Akihojiwa huhusu mafanikio ya CCM katika miaka 50 iliyopita Mchungaji Lusekelo Mzee wa Upako amesema:"Yaani ni sawa na mtu mzima kuvaa nepi; ndiyo nepi ni nguo lakini mtu mzima akivaa nepi anakuwa kichekesho. Haya wanayodai kwamba ni maendeleo ni sawa na mtu mzima kuvaa nepi halafu akaanza kujisifia" mwisho wa nukuu Gazeti la NYAKATI jumapili Octoba 30- Novemba 5 -2011. Pamoja na kwamba mimi si mshabiki au mojawapo wa kondoo wa Mzee wa Upako naona angalizo lake hili kuhusu miaka 50 ya CCM ni chakula cha vichwa(food for thought?) vya wachambuzi hapa JF. Karibuni!