CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Ninajaribu kufuatilia siasa na hasa bunge letu kwa karibu sana, kuna wabunge au wanasiasa ambao aidha kwa mchango wao bungeni wanaonekana kujua kile wanachokisema au kwa namna ingine mtiririko wa mawazo na changamoto zao inakuwa ni rahisi kwa wananchi kufuatilia. sihitaji kuingia kwa kina kutoa mifano ya wabunge ambao kwa namna moja wanaweza kuchangia hoja na kufuatilia kinachozungumzwa huku wakitofautiana au kukubaliana kwa points, takwimu au vielelezo.

Huyu mbunge Chacha Wangwe kwa mara moja au zaidi kwa mawazo yangu sioni kama anawasaidia sana wapinzani, kwa mtizamo wangu naona kama vile anaharibu credibility ya wapinzani. Inakuwa kama vile ana leta ubabaishaji kidogo hapa. Ningependa kunukuu kidogo hapa akiwa anachangia hoja ya Mheshimiwa Zitto Kabwe, Hoja ya kuundwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya Mikataba ya Madini na mazingira ya kusainiwa kwa Mkataba (MDA) mpya wa madini wa Buzwagi kulikofanywa na Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Nazir Karamagi (Mb) huko Uingereza Mwezi Februari 2007. Maelezo ni marefu kidogo ila haitakuwa haki kuweka nusu ya mchango wake wake bungeni:


"MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, asante sana kwa kunipa nafasi kuchangia hoja hii muhimu, kwanza kabisa napenda kukupa pole kwa msiba wa mjomba wako ambaye Tanzania inamtambua kama mwana harakati wa kweli ambaye alitumia muda wake mwingi sana kuwapigania wananchi na hakuona kama chama kilikuwa ni kigezo kikubwa ndiyo maana aliweza kuwa hata upande wa wapinzani. (Makofi)

Pia napenda kumpa pole Waziri wa Ardhi Mheshimiwa Magufuli kwa kifo cha Baba yake Mpendwa, Mheshimiwa Magufuli ameonyesha kwamba na yeye anauwezo wa kusimamia ukweli, na ndiyo maana wakati anakuwa na maadui wengi. Kwa sababu haki siku zote inaposimamiwa ni lazima wale wasiopenda haki wafanye uadui, na waweze kukejeli ili kuifunika haki. Lakini mimi nasema ya kwamba nikiwa kama Mbunge ambaye nimechaguliwa na nimekuja hapa pamoja na Wabunge wenzangu tukala kiapo kwa sababu sisi Wakurya na waafrika kwa ujumla tunaogopa sana kiapo. Unapoinua mkono wako hapa na kusema ya kwamba nitailinda na nitasema kweli daima, kinyume chake ni kwamba hivyo hicho kiapo kitakumaliza wewe, kwa hiyo wale ambao wanaikiuka viapo vyetu hapa kwa kutaka kugeuza uwongo uwe ukweli basi wananchi wanaona, Mungu anaona na wenyewe dhamiri ndani yao zinawashitaki kwamba haya wanayoyasimamia ni mambo ambayo hayana ukweli wowote.

Kwa kuwa Mungu ni Mungu wa haki na wananchi wa Tanzania wanachokitaka ni haki mimi naunga mkono hoja hii mia kwa mia kwamba ili tujiridhishe na pia Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye mimi namheshimu sana ni msomi mzuri na anafanya kazi kwa bidii ili hiki kiwingu cha kusema ameharibiwa jina kiondoke ni lazima kuwe na Tume ambayo itachunguza haya mambo na kuyaweka bayana ili wananchi wote wafahamu na Wabunge pamoja na mtoa hoja aridhike ya kwamba kweli hayo mambo yamechunguzwa, sababu tumeunda Tume nyingi tu hapa, na suala la select committees hizi Tume teule ni la kawaida katika Bunge lolote la common wealth, na tumeunda Tume hata za kumchunguza Mheshimwa Chacha Zakayo Wangwe kama amesema ukweli zimetumia fedha zikakaa huko Mara na zikagundua ya kwamba amesema ukweli. Tumeunda Tume hapa hata za kumchunguza Mheshimiwa Malima hizi Tume zinaundwa ni jambo la kawaida, kwanini hapa Wabunge Waheshimiwa kweli muone uzito sana na muone shida sana kwamba hii Tume itaundwa. (Makofi)

Kwanza kabisa...

SPIKA: Mheshimiwa Chacha Wangwe unachanganya mambo bure, kanuni ya 104 inaunda Kamati teule, hata neno Tume sijui mnalipata wapi hayo yote mengine unayoyataja Spika alikuwa anateua Wabunge wachache kwenye Kamati kuweza kumshauri juu ya ukweli wa jambo ni tofauti kabisa na Kamati teule chini ya Kanuni ya 104. Ningeomba Waheshimiwa Wabunge tunavyokwenda tunayo hoja ya Mheshimiwa Zitto, tunayo majibu ya Mheshimiwa Waziri yanasambazwa kwenu hivi sasa. Hivi kuna ugumu gani kwenda kwenye hoja mbona mnazungumza mambo, mnajaribu Baba wa Taifa muende wapi, twende kwenye hoja tujaribi kuzijibu ili tuzifafanue.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, asante nashukuru katika yote uniongezee dakika zangu tatu ili nimalizie. Hii ni tatizo la kiswahili mimi ni lugha yangu ya tatu, Tume, Kamati mimi nazungumzia select committee basi tuseme ni Kamati teule ndiyo maana yake na ndiyo tunayoizungumzia hapa Mimi nasema hili si liliagizwa na Rais siku alipozungumza hapa Bungeni akasema ya kwamba mikataba itapitiwa kwa hiyo sio lazima tumsubiri yeye aje kutuambia hapa, ameshatoa order agizo tayari kwamba mikataba ichunguzwe na hapa naona imeandikwa ya kwamba ni Tume teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya mikataba ya madini mazingira.

Kwa hiyo ni wakati umefika sasa ili haya mambo yachunguzwe kwa sababu wanataka kuyajua na sio hayo tu mimi naweza nikakupa mfano hayo, kwamba Waziri Karamagi si yeye wa kwanza kufanya kitu ambacho kinaonekana kiko kinyume hata waliotangulia na wote vilevile wa Wizara hiyo ni lazima wachunguzwe vilevile wengine wanashika nafasi za juu sana sasa hivi ni kwamba hata katika mwaka 1980 Sheria ya Madini inatamka bayana ya kwamba maeneo yaliyo kwa ajili ya wachimba wadogo wadogo na yale yaliyo wachimbaji wakubwa yatakuwa hivyo na wasiingiliane. Lakini tunaona ya kwamba maeneo ya Mara yote yalitengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo kuanzia mwaka 1980 na Mawaziri waliyalinda hadi mwaka 1996 lakini ilipofika tarehe 14 Juni, 2006 alikuja Waziri ambaye aliyageuza yale maeneo na kuwapa wachimbaji wakubwa bila ridhaa ya wananchi na bila vilevile kuzingatia sheria inakataa hilo nalo linahitaji kuchunguzwa ni sehemu ya haya.

Kuna mengi sana ambayo yanahitaji kuchunguzwa katika migodi yote ambayo imepewa makampuni makubwa na pamoja na hii kampuni ya Barick ambayo sasa hivi tunaamini ya kwamba ina ukaribu sana na Serikali na mikataba inaweza ikasainiwa hata Motrio Cananda lakini hiyo mikataba basi iletwe hapa tuione wananchi nao wajiridhishe kwamba kweli hiyo mikataba ilikuwa ni sahihi kuna tatizo gani, kwanini inakuwa hofu kubwa sana halafu Wabunge hapa wanataka kufanya kitu kama ushabiki hii ni kazi ya wananchi tumepewa hapa kesho na kesho kutwa watakuja wengine tunataka iwe on record kwamba hayo mambo ambayo yanasemekena yalikuwa ni kinyume yamekuwa straight.

Kwa hiyo mimi navyoona ni kwamba tusiwe tunatumia Bunge kama sehemu ya ku-justify mambo ambayo si ya kweli, tumeapa kwamba tutailinda Katiba, na ningependa kutumia hii nafasi kusema ya kwamba katika viongozi wetu ambao ni Mawaziri wawe wanasimama kutetea kiapo chetu na wasitake kugeuza hili Bunge kama sehemu yao ya kupinda sheria za Katiba ya nchi. Kwa mfano natoa mfano hai hivi majuzi niliuliza swali kwanini Tarime kwa mfano itawaliwe kinyume cha Katiba na Sheria, akasimama Waziri wa Utawala Bora, akasema kwamba wale watu sio Watanzania kama Watanzania wengine tangu ukoloni bila Katiba, akasimama Waziri Mkuu naye akathibitisha hivyo hivyo kwamba...

