Chadema kutokubali uchaguzi mdogo Arusha Mjini kunazua maswali!

hivi kuna sokoni1 na osokoni..osokoni umeonyesha uvivu wa kufatilia mambo lisha ya kuonyesha kama ulifatilia jambo hili na kujidai kupangilia kwa umakini lakini nashukru watu wamekushitukia mapema..kwanza idadi uliyoitoa ya madiwani siyo sawa,sababu ulizo zitoa za chadema kuamua kukata rufaa siyo sawa, maamzi ya Lema kutokata rufaa ilikuwa ni kabla ya kupitia hukumu lakini baada ya wanasheria wa chama na marafiki walishauri akate rufaa na mambo mengi yaliwekwa wazi na Mbowe trh 8.4.12..
 
Kwahiyo unamshauri Nape asimamishe zoezi la kukata rufaa Igunga?
 
Mtoa Mada uwe na uhakika kuwa wanachama wa chadema huwa tunafuatilia matamko ya viogozi wetu kwa umakini, huwezi kutudanganya. Kimsingi wananchi wa Arusha tulikuwa tunataka uchaguzi mpaka pale viongozi wetu walipo tuelimisha na tukaelewa, tunaweza kuishi bila mbunge na shughuli zitaendela kama kawaida, kwani kuwa na mbunge wa ccm ni sawa na kutokuwa na mbunge tu! Haki ni bora zaidi kuliko barabara za Lami!

"Haki ni bora kuliko Barabara za Lami".. Nimeipenda hiyo!.
 
Enyi magamba ni nani aliyewaroga? Hivi mu vipofu kiasi cha kushindwa kuiona kweli japo kweli i ndani ya mioyo yenu? Jiondoeni katika ibada za wanafiki, maana hamtahesabiwa haki kwa kujipaka majivu na kuvaa magunia huku mkipiga mayowe dunia nzima iwasikie na kuwasikitikia. Tendeni yaliyo mema na wana wema watawasikiliza.
 
Mimi nadhani wa kulaumiwa kwa kuwanyima Watu wa Arusha haki ya uwakilishi ni Serikali B "Mahakama" ambao wanaipeleka rufaa taratibu. Kama ingepangiwa tarehe mapema mara tu baada ya kuwasilishwa maamuzi yangefikiwa mapema na haki ingejulikana na Arusha wangepata uwakilishi. So we should not blame CDM hapa wa kulaumu ni mahakama na Serikali "inayoingilia" uhuru wa mahakama
 
Mkuu Osokoni leo umechemsha....sikubaliani na wewe hata kidogo,hata hivyo sababu za msingi za kukata rufaa zimeshaelezwa na wadau hapo juu na zipo clear kabisa!!!CHADEMA NI CHAMA MAKINI SANA!!
 
Hapo kwenye bold! Sababu ya kukata rufaa haikuwa moja, nimeamini wewe ni Gamba; Sababu ilikuwa 1. Kuweka record sahihi ya hukumu. 2.Kupinga kubambikizwa kwa makosa ya rushwa ambayo Lema hakushitakiwa kwayo. 3. Kupinga kuzuiwa kwa Lema kushiriki uchanguzi kwa miaka mitano. 4. Kulinda Heshima ya Mahakama.

Msimamo: Chadema hatuogopi uchaguzi wowote, mahali popote, muda wowote; we have the moral authority kusimama mbele ya watanzania na kuwaomba kura!

uwe mstaarabu kisa cha kuniita gamba ni nini? wewe unayejiita cdm hata kadi huna hata katiba ya chama hujui inafanana je sisi kwa tarifa yako ndio waanzilishi wa chama na makala kama hizi ni changamoto kwa chama chetu sasa usipende kuexpose ujinga wako kwenye jukwaa hili!
 
Mtoa mada from 2day ur out'f ma mind,.huwa nakuamini kamanda ila huna hoja at all.OSOKONI= GAMBA

kuna watu huwa wanakurupuka kutoa hoja kwa kudhani wanaoisoma wana akili kama yake. Kumbe kuna waliomzidi na walio chini yake. Huwezi kukubali hata uwe kichaa hukumu itolewe kwa kifungu kingine cha makosa na uadhibiwe kwa kutumia kifungu kingine! Mi niliingia humu nikijua cdm wamesema watagomea uchaguzi ukiitishwa tena!
 
