CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Haya sasa si unaona mkorogo huo wewe dogo Mnyika.. Shamsha Mwangunga kwao Kongwa Dodoma mnampa U-kilimanjaro mnachukua marehemu (Mbathia) mnatia kwenye hesabu... mnachukua hata walio jiuzuru ( Migiro ) ili kulazimisha hoja.

Endeleeni tu na M/kiti wenu kilaza....

Unamwonaje nabii wenu JK? Ningekuwa wewe ningenyamaza yaishe kimya kimya! Masatu unaonyesha chuki, huna hoja!
 
Mnyika usiondoke. Sikia kwanza mantiki ya lalamiko langu na hofu yangu. Ni kwamba nakatishwa tamaa kuona kwamba hata ninyi ambao tuliwategemea mtuletee jambo tofauti, zuri zaidi, mnaingia kwenye mtego huohuo. Mngeweza tu kujibu hizo tuhuma vizuri tu bila kulazimika kuanza kuorodhesha majina ya watu na makabila yao kwenye CCM. Hii orodha mnayotoa inajenga hisia kwamba wote ninyi, CCM na CHADEMA mna tatizo la uchaga, data mnazotoa ni ushahidi wa kufikisha watu kwenye consensus kama hiyo. Matokeo yake hao mnaoita wachaga watasakamwa huko CCM na kwenye CHADEMA na kwingineko, na itakuwa hatari. Wakiwamaliza hao, manazi watachagua kabila lingine, na baadhi yetu tayari tunajisikia vulnerable, ndio maana tuna hofu. Naomba tu ukubali kwamba haikuwa sahihi kwa mwenyekiti wako kujibu hoja hiyo kwa kuorodhesha wachaga wa CCM, kwani kufanya hivyo ni sawa na kumtusi aliyekutusi, kurekebisha kosa kwa kutumia kosa, ambayo kimantiki inafanya kosa liwe kubwa zaidi, na anayeonekana zaidi ni yule mkosaji wa mwisho. Ni hivyo tu ndugu Mnyika.

Kithuku

Naeleweka mantiki ya hisia zako. Pole sana kama umeumizwa na huu mjadala. Na najua kuna watu wataumia zaidi. Na naamini kabisa Kikwete atavyofanya mabadiliko ya baraza la mawaziri hivi karibuni, mjadala tunaoufanya hivi sasa utakuwa ni moja ya mambo ambayo yatamgusa. Hatupaswi kufika mahali ambapo tukalipeleka taifa letu katika mazingira ambayo baadhi ya watanzania wenzetu watajilaumu kwa kuwa wachaga! Hili lazima tuliepuke. Bahati mbaya wewe kithuku pamoja na watanzania wengi hamkuamka kukumea hisia hizo wakati CCM ilipokuwa ikitangaza kwamba CHADEMA ni chama cha wachaga. Unadhani wachaga walioko CHADEMA ama wanaotaka kushika nafasi za uongozi kupitia CHADEMA wanajisikiaje katika mazingira hayo? Let the golden rule apply and not the law of the jungle.

CHADEMA tumejitahidi kutumia busara zote kuepuka kuwataja watu majina, na tuliwaonya CCM kuwa wasitufikishe mahali tukaanza kutaja, kumbuka tamko hili ambalo tuliotoa mwaka jana:
Utangulizi:

Mwishoni mwaka 2006 na mwanzoni mwaka huu shutuma kadhaa zimeelekezwa kwa CHADEMA na viongozi wake hususani Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe. Mwanzoni shutuma hizi zimekuwa zikitolewa na wanasiasa wanaojitoa kambi ya upinzani na kujiunga na CCM. Shutuma hizi ni pamoja na:
1. Kuwa CHADEMA awali kilianzishwa wakati wa ukoloni kikijulikana kama Chagga Development Manifesto (CHADEMA) ambacho bado kinaendelea na mwelekeo huo(Rejea Majira: 24/12/2006.;
2. CHADEMA ina mrundikano wa watu wa kabila la wachagga. Haipaswi kuwa ‘chama cha demokrasia na maendeleo’ badala yake inapaswa kuitwa “chagga development manifesto” Rejea Mwananchi: 24/12/2006.(Hoja hii ilirudiwa katika vyombo mbalimbali vya habari kwa wiki kadhaa mfululizo wakinukuliwa viongozi wachache waliojitoa kutoka upinzani).

Awali CHADEMA tulipuuza uzushi huu. Lakini kutokana na kauli hizi kurudiwa rudiwa mara kwa mara tunaamini kuwa uwongo na upotoshaji huu unaweza kugeuzwa na umma watanzania ukaaminishwa kuwa ndio ukweli. Aidha tunatoa taarifa hii kufuatia taarifa ya Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Aggrey Mwanri iliyochapwa katika vyombo mbalimbali vya habari 5 Januari 2007 ambapo CCM imetoa shutuma kadhaa kwa CHADEMA na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe. Pia taarifa hii imenatolewa kujibu shutuma kadhaa zilizoelekezwa kwa Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kupitia maoni ya Mhariri wa gazeti la Mtanzania la tarehe 5 Januari 2007 yaliyokuwa na kichwa cha habari “Wapinzani tafuteni njia bora za kukubalika”.

SI KWELI KUWA CHADEMA NI CHAMA CHA WACHAGA KILICHOANZISHWA TOKA WAKATI WA KUDAI UHURU

Mtanzania yeyote mwenye ufahamu wa kawaida kabisa wa historia ya nchi yetu, atakubaliana nasi kuwa katika orodha ya vyama vya siasa vilivyokuwepo kabla ya uhuru, hakuna chama kilichoitwa CHADEMA. Ukweli ni kuwa CHADEMA ni chama kilichoanzishwa na kusajiliwa mara baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi. Hii inatufanya tubaki na maswali mengi kuhusu nia ya wanaosambaza uzushi huu.

SI KWELI KWAMBA CHADEMA IMEJAA WACHAGA

Kwa akili za kawaida, shutuma kwamba CHADEMA imejaa wachaga maana yake ni kwamba CHADEMA ina viongozi na wanachama wengi wachagga kuliko kabila lolote hapa Tanzania. Je ni kwa kiasi gani kauli hiyo ina ukweli?.

Katika safu ya juu ya uongozi wa kitaifa wa CHADEMA yenye viongozi sita: wenyeviti na makatibu mchaga ni mmoja tu-Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe. Viongozi wengine wanatoka makabila mengine kama MuIraq, Myao, Mpemba na MuUnguja.

Aidha katika sekretariati ya chama taifa ambacho ndio chombo kinachosimamia utekelezaji wa kila siku wa shughuli za chama kikiwa na kurugenzi 9, kati ya wakurugenzi wake mchaga ni mmoja tu. Na wasukuma ni watatu. Kwa nini hawasemi kwamba CHADEMA ni chama cha wasukuma?

Kadhalika mpaka sasa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameteua wajumbe wanne wa kamati kuu, kati yao hakuna na mchaga hata mmoja na kati yao wawili ni wahaya, Profesa Mwesiga Baregu na Balozi Ngaiza. Kwa nini hawakusema kwamba CHADEMA ni chama cha wahaya?

Kwa upande mwingine kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi uliopita, jimbo ambalo CHADEMA iliongoza kwa uwingi mkubwa zaidi wa kura ni Tarime ikiwa asilimia zaidi ya 64. Kama CHADEMA ni chama cha wachaga kwa nini jimbo la kwanza lisingekuwa la mkoa wa Kilimanjaro?
Kati ya majimbo kumi ambayo CHADEMA ilifanya vizuri zaidi, jimbo la Kilimanjaro ni moja tu la Moshi mjini huku mikoa kama Kigoma, Rukwa ikiwa na majimbo mawili ambayo CHADEMA imefanya vizuri zaidi. Kama CHADEMA ingekuwa chama cha wachaga si ingefanya vizuri zaidi katika majimbo ya Kilimanjaro?
Je, wanataka kutuambia kuwa Mara, Kigoma, Rukwa na mikoa mingine ambayo CHADEMA imefanya vizuri kote kumejaa wachaga?

Kwa mantiki hiyo basi, si kweli kwamba CHADEMA ni chama kilichojaa wachaga. CHADEMA ni chama cha kitaifa. Kinachojumuisha wanachama na wapenzi wa asili na hali mbalimbali. Lakini swali la kujiuliza ni je wachaga hawana haki ya kuwa sehemu ya viongozi katika taifa na wanachama wa CHADEMA?

Zaidi ya hayo tunawashangaa wakitoa hoja kwamba CHADEMA imejaa wachaga. Lakini tunawashangaa zaidi kwa kuwa hatukuwasikia akisema chochote pale Rais Kikwete alipoteua wachaga na watanzania wenye asili ya Kilimanjaro wengi zaidi katika baraza la mawaziri kuliko makabila mengine. Je, kwa mantiki ya wazushi kama hao serikali ya Kikwete ni ya wachaga? Je, kwa kuwa wachaga ndio kabila lenye wabunge wengi zaidi kati ya wabunge wa viti maalumu wa CCM na CHADEMA, Je kwa kigezo hiki tu tuseme kwamba CCM na CHADEMA ni vyama vya wachaga? Je, kwa CCM kuwa na wabunge wa viti maalum wachaga hata katika mikoa mingine ya nchi yetu zaidi ya Kilimanjaro wanapotoka wachaga je, kwa uchambuzi wa wazushi kama hao wanaweza kusema kwamba CCM ni chama cha wachaga?

Hatukupenda kujadili viongozi kwa kutazama makabila yao. Lakini tumeamua kutoa uchambuzi huu kwa sababu suala la ukabila ni nyeti sana kwa mustakabali wa nchi yetu na kwamba kwa kutoa mifano hai tutathibitisha wazi uzushi wa watu hawa. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuasa kwamba kufanya dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha.

Sisi tunaamini kauli za wazushi kama hawa zinapandikiza mbegu ya ubaguzi miongoni mwa watanzania na kuwashawishi watu kutazamana kwa misingi ya makabila yao. Tukiwaruhusu watu kama hawa tutaweka mashakani mshikamano na amani yetu hapa nchini. Tunatoa mwito kwa watanzania kupuuza na kukumea kauli za viongozi kama hawa. CCM inaendelea kukumbatia wazushi hawa na uzushi wao, watanzania watakuwa na kosa gani wakianza kuamini kwamba chama tawala kinapandikiza mbegu za ubaguzi? Na kwa upande mwingine, tunatoa rai kwa vyombo vya habari kuchambua kwa kina kauli za watu kama hawa kwani uwongo ukisemwa sana wananchi wanaweza kuaminishwa kwamba ni ukweli.

Katika taarifa yake CCM imeinukuu shutuma ya wanaotoka upinzani ya kulalamikia tabia za ubabe na udini ndani ya CHADEMA? Ni ubabe upi huo? Ni udini upi huo ulioko katika CHADEMA? Hivi katika vyama vikuu vya siasa hapa nchini kuna chama ambacho safu yake ya kitaifa ina uwiano wa kidini kama CHADEMA? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema pia kwamba katika kutafuta uongozi kuna watu wanaweza kutumia vigezo vya kijinga kama udini na ukabila kujihalalisha ili kufikia malengo yao na ndivyo wanavyofanya watu jamii hii.

Tamko linaendelea hapa:http://www.chadema.net/tamko/2007/mwanri.php

CCM hawakusikia kabisa, kwa mjadala huu wa sasa naamini kabisa, hata CCM wakirudia tena kuanza kutaja kwa majina wachaga wachache walioko CHADEMA na kuita CHADEMA ni chama cha wachaga utakuwa wa kwanza kuwakemea.

CCM wamesema CHADEMA ni chama cha wachaga mpaka baadhi ya wananchi wakaanza kuamini. Njia pekee ni kuufanya umma kuamini kwamba wachaga kama watanzania wengine wowote wapo kila mahali ikiwemo CCM na wana haki hiyo kabisa. And that is the spirit of Mbowe's statement- inawezekana habari husika haijabeba sura hiyo kwa ukamilifu wake kwa kuwa kuna mengi aliyoyasema yameachwa lakini natumai ujumbe umefika.

Unaniruhusu niondoke?

