CCM: ILIZALIWA, IKAKUA na SASA INAKUFA

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Moja kati ya Cheche alizozitema Mwanasheria mashuhuli inchi Mabere malando Jana ni Kuwa, Ccm ilizaliwa, ikakua na sasa ina kufa. Hivyo basi hainahaja na kuendelea kushangaa inapotafunwa na Makombora ya CDM, inapokosa maamuzi ya Pamoja kati ya Mkubwa na madogo ktk chama, Inaposhindwa kujibu hoja kwa hoja, Uozo wake unyozagaa kwenye vichwa vya watanzania kwa kasi.

Marando,Alitoa mifano ya vifungu vichache vilivyomo kwenye katiba mpya ya kenya mf.Waziri ni lazima asiwe mbunge na nilazima afanyiwe interview na bunge kabla,Pia mbunge yeyote itambidi kuachia ngazi endapo tu hatekelezi wajibu wake,Wakuu wa mikoa na wilaya watachaguliwa na wananchi nasio raisi.

Vivyo hivyo Dr.Slaa alitoa tamko kuwa wanaosema amechanganyikiwa hawakosei,Kwa sababu uwezo wake wa kufikiri na kiusomi upo umbali wa maili mia moja kuliko wana ccm wote.Pia akatuhumu raisi kupewa Phd na UDOM-Kwani Udom bado sana kufikia level hiyo na wanazidi kumuangamiza Jk coz elimu yake ipo kwenye vyeti nasio akili.

Pia akadokeza swala La udini linalong'ang'aniwa na CCM kuwa ni njama za kuwapoteza wananchi kuikosoa ktk mambo muhimu kama Dowans. Akampa pole Jk kwa kuomboleza na Udini wake bila kuchukua hatua(Watoto wakilia, baba akilia nani atatatua tatizo)
Mwisho akahoji Rex attonery ni nani ktk Dowans?alishauri nini serikali kuhusu dowans? Akamalizia kwa kusema atakuja na Bomu la Rex attonery dhidi ya Serikali.

Home work aliyoitoa-Nendeni kwenye kamsi kaangalieni maana ya maneno haya UDINI, DINI, SIASA, KUTOTAWALIKA na MALUMBANO.

CCM INAKATA ROHO, WASOMI NA WASIO WASOMI KAZANENI TUIMALIZIE THEN TUICHIMBIE KABURI KM 1 KWENDA CHINI ILI VIZAZI VIJAVYO VISIISIKIE HATA HARUFU.
 
Udini upo unahitaji kushughulikiwa iwe wameingia madaraka cdm, cuf au ccm...hiyo ni homework lazima wafanye..

Siasa pembeni
 
Dr. Slaa anakwambia udini haushughulikiwi majukwaani. Amemtaka kikwete ajifunze kwa Raisi.

Ally Hassan mwinyi mwaka 1987/1988 UDINI ulishamili kiasi kwamba taifa lilikuwa linagawanyika,But kamwe mzee Mwinyi hakuwahi simama Jukwaani na kuomboleza udini kama kikwete,bali alichukua hatu kwa kukutanisha dini zote kupitia vyombo vyake na kulimaliza kabisa tatizo la udini kipindi kile.

Sasa huyu JK yeye ni udini, udini, udini, udini kamasio kuchochea nini? Yeye ndiye Incharge ktk taifa hili hatakiwi kuomboleza but kuchukua hatua na kulitatua tatizo kama lipo.
 
Haya tumeyataka wenyewe; tumemkubali atutawale kwa kura asilimia 27%-haya ndiyo matokeo-UWT ni wa kubeba lawama ya taifa lote!!!!!!!!!!!!!!!
 
"......Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasiwasi!" (Ukurasa 66), Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Mwl Nyerere, 1993.
 
udini utaisha watu wakielimishwa.....haya mambo ya asilimia hamsini ya form four kufeli ndio yanasababisha hizi topic za udini ziendelee....watu hawaelewi hili wala lile, kufata mkumbo tu na ziro zao.
 
Kichwa cha bandiko lako kinatosha kujibu bandiko hili pasipo kusoma umeandika nini! CCM will be there for many years to come...
 
siku ya kiyama hakuna anayeweza kuamulia! naam, Mungu akisema basi anguko lake huya ni kuu!
 
Wewe jina lako,halileti maana na unachokihusudu.Akina sanga ni gifted na sio kama wewe
 
Nasikitika sana CCM inavyokosa mwelekeo sasa...CCM kwa mawazo ya waasisi ilikua nzuri ...tena sana...pamoja na mambo mengi 'mabaya' waliyofanya ila tusikatae ukeli kua kulikua na mshikamano wa kitaifa...hapakua na mambo ya kipuuzi sana na waliobainika kwenda kinyume walichukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni....pamoja na kwamba wakati ule tulikua kwenye mfumo wa chama kimoja na sasa ni vyama vingi sioni sababu ya Chama hiki kikongwe kupauka hivi...najiuliza maswali mengi sana ,hivi ndivyo tunamuenzi Hayati Sokoine,Nyerere,Dr Filbert Kleruu,Kawawa na wengine wachache waliokua na moyo wa kizalendo?
 
Wananchi wanampinga na kutaka aondoke madarakani yeye anatumia pesa za serikali safarini kwa manufaa ya ufisadi na ccm, huu sio uzembe na kutowajibika? Mawazo ya Kikwete ni kukiua chadema badala ya kutumia muda wake kujenga uchumi wa taifa

GO9G5073.JPG


ccm wakiwa dodoma leo wanatumia pesa za serikali. Matumaini ya watanzania ni kwamba ccm ife na tusahau yote mabaya na maovu yao.
DSC00020.JPG


Upinzani wa wananchi kupinga "Katiba ya ccm" na Hatuta kaa kimya kamwe.
Picha-no-12.jpg


Kikwete wananchi wamekufa Gongo la Mboto yeye akiwa France na Ngereja Kutafauta deals za kifisadi. Ripoti ya aliyojifunza France ikowapi?
03_11_052ew0.jpg


Mauaji ya Gongo la Mboto baada ya Mbagala bila Ripoti wala Uwajibikaji wa serikali ya Kikwete. Hii ni serikali au shirika la wauni
pandehizimabomugongola%2Bmboto.jpg


Kikwete akiwa Ivory Coast na Gbabgo wakati yeye mwenyewe kaiba kura kwa watanzania. Tunataka atoe Ripoti ya safari yake.
jk-ivory-coast.jpg


Siku hiyo hiyo serikali yake haijui kama ufisadi wa ugawaji wa ardhi upo Tanzania. Wananchi wanachinjana Tegeta. Huyu kikwete anamwongoza nani?

Grabbed_Frame_1.jpg


Kikwete alipo amuru polisi wawaue wananchi Arusha. Wafanye tena kama wanataka tumalize sisi wenyewe. Tutampinga Kikwete na ccm mpaka waondoke serikalini.
ameiumiamkeslaa.jpg
 
Back
Top Bottom