SPIKA: Mheshimiwa nenda kwenye hoja tuna hoja ya Mheshimiwa zito vinginevyo nitakuzuia kabisa kusema kwa sababu huelekei kuchangia hoja.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, nilikuwa natoa mfano jinsi Mawaziri wetu wanavyokiuka Katiba hapa Bunge na ingefaa waombe radhi kwa hayo waliyoyatamka kwa ajili ya watu wa Tarime, mimi nasisitiza ya kwamba kwa sababu mimi kitu cha kuogopa mimi sina bwana, nasikia mimi nawakilisha wananchi hapa. Nasema hivi hii Tume yaani hii Kamati teule ya Bunge iundwe ili ukweli uonekane...

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU: Muongozo wa Spika.

SPIKA: Muongozo wa Spika, Kanuni.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU: Kanuni ya 55, naomba muongozo wako Mheshimiwa Spika, kwa sababu mchangiaji wa hoja hii naona sasa hivi anageuza hoja hii kuwa ni kama uwanja wa kuanza kuleta malumbano na hoja ambazo hazina msingi na kutoa matamshi ambayo kwa kweli yanaendana na kupotosha watu kwamba kwanza naomba umtake aeleze na atoe ufafanuzi kwamba ni kwa vipi Mawaziri wanavunja Katiba na wanakwenda tofauti ya Katiba inavyoagiza. (Makofi)

Lakini pili tunamuomba Mheshimiwa Mbunge anavyozidi kuchangia aende kwenye hoja na asianze kutafuta mambo ambayo hayasiki, hapa Bunge hili sio mahali pa kuhalalisha uwongo kama anavyodai kwamba sasa hivi tunageuza uwongo kuwa ukweli sio kweli, ukweli umewekwa wazi na Mheshimiwa Waziri na kama hoja basi hoja itolewe kupinga yale yaliyozungumzwa na Mheshimiwa Waziri katika kujibu hoja za mtoa hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tatizo sio kuuliza swali, kila mtu anafursa ya kuuliza swali na akajibiwa tatizo ni jinsi lilivyoulizwa kwa kuuza kwamba Mheshimiwa Waziri amedanganya, ukianza na shutuma umejibiwa ukweli sasa Bunge linatakiwa hapa kusema kwamba je hiyo shutuma ilikuwa ni ya ukweli? Nashukuru. (Makofi)

SPIKA: Kwanza nikuhakikishie kwamba dakika zako tunazihifadhi, lakini ni wewe mwenyewe unajisababishia matatizo kwa kwenda nje kabisa ya mada na kanuni haziruhusu. Namshukuru sana Waziri wa Nchi anatukumbusha hilo tuhuma ya kusema kuna Mawaziri kadhaa wanavunja Katiba ndani ya Bunge ni nzito sana lakini hazihusiani na mada hii kilicho mbele yetu hapa ni Serikali kutiliana sahihi mkataba wa mgodi wa Buzwagi wala sio sera ya madini kama wengine mnavyoendelea mimi napenda Waheshimiwa turudi kwenye mada yenyewe ili tuweze kujua ukweli uko wapi na uwongo uko wapi iko wapi kabisa. Mheshimiwa Zitto ametoa hizo tuhuma kama 11 Waziri amezijibu kwa mpangilio moja baada ya nyingine, semeni majibu yanatosheleza wapi hayatoshelezi, tutafikia mwisho vizuri tu, kwa hiyo Mheshimiwa Chacha Wangwe kwa maelekezo hayo hebu endelea sasa kwenye mada.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, mimi naheshimu maelekezo yako na ninaamini kabisa ya kwamba unaongoza Bunge letu kwa njia nzuri, mimi nilikuwa najaribu kuelezea kile ambacho kimezungumzwa hata na Wabunge wenzangu hapa ya kwamba Mheshimiwa Waziri kwamba hadanganyi, na hoja iliyopo hapa ni kwamba anadanganya na mimi nikawa natoa mifano hai ambayo nimeishuhudia hapa na Wabunge wakaishuhudia na wananchi jinsi ambavyo Mawaziri wanadanganya hapa Bungeni.

MHE. HAROUB S. MASOUD: Mheshimiwa Spika, kuhusu utaratibu.

SPIKA: Mheshimiwa Masoud.

