"CCM imevaa nepi halafu inajisifia"- Mzee wa Upako-Lusekelo

KALABASH

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
493
205
Akihojiwa huhusu mafanikio ya CCM katika miaka 50 iliyopita Mchungaji Lusekelo Mzee wa Upako amesema:"Yaani ni sawa na mtu mzima kuvaa nepi; ndiyo nepi ni nguo lakini mtu mzima akivaa nepi anakuwa kichekesho. Haya wanayodai kwamba ni maendeleo ni sawa na mtu mzima kuvaa nepi halafu akaanza kujisifia" mwisho wa nukuu Gazeti la NYAKATI jumapili Octoba 30- Novemba 5 -2011. Pamoja na kwamba mimi si mshabiki au mojawapo wa kondoo wa Mzee wa Upako naona angalizo lake hili kuhusu miaka 50 ya CCM ni chakula cha vichwa(food for thought?) vya wachambuzi hapa JF. Karibuni!
 
Mzee wa upako aache kutumia lugha ya uchochezi,maana waumini wake wanaweza kugawanyika ndani ya kanisa.hata kama viongozi wa dini watakiwa kuikosoa serikali yetu wanapaswa kutumia lugha ya staha ingawa itakuwa ina uma kwa viongozi walioko madarakani.
 
labda kwa vile hapati ruzuku serikalini kama ilivo kwa makanisa mengine
angekuwa anapata asingebwabwaja kihivo.
 
mbona ccm haijafikisha miaka 50?au anamaanisha miaka 50 ya uhuru wa tanganyika?sijaelewa mkuu.
 
Mzee wa upako aache kutumia lugha ya uchochezi,maana waumini wake wanaweza kugawanyika ndani ya kanisa.hata kama viongozi wa dini watakiwa kuikosoa serikali yetu wanapaswa kutumia lugha ya staha ingawa itakuwa ina uma kwa viongozi walioko madarakani.

Una maana gani unaposema watumie lugha ya staha? Mbona jambo hili liko wazi sana? Ukuaji wa uchumi wa nchi yetu hauwiani na utajiri wa rasilimali tulizonazo. Hivi majuzi Lukuvi amedai pato la taifa limepanda kufikia Tsh. 770,000 kwa mwaka kutoka Tsh 770 wakati wa uhuru. Hajatuambia wakati ule thamani ya pesa yetu ilikuwa na uwiano gani na dola ya marekani. Anajua kuwa thamani ya pato la mwananchi wakati wa uhuru ni kubwa kuliko sasa!

Hakuna lugha mbadala ya kumuita fisadi, mwizi nk. Serikali yetu ni legelege, hakuna lugha ya staha zaidi ya hiyo.
 
Hawa mabwege lazima waambiwe ukweli. Lugha za staha na kuambiana "huyu ni mwenzetu" ndizo zimetufikisha hapa tulipo. Lazima tudai mabadiliko kwa hali na njia yoyote ile.
 
Akihojiwa huhusu mafanikio ya CCM katika miaka 50 iliyopita Mchungaji Lusekelo Mzee wa Upako amesema:"Yaani ni sawa na mtu mzima kuvaa nepi; ndiyo nepi ni nguo lakini mtu mzima akivaa nepi anakuwa kichekesho. Haya wanayodai kwamba ni maendeleo ni sawa na mtu mzima kuvaa nepi halafu akaanza kujisifia" mwisho wa nukuu Gazeti la NYAKATI jumapili Octoba 30- Novemba 5 -2011. Pamoja na kwamba mimi si mshabiki au mojawapo wa kondoo wa Mzee wa Upako naona angalizo lake hili kuhusu miaka 50 ya CCM ni chakula cha vichwa(food for thought?) vya wachambuzi hapa JF. Karibuni!

Siwezi kushangaa kwa hawa wachungaji wa sasa ambao dini leo imekua pazia ili nyuma yake warahisishe maslah yao kwa siri,leo wachungaji ndio wauza unga wakubwa,wachungaji leo wanawania nyazifa mbalimbali ktk siasa,kiukweli jamaa hana jipya!
 
mzee wa upako wewe endelea kufuga ngombe ukamue maziwa mambo ya siasa kwako ngumu mzee wa upako au nauku umetuma namba ya A/C
 
Una maana gani unaposema watumie lugha ya staha? Mbona jambo hili liko wazi sana? Ukuaji wa uchumi wa nchi yetu hauwiani na utajiri wa rasilimali tulizonazo. Hivi majuzi Lukuvi amedai pato la taifa limepanda kufikia Tsh. 770,000 kwa mwaka kutoka Tsh 770 wakati wa uhuru. Hajatuambia wakati ule thamani ya pesa yetu ilikuwa na uwiano gani na dola ya marekani. Anajua kuwa thamani ya pato la mwananchi wakati wa uhuru ni kubwa kuliko sasa!

Hakuna lugha mbadala ya kumuita fisadi, mwizi nk. Serikali yetu ni legelege, hakuna lugha ya staha zaidi ya hiyo.
saafi!
 
Uko sawa kabisa kuhusu kulinganisha mapato ya miaka tofauti.
hapa viongozi wa serikali huwa wananitia kichefuchefu wanapolinganisha uchumi, ukusanyaji wa kodi au maendeleo fulani katika miaka tofauti.
utakuta wanakuambia kodi imepanda kutoka bilioni 200 hadi bilioni 700 katika kipindi cha miaka 10. yaani huu ni usanii mkubwa. hawakuambii pesa imeshuka thamani kwa kiasi gani hvo bil 700 zina thamani gani ssa hivi. utakuta fedha imeshuka mara 3 au nne hvo bil 700 ni sawa tu na bil 200 ya wakati huo ila unapigwa changa la macho kuwa wanafanya kazi nzuri.
 
Una maana gani unaposema watumie lugha ya staha? Mbona jambo hili liko wazi sana? Ukuaji wa uchumi wa nchi yetu hauwiani na utajiri wa rasilimali tulizonazo. Hivi majuzi Lukuvi amedai pato la taifa limepanda kufikia Tsh. 770,000 kwa mwaka kutoka Tsh 770 wakati wa uhuru. Hajatuambia wakati ule thamani ya pesa yetu ilikuwa na uwiano gani na dola ya marekani. Anajua kuwa thamani ya pato la mwananchi wakati wa uhuru ni kubwa kuliko sasa!

Hakuna lugha mbadala ya kumuita fisadi, mwizi nk. Serikali yetu ni legelege, hakuna lugha ya staha zaidi ya hiyo.

Nadhani wakumbuka enzi za Mikingamoooo!!! walikuwa wana itwa wahujumu uchumi nadhani hilo ndilo walitaka au?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom