Chadema isitie aibu mrithi wa Regia!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
Wengi bado tuna kumbukumbu nzuri ya kilichotokea katika mchakato wa kuwapata wawakilishi wa viti maalum vya kina mama na vijana ndani ya CHADEMA wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ilikua aibu tupu.Waumini wa demokrasia tusingependa kuona chadema inatia tena aibu kwenye mchakato wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na mpiganaji Regia Mtema.

Tunajua yapo majina tayari ya wanaopaswa kuchukua nafasi hiyo kule tume ya uchaguzi kwa mujibu wa taratibu,hivyo basi tunaomba haki itendeke ndani ya chama hasa tukijiamisha ya kwamba chadema kama jina lake lilivyo ni chama cha kidemokrasia zaidi kuliko kisultani.

Nafasi hii itapendeza ikienda kwa mtoto wa mkulima kama alivyokuwa marehemu,sio lazima iende tena kwa watoto ama "wake" wa vigogo ndani ya chadema.Tunasema hivi kwa kuwa kuna dalili za kamchezo hako kuweko sana chadema na tumeshasikia tetesi kuna wake wa wakubwa huko wanaotajwa tajwa kumrithi marehemu na pia upo ushahidi uliozaa manung'uniko ya kuwepo kwa upendeleo wa ndugu na watoto wa vizito "kupewa" nafasi,mfano wapo watu sio wengi wanaolalamika na kudai watoto ama ndugu wa vigogo mfano ndesamburo,zitto n.k.

Walipendelewa kupata nafasi hizo kutokana na majina ya wakubwa hao..hili lisirudiwe kumrithi Regia.
 
Subirini, tusije tukaingilia chombo au mamlaka yenye maamuzi.
Naamini hiyo mamlaka itafanya uteuzi wa haki bila ubaguzi. Ila kwa maslahi ya taifa na chama, inaweza kufanya uteuzi wenye kuudhi wachache kwa maslahi ya wengi!
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki CHADEMA
 
Lazima kuwakumbushe nao ni binadamu,upo udhaifu wa kibinadamu,ndio tunakumbushana kilichotokea kwenye mchakato wa viti maalum ndani ya chadema kwenye uchaguzi mkuu,kila mkubwa alijaribu kuhakikisha mtu mwenye mahusiano nae anapta nafasi.Hayo mambo lazima yazungumzwe kwani yapo,ni kama hili suala la kumrithi Jemeriah sumari tunavyolizungumzwa even kabla ya hajazikwa,ni kwao tupende tusiprnde tutakua nalo!
 
Tunahitaji busara na umakini mkubwa utumike ili mtuletee kiongozi shupavu bila upendeleo wa aina yeyote! Kiongozi atakaekuwepo kwa ajili ya wananchi wake na sio kwa ajili yake au kwa ajili kachaguliwa na chama. Daima tusonge mbele na tusirudi nyuma!
 
nashukuru wadau tukisaidie hiki chama hata kam hakitachukua dola angalao kibwebweke kasi ya ufisadi ipungue maana wakti kiwira na epa zinatokea upinzani ulikuwa umeuliwa na mkapaism. pia tuwasidie kwa namna tutakavyoweza wasiangukie shimo la NCCR YA MREMA NA CUF YA MAALIM.
 
Hilo ndo tatizo la kutojua taratibu na kanuni zinazozingatiwa katika hoja unayoijadili,Ktk mchakato wa kumpata mrithi wa Regia kwa sasa Chadema hawana maamuzi mapya tena isipokuwa Tume humtangaza kuwa mbunge wa kurithi mtu anayefuatia katika orodha ilokwishawasilishwa awali kutoka pale walipokomea kutokana na idadi ya viti vya CHADEMA.

Ktk uchaguzi mkuu uliopita, isipokuwa ikiwa mtu huyo anyefuatia amekoma uanachama,amefariki au amepoteza sifa zinazomfanya aendelee kuwa mwanachama,watateua anayefuatia tena kutoka orodha ileile ya awali na ikiwa hana pingamizi lolote la chama lihusulo uanachama wake ndiye atakayetangazwa na tume.ACHA UMBEYA WAKO,UMEJAA HILA TUPU KAMA NYOKA,
 
itakuwa ni mistake kubwa kwa chadema kuiachia NEC iwachagulie mbunge kwa sababu mbili.

1. uchaguzi wa mwaka 2010 ulishakwisha hivyo huwezi kutumia matokeo ya uchaguzi uliokwisha kama vile ambavyo
huwezi kutumia matokeo ya ucahguzi wa arumeru mashariki kuipa chadema kiti cha ubunge utaitishwa uchaguzi
ili kila mtu apewe nafasi ya kugombea kwani hiyo demokrasia.

2. Regia Mtema alikuwa ni mbunge wa morogoro hatuna uhakika huyo aliye kwenye listi anatokea kama anatokea morogoro
itakuwa vyema lakini kama hatoki morogoro na hasa kilombero itakuwa ni kuwatupa watu wa kilombero waliokipa chama
cha chadema kura nyingi sana mwaka 2010. kwahiyo naomba musiwaangushe watu wa kilomebero warudishieni heshima
yao watu kilombero na ninammni mwaka 2015 watairudisha heshima hiyo kwenu.
 
Can anybody gues nani alikuwa anafuatia,

Hebu niambie Dr. (Phd) W. Slaa, Ninaomba awe.....................

Tunahitaji watu wenye hofu ya Mungu, sio tuende kwa nguvu za giza tu, hii nchi inamhitaji Mungu na watu wenye hofu yake, watsksoendas mbele zake wakilia kwa ajili ya TZ.
 
Tayari anaemfuata Regia ni diwani wa Karatu kwa Mujibu wa Tume,hayo hayapo ndani ya Uwezo wa Chadema tena ni tume baada ya Chama kupeleka majina zamaani kwa Mpangilio
 
Tayari anaemfuata Regia ni diwani wa Karatu kwa Mujibu wa Tume,hayo hayapo ndani ya Uwezo wa Chadema tena ni tume baada ya Chama kupeleka majina zamaani kwa Mpangilio

Mkuu Asante kwa ufafanuzi mzuri
 
Subirini, tusije tukaingilia chombo au mamlaka yenye maamuzi.
Naamini hiyo mamlaka itafanya uteuzi wa haki bila ubaguzi. Ila kwa maslahi ya taifa na chama, inaweza kufanya uteuzi wenye kuudhi wachache kwa maslahi ya wengi!
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki CHADEMA
Nilidhani mamlaka ipo chini ya watu/umma.
 
Ni vema kusubili na kuona kitakachoamliwa,si vizuri kutoa lawama kabla ya maamuzi kufanywa!
 
Ni vema kusubili na kuona kitakachoamliwa,si vizuri kutoa lawama kabla ya maamuzi kufanywa!
Tuantoa tahadhari kabla ya hatari ili kama kuna mchezo wahusika wanataka kuucheza wajue watu tuko macho,hiyo ya kututaka tusubiri mpaka maji yafike shingoni ndio tujue kumbe tunazama haisadii sana.
 
Tuantoa tahadhari kabla ya hatari ili kama kuna mchezo wahusika wanataka kuucheza wajue watu tuko macho,hiyo ya kututaka tusubiri mpaka maji yafike shingoni ndio tujue kumbe tunazama haisadii sana.

Kakate Majani ya Ng'ombe Mkuu maana its seems that is what you know better
 
Hilo ndo tatizo la kutojua taratibu na kanuni zinazozingatiwa katika hoja unayoijadili,Ktk mchakato wa kumpata mrithi wa Regia kwa sasa Chadema hawana maamuzi mapya tena isipokuwa Tume humtangaza kuwa mbunge wa kurithi mtu anayefuatia katika orodha ilokwishawasilishwa awali kutoka pale walipokomea kutokana na idadi ya viti vya CHADEMA.

Ktk uchaguzi mkuu uliopita, isipokuwa ikiwa mtu huyo anyefuatia amekoma uanachama,amefariki au amepoteza sifa zinazomfanya aendelee kuwa mwanachama,watateua anayefuatia tena kutoka orodha ileile ya awali na ikiwa hana pingamizi lolote la chama lihusulo uanachama wake ndiye atakayetangazwa na tume.ACHA UMBEYA WAKO,UMEJAA HILA TUPU KAMA NYOKA,

Mkuu unafikiri jamaa hajui huu utaratibu? Kama angekuwa anajua baada ya kusoma post yako angeacha kuendeleza speclulations za Kipumbavu hapa! Huyu jamaa analipwa na hii ni kazi ya ziada ila inamsaidia kuongeza kipato maana mishahara ya wakata Majani si unaijua Mkuu. Kwa Uzi huu Msela mkono unaenda Kinywani
 
Back
Top Bottom