Kwa sura za wanawake na wanaume zilizochangia 120M kwa Rais, hakuna aliyetoa fedha mfukoni hawa wote wamechukua fedha za perdiem na posho za vikao

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Hawa wanawake na wanaume wanaodai kuchangia 120M wametumia posho na fedha za serikali ambazo ni kodi za wananchi.

Wengi wametoka Dodoma na wanalipwa kwa kuwepo nje ya ofisi kikazi. Lakini wengi wao wana ndugu na jamaa wenye kukosa mahitaji muhimu. Wengine wana ndugu wasiomudu huduma za afya huku baadhi wakiwa wamedhulumu lengo waonekane wapo na viongozi wa serikali.

Kwanini tuwaze kumchukulia fomu leo 2024? Pamoja na matatizo yote tuliyonayo tumefanya kampeni kipaombele cha nchi miaka miwili kabla? Tutatumia kiasi gani cha kodi za umma hadi tufike wakati wa uchaguzi?

Hofu hii imetoka wapi? Mbona mapema sana kuanza kampeni? Mbona Marais waliotangulia walikuwa na subira? Kwanini tunataka kumfanya Rais aone kama kuna shida ya kukubalika? Nashauri tupunguze haya mambo yanakwaza wapiga kura kuliko kuwapendeza.....yanakwaza kwa sababu ni sura zile zile zinajigeuza katika majukwaa mbalimbali kwa majina tofauti.....
 
Mwanamke atoe pesa kwa ajili ya mwanamke mwenzake...ahahahaa,hyo biashara inaitwa nipe nkupe....kikubwa tuishi nao kwa akili
 
Nadhani ingekua bora wafanyakazi wa serikali kiraia waondolewe kwenye siasa na wadiwr hata kuwa na haki ya kupiga kura.
Hii ni moja ya njia ya kuondoa mgongano wa masilahi
 
Sijasoma comment na habari yenyewe, ila nachangia kupitia nilichoelewa kutoka kwenye heading.

Mtu anayevaa saa ya tsh 118m, anayetoa 5m kwa kila goli, UNAMCHANGIA shilingi ngapi? Ambayo yeye hana?

Pathetic fools
 
FB_IMG_1648410131191.jpg
 
Back
Top Bottom