OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,336
NI zaidi ya miezi minne sasa wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini, hawana mbunge wa kuwawakilisha katika vikao vya mikutano ya shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama ilivyo kwa majimbo karibu yote ya Tanzania Bara.
Jimbo lingine, ambalo halina mbunge kwa kipindi kama hicho, ni Sumbawanga Mjini, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga, kutengua ubunge wa Khalfan Aeshi (CCM).
Aesh alitiwa hatiani na mahakama kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 uliompa ushindi.
Jimbo la Arusha Mjini, ambalo ndiyo mada yangu ya leo, halina mbunge kwa sababu kuu mbili. Ya kwanza, ni hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha. Hukumu hiyo ilitengua ubunge wa Godbless Lema (Chadema) aliyekuwa akiliwakilisha jimbo hilo bungeni tangu mwaka 2010.
Hukumu hiyo ilitolewa Aprili 5, mwaka huu, na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila, baada ya kujiridhisha kuwa Lema alitumia kashfa, kejeli na udhalilishaji katika mikutano yake ya kampeni, kinyume cha kanuni, taratibu na sheria ya maadili ya uchaguzi ya mwaka 2010.
Sababu ya pili inayofanya jimbo hilo likose mbunge hadi sasa, ni rufaa iliyokatwa na Chadema kupinga hukumu hiyo ya Jaji Rwakibarila. Sheria inazuia kuitishwa uchaguzi hadi rufaa hiyo itakapoamuliwa.
Rufaa hiyo ndiyo kwanza imepangwa kusikilizwa Septemba 20, mwaka huu, mbele ya majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa; Natalia Kimaro, Mbarouk Salim Mbarouk na Salum Massati.
Kesi iliyotengua ubunge wa Lema, ilifunguliwa na wanachama watatu wa CCM; Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliodai kuwa wakati wa kampeni Lema alimdhalilisha aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian, ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania, nchini Kenya.
Baada ya hukumu ile, Lema alionekana kutokuwa na wazo kabisa la kukata rufaa. Kwani siku ileile saa chache baada ya hukumu kutolewa, alikaririwa akisema hatakata rufaa kwa kuwa hataki kuwa mbunge wa rufaa.
Msimamo huo wa Lema ulioana sawia na ule aliokuwa nao Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Mwigamba pamoja na mambo mengine, alikaririwa akisema haoni sababu ya kukata rufaa. Bali kujiandaa na kuingia kikamilifu katika uchaguzi wa marudio jimboni humo.
Alisema kukata rufaa ni kupoteza muda, kwani kinachotakiwa ni kujiandaa kikamilifu kuiangusha tena CCM katika uchaguzi wa marudio kwa kura nyingi tofauti na zile zilizopita.
Ni wazi kuwa kauli hiyo ya Lema inadhihirisha imani yake kwa Chadema kwamba, ina uwezo mkubwa wa kulirejesha jimbo hilo wakati wowote na saa yoyote kama atasimamishwa tena kulitetea.
Naweza kusema Lema hapo yuko sahihi. Kwamba, kwa hakika Jimbo la Arusha Mjini bado ni ngome ya Chadema. Vipo vigezo vingi vinavyoweza kuthibitisha ukweli huo.
Cha kwanza, ni matokeo halisi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 yaliyompa ushindi Lema. Matokeo hayo yanaonyesha kuwa Lema alimwangusha Dk. Burian kwa kumshinda karibu kura 20,000.
Kigezo cha pili, ni mchuano mkali uliopo katika idadi ya madiwani waliovunwa na Chadema dhidi ya madiwani, ambao CCM ilipata katika uchaguzi huo katika Manispaa ya Arusha.
Katika manispaa hiyo, CCM ilipata madiwani 16, Chadema 15 na Chama cha Tanzania Labour (TLP) wawili. Takwimu hiyo ni kabla ya madiwani watano wa Chadema kuvuliwa uanachama kwa kukiuka maamuzi na maelekezo ya chama.
Kigezo cha tatu, ni mwitikio wa watu, ambao umekuwa ukionekana katika mikutano ya hadhara, maandamano na shughuli nyingine za kisiasa na kijamii zinazoandaliwa na Chadema jimboni humo.
Kigezo cha nne, ni ushindi, ambao Chadema iliupata katika uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki.
Ni ukweli usiopingika kuwa ushindi huo alioupata aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chadema, Joshua Nassari, ulichangiwa na ushawishi mkubwa wa wananachi kutoka Jimbo la Arusha Mjini.
Kigezo cha tano, ni namna mwitikio wa wananchi ulioonekana mahakamani siku ya hukumu na katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na uongozi wa Chadema mjini Arusha baada ya hukumu hiyo.
Yawezekana vigezo hivyo ndivyo vilivyomfanya Lema aamini kuwa kushindwa kwake kesi si kwa sababu chama chake nay eye mwenyewe hawaungwi mkono na wananchi. La!
Bali aliamini na kudiriki kutamka kwamba, kulitokana na shinikizo la Ikulu, madai ambayo yalinushwa vikali na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu kwamba, ni ya upuuzi na ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima uliofanywa na Lema kwa mahakama na serikali.
Ni wazi kuwa hatua ya Lema kukata rufaa hiyo, haikuwa ni hiari yake. Bali ilikuwa ni kutekeleza uamuzi ya chama chake. Na pengine ulitokana na kuhofia yasije yakamkuta yaliyowakuta madiwani wale watano wa Chadema.
Uamuzi wa Chadema wa kukata rufaa, ulitangazwa na Mbowe katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya NMC, mjini Arusha, Aprili 8, mwaka huu.
Mbowe alisema licha ya Chadema kuwa na uhakika wa kushinda uchaguzi katika jimbo hilo, wameshauriana na wanasheria pamoja na viongozi wenzake.
Wameona ni vema wakakata rufaa kwa sababu ya jaji kutafsiri kuwa Lema alitukana, alibagua kijinsia na aliendesha kampeni zisizo za kistaarabu, jambo ambalo alidai kuwa halikuwa kweli na halikutokea.
Hata hivyo, uamuzi wa Chadema wa kutokubali kwenda kwenye uchaguzi mdogo jimboni humo ili kumrudisha mbunge wake, bado unazua maswali!
Mosi, kauli ya Lema kwamba, hataki kuwa mbunge wa rufaa, je, ilikuwa ni ya kukurupuka?
Pili, shinikizo la Ikulu lililodaiwa na Lema kuingilia kesi yake Mahakama Kuu na kutengua ubunge wake, je, haliwezi kupenya pia katika Mahakama ya Rufaa, ambako chama kimekimbilia huko, rufaa yake ikatupwa?
Tatu, ikiwa viongozi wakuu wa Chadema, Lema mwenyewe na wananchi, wana uhakika wa chama kushinda Arusha Mjini hata kama watasimamisha jiwe kugombea, kwanini basi wasikubali kuingia kwenye uchaguzi badala ya kupoteza muda wa rufaa?