S.Liondo
JF-Expert Member
- Apr 20, 2011
- 3,408
- 1,712
Kwa hali ilivyo hivi sasa ndani ya CCM, ni dhahiri kwamba wanachohitaji sio kujivua gamba, bali wanahitaji kufanyiwa upasuaji mkubwa. Kwa hakika CCM inaumwa tena Ugonjwa wake ni wa kufisha. Upasuaji wa kuitibu CCM ni kuruhusu sheria ichukue mkondo wake bila kutazama sura wala vyeo vya wahusika. Ikiwa watafanya hivyo basi uwezekano wa wao kurejesha nguvu yao ya awali ya kisiasa ni 98% kama sio 100%. Kinyume cha hapo ni anguko tu iwe in ndani ya muda mfupi au baada ya muda mrefu. Matibabu ya juu juu kama wanayoyafanya hivi sasa hayatasaidia sana maana kila siku wapinzani watakuwa na sababu ya kuwanyooshea kidole. Huwezi kutibu saratani kwa kupaka dawa na kufunga bandeji. Ni lazima kiungo kilichoathirika kikatwe hata kama hiyo inauma. Ninaishauri CCM kufanya kulingana na Ushauri huu vinginevyo wataanguka, na kishindo cha anguko lao kitasikika mpaka nje ya mipaka ya Tanzania.:angry: