Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,668
- 10,092
Ndugu zangu Watanzania,
Naomba nitumie jukwaa hili kwa siku ya leo kuwapa ukweli CHADEMA japo ni ukweli mchungu unaouma lakini ndio ukweli wenyewe na hauwezi kubadilika wala kubadilishwa. Napenda kuwaambia ya kuwa kuna majimbo hapa Nchini ambayo ningependa kuwaambia CHADEMA ya kuwa wasipoteze muda wala pesa wala nguvu zao wala kujichelewesha kufanya kampeni.
Na hivyo ni bora muda huo wakapeleka kwenye maeneo mengine ambako wataona wanaweza kuambulia chochote. Ni bora hata kuwekeza nguvu kwa majimbo machache na rasilimali zote yaani rasilimali fedha na watu kuweza kupambana kujaribu kupata wabunge kiasi kuliko kuweka na kusimamisha wagombea kila jimbo na mwisho wa siku kukosa kwote kwote.
Leo nitataja Machache na kwa uchache halafu siku nyingine nitawatajia mengine. Sitaki kuwachosa kwa andiko refu bali nataka nitaje machache kwanza halafu mpate muda wa kujitafakari. Hao wachache kwa leo ni kama ifuatavyo na kuwa kama watachukua Fomu na chama kuwasimamisha kupeperusha bendera, basi CHADEMA mkubali kuachana na majimbo hayo.
Mheshimiwa Dkt Tulia Acksoni Mwansasu. Huyu dada yangu napenda kuwaambieni na kuwathibitishia ya kuwa yeye atagombea, hilo nina uhakika nalo na sababu zinajulikana kabisa na zipo wazi kabisa.
Kwa sababu wana Mbeya hawawezi mkubalia asigombee maana wanamtegemea sana na wana mhitaji sana kuliko yeye anavyowahitaji wana mbeya, lakini pia ni Rais wa IPU ambapo nafasi hiyo inamtaka aendelee kuwa Mbunge.
Pili umri wake bado ni mdogo na unamruhusu kuendelea na mchaka mchaka wa kuwatumikia na kuwahudumia wana Mbeya katika nafasi ya ubunge. Mengi nitawachambulia Zaidi wakati mwingine kumhusu yeye hasa katika eneo la uchapa kazi wake na namna alivyogusa na kukonga mioyo ya wana Mbeya,ambao sasa wana tabasamu wakati wote.
- Mheshimiwa Kassimu Majaliwa Majaliwa.
- Mheshimiwa Dotto Biteko.
- Mheshimiwa Jenista Mhagama.
- Mheshimiwa Ummy Mwalimu.
- Mheshimiwa Innocent Bashungwa
- Mheshimiwa Dkt Mwigulu Nchemba.
- Mheshimiwa Hussein Bashe.
- Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete.
- Mheshimiwa January Makamba.
- Mheshimiwa Dkt Joseph Kasheku Msukuma.
_Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa.
_Mheshimiwa Juma Aweso.
Leo naishia hapa kwanza maana nimesema leo sitaki kuwachosha kwa andiko refu, hao waheshimiwa na majimbo yao ningewaomba na kuwaambia ukweli CHADEMA msipoteze muda wenu wala pesa zenu kuweka wagombea maana hamtaambulia kitu chochote kile.
Mtapigwa tu ikiwa hao waheshimiwa wataamua kugombea maana suala la kugombea lipo ndani ya moyo wa mhusika.
Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.