CCM yatoa tamko kupanda kwa posho za vikao kwa wabunge

Si hawa hawa walio toa tamko/agizo la serikali kushusha gharama za mafuta ya taa nini kimetokea badaa ya hapo
 
Naomi Kaliuki sijui anasemaje maana alisema hii janja ya CCM ili tuwe busy na posho badala katiba akaongeza kuwa wabunge wanalipwa posho ya sh 50,000/= tu na si 70,000/= wala hizo 200,000/=
 
imetoa msimamo wake kama ifuatavyo:-

  1. [*=left]Linapotekelezwa jambo lolote kwa kigezo cha ugumu wa maisha au kupanda kwa gharama za maisha, ni lazima jambo husika lilenge kutatua ugumu huo wa maisha kwa makundi yote katika jamii na si kwa makundi machache ndani ya jamii.
    [*=left]Kwa kuongeza kiwango hicho cha posho kwa wabunge ni kuongeza pengo/tofauti ya mapato kati ya wenye nacho na wasionacho katika jamii yetu hasa kwa kuegemea baadhi ya makundi.
    [*=left]Bunge ni chombo muhimu cha kutunga sheria, kinapoibuka na madai kwamba sababu za kuongezeka kwa posho hizo kunatokana na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma kama alivyoainisha Spika wa Bunge, ndiyo inasababishahofu na mashaka miongoni mwa Watanzania. Na kwa kweli swali kubwa kwa Watanzania hao ni je, maisha yanapanda Dodoma pekeake na kwa wabunge tu?

Bora Nape umerudi kutoa matamko ya chama maaana tuliambiwa Dodoma ulizuiwa na ulizila

  • Wabunge wa CCM ni wengi bunge je wao haoni haya yote hadi wanapitisha maazimio ya kinyonyaji kama haya
  • Unasemaje kuhusu Spika aliye idhinisha na kulipa malipo ya kidhalimu hata kabla raisi hajasaini
  • Chama kitachukua hatua gani kama agizo hili halitatekelezwa maana maagizo mengi yanatolewa lakini hayatelezwi na cha chama mnapotezea kimtindo eg suala mafuta ya taa bei kushuka
 
Tanzania nchi ya AMANI.

WIZI mtupu!!!!!!

Huku ndio kulewa madaraka alikosema Baba wa taifa.
 
Aibu ya uongezaji posho kwa wabunge wetu kwanza ni sababu za kuongeza posho za spika mama makinda hazina hoja zito ni pumba tu na za kudhalilisha chama cha mapinduzi hivi hapo dodoma ni hotel ngapi zina viwango vya tsh.100,000/= na kuendelea hivi kweli wabunge wote wanakaa huko?? makinda ameipata wapi hilo au amekurupuka kama wakati flani amewahi kuelezwa na mh. Sitta kuwa na tabia za kukurupuka!!! nadhani hilo kwasasa si issue ya msingi iliyo mbele taifa hili wasubiri mbeleni!!! aibu!!!!!!
 
Mnyonge mnyengeni lakini haki yake mpeni. Kwa tamko hili nimefurahishwa na CCM kuwaunga mkono wananchi dhidi ya ubinafsi wa wawakilishi wetu bungeni. Kwani wanaangalia masilahi yao binafsi badala ya uwatetea watumishi wote wa umma. Licha ya posho hizo kulalamikiwa na wabunge wa upinzani na kada mbalimbali nchini hapo awali, lakini wabunge wamekuwa kama wameweka pamba masikioni wakiongozwa na Speaker wao Anna Makinda kujitajirisha kupitia bosho za vikao na biya haya wanazidi kuongeza kiwango cha posho hizo zaidi ya asilimia 80.

Candid scope, hata wewe umenaswa na mtego mbovu kabisa. sikiza, baada ya kuona hoja ya katiba mpya kuasisiwa na upinzani inaungwa mkono na wananchi wengi, ccm wakaidaka, kuipigia debe sana na sasa wanaishia kuburuza, lengo lao ionekana ccm wanawajali watz, hoja ya posho imepingwa vikali bungeni na chadema, wote tumeona, ccm walivyogundua kuwa wananchi wamechukizwa na kuighadhibikia, ccm imejipanga kuudanganya umma kuwa ndiyo inapinga! kumbuka pinda alitetea posho bungeni karibu alie mbele ya wabunge huku mbowe akipinga almanusura mtwange mtu makonde kuonyesha haya masurufu ni batili kwa watz, nimetolea mfano wa viongozi wa chama, achana na kina lusinde sijui shibuda, focus kwa makinda na kashilila ambao ni wana ccm na ni viongozi waandamizi. ccm ingekuwa sahihi kama ingeunga mkono hoja ya wapinzani bungeni, hapa namaanisha chadema, kwa sasa ni mazingaombwe! labda ccm inatekeleza ushauri wa yule jamaa mbuge wa korogwe.
 
"kwenye suala hili la "posho", ambalo hasa ni ile sitting allowance. Some of us are against that. We shouldn't be paid just to go into a meeting! Its part of our job to attend meetings. We're already paid regular salary and, when on duty we get per diems for meals and lodgings. Sitting allowances, NO. Wabunge wengine wana haki ya kuwa na msimamo tofauti. Watoe hoja zao tuzipime tuone kama zina ushawishi" January Makamba

Source: Facebook page yake

Nionavyo
Kama kweli anayoyasema huyu kijana ni ya kweli, basi hili lichama huenda likapata nguvu ya ndani ya mabadiliko. Mwalimu Nyerere alipokuwa akieleza kwa nini yeye aliunga mkono vyama vingi alisema kuwa alifanya hivyo kwa sababu ccm haiwezi kupata msukumo wa ndani ya mabadiliko kwa kuwa kimelewa madaraka na hivyo kuhitaji nguvu ya nje ( upinzani) ili kulitisha. Nadhani vijana kama January wanapaswa kuungwa mkono na wana ccm ili hiki chama kibadilike!!

Uhuru na Kazi
GZ
 
January zikatae posho kwa vitendo kama alivyofanya Zitto Kabwe, unaongea sana mpaka tunashindwa kujua kama kweli unamaanisha. Hapo hakuna cha kujadili hizo posho ni wizi.
 
hizo ni mbwembwe za kutaka kujisafisha mbele ya jamii lakini still ni magamba tu wataleta hoja nyingine kuzipitisha hapa hamna kitu. Nashut down
 
Naamini kuwa hapa JF kuna magreat thinkers, lakini pia naamini hapa JF kuna watu ambao hata kama siyo great thinkers lakini wanaweza kutoa mchango muhimu kwa ustawi wa nchi yetu. Kwa maana hiyo basi ningeomba suala la posho ya wabunge litusaidie kutanua bongo zetu kuona jinsi gani tunaweza kusimamia masuala ya fedha ya nchi yetu (na hili tulifanye kuwa suala muhimu ndani ya katiba yetu). Kwa nasema hivi? Nina sababu kubwa zifuatazo:
  1. Siyo mara ya kwanza kwa wabunge wa bunge letu kujiongezea posho. Mtakumbuka wakati awamu ya nne inaingia wabunge waliomba kuongezewa posho na Spika wa wakati huo akasisitiza. Ingawaje Rais alijibu kuwa wabunge kwa sababu ni watu wazima watakuwa wamesikia kilio cha wananchi, lakini wote tunajua kuwa posho hizo ziliongezwa na wanachi hawakuweza kufanya kitu.
  2. Sasa hivi wabunge wameongezewa posho, Katibu wa Bunge kwanza alisema hakuna kitu kama hicho lakini Spika baadaye akakiri kuwa jamaa wameshaanza kulipwa posho mpya (ingawaje magazeti mengine wanasema Rais kakataa kusaini, kitu ambacho siwezi kuamini kwa sababu Wizara ya Fedha ilitowaje pesa kwenye kitu ambacho hakijapitishwa na serikali?). Hapo pia wananchi wameishia kuangalia tu na kupiga kelele
  3. Spika ni kiongozi wa wabunge hivyo yuko pale kwa matakwa ya wabunge. Sasa kama wabunge wanataka posho, je Spika anaweza kuwazuia? Hapa lazima tujiulize huku kwa Spika kuwajibika kwa Wabunge je hakuwapunguzii nguvu Maspika mbele ya wabunge. Suala hapa je nini kifanyike (au kwa maneno mengine wananchi wawe na sauti gani?) linapokuja suala ya maslahi ya wabunge? Kwa mtazamo ni lazima tuwe na chombo ambacho kitakuwa na jukumu la kusimamia maslahi ya viongozi wetu (hapa siyo wabunge tu na viongozi wa mihimili mingine).
  4. Posho za mhimili wa Mahakama hasa kwa majaji hatuzijui. Wao maslahi yao yanasimamiwa vipi na kwa kiasi gani posho zao zinaweza kudhibitiwa na wananchi. Je kama majaji wakitaka maslahi makubwa je Jaji Kiongozi kwa mfano anaweza kukataa? Na asipokataa nani anayeweza kukataa? (Hapa ningependa kujua posho zao ni kiasi gani pia kuanzia hakimu wa mahakama ya mwanzo hadi jjaji wa mahakama ya rufaa.
  5. Posho za mhimili wa serikali (yaani wafanyakazi wa serikali kuu kama vile makatibu wakuu, wakurugenzi) ambazo nazo hatuzijui kwa uwazi ni shilingi ngapi. Je ni kwa kiwango gani zinaweza kudhibitiwa na wananchi? Je wakitaka posho zaidi huwa inakuwaje?
  6. Vile vile posho za viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kama Polisi, Jeshi, Usalama nk ambazo nazo hatuzijui pamoja na maslahi yao. Je ni kwa kiwango gani zinaweza kudhibitiwa na wananchi? nk nk
Hizi zinanifanya nione kuwa suala la posho ya wabunge tulitumie kama "eye opener" litufungue tuone jinsi gani tunaweza kuboresha mfumo wetu wa usimamizi wa fedha. Suala la posho litumike kutuonyesha matundu mengine yako wapi?