MHE. HAROUB S. MASOUD: Mheshimiwa Spika, natumia kanuni Na. 50(8)(b) na naisoma kama ilivyo, inasema hivi kutumia haki yake ya kusema kwa madhumuni ya kutaka kuchelewesha shughuli za Bunge. Mhusika amefahamishwa na Mheshimiwa Waziri wa Nchi lakini bado anaendelea na kwa nia hii ina maana anataka kusababisha shughuli za Bunge zisiendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na wewe mwenyewe umemfahamisha vizuri sasa sielewi kama hajui kanuni au anataka kuibeza kanuni hii, naomba kuwasilisha. (Makofi)

SPIKA: Nampa nafasi ya mwisho Mheshimiwa Chacha Wangwe kurudi katika mada yenyewe, tafadhali rudi katika mada iliyo mbele yetu, ukirejea tena kwenye njia zako hizo ambazo hazielewiki itabidi nikusitishe.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kutambua kwamba wewe preciding wa ku-guide debate hapa Bunge. Na hawa wanaojaribu kunishika koo wangeacha nimalize kujenga hoja lakini basi kwa hivyo mimi narudi kwenye hoja maana mimi tunafahamiana hapa. Ni kwamba hoja iko pale pale kwamba ningeomba Waheshimiwa Wabunge ambao tunawakilisha wananchi waruhusu Kamati teule ya Bunge iundwe kwa ajili ya kuchunguza hii mikataba yote na mambo ambayo yamekuwa ni kero kwa wananchi kuhusiana na mambo ya migodi kuanzia mikataba na yale yaliyojitokeza juzi ya kuendelea kusaini mikataba mingine wakati ile aliyoisema Rais haijachunguzwa.

La kwangu ni hilo, lakini pia naomba uendelee kufanya nguvu ili hili Bunge lizindikuwa la kidemokrasia na lisiwe ni Bunge la mashabiki ambao wanakuja hapa kufanya kama kijiwe cha chama chao hapa. Nashukuru sana. (Makofi)"


Pia katika kuchangia hotuba ya waziri mkuu katika kikao cha bunge kinachoendelea kwa sasa hivi Mbunge Chacha Wangwe aliomba utaratibu wa bunge uzingatiwe kidogo wakati Malecela akitoa hoja yake. Mbunge Wangwe alifanya kitu kizuru kumstopisha bwana Malecela ila hakuwa na la maana la kusema baada ya naibu spika kumpa nafasi auongee, kwa mantiki hii Wangwe ananiacha na maswali mengi kichani zaidi ya majibu kama kweli anaisaidia kambi ya upinzani au kuinangusha, na sina uhakika kama kwa haya anasaidia wananchi pia. maelezo haya ni nukuu ya sehemu ya mazungumzo ya Mheshimiwa Malecela na Mbunge Wangwe alivyoitisha utaratibu wa katiba:

"Halafu jambo la pili nitoe mfano tu juzi hapa nyinyi wenyewe mliona Chama cha Mapinduzi, Mheshimiwa Mbunge wa Same Mashariki amesema kwa nguvu zake zote tunaye Mheshimiwa Mpendazoe Fred Mpendazoe Tungu, Mbunge wa Kishapu amesema kwa nguvu. Kwa hiyo ninataka niwahakikishie hata mimi ninarudia tena, hela za EPA zitarudi, lakini nataka nisem Mheshimi Naibu Spika, ndiye aliyeyaona maovi haya na yeye ndiye aliyeunda hiyo tume ambayo tunasomewa hapa vipande na akaahidi kwamba itakapokuwa tayari ataileta kwenye Bunge hili tuje tuizungumze kihakika.

Sasa mimi nashangaa kwamba kitu ambacho Rais alikiunda na tunamshukuru sana na tunampongeza kwamba alichukua hatua ya Chama cha Mapinduzi kupambana na ufisadi na akasema kwamba hela zote lazima zirudishwe chini ya EPA na ripoti italetwa Bungeni tutaizungumza, sasa wenzetu kama wanataka wangoje naona wanafanya haraka mno



.................................. KUHUSU UTARATIBU MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utaratibu.

NAIBU SPIKA: Kuhusu utaratibu, naomba nataka kusikiliza kuhusu utaratibu.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, Kanuni ya 68.

