Chadema na cuf nunueni majeneza na sanda...hamtufai Tanzania

Narudia tena hata kama hivi vyama havina udini vimecheza muziki wa CCM ili vionekane hivyo na vimefanya hivyo! kwa wao kutochukua hatua mbadala ni kujiridhisha kuwa haviko hivyo!
 
Sidhani kama unaitendea haki CUF kuwa wameshindwa kujitetea mbele ya umma kuwa wao si Mjahidina au wako upande wa dini fulani pale tu mikutano yao inapohudhuriwa na Umati wa Watu wanaodhaniwa kuwa ni Waislamu! au kwa sababu ya mavazi yao au lugha na salamu zinazoyumika ktk mikutano yao!

Kama kweli wewe una share pande zote mbili za Kiislamu na Kikristo basi uwe mkweli hapa na fafanua basi ni ipi hiyo salamu ya CUF ktk mikutano yao, mavazi gani huwa wanavaa kuonyesha kuwa ni Waislamu,na kiliconishangaza ni kuwa hata kama Mikutano ya CUF inahudhuriwa na Waislamu wengi wewe ulitaka CUF wawe na utaratibu maalum wa kuchuja wote wanaohudhuria mikutano yao ili kuwa na usawa wa dini kwa Wahudhuriaji? au ulitaka wafuasi wa CUF wawe waangalifu kwa uvaaji wao wanapokuja ktk mikutano ya CUF wasiwe wanavaa vazi fulani hivi?

Au nilini CUF waliwakataza WaTZ wengine wasihudhurie mikutano yao? au ni Mkristo gani aliyenyimwa Uanachama? Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa Mwenyekiti wa kwanza na muasisi wa CUF alikuwa Mkristo Marehemu Museni Mugobi na naibu Katibu mkuu bara alikuwa Mkristo Lwakatare! achilia mbali akina Tambwe Hiza na maafisa wengine waandamizi wa ngazi za juu!

CUF kutokubalika ktk baadhi ya mikoa ya bara sio ajabu kwa sababu hata TANU wakati ilipoanzishwa ilikubalika haraka zaidi ktk mikoa ya ukanda wa Pwani na maeneo walioishi Waislamu wengi huku bara kama Tabora, Ujiji na ktk mitaa ya mijini ktk maeneo wanaishi Waislamu wengi! mfano, hapa Moshi na Arusha Mjini, TANU ilikubalika haraka zaidi ktk Mitaa ya BONDENI wanapoishi Waislamu wengi!

Ndio maana CUF wameona wasitumie rasilimali za Chama kuendelea kujitangaza maeneo ambayo wameona wenzao CHADEMA wamekubalika na hivyo kuamua hata kuwaachia peke yao wagombee huku wenzao Chadema wanapeleka mgombea wao maeneo kama Chake Chake!! hiki ni kichekesho! halafu wakikosa kura huko wanalalamika kuwa CUF ni chama cha kidini!

Chadema wanasema CUF ni chama cha Waislamu kwa kutoa ushahidi wa mavazi ya Wahudhuriaji mikutano ya CUF huku wenzao CUF wakithibitisha CDM kuwa ni cha Wakristo kwa ushahidi ufuatao:
1) Makanisa kutangaza waziwazi kuipigia kura CDM uchaguzi mkuu 2010 mfano: Kakobe
2) Makanisa kufungwa siku ya uchaguzi! haijawahi kutokea ktk historia!
3) Chadema kumpitisha Padri na mlei wa Kanisa kuwa mgombea Urais!
4) Chadema kupinga waziwazi hoja ya Mahakama ya Kadhi!
4) Inapinga TZ kujiunga na OIC!
5) Sera yao ya kufanya maamuzi magumu kuhusu Shule za binafsi zimewashtua Waislamu!
6) CDM inapinga bila hoja Serikali ya Umoja wa Wazanzibari na kuwatia hofu Wananchi wa visiwani ambao ni Waislamu!
7) Ukiacha CUF vyama vyote vikuu vya upinzani vinaongozwa na Wakristo watupu na wote wanatoka mkoa mmoja wenye Wakristo wengi!Waheshimiwa MMM(Mbowe, Mbatia na Mrema)!!!!!

Mwisho:
Napendekeza kuwa kama CHADEMA wanataka kututhibitishia si chama cha kidini basi kiache kufanya kampeni Makanisani, kisiwapitishe Walei wa Kanisa kuwa wagombea wao, na mwisho kiache kauli za kebehi kwa Waislamu na kupinga kila chenye Maslahi na Waislamu!!!

ZUbeda
Una majibu mazuri sana,lakini kwa kumbu kumbu zangu wewe ni mdini wa ajabu humu JF
Unaonaje hizo sababu zako za kuitetea CUF ukaziweka na upande wa CHADEMA?
 
Narudia tena hata kama hivi vyama havina udini vimecheza muziki wa CCM ili vionekane hivyo na vimefanya hivyo! kwa wao kutochukua hatua mbadala ni kujiridhisha kuwa haviko hivyo!

Kinacho nishangaza ni kuwa maneno mengi vitendo ZERO huna maana then. Kama unadonge tafuta chako kiwe cha mfano. CUF and CDM leaders have acted.

Haina maana hata kidogo kujibishana na vichaa maana haata wananchi wanajua labda wewe ulielala.

Yani ukaambiwa wewe ni MJUSI utapoteza muda kupita barabara kuwaambiwa wewe ni binadamu? Endelea kukaa vijiweni tu na kupiga soga. Achana na siasa if you can not act.
 
Samahani...........

Wabe, una umri gani?

Makombora wanayorushiana CUF na CDM ni yapi? ya JF au? maana ninavyofahamu mimi (sijui wengine), over my dead body, sikuwahi kumsikia kiongozi yeyote wa chadema akisema cuf ni cha kidini, wala kiongozi wa kikristo akisema cuf ni cha kidini. huu ni uwongo wa mchana ndiyo maana nimehoji umri wako.

Wabe, nilishakueleza na nitakukumbusha tena. While you throw stones on our lovely Chadema, please provide us with an alternative party to go by. vinginevyo mawazo yako hayawezi kuungwa mkono na watanzania wanaotaka mabadiliko. kwa kuungana na ccm (tunayoipinga), cuf wamefeli. kwa uroho wa 'ulaji na ubinafsi' nccr, tlp, udp wamefeli. now where do you advice us to go? kwa kina beno malisa? ningefurahi sana kama ungekuja na ufafanuzi kwa nini umeme unawaka 24 hours tanzania wakati tunajua kulikuwa na tatizo, na hatukuambiwa limetatuliwaje. tatizo nchi hii siyo cuf wala chadema. tatizo ni ccm inayofanya mbinu za kuuwa chadema na cuf kwa kutumia mamluki kama Wabe. as for my understanding, chadema hakitakufa, rather it will stay strong, na mimi kama mwanachadema mpenda mabadiliko, huwa napatwa na hasira sana nikisoma pumba za watu kama Wabe.

Kama msomi you should know why Tanzanians, especially illiterate Tanzanians like Mufti Simba think CCM is better. Tatizo watanzania tunakosa kitu kinachitwa deviation wakati wa kupiga kura. Am not a political scientist, lakini hii dhana imekuwa ikiwasaidia sana watu wa marekani na mataifa mengine yaliyoendelea. kwamna m-democrat anaweza kumpigia kura m-republican kwa kuwa tu m-republican anamuhakikishia mmarekani kuwa atakaposhika hatamu P.A.Y.E itapungua kulinganisha na kiwango cha wakati huo. M-democrat akiahidiwa nafuu ya maisha na M-republican, hata awe kada namna gani, hawezi kumpigia kura M-democrat eti kwa kuwa ni mtu wa chama chake. huu ndiyo ugonjwa unatutafuna watanzania, hasa wasio na elimu dunia kama mufti wenu. Kwa hisia Wabe, umekwenda shule, lakini namna unavyoleta hoja za mchiriku hapa jamvini nachelea kusema, kichwani kwako umejaa madesa. cuf na chadema na jamii za watu. usituletee mada za kichonganishi hapa. tumia elimu yako kuelimisha watanzania namna na kuchagua viongozi. usijisahau sana kuwa uko Dar unakula nchi, kuna mamilioni ya Watanzania kijijini wasiojua haki na wajibu wao kwa sababu ya CCM hii hii. natamani kulia, lakini...............

Mkuu wow!

You have written as a man!

Issue ni kuwa TATIZO LIPO NA KUTOLISEMA AU KULIFANYIA KAZI NI UZEMBE MKUBWA NA SIYO FAIR AT ALL! kuvionya hivi vyama kuwa viangalie wapiga kura siyo kosa! JAMANI TATIZO LA CHADEMA KULAUMIWA LIPO SANA, WANALAUMIWA MISIKITINI, KWENYE MAREDIO NA ZUBEDA UMEONA HAPO JUU. ULIKUWA WAJIBU WA CHADEMA KU-ACT KATIKA HILI MAPEMA SANA! TENA SANA! IN other words mpaka Muft kufikia kusema wanaompinga Kikwete ni sababu ya udini KAZI IPO , you know what I am saying

Nimecheka umesema tatizo ni CCM, ndiyo tatizo ndiyo chanzo na ndiyo wanasema hivyo, CUF + CCM wameungana kuiponda CDM, in other words CDM haijafanya intelligent move ya kupinga hizi tuhuma! CCM ni haki yao na kama wanamapinduzi hili ni konde tuko uwanja wa mapambano kusema ni ngumi ya fulani ili hali inauma haisaidii, CCM wont leave these parties freely they will deveour them!

TELL CHADEMA TO ACT ACCORDINGLY kujifanya eti hamna tatizo ni kosa, practically is wrong. IN other words pamoja na nia nzuri ya cdm bado siyo kuwa safari ni SMOOTH
. eBU SOMA MAONI YA zUBENDA UTAPATA PICHA

Lingine msifanye kosa la mnavyowza nyie na wenzetu vijijini ndivyo wanavyowaza, CDM wameweka mazingiea ya kufikiriwa hivyo
Udini wa nini hapa? Tumesema kila kukicha tupeni evidence ya udini na ukabila na huyo mtu anayefanya hayo achukuliwe hatua stahiki....tutabwabwaja kila siku bila kuchukua hatua.................

Evidence:

Sikiliza kauli ya kiongozi mkuu wa waislamu! that if for sure a very serious allegations!

Sidhani kama unaitendea haki CUF kuwa wameshindwa kujitetea mbele ya umma kuwa wao si Mjahidina au wako upande wa dini fulani pale tu mikutano yao inapohudhuriwa na Umati wa Watu wanaodhaniwa kuwa ni Waislamu! au kwa sababu ya mavazi yao au lugha na salamu zinazoyumika ktk mikutano yao!

Kama kweli wewe una share pande zote mbili za Kiislamu na Kikristo basi uwe mkweli hapa na fafanua basi ni ipi hiyo salamu ya CUF ktk mikutano yao, mavazi gani huwa wanavaa kuonyesha kuwa ni Waislamu,na kiliconishangaza ni kuwa hata kama Mikutano ya CUF inahudhuriwa na Waislamu wengi wewe ulitaka CUF wawe na utaratibu maalum wa kuchuja wote wanaohudhuria mikutano yao ili kuwa na usawa wa dini kwa Wahudhuriaji? au ulitaka wafuasi wa CUF wawe waangalifu kwa uvaaji wao wanapokuja ktk mikutano ya CUF wasiwe wanavaa vazi fulani hivi?

Au nilini CUF waliwakataza WaTZ wengine wasihudhurie mikutano yao? au ni Mkristo gani aliyenyimwa Uanachama? Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa Mwenyekiti wa kwanza na muasisi wa CUF alikuwa Mkristo Marehemu Museni Mugobi na naibu Katibu mkuu bara alikuwa Mkristo Lwakatare! achilia mbali akina Tambwe Hiza na maafisa wengine waandamizi wa ngazi za juu!

CUF kutokubalika ktk baadhi ya mikoa ya bara sio ajabu kwa sababu hata TANU wakati ilipoanzishwa ilikubalika haraka zaidi ktk mikoa ya ukanda wa Pwani na maeneo walioishi Waislamu wengi huku bara kama Tabora, Ujiji na ktk mitaa ya mijini ktk maeneo wanaishi Waislamu wengi! mfano, hapa Moshi na Arusha Mjini, TANU ilikubalika haraka zaidi ktk Mitaa ya BONDENI wanapoishi Waislamu wengi!

Ndio maana CUF wameona wasitumie rasilimali za Chama kuendelea kujitangaza maeneo ambayo wameona wenzao CHADEMA wamekubalika na hivyo kuamua hata kuwaachia peke yao wagombee huku wenzao Chadema wanapeleka mgombea wao maeneo kama Chake Chake!! hiki ni kichekesho! halafu wakikosa kura huko wanalalamika kuwa CUF ni chama cha kidini!

