Uchawi na Rushwa Vyatawala uchaguzi wa CCM Wilaya ya Muleba

jembe2015

Senior Member
Sep 21, 2014
118
71
Juzi tarehe 5 Oktoba 2017 katika ukumbi wa Waisuka uliopo Muleba, ilitokea hali ya sintofahamu mara baada ya Katibu wa CCM Wilaya ya Muleba Bwana Anatory Nshange kuanguka na kuzimia ghafla mara baada ya kuanza kuhakiki wajumbe wa Mkutano huo.Tangu asubuhi Katibu Nshange alikuwa mzima wa Afya na kama kawaida yake hakutaka mchezo katika kazi yake. Alionyesha uwezo mkubwa ktk kuendesha mkutano ule ili kuepusha mambo yasiyostahili yasitokee. Mfano Kata ya Ibuga ya Muleba Kaskazini kwa Mhe Charles Mwijage ilidaiwa kupenyeza Wajumbe wasio halali katika mkutano. Katibu Nshange akang'ang'ana wote wahakikiwe na wasiostahili kutolewa nje.

Katikati ya zoezi la kuhakiki wajumbe, ndipo ghafla akaanguka chini na kuzimia kama vile alipigwa na radi. Nshange alibebwa akiwa hajitambui na kupelekwa Hospitali ya Kaigara ambapo alikua chini ya uangalizi wa mganga mkuu wa Wilaya Dr Modest Rwakahemula. Watu wengi hasa wajumbe na wgeni waliokuwepo ukumbini walihofia maisha yake.

Hali hii ya Katibu kupigwa na shambulizi lisiloeleweka mbele ya wajumbe zaidi ya 1200 ilileta taharuki kwenye mkutano na zoezi la kuhakiki wajumbe likaishia hapo.

Inasadikika kutokuwahakiki wajumbe kulimsaidia sana mgombea Athuman Kahara na kumpatia ushindi wa mashaka wa tofauti ya kura 15 tu.

Mshindani wake Cosmas Timanywa aliyetarajiwa kushinda kwa vigezo vya sifa uzoefu na umri akabwagwa kwa kupata kura 582 huku Athuman akipata 597.

Habari mitaani Muleba ni kwamba kumbe ili kujihakikishia ushindi Athuman alikwenda kwa mganga wa kienyeji ambaye alimuambia kwamba hapo jukwaani mtu yeyote atakayekuwa kikwazo kwake atapigwa na shambulizi ili aondoke na asimdhuru.

Vijana wa Muleba badala ya kusheherekea ushindi wa Athuman wamepigwa na butwaa na wengi wamechukizwa kwamba kijana huyo aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM kwa vipindi viwili angeliweza kuwa na tamaa ya cheo hicho kiasi cha kwenda kutambika kwa waganga na kuwadhuru waendesha uchaguzi huru na haki.

Wabunge wote wa wilaya ya muleba yani Jimbo la muleba kasikazini (Mwijage ambaye pia ni waziri wa viwanda na bihashara) na muleba kusini (mama Tibaijuka) walikuwepo katika mkutano huo pamoja na mkuu wa wilaya.

Wakati akihutubia mkutano huo Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage ambaye ni Mbunge wa Muleba Kaskazini na aliyesadikika kuwa akimuunga mkono mgombea kijana Athuman alisema maneno yafuatayo ambayo sasa yamekua gumzo na kuwawashangaza wengi mara baada ya kilichotokea,alisema:

"Mdogo wako akianguka siku ya kuoa si kifafa bali ni kwa sababu ya furaha".

Watu wameshangaa kauli hiyo baada ya Katibu kuanguka dakika chache baada ya kutolewa.

Wengine wamechukulia kwamba Team Mwijage ilitaka kushinda kwa gharama yoyote Ile ili kupunguza nguvu ya mama Tibaijuka na team yake almaharufu kama "Team mjengoni" Mbunge wa Muleba Kusini aliyekuwa anamuunga mkono mgombea mzee Cosmas Timanywa kwa madai kwamba kazi ya kukiongoza chama katika Wilaya hiyo kubwa inahitaji busara na hekima. Hiyo ni baada ya mihemuko ya mwenyekiti aliyekuwa anamaliza muda wake Muhaj Bushako akiwa chini ya onyo kali iliyopelekea kuzuiwa kugombea tena kiti hicho.

