Duble Chris
JF-Expert Member
- May 28, 2011
- 3,481
- 564
Si hawa hawa walio toa tamko/agizo la serikali kushusha gharama za mafuta ya taa nini kimetokea badaa ya hapo
imetoa msimamo wake kama ifuatavyo:-
[*=left]Linapotekelezwa jambo lolote kwa kigezo cha ugumu wa maisha au kupanda kwa gharama za maisha, ni lazima jambo husika lilenge kutatua ugumu huo wa maisha kwa makundi yote katika jamii na si kwa makundi machache ndani ya jamii.
[*=left]Kwa kuongeza kiwango hicho cha posho kwa wabunge ni kuongeza pengo/tofauti ya mapato kati ya wenye nacho na wasionacho katika jamii yetu hasa kwa kuegemea baadhi ya makundi.
[*=left]Bunge ni chombo muhimu cha kutunga sheria, kinapoibuka na madai kwamba sababu za kuongezeka kwa posho hizo kunatokana na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma kama alivyoainisha Spika wa Bunge, ndiyo inasababishahofu na mashaka miongoni mwa Watanzania. Na kwa kweli swali kubwa kwa Watanzania hao ni je, maisha yanapanda Dodoma pekeake na kwa wabunge tu?
Mnyonge mnyengeni lakini haki yake mpeni. Kwa tamko hili nimefurahishwa na CCM kuwaunga mkono wananchi dhidi ya ubinafsi wa wawakilishi wetu bungeni. Kwani wanaangalia masilahi yao binafsi badala ya uwatetea watumishi wote wa umma. Licha ya posho hizo kulalamikiwa na wabunge wa upinzani na kada mbalimbali nchini hapo awali, lakini wabunge wamekuwa kama wameweka pamba masikioni wakiongozwa na Speaker wao Anna Makinda kujitajirisha kupitia bosho za vikao na biya haya wanazidi kuongeza kiwango cha posho hizo zaidi ya asilimia 80.
Mkuu umesema ukweli, ila huyu kijana ameanza mbali kuzikataa hizi posho https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/195862-ukisikia-pinda-ni-mnafiki-ona-sasa-haya.htmlJanuary zikatae posho kwa vitendo kama alivyofanya Zitto Kabwe, unaongea sana mpaka tunashindwa kujua kama kweli unamaanisha. Hapo hakuna cha kujadili hizo posho ni wizi.
Naamini kuwa hapa JF kuna magreat thinkers, lakini pia naamini hapa JF kuna watu ambao hata kama siyo great thinkers lakini wanaweza kutoa mchango muhimu kwa ustawi wa nchi yetu.
Kwa maana hiyo basi ningeomba suala la posho ya wabunge litusaidie kutanua bongo zetu kuona jinsi gani tunaweza kusimamia masuala ya fedha ya nchi yetu (na hili tulifanye kuwa suala muhimu ndani ya katiba yetu). Kwa nini nasema hivi? Nina sababu kubwa zifuatazo:Hizi zinanifanya nione kuwa suala la posho ya wabunge tulitumie kama "eye opener" litufungue tuone jinsi gani tunaweza kuboresha mfumo wetu wa usimamizi wa fedha. Suala la posho litumike kutuonyesha matundu mengine yako wapi?
- Siyo mara ya kwanza kwa wabunge wa bunge letu kujiongezea posho. Mtakumbuka wakati awamu ya nne inaingia wabunge waliomba kuongezewa posho na Spika wa wakati huo akasisitiza. Ingawaje Rais alijibu kuwa wabunge kwa sababu ni watu wazima watakuwa wamesikia kilio cha wananchi, lakini wote tunajua kuwa posho hizo ziliongezwa na wanachi hawakuweza kufanya kitu.
- Sasa hivi wabunge wameongezewa posho, Katibu wa Bunge kwanza alisema hakuna kitu kama hicho lakini Spika baadaye akakiri kuwa jamaa wameshaanza kulipwa posho mpya (ingawaje magazeti mengine wanasema Rais kakataa kusaini, kitu ambacho siwezi kuamini kwa sababu Wizara ya Fedha ilitowaje pesa kwenye kitu ambacho hakijapitishwa na serikali?). Hapo pia wananchi wameishia kuangalia tu na kupiga kelele
- Spika ni kiongozi wa wabunge hivyo yuko pale kwa matakwa ya wabunge. Sasa kama wabunge wanataka posho, je Spika anaweza kuwazuia? Hapa lazima tujiulize huku kwa Spika kuwajibika kwa Wabunge je hakuwapunguzii nguvu Maspika mbele ya wabunge. Suala hapa je nini kifanyike (au kwa maneno mengine wananchi wawe na sauti gani?) linapokuja suala ya maslahi ya wabunge? Kwa mtazamo ni lazima tuwe na chombo ambacho kitakuwa na jukumu la kusimamia maslahi ya viongozi wetu (hapa siyo wabunge tu na viongozi wa mihimili mingine).
- Posho za mhimili wa Mahakama hasa kwa majaji hatuzijui. Wao maslahi yao yanasimamiwa vipi na kwa kiasi gani posho zao zinaweza kudhibitiwa na wananchi. Je kama majaji wakitaka maslahi makubwa je Jaji Kiongozi kwa mfano anaweza kukataa? Na asipokataa nani anayeweza kukataa? (Hapa ningependa kujua posho zao ni kiasi gani pia kuanzia hakimu wa mahakama ya mwanzo hadi Jaji wa mahakama ya rufaa.
- Posho za mhimili wa serikali (yaani wafanyakazi wa serikali kuu kama vile makatibu wakuu, wakurugenzi) ambazo nazo hatuzijui kwa uwazi ni shilingi ngapi. Je ni kwa kiwango gani zinaweza kudhibitiwa na wananchi? Je wakitaka posho zaidi huwa inakuwaje?
- Vile vile posho za viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kama Polisi, Jeshi, Usalama nk ambazo nazo hatuzijui pamoja na maslahi yao. Je ni kwa kiwango gani zinaweza kudhibitiwa na wananchi? nk nk
Nawakilisha