Chadema wanasema CUF ni chama cha Waislamu kwa kutoa ushahidi wa mavazi ya Wahudhuriaji mikutano ya CUF huku wenzao CUF wakithibitisha CDM kuwa ni cha Wakristo kwa ushahidi ufuatao:
1) Makanisa kutangaza waziwazi kuipigia kura CDM uchaguzi mkuu 2010 mfano: Kakobe
2) Makanisa kufungwa siku ya uchaguzi! haijawahi kutokea ktk historia!
3) Chadema kumpitisha Padri na mlei wa Kanisa kuwa mgombea Urais!
4) Chadema kupinga waziwazi hoja ya Mahakama ya Kadhi!
4) Inapinga TZ kujiunga na OIC!
5) Sera yao ya kufanya maamuzi magumu kuhusu Shule za binafsi zimewashtua Waislamu!
6) CDM inapinga bila hoja Serikali ya Umoja wa Wazanzibari na kuwatia hofu Wananchi wa visiwani ambao ni Waislamu!
7) Ukiacha CUF vyama vyote vikuu vya upinzani vinaongozwa na Wakristo watupu na wote wanatoka mkoa mmoja wenye Wakristo wengi!Waheshimiwa MMM(Mbowe, Mbatia na Mrema)!!!!!

Mwisho:
Napendekeza kuwa kama CHADEMA wanataka kututhibitishia si chama cha kidini basi kiache kufanya kampeni Makanisani, kisiwapitishe Walei wa Kanisa kuwa wagombea wao, na mwisho kiache kauli za kebehi kwa Waislamu na kupinga kila chenye Maslahi na Waislamu!!!

Cha kwanza umeconfirm kuwa ni JINSI GANI UNAVYOICHUKULIA CDM!! thanks for that

Pili sihitaji kuthibitisha kuwa salaam ya TAKBIR haisemwi, utakuwa ni muongo na mimi naogopa nisiseme kitu ambacho hakipo!

mtu anaye-connect dots inatosha kabisha kuthibitisha kuwa CUF kina udini mkubwa!! mbaya zaidi umeconfirma CDM wako hivyo

Ungekuwa hauna udini usingeleta tuhuma za CDM, umeona hivyo kwa CDM kwa sababu na nyie mko hivyo. I real blame CDM they have fallen in the same pit like you!
 
Kinacho nishangaza ni kuwa maneno mengi vitendo ZERO huna maana then. Kama unadonge tafuta chako kiwe cha mfano. CUF and CDM leaders have acted.

Haina maana hata kidogo kujibishana na vichaa maana haata wananchi wanajua labda wewe ulielala.

Yani ukaambiwa wewe ni MJUSI utapoteza muda kupita barabara kuwaambiwa wewe ni binadamu? Endelea kukaa vijiweni tu na kupiga soga. Achana na siasa if you can not act.

Waberoya anafahamika kwamba ni mfuasi mtiifu wa CCM na washirika wake.

Hajawahi kuwa na mapenzi wala uzalendo na nchi hii ya kambarage pamoja na kujinasibu kwamba anafanya hivyo kwa mapenzi mema na uzlendo wake. Kama uzalendo wake ni yeye kuwa mtanzania basi tunahiutaji kuweka madaraja ya uzalendo na katika hilo bila shaka ataangukia kwenye kundi la mwisho lililo na kiwango kidogo sana cha uzalendo ama kundi la watu wasio na uzalendo.

Waberoya hajawahi kuja hapa na hoja yoyote ya msingi ya kujenga na kuimarisha upinzani zaidi ya kuvurumsha kashfa, kejeli namatusi kwa chadema huku akijificha kwenye mgongo wa cuf, tlp, nccr mageuzi na ccm.

Yeye anachokiona ni kile tu kinachotoka kwa zitto, na kama zitto angekuwa mwenyekiti wa chadema basi kila siku angekuwa anakuja na mashairi marefu kama haya yakiwatukuza chadema lakini kwa kuwa swahiba wake zitto alijaribu kuwania uenyekiti lakini akashauriwa ajitoe kwa kuwa alikuwa hajafikia kiwango cha kuiongoza chadema basi maswahiba zake wamekuwa na kinyongo sana dhidi ya uongozi wa chadema uliopo na kumhusisha mzee mtei. Hawezi kujadili hoja ya chadema bila kumtaja mzee mtei na dr.slaa, hizi ni dalili za wazi za kuishiwa hoja na kwa kuwa unafanya kazi uliyotumwa kwa niaba ya swahiba wako, hautafanikiwa kamwe. Chadema inakubalika kona zote za nchi hii. Kanda ya ziwa tuko dini mchanganyiko lakini mwenyewe umeshuhudia ni kwa kiasi gani wananchi wa huko tunaiunga mkono chadema wala hatuulizani dini za viongozi wa chadema bali tunaangalia maslahi ya nchi kwanza, si maslahi ya mtu wako kwanza.

Lililo muhimu zaidi hapa ni wewe na rafiki zako mnaojifanya mnaipenda chadema muanze kuandaa sanda na majeneza kwa kuwa nyie ndo mtakao zikwa mapema wakati chadema ikiendelea kushamiri na hatimaye 2015 inachukua uongozi wa taifa hili.
 
wewe wasema!

Mufti naye ni ccm au yuko upande wa zitto? maana karusha kombora cdm!
 
My dissection of political representation in Tanzania:

CCM - Ali Baba and the forty thieves
Chadema - Online bigots
CUF - Zanzibari xenophobes
TLP and UDP - No marks, there are wapiga debe with more clout, integrity and credibility.

Time for independents. What do you stand for?
 
Mkuu,

Hizo INTELLIGENT MOVE za kupinga tuhuma za KIJINGA za CCM + CUF ni kama zipi?

Kujipendekeza! thats all! adui yako msogelee , jipendekeze , wanahitaji hilo tu! kuliko KUUA CHAMA AMBACHO KIMETOA JASHO KUFIKA KILIPO , just jishushe!

Let ccm go to those mikoa ambayo hawajajikita! ambayo maadui anaitumia kusema ni chama cha mikoa fulani!

marketing and gospel techniques zinahitajika! na hazina shida!

Hujagundua mpaka Muft kusema aliyoyasema anaonyesha kuna GAP sana kati ya yeye na chama? unapoingia mjini au mtaani kuna wazee wa kuwaona, Mdee analijua hili vizuri sana, ni kujifanya mjinga nyakati fulani, much know huwa inagonga mwamba sana!
 
wewe wasema!

Mufti naye ni ccm au yuko upande wa zitto? maana karusha kombora cdm!

Mufti anafahamika yuko chama gani,

Kama asingekuwa mfuasi wa hicho chama, asingekubali kukaa kimya chama tawala kikiwanyima waislamu haki yao ya "ibada ya mahakama ya kadhi" ambayo waliitumia katika ilani ya uchaguzi kujizolea kura za waislamu mwaka 2005.

Lakini kwakuwa ni chama chake ameamua kwa makusudi kuminya haki za waislamu kuwa na ibada ya mahakama ya kadhi na badala yake sasa anakisaidia chama chake kuendesha propaganda za kisisa dhidi ya chadema.

Kwa maneno machache sana, comment ya mufti dhidi ya chadema haina tofauti na mtazamo na msimamo wako dhidi ya chadema.
 
maneno sawia kabisa.

Chadema wana changamoto kubwa sana ya kukifanya chama hicho kiwe na sura ya kitaifa na kujivua joho lao la sasa la kuw Chama cha kikanda, kikabila na kidini
 
Mkuu Waberoya!
Ni uchungu ulioje mtu kuisoma mada hii!? Ni maumivu kiasi gani mtu kuisikia habari isiyompendeza masikioni na machoni pake?
Watanzania wengi hawahitaji kufikiria kama vile tunavyofikiria... wengi hawahitaji kuona kile kinachoonekana... wengi wetu tunapenda hata chongo tukiite kengeza!
Mkuu usikate wala kukatishwa tamaa... Ni kazi kuwaamsha waliokufa mioyo na kuishi kwa matumaini! Maana wao wanahitajia maneno ya faraja kuliko ukweli ambao ungeliweza kuwakomboa!
Nasisitiza....
Hivyo vyama viwili ni VIFU, na kinachovisababishia ufu wake ni kukosekana kwa mawazo mbadala... KWANI VIONGOZI WAKE WENGI WAMETOKANA NA MFUMO WA CCM, HIVYO BASI HAWANA JIPYA... (KASISI NI YULEYULE AMEBADILI JOBO TU)
 
