Chadema isitie aibu mrithi wa Regia!

Tukumbushane tu Mhe Mbatia alipofariki na Mch Dr Lwakatare kuchukua nafasi yake, ilikuwaje? sioni kama kuna haja ya kupoteza kuchangie thread hii.
 
Bila shaka anayefuatia atakuwa ni Josephina Mmbushi slaa. sioni hata cha kujadili hapa kwani hili lipo wazi. kwani ndo pekee aliyebaki. wenzake akisa rose slaa, christina lisu, lucy oweya etc tayari ni wabunge. this chama cha democrasia. demecrasia ya kweli inaanzia kwa viongozi kwa waongozwa baadaye na hasa wakati wa kuwapigia kura kwa mwanvuli wa nguvu ya umma. Period.
 
kama ni majina ya NEC list ya zamani hii hapa

Rachel Mashishanga (24), Sabrina Sungura (25), Rebecca Mngodo (26), Cecilia Pareso (27), Subira Waziri (28), Leticia Musore (29), Helen Kayanza (30).

rachel mashishanga ni mbunge.


 
  • Thanks
Reactions: SG8
mteule atakayechukua nafasi ya rejia atatoka kaskazini.
ni kweli atatoka kaskazini kwa mujibu wa orodha iliyoko tume.sasa cha ajabu nini? au ndo yale maneno yenu? ukiwa na nia mbaya daima utakuwa busaraless.
 
Yatatumika majina yale yale yaliyokwisha pendekezwa na Cdm na kupelekwa tume kwa uteuzi
 
Wengi bado tuna kumbukumbu nzuri ya kilichotokea katika mchakato wa kuwapata wawakilishi wa viti maalum vya kina mama na vijana ndani ya CHADEMA wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ilikua aibu tupu.Waumini wa demokrasia tusingependa kuona chadema inatia tena aibu kwenye mchakato wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na mpiganaji Regia Mtema.

Tunajua yapo majina tayari ya wanaopaswa kuchukua nafasi hiyo kule tume ya uchaguzi kwa mujibu wa taratibu,hivyo basi tunaomba haki itendeke ndani ya chama hasa tukijiamisha ya kwamba chadema kama jina lake lilivyo ni chama cha kidemokrasia zaidi kuliko kisultani.

Nafasi hii itapendeza ikienda kwa mtoto wa mkulima kama alivyokuwa marehemu,sio lazima iende tena kwa watoto ama "wake" wa vigogo ndani ya chadema.Tunasema hivi kwa kuwa kuna dalili za kamchezo hako kuweko sana chadema na tumeshasikia tetesi kuna wake wa wakubwa huko wanaotajwa tajwa kumrithi marehemu na pia upo ushahidi uliozaa manung'uniko ya kuwepo kwa upendeleo wa ndugu na watoto wa vizito "kupewa" nafasi,mfano wapo watu sio wengi wanaolalamika na kudai watoto ama ndugu wa vigogo mfano ndesamburo,zitto n.k.

Walipendelewa kupata nafasi hizo kutokana na majina ya wakubwa hao..hili lisirudiwe kumrithi Regia.
Kama CHADEMA kuna upendeleo bila vigezo kuzingatiwa huyo mtoto wa mkulima Regia alipataje nafasi? au nae ni mtoto, mke au kimada wa kigogo. Kama Regia ni mtoto wa mkulima na alipata nafasi basi ujue chadema hamna tatizo. Vigezo vilivyotumika last time naviunga mkono na ndio vimeleta wabunge wenye uhai ukilinganisha na wabunge wa viti maalum ccm. Ktk bunge la sasa huwezi kupeleka wabunge wa darasa la saba maana hawawezi kwenda na kasi ya chadema.
 
Wengi bado tuna kumbukumbu nzuri ya kilichotokea katika mchakato wa kuwapata wawakilishi wa viti maalum vya kina mama na vijana ndani ya CHADEMA wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ilikua aibu tupu.Waumini wa demokrasia tusingependa kuona chadema inatia tena aibu kwenye mchakato wa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na mpiganaji Regia Mtema.Tunajua yapo majina tayari ya wanaopaswa kuchukua nafasi hiyo kule tume ya uchaguzi kwa mujibu wa taratibu,hivyo basi tunaomba haki itendeke ndani ya chama hasa tukijiamisha ya kwamba chadema kama jina lake lilivyo ni chama cha kidemokrasia zaidi kuliko kisultani.

Nafasi hii itapendeza ikienda kwa mtoto wa mkulima kama alivyokuwa marehemu,sio lazima iende tena kwa watoto ama "wake" wa vigogo ndani ya chadema.Tunasema hivi kwa kuwa kuna dalili za kamchezo hako kuweko sana chadema na tumeshasikia tetesi kuna wake wa wakubwa huko wanaotajwa tajwa kumrithi marehemu na pia upo ushahidi uliozaa manung'uniko ya kuwepo kwa upendeleo wa ndugu na watoto wa vizito "kupewa" nafasi,mfano wapo watu sio wengi wanaolalamika na kudai watoto ama ndugu wa vigogo mfano ndesamburo,zitto n.k.

Walipendelewa kupata nafasi hizo kutokana na majina ya wakubwa hao..hili lisirudiwe kumrithi Regia.

Nyie ndo marehemu kafariki na bado yuko Hospitali, mkisikia huku nyumbani mnaanza kugawana mali alizoacha mwe!!!!!!
 
kila chama kina taratibu zake za kuchagua wabunge wa viti maalum, huu mjadala sio relevant kwan vigezo vilivyotumika kumpata kamanda regia vitatumika kumpata mrith wake bila kujal atatoka pande gan ya tanzania.
 
kama ni majina ya NEC list ya zamani hii hapaRachel Mashishanga (24), Sabrina Sungura (25), Rebecca Mngodo (26), Cecilia Pareso (27), Subira Waziri (28), Leticia Musore (29), Helen Kayanza (30).rachel mashishanga ni mbunge.
Ni Cecilia Masore au Subira Waziri, Sabrina na Rebecca Mngodo tayari ni Wabunge
 
watanzania wanaanza kuwawaamini kama tunaitaka tanzania tusiangaliane usoni tufuate taratibu kupata viongozi wetu kujuana ukigogo ufisadi ndio vitu vilivyotuondoa ccm mkivikaribisha cdm tutawamwaga nyinyi si mama zetu
 
Kumbukumbu ipi hv we unajua mizengwe ambayo hutumika na CCM kupata hawa wabunge wa viti maalumu? Chadma ni chama ambacho kwa hilo walijitahidi sema watu tumejaa hila kwani kama mtu ni ndugu na viongozi wa chadema hawaruhusiwi kuwa wabunge? mbona hauhoji mtu kama zainabu Kawawa ambaye najua yeye alifight hakubebwa, haya kina Ana Abdalah na wengine wengi tu. Chadema walitumia mtaalamu mshauri bwana Kitila Mkumbo na waliweka vigezo baadhi ya akina mama walidhani ukiwa kiongozi wa juumuiya basi inakuwa first priority ndo maana mkti wa wanawake chadema alihama kwa kuwa alikosa sifa hizo na akatoka na shutuma nzito.

CHADEMA walichofanya cha kwanza ni kuwa akina mama wote waliogombea ndo walipewa first priority kwa kwanza kuthubutu kuingia kwenye mapambano jukwaa na ndo kilichompatia pia na Marehemu Regia Ubunge. ni ile nguvu na uthubutu wake wa kujitokeza kugombea ndo maana wanawake nadhani wote waliogombea ubunge kwa chadema walipokosa wamepewa viti maalumu. Hata Mdee angekosa angepewa maana walishaonyesha ile sense ya leadership kumbuka Rose Kamili ambaye alihama CCM akiwa diwani na akagombea matokeo yalikuwa na utata nadhani Mh Nagu alitangazwa na tume. Hivyo tuache upashkuna na tena wewe thread nyingi ni za kimalaria sugu nashangaa unapojifanya unawahurumia chadema. Mimi si cdm lkn ni mfuatiliaji

Nashukuru kwa mchango wako ila punguza jazba,lazima muwe challenged cuz it's a political party.Kitu kingine ina maana ccm ndio role model wa cdm? kwanini mnapenda kujilinganisha na ccm kwa kila jambo?huo ni unyonge.Ina maana ccm wakikosea kitu na nyie lazima muwaige?nyie inabidi muwe tofauti na ccm kidogo.

