CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Kutokana na mjadala mrefu uliokuwepo kutokana na Taarifa ya "Kamati ya Wazee", Kamati Kuu, kwa kuzingatia mwenendo wako ambao kwa dhahiri unakiuka Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Taifa, Kifungu cha 10(1)(viii), (ix),(x),(xi) na (xii).

Hii ni sehemu ya taarifa inayotegemea kutolewa leo kwa waandishi wa habari.
 
Mmmmhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!! mambo yale yale ya CCM, ZANU, KANU na vyama vingine vya wajinga Afrika.

Aliyechaguliwa na wananchi kwenye mkutano mkuu wa chama, anasimamishwa na kamati ya wapambe.

Adhabu ya mwanasiasa inapatikana kwenye uchaguzi, haya mambo ya kusimamishana yananikumbusha vyama vya Wakomunisti na hivyo vyama vyetu vya Afrika vinavyojaza wapambe kwenye kamati kuu.

Nilikuwa nafikiri CHADEMA ni chama makini, kumbe na wao ni yale yale tu. Je vipi Wangwe hajaanguka kwa BP?

Mkuu MK, wengine tunajua ulikuwepo kwenye hiyo kamati yenu, tuambie kilichotokea na sio hizi craps za taarifa ya chama. Naona hapa naangalia picha ambayo nilishaiona mwanzoni, tofauti tu ni mchezaji kabadilika. Badala ya main actor kuwa CCM sasa nao CHADEMA mnacheza kamchezo kale kale. Aibu kweli kweli.
 
Mmmmhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!! mambo yale yale ya CCM, ZANU, KANU na vyama vingine vya wajinga Afrika.

Duuuh ,hii sio haki kuita vyama vya wajinga afrika.....
 
vyama vingi duniani (hata vya kimagharibi) hutumia sera hiyo ya kumsimamisha mtu kwa kutumia kamati kuu.
muhimu ni kuangalia jee alistahiki au ni propaganda za kugombeana nafasi tu?
 
Aliyechaguliwa na wananchi kwenye mkutano mkuu wa chama, anasimamishwa na kamati ya wapambe.

Soma katiba ya CHADEMA kwani itakuonyesha alichaguliwa na nani ,huyu hakuchaguliwa na mkutano mkuu wa chama kwani aliwekwa kukaimu nafasi hiyo baada ya kuachwa wazi na Kabourou .

Haya ni maamuzi mazito na kwa vyovyote vile lazima yatasababisha chama hicho kutikisika ila kutokana na kulinda katiba ya chama hicho nafikiri watakuwa tayari kuelezea umma ni kwa nini wameamua kufikia uamuzi huo mkubwa na mkali kiasi hicho.
 
Mmmmhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!! mambo yale yale ya CCM, ZANU, KANU na vyama vingine vya wajinga Afrika.

Duuuh ,hii sio haki kuita vyama vya wajinga afrika.....

Mkuu MK,

Vyama vyetu visingelikuwa vya wajinga, tusingelikuwa hapo tulipo.

Mnaotaka kuongoza Afrika lazima mbadilika na sio kuendeleza ujinga ule ule ambao ndio umetukwamisha.

Sina mapenzi na Wangwe na najua sio mwanasiasa makini lakini siungi mkono kabisa haya mambo ya viongozi wanaochaguliwa na watu walio wengi kufukuzwa na kakundi ka wapambe wachache.

Ningewaona wa maana kama mungejiuzulu wote na kuitisha uchaguzi upya ili wanachama wa CHADEMA waamue wamrudishe nani na wamlime nani. Haya mambo ya kufukuzana na kusimamishana kwenye vyama ni ujinga tu.

Kama kumsimamisha basi hicho kikao kilichomchagua ndio kingemsimamisha. Kila mtu anayefuatilia siasa za CHADEMA anajua Wangwe alikuwa haungwi mkono na kamati kuu ya CHADEMA. Sasa mmepata nafasi ya kufanya yale ambayo mlishindwa kufanya kwa kura kwenye mkutano wa CHADEMA. Ndio ujinga tunaousema wengine.
 
Mi sisemi hivyo lakini najua muda si mrefu kuna watu wakiingia humu watasema ni kwa kuwa tu si mchaga!
 
vyama vingi duniani (hata vya kimagharibi) hutumia sera hiyo ya kumsimamisha mtu kwa kutumia kamati kuu.
muhimu ni kuangalia jee alistahiki au ni propaganda za kugombeana nafasi tu?