Mkuu Waberoya!
Ni uchungu ulioje mtu kuisoma mada hii!? Ni maumivu kiasi gani mtu kuisikia habari isiyompendeza masikioni na machoni pake?
Watanzania wengi hawahitaji kufikiria kama vile tunavyofikiria... wengi hawahitaji kuona kile kinachoonekana... wengi wetu tunapenda hata chongo tukiite kengeza!
Mkuu usikate wala kukatishwa tamaa... Ni kazi kuwaamsha waliokufa mioyo na kuishi kwa matumaini! Maana wao wanahitajia maneno ya faraja kuliko ukweli ambao ungeliweza kuwakomboa!
Nasisitiza....
Hivyo vyama viwili ni VIFU, na kinachovisababishia ufu wake ni kukosekana kwa mawazo mbadala... KWANI VIONGOZI WAKE WENGI WAMETOKANA NA MFUMO WA CCM, HIVYO BASI HAWANA JIPYA... (KASISI NI YULEYULE AMEBADILI JOHO TU)
 
Kujipendekeza! thats all! adui yako msogelee , jipendekeze , wanahitaji hilo tu! kuliko KUUA CHAMA AMBACHO KIMETOA JASHO KUFIKA KILIPO , just jishushe!

Let ccm go to those mikoa ambayo hawajajikita! ambayo maadui anaitumia kusema ni chama cha mikoa fulani!

marketing and gospel techniques zinahitajika! na hazina shida!

Hujagundua mpaka Muft kusema aliyoyasema anaonyesha kuna GAP sana kati ya yeye na chama? unapoingia mjini au mtaani kuna wazee wa kuwaona, Mdee analijua hili vizuri sana, ni kujifanya mjinga nyakati fulani, much know huwa inagonga mwamba sana!

Nadhani nadharia zako juu ya kuendesha chama cha siasa katika nchi hii ziko outdated,

Chama cha upinzani hakihitaji kujishusha kwa ccm, yaani ccm anakufanyia hujuma za waziwazi halafu wewe ujishushe na kujipendekeza kwake?? hizo ni strategies za cuf lakini si chadema. Kama lengo kuu la chama cha siasa ni kuchukua madaraka na uongozi wa nchi, na cuf walipogundua kwamba hawawezi kamwe kuingoza nchi, mathalani hawawezi kushinda uchaguzi visiwani zanzibar ndo wakaamua kujishusha na kujipendekeza kwa ccm.

Chadema ni chama tofauti sana na cuf, hawawezi kuendesha siasa za cuf, ndo maana unaona mikakati yao ya kisiasa ni tofauti sana hata cuf wenyewe wanaiga na kuhusudu.Hapo ndipo unaonekana dhahiri ufuasi wako wa ccm kwa kuwashauri chadema wafuate mkumbo wa cuf ili wafikie hatua ya kufa kama unavyotabiri.Chadema itaendelea kusonga mbele na utaendelea kuumia tu na roho yako.
 
Haya ndo unayo tu? au umemega? GO DOWN TO EARTH AU KAJITUNDIKE.

Tatizo lako unahisi unajua kuliko vichwa vyote pale CUF na CDM kumbe mdomo tu kwa kuwa haulipiwi kodi. Tafadhali naomba ELIMU na UZOEFU wako katika SIASA.
 
Mkuu Waberoya!
Ni uchungu ulioje mtu kuisoma mada hii!? Ni maumivu kiasi gani mtu kuisikia habari isiyompendeza masikioni na machoni pake?
Watanzania wengi hawahitaji kufikiria kama vile tunavyofikiria... wengi hawahitaji kuona kile kinachoonekana... wengi wetu tunapenda hata chongo tukiite kengeza!
Mkuu usikate wala kukatishwa tamaa... Ni kazi kuwaamsha waliokufa mioyo na kuishi kwa matumaini! Maana wao wanahitajia maneno ya faraja kuliko ukweli ambao ungeliweza kuwakomboa!
sishangai kuona mtu anaona baadhi tu...kuwa ndio kiini cha mada hii... lakini mada hii ina maana kubwa sana wa watu wenye kufikiri Ila kwa wenye kufuata mapenzi na propaganda.. hawataona chochote katika mada hii....
Mkuu Wabe' hakika unaona mbali sana... zaidi ya pale wengi wetu wanapoona! Ila ni lazima kusema... wakitukana sawa... waseme vyovyote vile ilimradi dawa inapenya!