Nawakilisha
 
Naamini kuwa hapa JF kuna magreat thinkers, lakini pia naamini hapa JF kuna watu ambao hata kama siyo great thinkers lakini wanaweza kutoa mchango muhimu kwa ustawi wa nchi yetu.

Kwa maana hiyo basi ningeomba suala la posho ya wabunge litusaidie kutanua bongo zetu kuona jinsi gani tunaweza kusimamia masuala ya fedha ya nchi yetu (na hili tulifanye kuwa suala muhimu ndani ya katiba yetu). Kwa nini nasema hivi? Nina sababu kubwa zifuatazo:
  1. Siyo mara ya kwanza kwa wabunge wa bunge letu kujiongezea posho. Mtakumbuka wakati awamu ya nne inaingia wabunge waliomba kuongezewa posho na Spika wa wakati huo akasisitiza. Ingawaje Rais alijibu kuwa wabunge kwa sababu ni watu wazima watakuwa wamesikia kilio cha wananchi, lakini wote tunajua kuwa posho hizo ziliongezwa na wanachi hawakuweza kufanya kitu.
  2. Sasa hivi wabunge wameongezewa posho, Katibu wa Bunge kwanza alisema hakuna kitu kama hicho lakini Spika baadaye akakiri kuwa jamaa wameshaanza kulipwa posho mpya (ingawaje magazeti mengine wanasema Rais kakataa kusaini, kitu ambacho siwezi kuamini kwa sababu Wizara ya Fedha ilitowaje pesa kwenye kitu ambacho hakijapitishwa na serikali?). Hapo pia wananchi wameishia kuangalia tu na kupiga kelele
  3. Spika ni kiongozi wa wabunge hivyo yuko pale kwa matakwa ya wabunge. Sasa kama wabunge wanataka posho, je Spika anaweza kuwazuia? Hapa lazima tujiulize huku kwa Spika kuwajibika kwa Wabunge je hakuwapunguzii nguvu Maspika mbele ya wabunge. Suala hapa je nini kifanyike (au kwa maneno mengine wananchi wawe na sauti gani?) linapokuja suala ya maslahi ya wabunge? Kwa mtazamo ni lazima tuwe na chombo ambacho kitakuwa na jukumu la kusimamia maslahi ya viongozi wetu (hapa siyo wabunge tu na viongozi wa mihimili mingine).
  4. Posho za mhimili wa Mahakama hasa kwa majaji hatuzijui. Wao maslahi yao yanasimamiwa vipi na kwa kiasi gani posho zao zinaweza kudhibitiwa na wananchi. Je kama majaji wakitaka maslahi makubwa je Jaji Kiongozi kwa mfano anaweza kukataa? Na asipokataa nani anayeweza kukataa? (Hapa ningependa kujua posho zao ni kiasi gani pia kuanzia hakimu wa mahakama ya mwanzo hadi Jaji wa mahakama ya rufaa.

Mimi ndo maana naunga mkono msimamo wa G.lema na CDM kwa ujumla kuwa tatizo ni mfumo unaoruhusu watu kulipana posho haudhibitiki kwa hiyo ni bora posho zifutwe hasa hizi za kukaa tu.Mfumo uliopo haufai na unatajirisha sana senior officers
 
GUD! Naunga nkono hoja!
 
Fedha za budget kwa bunge la Tanzania huwa zinapitia bunge gani.Mimim sijawahi kuona na kusikia matumizi ya bunge yakijadiliwa bungeni na waheshimiwa wabunge.
Tatizo kubwa lililojitokeza katika posho za wabunge ni Viongozi wakuu kutojipanga na kutofautiana,kitu ambacho kwa sasa kinaanza kuwa fasheni kwa serikali ,maana tuliona RAIS ALITOFAOTIANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI kuhusu Jairo.Mama Anne Makinda anatofautiana na kitibu wa bunge juu ya posho.HAPA KULIKONI?
Turudi kwenye ugumu wa maisha kwa wabunge wawapo Dodoma,HIVI ni kweli kuwa ugumu wa maisha upo kwa wabunge pekee ambao mshahara na marupurupu kabla ya nyongeza hii ni zaidi ya Tshs 7,000,000 kwa mwezi?
Hivi mtu anayepata Tshs 7,000,000 akiona ugumu wa maisha apataye Tshs 150,000 ambacho ni kina cha chini, na kwa mujibu wa sheria ya sasa amapaswa kulipa kodi(PAYE) aseme nini?
 
Posho and marupurupu must be tied to the performance and not to be paid just by sitting down that is insane.
can you imagine if the companies were to pay people left and right like the way the bunge is doing, no single company
would have been arround today.
 
tupinge kwanza ndoo tutafute mfumo namna ya kukontroo hizo posho.
hatuwezi kujadili mfumo huku wanazidi kutunyonya!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom