Benki ya Dunia imefichua ukweli kuwa lindi la umasikini linaongezeka kwa watanzania!

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Tofauti na propaganda za serikali ya wanaccm za kila mwaka, kuwa uchumi wa watanzania unakuwa kwa asilimia kubwa kila mwaka, benki ya Dunia imewashushua waendesha propaganda hizo kwa kueleza ukweli kuwa hali ya maisha ya watanzania walio wengi, hususani wale wa hali ya chini, inazidi kudorora, jinsi miaka inavyokwenda mbele.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Benki ya Dunia, inaeleza kuwa watanzania waliokuwa wakiishi katika hali ya umasikini sana, chini ya dollar moja ya kimarekani, imeongezeka kutoka watanzania milioni 14 mwaka 2018 hadi kufikia zaidi ya watanzania milioni 17 mwishoni maa mwaka 2023.

Taarifa hiyo inapingana vikali na taarifa za (kupikwa) zinazotolewa kila mwaka na serikali hii ya CCM, kuwa hali ya maisha ya watanzania inazidi kuboreka kila mwaka!

Wakati watanzania kila mwaka wanaendelea kulalamika kuhusu gharama za maisha kupanda, serikali ya CCM, imeendelea kutupiga propaganda kuwa hali za maisha ya watanzania inazidi kuboreka kila mwaka.

Katika hali halisi, ingawa benki ya Dunia, imekiri kuwa kuna ongezeko la ukuaji wa uchumi nchini wa asilimia kama 5 hivi, lakini imetahadharisha kuwa ongezeko hilo linawafaidisha watanzania wachache ambao ni matajiri sana.

Kwa hiyo Benki ya Dunia imetutegulia kitendawili cha muda mrefu kilichokuwa kinawasunbua watanzania walio wengi kuwa maisha ya watanzania yanazidi kudorora jinsi siku zinavyozidi kusonga mbele.
 
Temeke kwa sasa wananchi wengi wanakula mlo mmoja kwa siku , ugali mtupu kwenye familia unapikwa saa 10 jioni , kila mtu atafute mboga yake

Nakulilia Tanzania
Hayo ndiyo maisha ya watanzania walio wengi.

Watanzania wachache kina Mwigiluuu, ndiyo wanaoogelea kwenye utajiri wa kutisha!😁

Kuna methali ya Kiswahili inayosema, aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
 
Mbona siku hizi mama hamalizi $500 kwa mwezi? Zamani ilikuwa haifiki tarahe 20 ninapokea bili, lakini siku hizi anakaa nazo mpaka paychecks zinaoverlap; nafikiria kupunguza allowance hiyo zisitumike hovyo
Ana watu wangapi wanaomsaidia kuila hiyo allowance?
 
Lakini Bank ya Dunia,on a regular basis,inasema Tanzania inafanya vizuri kiuchumi.

In fact,hilo ndilo jambo lililofanya yule jamaa wa Chadema akamatwe juzi ma kupelekwa kituo cha polisi bandari.

Anaitwa nani yule,Soka,nadhani. Amekamatwa kwa kuikashifu serikali.

Inakuwaje,all of a sudden Bank ya Dunia inatuambia tumfukuze kazi Rais Samia ASAP(as soon as possible)?

Halafu ipo YouTube video nimeiona two months ago inasema Joe Biden amefurahishwa sana na project alizopanga Mama Samia kwa 2024-2028.

Ile video ipo kwenye Facebook account yangu( ingàwa,frankly,I don't remember putting it there).
 
Temeke kwa sasa wananchi wengi wanakula mlo mmoja kwa siku, ugali mtupu kwenye familia unapikwa saa 10 jioni , kila mtu atafute mboga yake , hakuna Chai wala uji asubuhi

Nakulilia Tanzania
Acha uongo na chuki zako dhidi ya serikali, kweli mlo mmoja ili khali debe la mahindi kwa sasa ni sh 8000!!!!?
 
Acha uongo na chuki zako dhidi ya serikali, kweli mlo mmoja ili khali debe la mahindi kwa sasa ni sh 8000!!!!?
8000 kwako nindogo kwawengine kuipata nivigum hata ukiomba wakusaidie hiyo 8000 serikali inachukuwa mchango unaoitwa Tozo kwenge huo msaada wako
 
Temeke kwa sasa wananchi wengi wanakula mlo mmoja kwa siku, ugali mtupu kwenye familia unapikwa saa 10 jioni , kila mtu atafute mboga yake , hakuna Chai wala uji asubuhi

Nakulilia Tanzania
Msosi ushakuwa anasa kwenye nchi hii

  • ma LC300 kila kona ya nchi kwa kila kiongozi kuanzia level ya idara serikalini
  • Discovery ni kwa wale wote walioibukia kipindi cha mama na Forester, CRV, Volvo TC, Highlander, Vanguard, Lexus, Harrier kalio la ngedere, ML, BMW X1, 3 na 5 n.k ikiwa ndo watumishi wenye mianya yao na wafanyabiashara wa kawaida!

- Dualis, Rumion, IST, n.k imekuwa ni kwa wale waliokosa namna ndani ya kizimkazi

Sasa hilo kundi hapo juu, halizidi watu milioni moja kwa Dar es salaam na milioni 5 kwa nchi nzima.

Watu zaidi ya milioni 50 wa hili pande la ardhi, ndio hao wanasubiri ruzuku na makombo yanayobakia mezani baada ya hao wezi kusaza.

Nimesikia kiongozi wao kasema, mihela yote inaelekezwa kuhonga wapiga kura kwenye hizi siku 731.5 sijazo.

Ukiingia kwenye data zao, inflation haijawahi kufika 5, ukiangalia bidhaa moja kubwa inayoadhiri kila kitu, ime-inflate kwa takribani mara mbili na kusababisha kila kitu kitikisike, bado wasomi wanasema inflation ni 3.5%....nadhani mwenzao aliposema kule wanakopewa hayo maarifa ni jalalani, alikuwa 99.99% sawia.
 
Back
Top Bottom