JJ
 
Waliojibu swali la mwandishi walimsoma aliayeuliza, na wanajua siri ya propaganda za CCM. Kufanya propaganda dhidi ya propaganda ni mchezo safi kisiasa,. Inawaudhi mashabiki kwa sababu udhaifu wenu umezungumzwa mahali ambapo mlitaka wa adui yenu ndio usemwe. CHADEMA hawawezi kuacha fursa kama hii, kwa kuogopa criticism ya watu wale wale walioshibishwa propaganda za CCM, eti kwa wao kutafuta kujibu kistaarabu! Kwa faida ya CCM? No, hapa wamepatia. Auaye kwa panga atakufa kwa panga! Hicho ndicho kinachowapata CCM sasa. Meza wembe!
 
wahaya bada ya miaka mingi ya kusemwa vibaya kuhusu ukabila na kuchukiwa wazi wazi wao ni watu arrogant sana na wakabila na kuna wakati watu waliamini muhaya hawezi kuwa raisi na Nyerere na awamu nyingine ziliwadhibiti wahaya...sasa baada ya miaka mingi naona wahaya wamekuwa very smart na kuachana na maneno maneno hayo na kuamua kuufanya mkoa wao best katika elimu maana ndio maendeleo ya kweli yananzia hapo,sasa ndugu wananchi watch out huo mkoa baada ya miaka kadhaa utakuwa umeendelea sana halafu muendelee kusema ukabila,mwaka huu wamekuwa wa kwanza Tanzania nzima matokeo ya shule za msingi na hata Dar hawakufua dafu na wamechanga mabilioni na misaada kibao inamwagika huko kagera kuendeleza Elimu na shule zinafunguliwa na wananchi wanaajiri walimu bila kusubiri serikali...sasa baadaye wakija kushika kila kitu muwaite wakabila maana mmekalia kupiga miluzi tuu huku wao wakifanya kweli,mnalalamika faculty imejaa wahaya sasa subirini mje kulalamika vyuo vikuu vyote wanafunzi ni wahaya
 
Kithuku

Naeleweka mantiki ya hisia zako. Pole sana kama umeumizwa na huu mjadala. Na najua kuna watu wataumia zaidi. Na naamini kabisa Kikwete atavyofanya mabadiliko ya baraza la mawaziri hivi karibuni, mjadala tunaoufanya hivi sasa utakuwa ni moja ya mambo ambayo yatamgusa. Hatupaswi kufika mahali ambapo tukalipeleka taifa letu katika mazingira ambayo baadhi ya watanzania wenzetu watajilaumu kwa kuwa wachaga! Hili lazima tuliepuke. Bahati mbaya wewe kithuku pamoja na watanzania wengi hamkuamka kukumea hisia hizo wakati CCM ilipokuwa ikitangaza kwamba CHADEMA ni chama cha wachaga. Unadhani wachaga walioko CHADEMA ama wanaotaka kushika nafasi za uongozi kupitia CHADEMA wanajisikiaje katika mazingira hayo? Let the golden rule apply and not the law of the jungle.

CHADEMA tumejitahidi kutumia busara zote kuepuka kuwataja watu majina, na tuliwaonya CCM kuwa wasitufikishe mahali tukaanza kutaja, kumbuka tamko hili ambalo tuliotoa mwaka jana:
Utangulizi:

Mwishoni mwaka 2006 na mwanzoni mwaka huu shutuma kadhaa zimeelekezwa kwa CHADEMA na viongozi wake hususani Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe. Mwanzoni shutuma hizi zimekuwa zikitolewa na wanasiasa wanaojitoa kambi ya upinzani na kujiunga na CCM. Shutuma hizi ni pamoja na:
1. Kuwa CHADEMA awali kilianzishwa wakati wa ukoloni kikijulikana kama Chagga Development Manifesto (CHADEMA) ambacho bado kinaendelea na mwelekeo huo(Rejea Majira: 24/12/2006.;
2. CHADEMA ina mrundikano wa watu wa kabila la wachagga. Haipaswi kuwa ‘chama cha demokrasia na maendeleo’ badala yake inapaswa kuitwa “chagga development manifesto” Rejea Mwananchi: 24/12/2006.(Hoja hii ilirudiwa katika vyombo mbalimbali vya habari kwa wiki kadhaa mfululizo wakinukuliwa viongozi wachache waliojitoa kutoka upinzani).

Awali CHADEMA tulipuuza uzushi huu. Lakini kutokana na kauli hizi kurudiwa rudiwa mara kwa mara tunaamini kuwa uwongo na upotoshaji huu unaweza kugeuzwa na umma watanzania ukaaminishwa kuwa ndio ukweli. Aidha tunatoa taarifa hii kufuatia taarifa ya Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Aggrey Mwanri iliyochapwa katika vyombo mbalimbali vya habari 5 Januari 2007 ambapo CCM imetoa shutuma kadhaa kwa CHADEMA na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe. Pia taarifa hii imenatolewa kujibu shutuma kadhaa zilizoelekezwa kwa Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kupitia maoni ya Mhariri wa gazeti la Mtanzania la tarehe 5 Januari 2007 yaliyokuwa na kichwa cha habari “Wapinzani tafuteni njia bora za kukubalika”.

SI KWELI KUWA CHADEMA NI CHAMA CHA WACHAGA KILICHOANZISHWA TOKA WAKATI WA KUDAI UHURU

Mtanzania yeyote mwenye ufahamu wa kawaida kabisa wa historia ya nchi yetu, atakubaliana nasi kuwa katika orodha ya vyama vya siasa vilivyokuwepo kabla ya uhuru, hakuna chama kilichoitwa CHADEMA. Ukweli ni kuwa CHADEMA ni chama kilichoanzishwa na kusajiliwa mara baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi. Hii inatufanya tubaki na maswali mengi kuhusu nia ya wanaosambaza uzushi huu.

SI KWELI KWAMBA CHADEMA IMEJAA WACHAGA

Kwa akili za kawaida, shutuma kwamba CHADEMA imejaa wachaga maana yake ni kwamba CHADEMA ina viongozi na wanachama wengi wachagga kuliko kabila lolote hapa Tanzania. Je ni kwa kiasi gani kauli hiyo ina ukweli?.

Katika safu ya juu ya uongozi wa kitaifa wa CHADEMA yenye viongozi sita: wenyeviti na makatibu mchaga ni mmoja tu-Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe. Viongozi wengine wanatoka makabila mengine kama MuIraq, Myao, Mpemba na MuUnguja.

