KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,139
Wengi bado tuna kumbukumbu nzuri ya kilichotokea katika mchakato wa kuwapata wawakilishi wa viti maalum vya kina mama na vijana ndani ya CHADEMA wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ilikua aibu tupu.Waumini wa demokrasia tusingependa kuona chadema inatia tena aibu kwenye mchakato wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na mpiganaji Regia Mtema.
Tunajua yapo majina tayari ya wanaopaswa kuchukua nafasi hiyo kule tume ya uchaguzi kwa mujibu wa taratibu,hivyo basi tunaomba haki itendeke ndani ya chama hasa tukijiamisha ya kwamba chadema kama jina lake lilivyo ni chama cha kidemokrasia zaidi kuliko kisultani.
Nafasi hii itapendeza ikienda kwa mtoto wa mkulima kama alivyokuwa marehemu,sio lazima iende tena kwa watoto ama "wake" wa vigogo ndani ya chadema.Tunasema hivi kwa kuwa kuna dalili za kamchezo hako kuweko sana chadema na tumeshasikia tetesi kuna wake wa wakubwa huko wanaotajwa tajwa kumrithi marehemu na pia upo ushahidi uliozaa manung'uniko ya kuwepo kwa upendeleo wa ndugu na watoto wa vizito "kupewa" nafasi,mfano wapo watu sio wengi wanaolalamika na kudai watoto ama ndugu wa vigogo mfano ndesamburo,zitto n.k.
Walipendelewa kupata nafasi hizo kutokana na majina ya wakubwa hao..hili lisirudiwe kumrithi Regia.