Waziri Mwijage anasemekana kutofautiana sana na Profesa Tibaijuka katika mtizamo wa mambo kwani Mwijage hupenda Halmshauri kupeleka fedha na miradi mingi zaidi kwenye jimbo lake dogo la Kaskazini ukilinganisha na jimbo kubwa zaidi la Kusini ambalo linapunjwa katika mgao.

Aidha mvutano wa chinichini kati ya Wabunge hawa wawili katika Wilaya moja pia hutokana na historia kwamba Mwijage alipewa uwaziri baada ya Profesa Tibaijuka kukumbwa na Kashfa ya mgao wa fedha za escrow wakati wa Serikali ya awamu ya nne. Mwijage alihofia sana kwamba kama akishinda ubunge tena Mama huyo angeliweza kuchaguliwa kuingia baraza la mawaziri la serikali ya awamu ya tano na yeye Mwijage kuachwa. Hofu hiyo ikamfanya Mwijage kushirikiana na kuwawezesha baadhi ya vijana wa Muleba Kusini akiwemo Muhaj(mwenyekiti wa zamani wa ccm wilaya) na Athuman (mwenyekiti mpya ) kumpinga na kumuhujumu Mama Tibaijuka wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015 . Hata hivyo hawakufanikiwa. Wananchi wengi walipuuza tuhuma hiyo na kumchagua tena.

Tangu wakati huo Mwijage amekuwa hajiamini na hufadhili kundi la vijana Muleba Kusini kumsumbua Profesa Tibaijuka katika mitandao huku yeye Mwijage akisifiwa sana na vijana hao hao. Shida ni Mwijage kuogopa kivuli cha huyu mama ambaye bado anasikilizwa sana Wilayani Muleba na Mkoa wa Kagera kwa ujumla. Aidha wafanya biashara mashuhuri wa Wilaya hiyo kama Josphat Rweyemamu al maarufu JR wanakuwa upande wa Mama Tibaijuka hivyo kufanya team Mjengoni kuwa na nguvu sana na kuogopwa.

Safari hii Waziri Mwijage alichukua livu maalum ili kuzama jimboni kwake na kuhakikisha kijana wake Athuman anashinda uenyekiti wa wilaya na sifa za Team mjengoni zinapungua. Taarifa zimezagaa Mwijage alitoa fedha kwa Athumani ili kugawa kwa wajumbe nje ya kile kiwango kilichopangwa kutolewa na Wabunge kwa utaratibu wa Chama ambao ni elfu tano za nauli kwa kila mjumbe. Wajumbe kutoka kata ya Kimwani iliyoko Muleba Kusini kwa Mama Tibaijuka walieleza walipewa elfu thelathini kila mmoja na Team ya Athuman. Huku kundi la Athuman likipiga kelele kwenye mitandao kwamba kundi la Mama Tibaijuka linagawa fedha, ni hilo hilo kundi la Athuman lililogawa fedha hadi kwenye maeneo ya ukumbi na ndani ya vyoo. Hali ilikuwa mbaya na Mwendesha Uchaguzi Bi Redempta Majigwa ambaye ni Katibu wa UWT Mkoa wa Kagera kutoa Bukoba kutoa onyo kwamba vitendo hivyo vikome mahala hapo. Mkuu wa Wilaya Muhandisi Richard Ruyango aliwataka Takukuru kufanya kazi yao ingawaje hakuna taarifa kama kuna waliohojiwa.

Hivi sasa hali ya Katibu Nshange inasemekana kuimarika na tayari karuhusiwa na kutoka hospitali.
Akisimulia tukio hilo mara baada ya kupata ahueni katibu Nshange anasema wakati akiendelea na utaratibu wa kuhakiki wajumbe,ghafla aliona kiza kinene na kupoteza fahamu,akaanguka chini na alipo zinduka alijikuta hospitali.

Jambo hili limekua gumzo wilayani muleba na vijiweni,hali inayoacha maswali mengi kwa wananchi.

Je uenyekiti wa mazinga ombwe utaijenga CCM?
 
Kuna mmoja alirogwa ulimi ukavimba na kujaa mdomoni akashindwa kuongea,akabaki kuwaangalia wajumbe tu,mwenzie akaja akajieleza akapeta,ccm inamiliki wachawi kwa asilimia kubwa
 
Back
Top Bottom