NAIBU SPIKA: Soma, naomba uisome Kanuni.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Kama huna kanuni wewe shauri yako. (Kicheko/Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kujua kama ni utaratibu kuzungumzia ................................... (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tafadhali soma.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nitaisoma wengine hapa hawasomi, Kanuni ya 68 inasema, Mbunge anaweza kusimama wakati wowote na kusema maneno kuhusu utaratibu ambapo Mbunge yeyote ambaye wakati huo atakuwa anasema atanyamaza na kukaa chini, na Spika atamtaka Mbunge aliyedai utaratibu ataje Kanuni au sehemu ya Kanuni iliyokiuka. (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Sasa ndiyo hiyo taja sasa. (Makofi)

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Kanuni ambayo imekiukwa ni Kanuni ya 68 (7) inasema, hali kadhalika Mbunge anaweza kusimama wakati wowote ambapo hakuna Mbunge mwingine anayesema. (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge naomba usipoteze muda, Mheshimiwa Mbunge .............................. (Kicheko/Makofi)

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, ngoja ............................... (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa kaa chini. (Kicheko/Makofi)

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, naomba unilinde nimalize. Kama ni sahihi kuzungumzia mwenendo wa Rais ………………… (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge nimesimama naomba ukae chini. Mheshimiwa Chacha Wangwe Spika akisimama unatakiwa Mbunge ukae chini na Kuhusu Utaratibu ni vizuri ukajiandaa halafu unaenda kwenye ……..……..……, tumeshapoteza dakika tano, kwa hiyo naomba aliyekuwa anazungumza aendelee. (Makofi)

MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na ninapenda niendelee. Kama nilivyokuwa nikisema CCM kamwe haitalinda ufisadi na tutapambana na ufisadi kwa nguvu zetu zote na mimi nina hakika sisi wote tutamuunga mkono kama Rais wetu alivyosema kwamba hela za EPA zirudi na zitarudi na zisiporudi ni kweli kwamba tutakuwa na haki ya kuuliza kwa nini hazikurudi. Lakini mimi nina imani na Rais wetu na kwamba akishasema yale aliyosema nina hakika yatatekelezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwamba viti vya Bunge letu vimesimikwa kwa bolt, otherwise kwa hali ya namna hii kusimama tu mtu hata hana pointi na wala hajui ile order ni namba ngapi, katika Mabunge mengine watu huinua viti halafu kuanza kutupiana. (Kicheko/Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, ………………….

KUHUSU UTARATIBU MHE. CHACHA Z. WANGWE: Kuhusu utaratibu.

NAIBU SPIKA: Kuhusu utaratibu, kifungu namba gani?

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu namba 64 katika e inasema, hatazungumzia mwenendo wa Rais, Spika, Mbunge, Jaji, Hakimu au mtu mwingine yeyote anayeshughulikia utoaji wa haki isipokuwa tu kama kumtolea hoja mahususi kuhusu jambo fulani. Sasa msemaji alikuwa anamzungumzia Rais na mwenendo wake kuhusiana na suala la EPA. Je, hajavunja hiyo? (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge naomba mnisikilize, nadhani tunayo kazi kubwa ya kuweza kusoma kanuni. (Makofi) Kwa hiyo swali la kumzungumzia Rais, anasema Rais ameahidi kwamba anameunda tume ambayo ina miezi sita na alichosema msemaji mimi nimesikia kwamba atakapotoa Rais kama hatujaridhika ndio tutauliza, sasa hapa hajamsema Rais, naomba tuendelee mzee. (Makofi)

MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, nina matumaini yangu kwamba muda nitaongezwa.

NAIBU SPIKA: Unaongezwa.

MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, lakini huyo ni Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA sishangai, ninaendelea. (Kicheko/Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ningependa kwenda kwenye suala la Serikali la Mitaa, ..................................

KUHUSU UTARATIBU MHE. CHACHA Z. WANGWE: Kuhusu utaratibu. (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge naona sasa tunaanza kutumia nyumba vibaya, tunaanza kutumia nyumba vibaya kwa sababu hakuna alichokisema Mzee Malecela toka wakati ule.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kipo hapa.

