizio chochote kile cha "kulinda amani na utulivu, ama kutii sheria halali za igp mwema". Chadema hawana jeshi, au wewe ulitaka waanzishe uasi kama libya?? Kazi ya chadema ni kuwaeleza ukweli wananchi na ndicho kitu wamekifanya kwa suala la mauaji ya arusha.
Mnatakiwa kufahamu kwamba ccm itaendelea kutumia vyombo vya dola kujilinda na kufanya kila aina ya propaganda na chadema kikiwa chama mbadala kazi yake ni kuwaelimisha tu wananchi ili waweze kujua haki zao za msingi na matarajio yao kutoka kwa serikali yao waliyoichagua. Watakapopata elimu ya kutosha na kugundua kwamba hawawezi kamwe kujipatia maendeleo ya kweli chini ya ccm basi itakuwa ni kazi nyepesi mno kuing'oa ccm madarakani. Haya maandamano ya kanda ya ziwa tu yamewatia kizunguzungu, sasa huwezi kuona kwamba chadema wanajua kuweka mikakati ya kuwaamsha watanzania?? na wakishajua propaganda za ccm wataendelea tu kuiunga mkono chadema na hatimaye kuikabidhi uongozi wa nchi hii.
Jambo la msingi hapa ni wazi kwamba siasa ya chadema inawatisha ccm na hata vyama uchwara vya upinzani kama tlp na nccr mageuzi kwahiyo wanaungana na ccm kuishambulkia chadema lakini hamtofanikiwa kwa kuwa wananchi wa kizazi hiki si wale wale mlizoea kuwapa kanga na ubwabwa wanakupigia kura, sasa hivi wanakula ubwabwa wako kama ilivyotokea arusha kura wanampigia wanayemtaka!!