@OSOKONI, umechemsha. Habari ya IPPMEDIA wewe umeiweka hapa bila kuandika umeitowa wapi?

HESHIMU kazi za watu, tutakuita Mwizi. Mwenzio Mo Dewji alikuja hapa tukamtoa baru na kazi za watu.....


Chadema kutokubali uchaguzi mdogo Arusha Mjini kunazua maswali!

BY MUHIBU SAID,
19th August 2012

NI zaidi ya miezi minne sasa wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini, hawana mbunge wa kuwawakilisha katika vikao vya mikutano ya shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama ilivyo kwa majimbo karibu yote ya Tanzania Bara.

Jimbo lingine, ambalo halina mbunge kwa kipindi kama hicho, ni Sumbawanga Mjini, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga, kutengua ubunge wa Khalfan Aeshi (CCM).

Aesh alitiwa hatiani na mahakama kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 uliompa ushindi.

Jimbo la Arusha Mjini, ambalo ndiyo mada yangu ya leo, halina mbunge kwa sababu kuu mbili. Ya kwanza, ni hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha. Hukumu hiyo ilitengua ubunge wa Godbless Lema (Chadema) aliyekuwa akiliwakilisha jimbo hilo bungeni tangu mwaka 2010.

Hukumu hiyo ilitolewa Aprili 5, mwaka huu, na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila, baada ya kujiridhisha kuwa Lema alitumia kashfa, kejeli na udhalilishaji katika mikutano yake ya kampeni, kinyume cha kanuni, taratibu na sheria ya maadili ya uchaguzi ya mwaka 2010.

Sababu ya pili inayofanya jimbo hilo likose mbunge hadi sasa, ni rufaa iliyokatwa na Chadema kupinga hukumu hiyo ya Jaji Rwakibarila. Sheria inazuia kuitishwa uchaguzi hadi rufaa hiyo itakapoamuliwa.

Rufaa hiyo ndiyo kwanza imepangwa kusikilizwa Septemba 20, mwaka huu, mbele ya majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa; Natalia Kimaro, Mbarouk Salim Mbarouk na Salum Massati.

Kesi iliyotengua ubunge wa Lema, ilifunguliwa na wanachama watatu wa CCM; Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliodai kuwa wakati wa kampeni Lema alimdhalilisha aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian, ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania, nchini Kenya.

Baada ya hukumu ile, Lema alionekana kutokuwa na wazo kabisa la kukata rufaa. Kwani siku ileile saa chache baada ya hukumu kutolewa, alikaririwa akisema hatakata rufaa kwa kuwa hataki kuwa mbunge wa rufaa.

Msimamo huo wa Lema ulioana sawia na ule aliokuwa nao Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Mwigamba pamoja na mambo mengine, alikaririwa akisema haoni sababu ya kukata rufaa. Bali kujiandaa na kuingia kikamilifu katika uchaguzi wa marudio jimboni humo.

Alisema kukata rufaa ni kupoteza muda, kwani kinachotakiwa ni kujiandaa kikamilifu kuiangusha tena CCM katika uchaguzi wa marudio kwa kura nyingi tofauti na zile zilizopita.

Ni wazi kuwa kauli hiyo ya Lema inadhihirisha imani yake kwa Chadema kwamba, ina uwezo mkubwa wa kulirejesha jimbo hilo wakati wowote na saa yoyote kama atasimamishwa tena kulitetea.

Naweza kusema Lema hapo yuko sahihi. Kwamba, kwa hakika Jimbo la Arusha Mjini bado ni ngome ya Chadema. Vipo vigezo vingi vinavyoweza kuthibitisha ukweli huo.

Cha kwanza, ni matokeo halisi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 yaliyompa ushindi Lema. Matokeo hayo yanaonyesha kuwa Lema alimwangusha Dk. Burian kwa kumshinda karibu kura 20,000.

Kigezo cha pili, ni mchuano mkali uliopo katika idadi ya madiwani waliovunwa na Chadema dhidi ya madiwani, ambao CCM ilipata katika uchaguzi huo katika Manispaa ya Arusha.

Katika manispaa hiyo, CCM ilipata madiwani 16, Chadema 15 na Chama cha Tanzania Labour (TLP) wawili. Takwimu hiyo ni kabla ya madiwani watano wa Chadema kuvuliwa uanachama kwa kukiuka maamuzi na maelekezo ya chama.

Kigezo cha tatu, ni mwitikio wa watu, ambao umekuwa ukionekana katika mikutano ya hadhara, maandamano na shughuli nyingine za kisiasa na kijamii zinazoandaliwa na Chadema jimboni humo.

Kigezo cha nne, ni ushindi, ambao Chadema iliupata katika uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki.

Ni ukweli usiopingika kuwa ushindi huo alioupata aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chadema, Joshua Nassari, ulichangiwa na ushawishi mkubwa wa wananachi kutoka Jimbo la Arusha Mjini.

Kigezo cha tano, ni namna mwitikio wa wananchi ulioonekana mahakamani siku ya hukumu na katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na uongozi wa Chadema mjini Arusha baada ya hukumu hiyo.

Yawezekana vigezo hivyo ndivyo vilivyomfanya Lema aamini kuwa kushindwa kwake kesi si kwa sababu chama chake nay eye mwenyewe hawaungwi mkono na wananchi. La!

Bali aliamini na kudiriki kutamka kwamba, kulitokana na shinikizo la Ikulu, madai ambayo yalinushwa vikali na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu kwamba, ni ya upuuzi na ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima uliofanywa na Lema kwa mahakama na serikali.

Ni wazi kuwa hatua ya Lema kukata rufaa hiyo, haikuwa ni hiari yake. Bali ilikuwa ni kutekeleza uamuzi ya chama chake. Na pengine ulitokana na kuhofia yasije yakamkuta yaliyowakuta madiwani wale watano wa Chadema.

Uamuzi wa Chadema wa kukata rufaa, ulitangazwa na Mbowe katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya NMC, mjini Arusha, Aprili 8, mwaka huu.

Mbowe alisema licha ya Chadema kuwa na uhakika wa kushinda uchaguzi katika jimbo hilo, wameshauriana na wanasheria pamoja na viongozi wenzake.

Wameona ni vema wakakata rufaa kwa sababu ya jaji kutafsiri kuwa Lema alitukana, alibagua kijinsia na aliendesha kampeni zisizo za kistaarabu, jambo ambalo alidai kuwa halikuwa kweli na halikutokea.

Hata hivyo, uamuzi wa Chadema wa kutokubali kwenda kwenye uchaguzi mdogo jimboni humo ili kumrudisha mbunge wake, bado unazua maswali!

Mosi, kauli ya Lema kwamba, hataki kuwa mbunge wa rufaa, je, ilikuwa ni ya kukurupuka?

Pili, shinikizo la Ikulu lililodaiwa na Lema kuingilia kesi yake Mahakama Kuu na kutengua ubunge wake, je, haliwezi ‘kupenya' pia katika Mahakama ya Rufaa, ambako chama kimekimbilia huko, rufaa yake ikatupwa?

Tatu, ikiwa viongozi wakuu wa Chadema, Lema mwenyewe na wananchi, wana uhakika wa chama kushinda Arusha Mjini hata kama watasimamisha jiwe kugombea, kwanini basi wasikubali kuingia kwenye uchaguzi badala ya kupoteza muda wa rufaa?

Muhibu Said ni mwandishi wa habari wa gazeti la NIPASHE. Simu: 0717055551 au 0755925656. Barua pepe: muhibu72@yahoo.co.uk




From: http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=44959
 
Osokoni hata kama wewe ni moja ya waanzilishi wa chadema hatuta kubaliana na utumbo kisa umeletwa na mwanzili wa chama ila na kusamehe kwa kuwa umecopy na kupaste..hahahaahaahahaha
 
Wewe kweli ni OSOKONI au kuna mtu ulimtuma kukupostia kwa password yako?
Think Twice!!!!!!
 