Nasisitiza....
Hivyo vyama viwili ni VIFU, na kinachovisababishia ufu wake ni kukosekana kwa mawazo mbadala... KWANI VIONGOZI WAKE WENGI WAMETOKANA NA MFUMO WA CCM, HIVYO BASI HAWANA JIPYA... (KASISI NI YULEYULE AMEBADILI JOHO TU)
 
Hujagundua mpaka Muft kusema aliyoyasema anaonyesha kuna GAP sana kati ya yeye na chama? unapoingia mjini au mtaani kuna wazee wa kuwaona, Mdee analijua hili vizuri sana, ni kujifanya mjinga nyakati fulani, much know huwa inagonga mwamba sana!

Unaposema GAP kati kati yake na Chama unamaanisha yeye binafsi au na anaowawakilisha? Hivi unataka kusema yale maandamano ya CDM yalikuwa ni ya wakristo peke yao???
 
Mufti anafahamika yuko chama gani,

Kama asingekuwa mfuasi wa hicho chama, asingekubali kukaa kimya chama tawala kikiwanyima waislamu haki yao ya "ibada ya mahakama ya kadhi" ambayo waliitumia katika ilani ya uchaguzi kujizolea kura za waislamu mwaka 2005.

Lakini kwakuwa ni chama chake ameamua kwa makusudi kuminya haki za waislamu kuwa na ibada ya mahakama ya kadhi na badala yake sasa anakisaidia chama chake kuendesha propaganda za kisisa dhidi ya chadema.

Kwa maneno machache sana, comment ya mufti dhidi ya chadema haina tofauti na mtazamo na msimamo wako dhidi ya chadema.

Pengo yuko chama gani?

Nadhani nadharia zako juu ya kuendesha chama cha siasa katika nchi hii ziko outdated,

Chama cha upinzani hakihitaji kujishusha kwa ccm, yaani ccm anakufanyia hujuma za waziwazi halafu wewe ujishushe na kujipendekeza kwake?? hizo ni strategies za cuf lakini si chadema. Kama lengo kuu la chama cha siasa ni kuchukua madaraka na uongozi wa nchi, na cuf walipogundua kwamba hawawezi kamwe kuingoza nchi, mathalani hawawezi kushinda uchaguzi visiwani zanzibar ndo wakaamua kujishusha na kujipendekeza kwa ccm.

Chadema ni chama tofauti sana na cuf, hawawezi kuendesha siasa za cuf, ndo maana unaona mikakati yao ya kisiasa ni tofauti sana hata cuf wenyewe wanaiga na kuhusudu.Hapo ndipo unaonekana dhahiri ufuasi wako wa ccm kwa kuwashauri chadema wafuate mkumbo wa cuf ili wafikie hatua ya kufa kama unavyotabiri.Chadema itaendelea kusonga mbele na utaendelea kuumia tu na roho yako.

Poor Mwita!

Sijasema CDM kijishushe kwa CCM! No where in my post I have indicated that!

Nimesema kijishushe kwa jamii ile ambayo wanaambiwa hawapo!

Hivi leo hii CDM ikaamua kutumia sh. laki moja tu kusema imetoa msaada wa madaftari shule ya sekondari Al-almain kuna kosa?
Leo hii CDM wakisema wanamtembela Mufti na kuuliza Bakwata inafanyaje kazi na kutoa pongezi kwa kazi nzito ya kuongoza Bakwa ni kosa/
Leo hii sikuu ya Idd ikifika na CDM ikatoa mdaada kwa watoto mayatima ni kosa

Kwa kufanya hayo au yanayofanana na hayo CDM itakuwa kwa kiasi gani imejivua hizi TUHUMA

Mwita, I know you hate me, because you think I hate CDM, I dont hate anybody NINACHOKASIRIKA NI KUFANYA MATENDO YASIYOPELEKA KUIONDOA CCM, ILI HALI MIJIAMINISHA MTAKA KUINDOA CCM! this is a lie and must stop!

Vodaco, zain, tigo wanapata wateja kwa style nyingi, Je haiwezekani CDM ikavuna watu woote kwa style hii

Kama CDM ilianzisha operation SANGARA MWANZA, leo hii HAIWEZI KUANZISHA OPERATIONS KOROSHO MTWARA? au CDM itoiondoa ccm kwa mikoa fulani tu..BULLSHIT!!

Mimi ninayesema haya naonekana mbaya kwa lipi? wakati I believe I am posing challenge to chadema for good!!