NAIBU SPIKA: Wewe siyo Makamu Mwenyekiti.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, maana unamlinda sana, usimlinde zaidi ya mahitaji. (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Haya tunaendelea, mzee Malecela unaendelea, kwa sababu sasa tunafanya utani ndani ya Bunge hili, naomba tuendelee naona sasa tunafanya utani. (Makofi/Kicheko)

MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaendelea kama nilivyokuwa nasema sasa nataka nije kwenye suala la Serikali za Mitaa. Watanzania na Waheshimiwa Wabunge wenzangu mtakumbuka kwamba tangu mwaka 1974 tulishughulika sana kuunda vijiji na haja yetu ilikuwa kwamba kuwaleta wananchi wetu pamoja ili tuweze kuwapa maendelea, sasa mimi kwanza pendekezo langu la kwanza ningependa nimuombe Waziri Mkuu kwamba aunde katume ka watendaji siyo ka Wabunge hapana, ka watendaji waende wakaangalie hivi vile vijiji tulivyoviunda tukaambiwa viwe na Serikali na Serikali za vijiji zipo lakini je, zinaendesha mambo kama inavyotakiwa?"
 
Last edited:
Hadi hapo sheria itakapopitishwa ya wagombea binafsi then kwa sasa hivi bado inabidi mtu uwe kwenye chama. Ubaya ni kwamba hivi vyama vinaweza vikawa havisimamii maslahi ya mtu yeyote hasa mwananchi.
 
Wenye maslahi ya chama chochote kwasasa ni wa kuogopwa kama UKOMA!

Sasa wataogopwa wangapi kwa sababu hakuna hata mmoja asiyejali maslahi ya chama chake.ni sawa na wasafiri wa ngalawa, wakati wote usalama wa ngalawa hiyo ndio usalama wao.
 
Naandika leo baada ya kukaa zaidi ya miezi sita na ushee hivi.

Huu ni wakati muafaka wa kuhakikisha kuwa watanzania wanapata matumaini kwani CCM wanapoteza muelekeo huku CHADEMA wakiwa na makamu mwenyekiti ambaye anakidhalilisha chama na hata kufikia mahali kuwa wananchi tunapoteza imani na chama hicho .

CHADEMA wanatakiwa kuhakikisha kuwa ,wanamfukuza umakamu aende akajifunze kwanza kwani anaonekana kutokujua hata kanuni za Bunge,na hili linawapa faida CCM bungeni kuwa kama huyu ndio makamu mwenyekiti basi chama hicho hakiwezi kupewa fursa ya kutawala.

Naona kuwa kama wakiendelea naye wanapaswa kuhakikisha kuwa wanamfanya akae kimya ama awekewe Break kama Makamba alivyowekewa break kwenye chama chake ila break ya huyu iwe ni ndani ya Bunge kwani huko ndio anavuruga sana na kuharibu sana .

Huu ni wito tuu kwa CHADEMA kwani hata mimi nimepoteza imani na CCM sasa.

will be back soon....
 
Huu ni wakati muafaka wa kuhakikisha kuwa watanzania wanapata matumaini kwani CCM wanapoteza muelekeo huku CHADEMA wakiwa na makamu mwenyekiti ambaye anakidhalilisha chama na hata kufikia mahali kuwa wananchi tunapoteza imani na chama hicho .
Kwanza CCM haijapoteza Muelekeo il ni serikali ya Awamu ya Nne,Embu tuambie Chacha Wangwe amekidhalilisha vipi CHADEMA?
CHADEMA wanatakiwa kuhakikisha kuwa ,wanamfukuza umakamu aende akajifunze kwanza kwani anaonekana kutokujua hata kanuni za Bunge,na hili linawapa faida CCM bungeni kuwa kama huyu ndio makamu mwenyekiti basi chama hicho hakiwezi kupewa fursa ya kutawala.

Unataka wamfukuze akijifunze nini na wapi?Kujua kanuni za Buneg siyo kigezo cha wewe kuwa kiongozi Bora.

Najua unatumwa na moyo wako kusema haya ambyo siyo ya kweli.Najua kwanini unasmea haya,Mpaka Kieleweke naomba umwambie..
 
naandika Leo Baada Ya Kukaa Zaidi Ya Miezi Sita Na Ushee Hivi.

Huu Ni Wakati Muafaka Wa Kuhakikisha Kuwa Watanzania Wanapata Matumaini Kwani Ccm Wanapoteza Muelekeo Huku Chadema Wakiwa Na Makamu Mwenyekiti Ambaye Anakidhalilisha Chama Na Hata Kufikia Mahali Kuwa Wananchi Tunapoteza Imani Na Chama Hicho .

