Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 322
- 645
CCM MBEYA MJINI, WAIJIBU CHADEMA
Na Elius Ndabila
Wiki iliyopita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walifanya mkutano mkubwa wa Kampeni kwenye viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya. Mkutano huo ambao ulikuwa ni wa kuomba kura kwa Mh Lisu anaye gombea Urais ulihudhuriwa na watu wengi kiasi kwamba watu wengi mitandaoni walisema CCM Mbeya itaendelea kuisoma namba.
Wakati watu wakiwa busy kujadili uwingi ule wa watu, mimi nilisema ule Umati ulikuwa ni wa kumpokea Lisu na si Sugu au madiwani wa CDM Mbeya Mjini. Nilienda mbali kwa kusema uwingi wa mahudhurio yale tutaupima na uwingi wa watu watakaompokea JPM atakapo kuja Mbeya. Nilisistiza kuwa kuwa ule mkutano haukuwa wa Sugu bali wa Lisu mgombea Urais. Na kwa tafsiri rahisi ule mkutano ulihudhuriwa na watu wa Wilaya zote. Nilisema ili tujue bado Sugu ana nguvu Mbeya aitishe mkutano wa kwake pale uwanjani ili tuone kama atapata idadi ile ya watu ambayo hata hivyo ilikuwa ndogo kuliko iliyowahi kuhudhuriwa uwanjani hapo wakati wa Dkt Slaa na Mh Lowasa.
Jana Chama cha Mapinduzi kupitia kwa mgombea wao wa Ubunge jiji la Mbeya Dkt Tulia Ackson walifanya uzinduzi kwenye uwanja huo huo ambao CHADEMA walifanyia mkutano wa Kampeni za Urais. Ukweli ni kuwa uwanja ulitapika, Uwanja ulijaa pomoni, Uwanja ulikuwa full park. Mkutano wa jana ambao ni wa Mbunge tu ulikuwa sawa kama si zaidi ya ule wa Mgombea Urais wa CDM. Ni dhahiri uwingi ule unaonyesha kuwa Mbeya wana jambo lao na wameamua kuupumzisha CDM. Idadi ile inawakumbusha CCM Mkoa wa Mbeya kuwa Mh Rais JPM atakapokuja inatakiwa mkutano ukafanyike uwanja wa Sokoine kwani kama tu Mbunge ameujaza Ruanda Nzovwe basi Rais patakuwa hapatoshi.
Wakati Dkt Tulia akifanyia mkutano wake katika eneo la wazi na Uwanjani, Mh Sugu amekuwa anavizia mikutano kwenye Vilabu na kwenda kwenye masoko. Jumatatu alifanyia mkutano wake kwenye soko la Maendeleo Iyela na Jana amefanyia kwenye soko la Isanga. Anafanya hivyo ili kuaminisha watu kuwa mikutano yake inakuwa na watu wakati watu wanakuwa kwenye shughuli zao za kibiashara.
Jana CCM walikuwa wanawasha mitambo, na hakika mitambo iliwashwa na imekubali.