Aidha katika sekretariati ya chama taifa ambacho ndio chombo kinachosimamia utekelezaji wa kila siku wa shughuli za chama kikiwa na kurugenzi 9, kati ya wakurugenzi wake mchaga ni mmoja tu. Na wasukuma ni watatu. Kwa nini hawasemi kwamba CHADEMA ni chama cha wasukuma?

Kadhalika mpaka sasa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameteua wajumbe wanne wa kamati kuu, kati yao hakuna na mchaga hata mmoja na kati yao wawili ni wahaya, Profesa Mwesiga Baregu na Balozi Ngaiza. Kwa nini hawakusema kwamba CHADEMA ni chama cha wahaya?

Kwa upande mwingine kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi uliopita, jimbo ambalo CHADEMA iliongoza kwa uwingi mkubwa zaidi wa kura ni Tarime ikiwa asilimia zaidi ya 64. Kama CHADEMA ni chama cha wachaga kwa nini jimbo la kwanza lisingekuwa la mkoa wa Kilimanjaro?
Kati ya majimbo kumi ambayo CHADEMA ilifanya vizuri zaidi, jimbo la Kilimanjaro ni moja tu la Moshi mjini huku mikoa kama Kigoma, Rukwa ikiwa na majimbo mawili ambayo CHADEMA imefanya vizuri zaidi. Kama CHADEMA ingekuwa chama cha wachaga si ingefanya vizuri zaidi katika majimbo ya Kilimanjaro?
Je, wanataka kutuambia kuwa Mara, Kigoma, Rukwa na mikoa mingine ambayo CHADEMA imefanya vizuri kote kumejaa wachaga?

Kwa mantiki hiyo basi, si kweli kwamba CHADEMA ni chama kilichojaa wachaga. CHADEMA ni chama cha kitaifa. Kinachojumuisha wanachama na wapenzi wa asili na hali mbalimbali. Lakini swali la kujiuliza ni je wachaga hawana haki ya kuwa sehemu ya viongozi katika taifa na wanachama wa CHADEMA?

Zaidi ya hayo tunawashangaa wakitoa hoja kwamba CHADEMA imejaa wachaga. Lakini tunawashangaa zaidi kwa kuwa hatukuwasikia akisema chochote pale Rais Kikwete alipoteua wachaga na watanzania wenye asili ya Kilimanjaro wengi zaidi katika baraza la mawaziri kuliko makabila mengine. Je, kwa mantiki ya wazushi kama hao serikali ya Kikwete ni ya wachaga? Je, kwa kuwa wachaga ndio kabila lenye wabunge wengi zaidi kati ya wabunge wa viti maalumu wa CCM na CHADEMA, Je kwa kigezo hiki tu tuseme kwamba CCM na CHADEMA ni vyama vya wachaga? Je, kwa CCM kuwa na wabunge wa viti maalum wachaga hata katika mikoa mingine ya nchi yetu zaidi ya Kilimanjaro wanapotoka wachaga je, kwa uchambuzi wa wazushi kama hao wanaweza kusema kwamba CCM ni chama cha wachaga?

Hatukupenda kujadili viongozi kwa kutazama makabila yao. Lakini tumeamua kutoa uchambuzi huu kwa sababu suala la ukabila ni nyeti sana kwa mustakabali wa nchi yetu na kwamba kwa kutoa mifano hai tutathibitisha wazi uzushi wa watu hawa. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuasa kwamba kufanya dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha.

Sisi tunaamini kauli za wazushi kama hawa zinapandikiza mbegu ya ubaguzi miongoni mwa watanzania na kuwashawishi watu kutazamana kwa misingi ya makabila yao. Tukiwaruhusu watu kama hawa tutaweka mashakani mshikamano na amani yetu hapa nchini. Tunatoa mwito kwa watanzania kupuuza na kukumea kauli za viongozi kama hawa. CCM inaendelea kukumbatia wazushi hawa na uzushi wao, watanzania watakuwa na kosa gani wakianza kuamini kwamba chama tawala kinapandikiza mbegu za ubaguzi? Na kwa upande mwingine, tunatoa rai kwa vyombo vya habari kuchambua kwa kina kauli za watu kama hawa kwani uwongo ukisemwa sana wananchi wanaweza kuaminishwa kwamba ni ukweli.

Katika taarifa yake CCM imeinukuu shutuma ya wanaotoka upinzani ya kulalamikia tabia za ubabe na udini ndani ya CHADEMA? Ni ubabe upi huo? Ni udini upi huo ulioko katika CHADEMA? Hivi katika vyama vikuu vya siasa hapa nchini kuna chama ambacho safu yake ya kitaifa ina uwiano wa kidini kama CHADEMA? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema pia kwamba katika kutafuta uongozi kuna watu wanaweza kutumia vigezo vya kijinga kama udini na ukabila kujihalalisha ili kufikia malengo yao na ndivyo wanavyofanya watu jamii hii.

Tamko linaendelea hapa:http://www.chadema.net/tamko/2007/mwanri.php

CCM hawakusikia kabisa, kwa mjadala huu wa sasa naamini kabisa, hata CCM wakirudia tena kuanza kutaja kwa majina wachaga wachache walioko CHADEMA na kuita CHADEMA ni chama cha wachaga utakuwa wa kwanza kuwakemea.

CCM wamesema CHADEMA ni chama cha wachaga mpaka baadhi ya wananchi wakaanza kuamini. Njia pekee ni kuufanya umma kuamini kwamba wachaga kama watanzania wengine wowote wapo kila mahali ikiwemo CCM na wana haki hiyo kabisa. And that is the spirit of Mbowe's statement- inawezekana habari husika haijabeba sura hiyo kwa ukamilifu wake kwa kuwa kuna mengi aliyoyasema yameachwa lakini natumai ujumbe umefika.

Unaniruhusu niondoke?

JJ

duh mkuu kama ccm iliwasha moto kuhusu wachagga, naona nyie mmeamua kutia petroli sasa moto unarindima.

alaa kumbe hivi ndivyo wachagga wanavyoitawala tanzania? yaani wanahahkikisha kokote kule watanzanias wengi hawana mamlaka!!
 
Mnyika bado niko na wewe na hiyo CHADEMA.
Haya ndiyo niliyokuwa nayahofia. Na wako wengi watakaoelewa kama huyu Mtu wa Pwani. Unadhani hatima ya hawa wachaga itakuwa nini? Na nini kitafuata kwa sisi wengine? Hebu rekebisheni haraka maana mmeharibu kabisa! Maana inavyoonekana hapa, ninyi CHADEMA badala ya kupambana na CCM mmeamua kupambana na wachaga. Siku nyingine mkituhumiwa chama chenu kina watu wa umri fulani kwa wingi, au dini fulani, au category yoyote ya watu mtaanza tena kupambana na watu hao badala ya kujibu hoja! Ukweli ni kwamba mnawasababishia wananchi hao matatizo zaidi! Kwa nini unashindwa kuona mnapokosea, unanishangaza kabisa!
 
Kithuku,

Ukisoma hoja zangu zote katika thread zote mbili utagundua kwamba CHADEMA hatupambani na wachaga. Na pamoja na maneno yote ya CCM bado tunawatazama wachaga kama makabila mengine. Kuwa mchaga hakumuondolea fursa katika CHADEMA. Tunachotazama ni vigezo tu vingine vinavyohitajika. CHADEMA hatuvumilii ubaguzi wa aina yoyote.

Naona ni vyema tukakubaliana kutokukukubaliana. Naelewa mantiki ya hoja yako, naelewa vilevile CCM wako katika mtanziko gani hivi sasa, naelewa CHADEMA wana mtazamo gani hivi sasa. Yatosha tu kusema kwamba ujumbe umefika. Ubarikiwe! Tuendelee na mijadala mingine.

JJ

JJ
 
Mnyika,

Kubali kitu kimoja tu!!! Kwamba hapakuwa na ulazima wa kuendeleza hoja ya wachaga mngejibu tuhuma zenu na mngeishia hapo!!! Kwa hili kuna mawili tu na sio zaidi ya hapo!!! Hapa inaonyesha ukomavu bado,,, ndio maana bado siamini kwamba mnastahili kupewa nchi,,, vitu vidogo kama hivi badala ya kuvijibu na kuishia hapo, ninyi mnaweka Petrol!!!

1. Mumeteleza kwa hiyo muombe watanzania (walioko na vyama na wasiokuwa na vyama) msamaha,,,
2. Mumefanya kwa makusudi kwa hiyo nanyi ni manazi kama CCM!!!

Mwisho!!!
Naomba niseme jambo moja pamoja na kwamba mimi simkabila!!! itachukuwa miaka kwa kabila lolote kubwa kutoa Rais wa Jamhuri!!!

NB: Kuna hoja ya Wangwe kuwasema kuhusu ufamilia na Ukabila,,, Je? Chacha Wangwe ni mwanaCCM, au ndio kumtukana mtu mzima kimafumbo!!!
 
SASA NIMEANZA KUELEWA KILIO CHA WAZARAMU KUINGILIWA KWENYE MJI WAO.

HIVI DARA WACHAGGA WAWE WAKUU NA KULE KWAO WAWE WAKUU TENE

HUYU M SHAIRI KANENA.

Mzizima Imezimika

1. Wako wapi walokuwa, kujifanya ndio kwao?
Taratibu wamerowa, kwa kuporwa vyeo vyao,
Kwa majungu kufanyiwa, Ndengereko si kwao,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

2. Fitina haibebeki, kwa mwenyeji wala mgeni,
Muungwana haitaki, hata kama kwa mapeni,
Japo ukitowa laki, ataepata mgeni,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

3. Zama zile za Diwani, Chambuso shika sukani,
Udugu liwika Pwani, pendo hata kwa jirani,
Sasa hiyo tafurani, kushinda wenye medani,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

4. Vile tulivyo zoweya, sasa havikubaliki,
Kwa fitina na umbeya, wanashinda kwa miliki,
Wao wenye roho mbaya, ndio sifa za miliki,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

5. Kinyume na mikoani, wa Pwani haba kushinda!
Huwaita wanyamwani, wa mambo mengi kupinda,
Wala hawawaamini, hata kama wakishinda,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

6. Vipi Pwani kuwe chee, hata kwa mtoka mbali?
Ila bara iwe ngee, kwa wa pwani ni mhali!
Msojuwa mtembee, ipatikane halali,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

7. Uwapi huo usawa, wakuwabwaga wapwani,
Hata kama hivyo sawa, ni vipi hamuyaoni?
Ni vema ikawa sawa, uongozi wa nchini,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

8. Kama ni haki kwa wote, kila mkoa yawepo,
Isiwe Dar kwa wote, na kwengine yasiwepo!
Hili tujadili sote, pia bungeni liwepo,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

9. Kama pole wakupewa, wenyeji Darisalama,
Wala si walipwerewa, ndio walofanywa kima,
Kama kosa ni uzawa, utaifa uwe dhima,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

10. Beti kumi maridadi, mezipanga kwa mpango,
Dhuluma haishadidi, kwa fatani na muwongo,
Malenga mlo stadi, endelezeni kwa usongo,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani
 
Mtu wa Pwani,

Hili shairi ni la kwako au umenakili kwa nani? Tafadhali tutajie jina la mtunzi.

Linanikumbusha "Mashairi ya Saadani" kulikuwa na moja linasema:
"Kwao si kwetu kwa nini, na kwetu kwao kwa nini?" ambapo yeye alikuwa anazungumzia wakoloni.

Lakini Mtu wa Pwani ningependa kukusahihisha kuwa hali iliyoko Tanzania si hivyo. Ni kweli watu wa Pwani wamekaribisha watu wengi kwenye maeneo yao na kuwapa makazi. Lakini SI kweli kwamba watu wa Pwani wanazuiwa kuhamia Tabora, Rukwa, Kagera nk, hakuna anayewazuia wao pia kwenda huko kulima mahindi, mpunga, au kufanya shughuli zozote zinazofanyika huko, hii ni nchi huru. Kwa msingi huo, hili shairi lina mwelekeo wa kibaguzi.
 
SASA NIMEANZA KUELEWA KILIO CHA WAZARAMU KUINGILIWA KWENYE MJI WAO.

HIVI DARA WACHAGGA WAWE WAKUU NA KULE KWAO WAWE WAKUU TENE

HUYU M SHAIRI KANENA.

Mzizima Imezimika

1. Wako wapi walokuwa, kujifanya ndio kwao?
Taratibu wamerowa, kwa kuporwa vyeo vyao,
Kwa majungu kufanyiwa, Ndengereko si kwao,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

2. Fitina haibebeki, kwa mwenyeji wala mgeni,
Muungwana haitaki, hata kama kwa mapeni,
Japo ukitowa laki, ataepata mgeni,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

3. Zama zile za Diwani, Chambuso shika sukani,
Udugu liwika Pwani, pendo hata kwa jirani,
Sasa hiyo tafurani, kushinda wenye medani,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

4. Vile tulivyo zoweya, sasa havikubaliki,
Kwa fitina na umbeya, wanashinda kwa miliki,
Wao wenye roho mbaya, ndio sifa za miliki,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

5. Kinyume na mikoani, wa Pwani haba kushinda!
Huwaita wanyamwani, wa mambo mengi kupinda,
Wala hawawaamini, hata kama wakishinda,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.
6. Vipi Pwani kuwe chee, hata kwa mtoka mbali?
Ila bara iwe ngee, kwa wa pwani ni mhali!
Msojuwa mtembee, ipatikane halali,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

7. Uwapi huo usawa, wakuwabwaga wapwani,
Hata kama hivyo sawa, ni vipi hamuyaoni?
Ni vema ikawa sawa, uongozi wa nchini,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

8. Kama ni haki kwa wote, kila mkoa yawepo,
Isiwe Dar kwa wote, na kwengine yasiwepo!
Hili tujadili sote, pia bungeni liwepo,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.
9. Kama pole wakupewa, wenyeji Darisalama,
Wala si walipwerewa, ndio walofanywa kima,
Kama kosa ni uzawa, utaifa uwe dhima,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani.

10. Beti kumi maridadi, mezipanga kwa mpango,
Dhuluma haishadidi, kwa fatani na muwongo,
Malenga mlo stadi, endelezeni kwa usongo,
Mzizima mezimika, wakuja ndio sukani

HAPA INAONYESHA JINSI GANI MSHAIRI ANAVYOONYESHA MAKABILA MENGI YALIVYOANDAMA MIKOA YA PWANI HASA KABILA LILOTAJWA LKN MTU WA PWANI HUSIKII KUWA MBUNGE KILIMANJARO.

BETI YA TANO NDIO INAONYESHA JINSI GANI MTU WA PWANI AKIWA KTK MIKOA HIYO HUWA AU HUFANYWA

SHAIRI HILI NIMELICHUKUA KWENYE GAZETI LA MTANZANIA
 
Ninachosema ni kwamba malalamiko ya huyu mshairi si ya kweli. Watu hutaniwa popote wanapoenda kuendana na mila za wenyeji wa pale. Mie niliishi Moshi 1980-1990, wenyeji walikuwa wanatuita "kyasaka", lakini tulikuwa na shughuli zetu, tunashindana nao kama kawaida. Baba alikuwa na shamba sehemu inaitwa Mabogini, hakuna aliyetuzuia kulima. Huko Pwani wasokuwa wa Pwani mwawaita "wakuja", na hata wanyamwezi mnawaita "chapang'ombe", sasa kuna ajabu gani huko kwa wengine mkiitwa "wanyamwani?"
 
Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti na jinsi ulivyoitikisa CHADEMA
Theopista Nsanzugwanko
HabariLeo; Tuesday,January 08, 2008 @00:04

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni moja ya vyama vikubwa vya siasa nchini. Kilianzishwa kwa juhudi za waasisi kadhaa wa chama hicho, ambao ni pamoja na Edwin Mtei na Bob Makani.

Mkutano mkuu wake wa kwanza wa chama hicho, ulifanyika katika kituo cha Msimbazi Dar es Salaam kuanzia Desemba 15-17, 1992. Mkutano huu ulihudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa yote ya Tanzania na ulichagua viongozi wa kwanza wa chama hicho, majina na vyeo vyao kwenye mabano ni: Edwin Mtei (Mwenyekiti), Ali Suleiman Ahmed (Makamu Mwenyekiti upande wa Zanzibar), Brown Ngwilulupi (Makamu Mwenyekiti Bara), Bob Makani (Katibu Mkuu), Mustafa S. Simba (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar) na Eric Mchatta (Naibu Katibu Mkuu Bara).

Tangu mwaka huo 1992, chama hicho kimeendelea kukua na kufanya uchaguzi wa viongozi wake kila inapobidi. Pia, tangu mwaka huo kimekuwa kikishiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais. Matokeo ya kura katika chaguzi hizo yamekuwa ya kuridhisha na hali ya utulivu imekuwa pia inaridhisha.

Hata hivyo, hivi karibuni chama hicho kimetikiswa sana na suala la uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema upande wa Tanzania Bara. Hali hiyo ilijitokeza dhahiri katika vikao vya Kamati Kuu na Baraza Kuu vilivyofanyika Dar es Salaam, ambapo baada ya mvutano wa muda mrefu hatimaye alipatikana mshindi, ambaye ni Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya chama hicho, Chacha Wangwe.

Wakati wa kampeni ya kugombea nafasi hiyo, madai mengi yalitolewa na baadhi ya wanachama wao, kuhusiana na chama hicho hadi ikafika mahali Katibu Mkuu wao, Dk.Wilbrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, kudaiwa kutaka kujiuzulu nyadhifa zao.

Wanadaiwa walitaka kujiuzulu baada ya kuchukizwa na kitendo cha Chacha Wangwe, ambaye alikuwa mgombea wa nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti, kukishutumu chama kupitia vipeperushi vilivyosambazwa nchi nzima. Katika vipeperushi hivyo, Wangwe anadaiwa kusema kwamba chama kimegeuzwa kuwa mali ya ukoo na baadhi ya viongozi wa makao makuu.

Vipeperushi hivyo vilisambazwa na wafuasi wa chama hicho, waliokuwa wakimuunga mkono Wangwe katika kinyang'anyiro hicho. Habari kutoka ndani ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho, zinadai Dk Slaa ambaye ni Mbunge wa Karatu na Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, walifikia uamuzi huo, baada ya hoja kuhusu vipeperushi hivyo kujadiliwa katika kikao hicho.