Kuhusu wanawake waliojaribu bungeni ndio waliopewa kipaumbele kidogo nina mashaka labda kama utaniondoa mashaka hayo.Nakuuliza hivi dadake ZITTO na Mtoto wa mzee ndesamburo waligombea majimbo gani na gani hapa nchini then wakaanguka halafu ndio wakapewa special seats for second time?kumbuka Zitto na Ndesamburo ni wajumbe wa CC ya chadema!
 
Ndio matatizo ya waafirka siku zote kugombania URITHI. Kinachofanyika hapa hakina tofauti kabisa na mila chafu ya kugombania urithi wakati ndugu, jamaa namarafiki bado wapo ktk maombolezi..Sijui nani aloturoga Miafrika!
 
Ndiyo tatizo la kushiriksha masaburi katika kutoa hoja. Bosi wako washamlambisha sumu huko Mwanza, sijui nani atakuwa anawapa posho za kuleta upupu hapa jamvini.

kumbe tradition ya humu ni lazima uwe na bosi ?hii sikuifahamu kumbe mimi nimeingia kichwa kichwa ngoja nimtafute bosi wangu na mimi!kwani wewe bosi wako nani?
 
Tukumbushane tu Mhe Mbatia alipofariki na Mch Dr Lwakatare kuchukua nafasi yake, ilikuwaje? sioni kama kuna haja ya kupoteza kuchangie thread hii.

Huoni kama ipo haja ya kuchangia baada ya kuchangia sio?
 
Mkuu unafikiri jamaa hajui huu utaratibu? Kama angekuwa anajua baada ya kusoma post yako angeacha kuendeleza speclulations za Kipumbavu hapa! Huyu jamaa analipwa na hii ni kazi ya ziada ila inamsaidia kuongeza kipato maana mishahara ya wakata Majani si unaijua Mkuu. Kwa Uzi huu Msela mkono unaenda Kinywani

kwani alichokuudhi nini babaangu?mbona umemkazania namna hiyo amekushika pabaya nini?au na wewe ni mmoja wa wanaokinyatia kiti cha marehemu kwa kutumia "mbeleko" ya mjomba ambae ni kigogo wa chadema sasa unaona jamaa anawashtua waliolala na kuhatarisha ulaji wako?na hivi iko chama chenu hakitaki wakata majani ya ng'ombe kumbe?mtuambie mapema tujitoe twende kwenye vyama vya wakulima na wafanyakazi tukiwemo wakata majani ya ng'ombe zenu huko uzunguni kwenu!
 
watanzania wanaanza kuwawaamini kama tunaitaka tanzania tusiangaliane usoni tufuate taratibu kupata viongozi wetu kujuana ukigogo ufisadi ndio vitu vilivyotuondoa ccm mkivikaribisha cdm tutawamwaga nyinyi si mama zetu

Ndugu kuna watu hawataki hilo,yaani mtu hatakiwi kuhojihoji,vinginevyo anaambiwa katumwa na Nape yaani watu wamekuwa ni misukule ya vyama.

Hawajui kwamba 2015 Chama chenye kura nyingi ndio kitachoshinda na sio chenye kejeli
nyingi.


Mtu anapotoa comment kinyume na chama siku zote mwanachama anapaswa atoe maelezo kwa muhusika bila kuchoka ili mwisho wa siku ahamie kwenye chama chako,
ukijua kwamba kura moja ni dhahabu sasa hapa wanatukana na kukejeli wakitegemea 2015 watajitosheleza wenyewe,wakati ili upinzani ushinde ni lazima wapate ushindi wa Kimbunga.

Kifupi uchanga bado uko mwingi sana saana.
 
Back
Top Bottom