Chadema Wanatakiwa Kuhakikisha Kuwa ,wanamfukuza Umakamu Aende Akajifunze Kwanza Kwani Anaonekana Kutokujua Hata Kanuni Za Bunge,na Hili Linawapa Faida Ccm Bungeni Kuwa Kama Huyu Ndio Makamu Mwenyekiti Basi Chama Hicho Hakiwezi Kupewa Fursa Ya Kutawala.

Naona Kuwa Kama Wakiendelea Naye Wanapaswa Kuhakikisha Kuwa Wanamfanya Akae Kimya Ama Awekewe Break Kama Makamba Alivyowekewa Break Kwenye Chama Chake Ila Break Ya Huyu Iwe Ni Ndani Ya Bunge Kwani Huko Ndio Anavuruga Sana Na Kuharibu Sana .

Huu Ni Wito Tuu Kwa Chadema Kwani Hata Mimi Nimepoteza Imani Na Ccm Sasa.

Will Be Back Soon....
Eleza Wapi Chacha Alipo Potoka
 
Eleza Wapi Chacha Alipo Potoka

Huyo Chacha is totally a joke. Alikutana na ubunge kwa bahati mbaya sana wakati mpuuzi mwingine mkubwa zaidi wa CCM alipozidisha wizi, uchawi na uzembe.
Baada ya hapo ubunge jimboni hapo ukawa ni "loose ball". Na wananchi walikuwa wamechoka kiasi ambacho hawakuwa tena wanataka mbunge mwenye sifa bali kiumbe chochote ambacho kingeruhusiwa kikatiba kuwepo badala ya mbunge huyo mwizi wa CCM basi wananchi walikuwa tayari. Kwao ilikuwa ni afadhali shetani usiyemjua kuliko Mbunge huo wa awali wa CCM.
Kuna habari kwamba huyo Chacha hakuwa na mahala pa kuishi (homeles) kabla ya kupata ubunge. Alikuwa muhuni fulani tu. Inasemekana pia ni mwizi (aliwahi kufungwa) na alighushi vyeti vya shule (kihiyo) at one time.
 
Haki sawa, usishangazwe sana na Chacha Wangwe, CHADEMA zima ndivyo ilivyo. Kila kiongozi wa CHADEMA ana sera zake mwenyewe!
 
mwenyekiti wao ni mwanachama wa WAPUKI na wanaoijua wapuki watakueleza nini kilikuwa kinatendeka huko

ndege wa jamii moja huruka pamoja
 
ndege wa jamii moja huruka pamoja


wacha wengine tuimbe....nyimbo zetu za uhamasishaji wakati wa vijiji vya ujamaa na operesheni nguvu kazi....tukipita mitaani na magwanda yetu ya kijani kwa mujibu wa sheria kukamata wazururaji na wazembe ...that a


...gezaulole mama ..gezaulole maama wee..

..biashara ya njugu na korosho baba haitufai eeh

...twendeni kijiji gezaulole mama ,kwenye makao mapya eeh!!

au

..umevunja duka la ushirika bunduki imelia ,shaba yaingia mwilini mwako waona uchunguuu

...mguu umevunja hospitali umelazwa ,pingu zipo mikononi mwako mwanaangu,

umefungwa....

eeh mwana hukusikia tuliyokuambia ,balaa kutuletea nyumbani eeh mwana..

wazee wenzangu pia walikuketisha chini..............
 
Kamati kuu ya CHADEMA iliyokaa jana mjini Dodoma imemsimamisha uongozi makamu mwenyekiti wa chama hicho Bara Mhe.Chacha Wangwe .

Kamati kuu hiyo ilimsimamisha kutokana na kukiuka maadili ya viongozi kwa mujibu wa katiba ya chama hicho .

Naambiwa kuwa muda sio mrefu watatoa taarifa rasmi kwa waandishi wa habari waliopo mjini Dodoma juu ya nini kilipelekea uamuzi huo kufanyika.

more news to come.
 
Matokeo ya Kura za kutokuwa na Imani yalikuwa kama ifuatavyo:
Idadi ya Wapiga kura wote 31
Kura zilizopigwa 31
Kura zilizoharibika 0 0
Kura za Hapana 07
Kura za ndiyo 24

Hizi ndio kura na jinsi zilivyopigwa na kumngoa makamu huyo wa mwenyekiti,hapa wanaonnyesha kukerwa na matendo na kauli zake ama ni kukomaa kwa chama ?
 
Back
Top Bottom