Hata hivyo, waasisi wa chama hicho, Edwin Mtei na Bob Makani walifanya kazi ya ziada kuwashawishi Dk Slaa na Zitto kubadili uamuzi wao wa kujiuzulu na kuendelea na nyadhifa zao ili kulinda chama kisigawanyike. Chanzo chetu kilichokuwa ndani ya kikao hicho cha Kamati Kuu, kilisema kuwa "Ni kweli Zitto na Slaa walitangaza kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na vipeperushi vya Wangwe, lakini baada ya mambo kuwekwa sawa na waasisi hao wa chama, walikubali kurejea kwenye nyadhifa zao."

Kutokana na kitendo hicho, Kamati Kuu ilimuonya Wangwe na pia Kamati Kuu ilitishia kufuta uchaguzi huo. Hata hivyo, baadaye Kamati Kuu iliridhia kuwa uchaguzi huo ufanyike. Ilitoa uamuzi huo baada ya wajumbe wa kamati hiyo kupiga kura, ambapo 14 walisema ufanyike na 11 wakasema usifanyike. Ndipo kikao hicho kilifanyika chini ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kuandaa ajenda ambazo zingejadiliwa katika kikao cha Baraza Kuu.

Nalo Baraza Kuu baada ya kujadili ajenda hizo, liliendelea na ajenda ya kumchagua mwanachama atakayejaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti, iliyoachwa wazi na Amani Walid Kabourou, aliyejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka jana. Lakini, pamoja na kuonywa, Wangwe aliendelea kushikilia msimamo wake ulioko kwenye vipeperushi vyake katika kikao hicho pia. V

ipeperushi hivyo vinawatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema kuendesha chama kwa upendeleo, hasa katika mgawo wa ruzuku. Pia, kinawatuhumu viongozi wa Chadema kwa ubaguzi wa misingi ya kidini na Kikanda. Katika vipeperushi hivyo, Wangwe anadai kuwa kutokana na kasoro hizo, atahakikisha analeta mabadiliko ya kweli ndani ya chama ili kukiepusha kuendeshwa kama shirika lisilo la kiserikali (NGO).

"Tunataka kiwe chama cha siasa chenye lengo la kuking'oa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010," anasema Wangwe. Anasisitiza kuwa jambo kubwa linalokitia dosari CHADEMA ni ofisi za wilaya na kata kutokuwa na mawasiliano na makao makuu, hasa katika mgawo wa ruzuku na uteuzi wa wabunge wa viti maalumu.

Wangwe anadai mgawo wa ruzuku na uteuzi wa wabunge wa viti maalumu, vimekuwa vikitolewa na uongozi wa Chadema kwa kuangalia upande mmoja wa wanachama wanaotoka Kanda ya Kaskazini hapa nchini. "Chama kimekuwa mali ya koo na familia fulani. Tunataka kiwe cha wanachama," anadai Wangwe, ambaye baadaye alifanikiwa kupata nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti.

Alimshinda Mbunge wa Mpanda Kati kwa tiketi ya Chadema, Said Arfi. Wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono Wangwe katika kinyang'anyiro hicho, waliendelea kusambaza vipeperushi hivyo vinavyotuhumu kuwapo na upendeleo katika mgawo wa ruzuku za chama na ubaguzi wa kidini na kikanda katika chama hicho.

Vipeperushi hivyo vilitawanywa makao makuu ya Chadema, mikoani, wilayani na katika eneo ambalo Kamati Kuu ilikutana na vinadai kwamba chama hicho kimekuwa kikipata ruzuku ya Sh milioni 60 kila mwezi, lakini fedha hizo zimekuwa zikiishia makao makuu huku matumizi yake hayawekwi bayana.

"Tunasema inawezekana kila mkoa ukapata Sh milioni 1.5 kila mwezi na makao makuu itabaki na zaidi ya Sh milioni 10 ambazo zinawatosha kwa shughuli za chama," inaeleza sehemu ya kipeperushi hicho.

Kipeperushi kinadai kuwapo kwa "ubinafsi" katika chama, ambao umesababisha karibu wabunge wote wa viti maalumu kuteuliwa kutoka katika mkoa mmoja uliopo eneo la Kaskazini mwa nchi. "Tumchague Chacha ili aweze kubeba majukumu hayo na kuyavalia njuga ili ruzuku igawanywe katika mikoa yote. Chacha pambana kama unavyopambana na CCM katika Jimbo lako la Tarime," kinaeleza kipeperushi hicho.

Kipeperushi hicho kinawataka wajumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu kutoingia kwenye mtego wa kidini, kwa madai kwamba chama hicho siyo msikiti wala kanisa. "Ni chama cha siasa kinachotaka kuendelezwa na kiongozi jasiri kama Chacha (Wangwe). Hatusemi kwa ushabiki, angalia ukweli hapo makao makuu. Chadema ni chama chetu siyo kampuni ya watu binafsi, tubadilishe hali hii," kilieleza kipeperushi hicho.

Baada ya kutolewa kwa malalamiko hayo yaliyopo katika vipeperushi, Dk.Slaa alikanusha madai yaliyotolewa na kusema kuwa pesa zote za ruzuku, hutumika kutokana na maamuzi ya vikao vya chama.

Pia, alizungumza kuhusu wabunge wa viti maalumu karibu wote kutoka upande mmoja wa Kaskazini, ambapo alisema kutokana na chama hicho kuwa na wabunge wachache, inawabidi kutafuta wenye uwezo katika kutoa hoja za msingi bungeni. “Wabunge huteuliwa kwa kuangalia utendaji wa kazi zao ambazo zinaonekana wakiwa bungeni.

Kule bungeni hatupeleki sura, bali watendakazi ambao ndio jeuri ya chama chetu,” anasema. Dk Slaa anasema shutuma zilizotolewa na Wangwe, ambaye alikuwa anagombea umakamu mwenyekiti, ni maneno tu ya kumtaka apate nafasi hiyo.

Wlizungumzia baadhi ya matumizi yaliyoamuliwa katika vikao vya chama, kuwa ni pamoja na kuzunguka nchi nzima kukitambulisha chama kwa Watanzania, ambazo ukiacha usafiri na gharama nyingine zimetumika zaidi ya Sh milioni 200 kutengeneza bendera, kadi na vipeperushi.

Dk. Slaa anasema matumizi kama hayo siyo kwa manufaa ya makao makuu pekee, bali kwa mikoa yote waliyotembelea, ukiacha Mtwara na Lindi, ambayo bado hawajaitembelea kwa lengo la kuwajulisha Watanzania walioko mikoani sera za chama hicho.

“Hakuna chama kingine cha siasa ukiacha chama tawala kilichoweza kuzunguka mikoani na kujitambulisha kwa wananchi kama tulivyofanya sisi kwa shilingi milioni 60 kila mwaka,” anasisitiza. Akifungua Baraza Kuu la chama hicho, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alidai suala la kusitishwa kwa mjadala wa Katiba ni ukiritimba. Anasema katiba inapaswa kujadiliwa wakati wowote kwa kuwa ni mali ya wananchi.

Pia, alisema baada ya kutimiza miaka miwili, Rais Jakaya Kikwete inabidi afanyiwe tathmini ya uongozi wake na pia alidai kuwa wananchi wamechoka na kauli za kutia matumaini huku hali ya maisha ikizidi kuwa ngumu. Pia, Mbowe anawataka Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, kutoa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwani kampuni iliyopewa kazi ya kuichunguza ilipewa siku 28 tu kukamilisha uchunguzi na kutoa ripoti.

Anadai kuwa siku zimeisha, lakini wananchi bado hawajapewa ripoti hiyo. Baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha Baraza Kuu, Mbowe alikanusha kuwa kuna migogoro katika chama chake hicho. Pia, alisema kuwa Chadema itaendelea kutumia helikopta katika awamu nyingine ya ziara zake, baada ya kutafakari gharama za ziara za helikopta.

“Baraza Kuu limetafakari gharama za ziara za helikopta na kuwianisha na ziara nyingine na kuazimia kwa kauli moja kuendelea kutumia usafiri huo katika awamu nyingine ya ziara,” anasema.

Mbowe anasema maazimio mengine waliyoyafikia ni pamoja na kuweka hadharani hesabu ya mapato na matumizi, kwani kila mwanachama wa chama hicho ana uhuru wa kufahamu hilo. Alitaka wengine wanaotaka kujua hesabu hizo wafike makao makuu. Pia, Baraza Kuu liliamua kuendeleza ushirikiano wa vyama kwa lengo la kudumisha demokrasia nchini na kuunganisha nguvu katika kutetea maendeleo na hatimaye upinzani uweze kuchukua dola. Baraza hilo lilipitisha azimio la kutangaza ratiba ya uchaguzi wa chama hicho, utakaofanyika kuanzia mwezi Januari hadi Desemba.

Anasema uchaguzi huo utaanzia katika vitongoji, kata, jimbo, wilaya, mikoa na Kanda. Pia, kutakuwa na uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Taifa. Katika uchaguzi wa Makamu wa Mwenyekiti upande wa Tanzania Bara, Baraza Kuu lilimchagua Chacha Wangwe kushika nafasi hiyo, baada ya kupata kura 56 kati ya 94 zilizopigwa. Mpinzani wake Mbunge wa Mpanda Kati, Said Amour Arfi, alipata kura 38. Akitoa shukrani zake baada ya kutambulishwa rasmi kuwa Makamu, Wangwe anasema atatumia nafasi hiyo kurudisha demokrasia iliyoanza kupotea katika chama hicho. Anasema atafanya hivyo kwa kutumia vikao vya viongozi wa ngazi za juu.

Wangwe anasema kutokana na chama hicho kuwa cha kidemokrasia, mambo yote yaliyotokea ni harakati za kuimarisha demokrasia, hivyo yalikuwa ni sehemu ya midahalo tu; na wala sio migogoro, kama wengi walivyodhania.

Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved
 
Ndiyo Demokrasi ile ndani ya Chadema
Lumbana na baadaye fanya unayo takiwa na si kungoja kusemea kwenye mikitano ya ndani pekee hapana . Kweli Chadea wamekoaa naamini .
 
propaganda tu za kumaliza suala la Kubenea,Hiyo makala imeandikwa katika Gazeti la Habari Leo.Habari ya zamani imetolewa leo??
Wakati mwingine we need to be realistic,sitakli kuunga mkono na hili.sitaki kuamini kama kuan taitpu ya waandishi kama binti huyu wa nsanzugwanko.

Kada maarufu wa Chama cha mapinduzi.
 
Mwenyekiti Wa Chadema Bwana Mbowe Amekuwa Akipita Kila Tawi La Chadema Na Kumpa Shutuma Kali Makamu Mwenyikiti Wake Kuwa Hana Nia Njema Na Chadema.

Ugomvi Wao Ulianza Wakati Wa Uchaguzi Wa Kutafuta Makamu Wa Mwenyekiti Wa Taifa Chadema Ambapo Bwana Mbowe Alikuwa Akimsupport Bwana Alfu.

Lakini Chacha Wangwe Alishinda Kiti Na Sasa Anahujumiwa Na Mbowe.
 
Haya nayo makubwa, sasa hizi sio siasa tena ni mchezo mchafu sasa
Haya tupe vidhibitisho vya kusupport thread yako ili tumjadili naye huyu
CHINGA UKIRUDI LETA UTHIBITISHO......! AU KAMA KUNA MWINGINE MWENYE UTHIBITISHO AUDONDOSHE JAMVINI....NA KAMA KUNA MWENYE KUKANUSHA KWA USHAHIDI NAYE....TWAMKARIBISHA....!
 
Mwenyekiti Wa Chadema Bwana Mbowe Amekuwa Akipita Kila Tawi La Chadema Na Kumpa Shutuma Kali Makamu Mwenyikiti Wake Kuwa Hana Nia Njema Na Chadema.

Ugomvi Wao Ulianza Wakati Wa Uchaguzi Wa Kutafuta Makamu Wa Mwenyekiti Wa Taifa Chadema Ambapo Bwana Mbowe Alikuwa Akimsupport Bwana Alfu.

Lakini Chacha Wangwe Alishinda Kiti Na Sasa Anahujumiwa Na Mbowe.

Heshima Chingaman

Tunaomba uthibitisho wa hili mkuu usije kuwa umeendeleza propaganda na ndoto za alinacha na alfu lela ulela...
 
Back
Top Bottom