Jamani ukweli utasimama na hata sasa watu wanajua nasimamia wapi, Come on, kupeana moyo na kutokosoana ni makosa na kama ni hivyo, I am sorry for you
 
Unaposema GAP kati kati yake na Chama unamaanisha yeye binafsi au na anaowawakilisha? Hivi unataka kusema yale maandamano ya CDM yalikuwa ni ya wakristo peke yao???

Mkuu anayejua hawakuwa wakristo peke yao ni mimi na wewe! Mufti angejua hilo angesema alichosema? au unataka kusema haujaona athari za maneno yake kwa nafasi yake? My take here is HOW CDM acts in allegations like these? can you help! au umeshawahi kufikiria kukisaidia chama?
 
Mkuu Waberoya!
Ni uchungu ulioje mtu kuisoma mada hii!? Ni maumivu kiasi gani mtu kuisikia habari isiyompendeza masikioni na machoni pake?
Watanzania wengi hawahitaji kufikiria kama vile tunavyofikiria... wengi hawahitaji kuona kile kinachoonekana... wengi wetu tunapenda hata chongo tukiite kengeza!
Mkuu usikate wala kukatishwa tamaa... Ni kazi kuwaamsha waliokufa mioyo na kuishi kwa matumaini! Maana wao wanahitajia maneno ya faraja kuliko ukweli ambao ungeliweza kuwakomboa!
sishangai kuona mtu anaona baadhi tu...kuwa ndio kiini cha mada hii... lakini mada hii ina maana kubwa sana wa watu wenye kufikiri Ila kwa wenye kufuata mapenzi na propaganda.. hawataona chochote katika mada hii....
Mkuu Wabe' hakika unaona mbali sana... zaidi ya pale wengi wetu wanapoona! Ila ni lazima kusema... wakitukana sawa... waseme vyovyote vile ilimradi dawa inapenya!

Nasisitiza....
Hivyo vyama viwili ni VIFU, na kinachovisababishia ufu wake ni kukosekana kwa mawazo mbadala... KWANI VIONGOZI WAKE WENGI WAMETOKANA NA MFUMO WA CCM, HIVYO BASI HAWANA JIPYA... (KASISI NI YULEYULE AMEBADILI JOHO TU)

Good to hear from you!

Ikiwa hivi vyama tunavitegemea kuiondoa CCM, vinaishi na Kufanya kama wanayoyafanya, wanaambiwa wadini na kweli kabisa kila wanalotenda linaconfirm wanachosema mahasimu wao!???

Ikifikia kutopewa kura wanasema kura zimeibiwa, ukiwauliza mlifika Lindi na Mtwara na kufanya lile lile mlilofanya kanda ya ziwa ..kimya!

Ukiwaulzia CUF mlifika mbeya ? kimya!

Ukikaa chini utagundua si vyama vya KISIASA IS JUST A BUNCH OF JOBLESS people who wants their life to move on! kama wako serious na siasa wangefanya kila njia kuziba tuhuma za kidini ambazo CCM wanaelekeza kwao

ukiwauliza vilaza wengi humu..WANASEMA NI TUHUMA ZA ccm? sasa ulitaka ziwe tuhuma za nani?....kimya!

I once said haviko kwa ajili ya maslahi ya nchi, KUIGAWA TANZANIA KWA STYLE YOYOTE ILE NI HATARI NA HIVYO HAVITUFAI.period!,

Kwa wanasiasa makini sana, Slaa hakupaswa kugombea urais kwa background yake, That decision have arleady killed chadema-Mbowe hakuwa na tuhuma hizi za udini!, they dont care, why?? kwa sababu wanakula na kucheua ruzuku ambazo ni kodi zetu??! wachache humu JF wanataka kutuaminisha wako kwa maslahi ya TAIFA ! unapotoa challenge kama hizi ambazo ziko so OBVIOUS WANATOA MATUSI, WANASHINDWA KUJIBU AU HOJA ZAO INABIDI WENGINE TUCHEKE!!!

Wembe ule ule tunaoutumia kuinyoa CCM ni ule ule utatumika kwenye kila chama, maana wana siasa ni binadamu si malaika anayefikiria kinyume na hapo ...nampa pole!

wako wengine wanataka kutuaminisha eti hakuna tatizo...waendelee hivi hivi mpaka 2015! wakishindwa watashtuka kidogo na kupiga kelele za tumeibiwa , baadae maisha yanaendela kama kaiwada INAKUWA USIKU INAKUWA MCHANA MWAKA 2030-CCM is there!! No it has to end now! huu ni ufisadi mwingine!
 
Back
Top Bottom