Chadema kutokubali uchaguzi mdogo Arusha Mjini kunazua maswali!

Mkuu Osokoni,
1. Naona umeamua kuweka habari kutoka kwenye Nipashe pasipo mwisho wa habari yenyewe kuweka source. Hii imetufanya wengi wetu tudhanie kuwa ni wewe ndio uliyeiasisi na kuiweka na hivyo kupokea mashambulizi mengi. Tungeendelea kuamini hivyo kama isingewekwa habari yanyewe, tarehe ya kuandikwa na jina la Mwandishi. Hata hivyo, tutaichangia mada kama ilivyo.

2. Kwa waliokuwepo pale Viwanja vya NMC siku ile ya Jumamosi ya tarehe 08. 04. 2012, watakubaliana nami kuwa 'kipande nilichonukuu' ndiyo haswa msingi wa CHADEMA na Lema kukata rufaa. Wananchi wa Arusha mpaka Mh Mbowe alipooa kauli ile walikuwa na AMRI na NIA ya kuingia tena kwenye uchaguzi na walidhamiria kulinda kura zao (kutokana na uzoefu walioupata kutoka Arumeru Mashariki juma moja tu lililopita) . Lakini Mh. Mbowe alieleza kuwa, "kuyakubali maamuzi yale ya Mahakama na Kukubali Kuingia Kwenye Uchaguzi Mdogo, Hata Kama Una uhakika kwa Kushinda, utakuwa umemaanisha kuwa, unakubaliana na mwenendo mzima wa mashtaka na shauri lenyewe. Kwamba CHADEMA na Lema, ni chama cha kuwadhalilisha wanawake; na ni chama cha ubaguzi. Lakini pia, hukumu ile ya kibaguzi na kionevu, itatumika kama rejea ya mahakama (Judicial Precedence) katika kutolea maamuzi siku zijazo. Watoto wetu wataonewa na kugandamizwa. Wataporwa Haki zao. Kuikubali hukumu ile, kutamaanisha kuwa wananchi maskini wa kitanzania, wataenda tena kugharamia uchaguzi ule mdogo (sikumbuki vizuri, ila nadhani alisema ni 4bn). Hukumu ile, haisemi hatma ya Mh. Lema kama anaruhusiwa kugombea au la. Amepewa hukumu ya kosa ambalo si la kwake"

3. Ukisoma makala hii tu kwa juu juu bila ya kumfahamu Mwandishi Mwenyewe wa Makala na aina ya uandishi wake utakuwa unakosea. Kwa wale ambao hawafahamu ni kuwa, uandishi wa habari wa Tanzania wa habari za kiuchunguzi/makala au michezo unafanana. Kwamba kuna waandishi wenye kambi ya Simba na Yanga. Na waandishi wa habari za Siasa, nao wako kwenye kambi hizo pia. CCM, CHADEMA, CUF n.k. Makala na habari za Muhibu Said tangu akiwa anaandikia gazeti la Mwananchi kama freelancer, zilikuwa zinaonyesha dhahiri upande aliopo. Na kwa muda wote, alikuwa akiripoti habari zilizohusu Chama Cha Wananchi (CUF). Alizunguka katika misafara yote ya Pr. Lipumba na hata lile tukio la yule mtoto inayesemekana kuiba sanduku la kura na kupigwa risasi na Mkurugenzi wa Temeke, ni yeye ndiye alikuwa anaripoti. Na hata alipojiunga na Nipashe, ameendelea kuandika, kwa asilimia kubwa, habari zinazomhusu Lipumba na chama cha CUF.
Hivyo, sikushangaa kusoma makala kama haya kutoka kwa mwandishi mwenye 'calibre' ya Muhibu. Ni nani amesahau namna Novatus Makunga (aliyewahi Kugombea Kura za Maoni Ubunge kupitia CCM) alivyokuwa anaripoti kampeni, upigaji kura na hata kuwasilisha matokeo ya awali katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Arumeru Mashariki?

- Ni Makunga aliyekuwa kila akiripoti habari za Sioi, anaweka picha za kampeni za urais mwaka 2010 kuonyesha watazamaji wa ITV kuwa wale walikuwa ni wahudhuriaji wa mikutano ya kampeni wa Sioi.

- Ni Makunga ambaye wakati akiripoti kuhusu watu waliojitokeza kwenye kupiga kura, alieleza kuwa " waliojitokeza kwenye upigani wa kura ni wazee tu, na vijana hawakuwepo, tofauti na wakati wa mikutano ya kampeni walikuwa wengi", wakati mtangazaji mwenzake, Asraj Mvungi 'akielezea kuwa Vijana walijitokeza kwa wingi katika upigaji wa kura, kama ilivyokuwa katika mikutano ya kampeni'.

- Ni Novatus Makunga huyu huyu, miezi michache baadaye, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai!



Kama Great Thinkers ( GT), inatupasa kuthink Critically.

ndugu yangu opotoshaji wa namna hii hauleti tija hata kidogo kama unavyojiita mwenyewe kuwa ni great thinker,kwanza katika kampeni za arumeru sijawahi hata tukio moja kutumia picha za zamani,nilikuwa najipanga nahudhuria mkutano mmoja tu mkubwa napata picha nzuri kwa siku na kwa kukuongezea mimi katika coverage ya uchaguzi mkuu sikushiriki hivyo sikuwa na picha, lakini cha pili uliza mtu yeyote yule idadi ya wapiga kura wengi arumeru si vijana ingawa ni wakazi wa arumeru idadi kubwa ya vijana walijiandikisha arusha mjini lakini kukuongezea uelewa tu ripota aliyeko eneo kama usa river na tengeru atakuwa tofauti na yule aliyeko mbuguni na makiba hivyo kama tulikuwa maeneo tofauti na asraj usitegemee tutaripoti sawasawa,hivyo nawasihi jamani taarifa za kufikirika ama za kuzua tungeziacha.nitafute hata leo nitakuonyesha picha zote kuanzia story yangu ya kwanza mpaka ya mwisho.
 
Wanasheria ndio watakua walishauri kukata rufaa kwani mabere marando alisema kutokukata rufaa hukumu ya kesi ile itakuwa bad precedent maana chadema siyo chama cha kuchangia maendeleo mengine hata maeneleo ya sheria pia. Hakuna cha kuogopesha CDM kuingia kwenye uchaguzi
 
Kukubali kuwa Lema ametukana na kudhalilisha kijinsia ingekuwa pigo kwa future ya Lema na CDM kwa ujumla.
Hivyo rufaa haiepukiki.
 
Pole sana kwa thread ndefu lakini analysis yako imepitwa na wakati (time barred!!), kwa hiyo haina mantiki wala tija. Between then and now, a lot of water has passed under the bridge, no cause for shedding Crocodile tears my buddy!!!

Sasa ni kusubiri hukumu ya rufaa, Lema na Mwigamba walisema nini wakati ule haitusaidii!

The fact of the matter ni kwamba CDM ilikata rufaa. What is important ni huko tunakoelekea tutafanya nini. yaani strategising for the future as we move forward, period.
 
Eti ni kweli yule judge aliyeamua kesi ya mh lema ndie aliyemfunga maisha Babu Seya na wanawe?
 
Chadema wanaogopa kurudia uchaguzi arusha kwa sababu kubwa mbil 1;ilikuwa ni mapema mno kurudia uchaguzi kabla hawajaenda kuwapigia magoti wahisani wa nje kuomba mabilioni ya pesa ili wachakachue nakudanganya kuwa ghalama za kurudia uchaguzi zimetokana na michango ya wananchi.na mabilion hayo yakielekezwa tumboni street kwa wakubwa wachache wa cdm,2 sababu nyingine wanajua jinsi gani lema alivyowachafua wananchi wa arusha na watanzania kwa ujumla kwa siasa zake .kwahiiyo wanajipanga kumpata mgombea mwingine kwani lema hauziki kwasasa.lakini pia wanajua kuwa ccm wamejipanga kurudisha heshima ya mji wa arusha
 
Nachukia sana watu wanokuja na copy and paste bila kutupa source

Watu wanakushambulia huna la kujibu sababu tu umeiba kazi ya watu bila kusema

Umeondoa ladha nzima ya hoja kwa sababu tu hujaweka source

Watu wanahitaji kujua kama ni mawazo yako au ya mwingine ili wawe kwenye nafasi nzuri ya kuijadili hoja

BTW nadhani Mh Mbowe alisha litole ufafanuzi wa kina baada ya uongozi mzima wa CDM kupata ushauri wa kitaalamu wa wanasheria wake,wadau wengi wamelifafanua hili kwa kina
 
Mkuu itendee haki hii habari kuna sehemu nimeisoma hii habari weka chanzo.
 
Strategic thinking Mwanzoni Hupingwa ila mwishoni hueleweka na kukubalika e.g. Slaa kugombea urais na kuacha Ubunge.
Mara nyingi maamuzi ya vichwa makini huwa tofauti na matarajio ya wengi ila baadaye umakini wao hujidhihirisha bayana. Usichezee vichwa ndani ya CDM.
 
Back
Top Bottom