Kamende
JF-Expert Member
- Mar 1, 2008
- 416
- 45
Sijui ugumu wa kuelewa unatoka wapi?
Mch. Lusekelo amesema kuwa CCM imevaa NEPI halafu inajisifia. Sasa humu ndani watu badala ya kujadili hiyo hoja wanamshambulia Mchungaji.
Ni matarajio ya wafikirifu makini kuona kuwa baada ya pastor kusema hayo yangetokea makundi mawili: Moja likiwa linaona kuwa maneno hayo ni ya KWELI na hapo wangeyatumia hata kufukia kutoa maoni namna ya kuikomboa Tanzania dhidi ya mfubao huo. Kundi la pili lingekuwa lile linaloona kuwa maneno hayo ni UONGO. Hawa wangeleta hoja za kuthibitisha kuwa kwa miaka 50 ya uhuru Tanzania imepiga hatua kubwa kama ilivyotarajiwa na au zaidi.
Kimenishangaza tu kwamba hapa katika jukwaa la wafikirifu makini badala ya hoja kujadiliwa wametokea wachangiaji ambao hawataki kujadili hoja hizi bali wanaanza kumshambulia mtoa hoja.
Nitoe tu taarifa kidogo kuhusu WACHUNGAJI WANAOTUMIA MUDA MWINGI KUPAMBANA NA SHETANI. Wachungaji hawa wana utamaduni wa kutangaza ukuu wa MUNGU na ubaya wa SHETANI.
Wanapomwelezea MUNGU wanajaa TABASAMU na UKARIMU mkubwa. Lakini wanapomkemea SHETANI wanakuwa wakali sana na hutoa sauti kubwa. Ni imani ya wengi kwamba huwezi kumhubiri MUNGU usimkemee SHETANI. Na huwezi kumkemea shetani kistaarabu au kiupole. Lazima utumie MAMLAKA.