KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,139
- Thread starter
- #61
Ndugu kuna watu hawataki hilo,yaani mtu hatakiwi kuhojihoji,vinginevyo anaambiwa katumwa na Nape yaani watu wamekuwa ni misukule ya vyama.
Hawajui kwamba 2015 Chama chenye kura nyingi ndio kitachoshinda na sio chenye kejeli
nyingi.
Mtu anapotoa comment kinyume na chama siku zote mwanachama anapaswa atoe maelezo kwa muhusika bila kuchoka ili mwisho wa siku ahamie kwenye chama chako,
ukijua kwamba kura moja ni dhahabu sasa hapa wanatukana na kukejeli wakitegemea 2015 watajitosheleza wenyewe,wakati ili upinzani ushinde ni lazima wapate ushindi wa Kimbunga.
Kifupi uchanga bado uko mwingi sana saana.
Ndio maana nimeamua ku dedicate time yangu ya kutosha kuwafundisha namna ya kufanya siasa hawa vijana "wanaojituma" humu kwa ajili ya chadema,wataelewa tu hata kwa kuwaburuza ikibidi,chama kimekuwa kikifanya vibaya kwenye chaguzi mbalimbali wakati mwingine kutokana kuwa na makada wa aina hii uliyoizungumza hapo juu,mfano kuna mmoja kaniita mimi mkata majani ya ng'ombe twice!yeye anaona kanikomesha mimi lakini anashindwa kuelewa hesabu rahisi tu kwamba kuna wakata majani ya ng'ombe wangapi kama mimi hapa nchini na je kwa kauli yake hiyo anadhani umaarufu wa chadema kwa wakata majani ya ng'ombe hautaathirika?sasa utaona ni suala la kutokufikiri tu hapa,anadhani kura yake tu na ya watu walio na maisha bora ndio itatosha kuipa ushindi cdm,ccm wanawashindia hapo ndugu zangu hawa lakini bahati mbaya hata wakishindwa huwa hawaji hapa kuambiana ukweli bali wanakuja hapa na visingizio vya kuibiwa kura kutwa wanaibiwa kura wao tu,lakini ukiwaambia mbona mzee wangu ndesamburo pale moshi au zitto kabwe kule kwake haibiwi kura zake,wanakaa kimya!