Gaijin,

Toa mfano maana haitoshi kusema hata vyama vya magharibi vinafanya hivyo. Kikawaida magharibi, unaondolewa uongozi na mtu aliyekuweka na wala sio hizo kamati kuu za vyama ambazo ukiangalia walio wengi wanakuwa wapambe wa mwenyekiti.
 
watatoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari while kwenye gazeti la Tanzania daima wameshaitoa hiyo habari? kwanini hawakuchukua fursa ya kuvitaarifu vyombo vyote vya habari kiasi kwamba watoe kwenye gazeti lao tu??

Nahitaji kujua tu....
 
Huyu bwana kwa kweli alikuwa anakera sana wakati mwingine! Yaani si mtu makini kama tulivyowazoea viongozi wengine wa CHADEMA. Najua yafuata maneno mengi na labda watu wa tarime watareact sana, lakini lazima tukubali ili kuwa na upinzani makini lazima na watu wake wawe makini sana! Mimi naamini wabunge wa upinzani (individually) ni competent zaidi ya wale wa CCM kwa sababu wanafanya kazi na kushinda katika mazingira magumu sana. Pia hata ukinagalia wanavyojenga hoja, za wapinzani nyingi utakuta zimejaa akili. CCM imejaza watu weak sana! Upinzani pia labda kuna problem kidogo kwa baadhi ya wabunge wanaotokea upande wa Zanzibar ukiachia akina Hamad Rashid na wengine wachache
 
MK,

Website yenu kule haifanyi kazi, rekebisheni maana uki click kwenye kamati kuu, hakuna kitu. Tunataka kuwajua hao walioamua kumsimamisha Wangwe.

Wanaanchi walikuwa wanaanza kuwa na imani na hawa CHADEMA sasa nao wanaanza kuchemsha, kweli Waafrika ndivyo tulivyo.
 
Mama si unajua adui yako muombee Njaa wewe waache tu hapa CCM inazidi kujikita zaidi na zaidi!na 2010 ni CCM as usual

Hollo sisiemu yenu ina mambo, lakini upinzani kuko kama kuna mambo zaidi (kama ajira sector binafsi vile) he he heee. Langu jicho, mkono na shavu langu.
 
KOMBA ALIWAHI KUIMBA WIMBO.....!
SASA KUMEKUCHA.....X2
JOGOO LISHAWIKA 'dodoma'.....!
TUNASUBIRI KUSIKIA TOKA KWENU....!
 
Aliyechaguliwa na wananchi kwenye mkutano mkuu wa chama, anasimamishwa na kamati ya wapambe.

Soma katiba ya CHADEMA kwani itakuonyesha alichaguliwa na nani ,huyu hakuchaguliwa na mkutano mkuu wa chama kwani aliwekwa kukaimu nafasi hiyo baada ya kuachwa wazi na Kabourou .

Haya ni maamuzi mazito na kwa vyovyote vile lazima yatasababisha chama hicho kutikisika ila kutokana na kulinda katiba ya chama hicho nafikiri watakuwa tayari kuelezea umma ni kwa nini wameamua kufikia uamuzi huo mkubwa na mkali kiasi hicho.

Ule mkutano mkuu ulofanyika Dar ulimchagua nani?Tena nakumbuka hata kwenye mkutano huo ilikuwa na kelele tu vimemo kibao na vipeperushi vya kutishana sijui na ukabila!Chadema bado sana sana!
Ndo maana jana Bob Makani alikuwa Dodoma du si mchezo
 
Kwa vyovyote vile huu uamuzi utakitikisa chama kiasi chake hasa kwa upande wa 'kambi' Wangwe kwenye uchaguzi uliotawaliwa na vituko kinamna wa nafasi ya makamu mwenyekiti

La muhimu ni kuangalia sababu za kusimamishwa kwake kama zinaleta 'maana' kwa walio wengi

je amevuliwa pia uanachama au 'kasimamishwa' tu?
 
JE CHADEMA ITASALIMIKA......! KAMA KUNA WAO......(wachaga) NA SISI ....(makabila mengine)....! DHAMBI HII IKISHAKUWALA BADO ITAENDELEA NA KWA.....!
tik...tak....tik...tak...!
 
Mhe. Chacha Wangwe alishaonyesha kwamba hana haiba ya uongozi hata kabla ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo, ila anafaa kwenye ubunge kwani anaweza kutetea watu hasa kwa kulalamika na kulalama. Mimi nadhani CHADEMA wamwfanya sahihi ili kukinusuru chama chao.

Kumpatia Umakamu Mwenyekiti huyo Mheshimiwa na sawa na CCM kumpatia Mhe. Shibuda awe Makamu Mwenyekiti.
 
Back
Top Bottom