Mtoa mada kakurupuka tu. sababu kubwa ya CDM kukata rufaa Arusha ni kwamba katika hukumu ya mahakama Kuu haikuelezwa kwa bayana kabisa kuhusu suala la rushwa - iwapo Lema alitoa hongo etc na hivyo kutogombea tena ubunge kwa kipindi fulani. Hukumu haikuwa wazi, nadhani iliachwa hivyo kimakusudi tu katika hilo.

Hivyo Lema angegombea tena, CCM wangeweza kuweka pingamizi kwa Tume ya uchaguzi - NEC -kumuengua wakati wa uteuzi na kufanikiwa, na hivyo kuiwezesha CCM kulichukuwa jimbo kwa ulaini. Si unajua tena mara nyingi Tume ya Uchaguzi siyo huru.

Hilo ndilo walikuwa wanahofia CDM na ndiyo maana wamekata rufaa, na katika rufaa hiyo CDM wanaomba Mahakama ya Rufaa ifafanue pia kuhusu suala la rushwa.
Mkuu counterpunch kwa maelezo hayo nadhani mleta mada ya kiunafiki amekuelewa!! Mpe hai siku njema!!

 
Mada za kupewa. Mkuu umeipaste bila kuipitia kidogo. Nilikuwa natafuta ni kwa nini umeibatiza jina la CDM kutokubalika nilipoikosa nimeshawishika kuwa kuna mtu kakupa hii text ukaja kuilump bila kuiorganize
 

Uamuzi wa Chadema wa kukata rufaa, ulitangazwa na Mbowe katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya NMC, mjini Arusha, Aprili 8, mwaka huu.

Mbowe alisema licha ya Chadema kuwa na uhakika wa kushinda uchaguzi katika jimbo hilo, wameshauriana na wanasheria pamoja na viongozi wenzake.

Wameona ni vema wakakata rufaa kwa sababu ya jaji kutafsiri kuwa Lema alitukana, alibagua kijinsia na aliendesha kampeni zisizo za kistaarabu, jambo ambalo alidai kuwa halikuwa kweli na halikutokea.


Mkuu Osokoni,
1. Naona umeamua kuweka habari kutoka kwenye Nipashe pasipo mwisho wa habari yenyewe kuweka source. Hii imetufanya wengi wetu tudhanie kuwa ni wewe ndio uliyeiasisi na kuiweka na hivyo kupokea mashambulizi mengi. Tungeendelea kuamini hivyo kama isingewekwa habari yanyewe, tarehe ya kuandikwa na jina la Mwandishi. Hata hivyo, tutaichangia mada kama ilivyo.

2. Kwa waliokuwepo pale Viwanja vya NMC siku ile ya Jumamosi ya tarehe 08. 04. 2012, watakubaliana nami kuwa 'kipande nilichonukuu' ndiyo haswa msingi wa CHADEMA na Lema kukata rufaa. Wananchi wa Arusha mpaka Mh Mbowe alipooa kauli ile walikuwa na AMRI na NIA ya kuingia tena kwenye uchaguzi na walidhamiria kulinda kura zao (kutokana na uzoefu walioupata kutoka Arumeru Mashariki juma moja tu lililopita) . Lakini Mh. Mbowe alieleza kuwa, "kuyakubali maamuzi yale ya Mahakama na Kukubali Kuingia Kwenye Uchaguzi Mdogo, Hata Kama Una uhakika kwa Kushinda, utakuwa umemaanisha kuwa, unakubaliana na mwenendo mzima wa mashtaka na shauri lenyewe. Kwamba CHADEMA na Lema, ni chama cha kuwadhalilisha wanawake; na ni chama cha ubaguzi. Lakini pia, hukumu ile ya kibaguzi na kionevu, itatumika kama rejea ya mahakama (Judicial Precedence) katika kutolea maamuzi siku zijazo. Watoto wetu wataonewa na kugandamizwa. Wataporwa Haki zao. Kuikubali hukumu ile, kutamaanisha kuwa wananchi maskini wa kitanzania, wataenda tena kugharamia uchaguzi ule mdogo (sikumbuki vizuri, ila nadhani alisema ni 4bn). Hukumu ile, haisemi hatma ya Mh. Lema kama anaruhusiwa kugombea au la. Amepewa hukumu ya kosa ambalo si la kwake"

3. Ukisoma makala hii tu kwa juu juu bila ya kumfahamu Mwandishi Mwenyewe wa Makala na aina ya uandishi wake utakuwa unakosea. Kwa wale ambao hawafahamu ni kuwa, uandishi wa habari wa Tanzania wa habari za kiuchunguzi/makala au michezo unafanana. Kwamba kuna waandishi wenye kambi ya Simba na Yanga. Na waandishi wa habari za Siasa, nao wako kwenye kambi hizo pia. CCM, CHADEMA, CUF n.k. Makala na habari za Muhibu Said tangu akiwa anaandikia gazeti la Mwananchi kama freelancer, zilikuwa zinaonyesha dhahiri upande aliopo. Na kwa muda wote, alikuwa akiripoti habari zilizohusu Chama Cha Wananchi (CUF). Alizunguka katika misafara yote ya Pr. Lipumba na hata lile tukio la yule mtoto inayesemekana kuiba sanduku la kura na kupigwa risasi na Mkurugenzi wa Temeke, ni yeye ndiye alikuwa anaripoti. Na hata alipojiunga na Nipashe, ameendelea kuandika, kwa asilimia kubwa, habari zinazomhusu Lipumba na chama cha CUF.
Hivyo, sikushangaa kusoma makala kama haya kutoka kwa mwandishi mwenye 'calibre' ya Muhibu. Ni nani amesahau namna Novatus Makunga (aliyewahi Kugombea Kura za Maoni Ubunge kupitia CCM) alivyokuwa anaripoti kampeni, upigaji kura na hata kuwasilisha matokeo ya awali katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Arumeru Mashariki?

- Ni Makunga aliyekuwa kila akiripoti habari za Sioi, anaweka picha za kampeni za urais mwaka 2010 kuonyesha watazamaji wa ITV kuwa wale walikuwa ni wahudhuriaji wa mikutano ya kampeni wa Sioi.

- Ni Makunga ambaye wakati akiripoti kuhusu watu waliojitokeza kwenye kupiga kura, alieleza kuwa " waliojitokeza kwenye upigani wa kura ni wazee tu, na vijana hawakuwepo, tofauti na wakati wa mikutano ya kampeni walikuwa wengi", wakati mtangazaji mwenzake, Asraj Mvungi 'akielezea kuwa Vijana walijitokeza kwa wingi katika upigaji wa kura, kama ilivyokuwa katika mikutano ya kampeni'.

- Ni Novatus Makunga huyu huyu, miezi michache baadaye, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai!



Kama Great Thinkers ( GT), inatupasa kuthink Critically.
 
Nashikwa na kigugumizi kuchangia mada hii, Hivi majaji wa Kesi ya LEMA na wale walioamua kezi za Igunga na Sumbawanga tofauti zao nini, CDM wakishinda, jaji mzuri, wakishindwa, jaji wa CCM. Haya mambo yanakuaje? si tuachane na haya mambo ya vyama vingi? Haya mambo ya wazungu bwana, Afrika tunadandia gari kwa mbele.

Another silly season! Wewe ndo huelewi kitu kabisa! Unafikiri chadema huwa tunakurupuka kusema kutokana na matukio eeh! Tunataka kuona haki haipindishwi! Hatutaki kushinda kesi tu hata tukishindwa kihalali tutakubali, lakini hatuwezi acha haki ikafukiwa..
 
Habari ya OSOKONI ni ya gazeti la NIPASHE. Msiendelee kumshambulia OSOKONI.

Kosa alilofanya ni kutokuweka sehemu alipoitowa.
 
Wanachelewesha tu ushindi kwa CDM, na SSM wanajua hilo. Hata wakitupilia hukumu kule kuzimu but uchaguzi jimbo la Arusha mjini = Chadema.
 
Back
Top Bottom