CCM: ILIZALIWA, IKAKUA na SASA INAKUFA

Kwa hali ilivyo hivi sasa ndani ya CCM, ni dhahiri kwamba wanachohitaji sio kujivua gamba, bali wanahitaji kufanyiwa upasuaji mkubwa. Kwa hakika CCM inaumwa tena Ugonjwa wake ni wa kufisha. Upasuaji wa kuitibu CCM ni kuruhusu sheria ichukue mkondo wake bila kutazama sura wala vyeo vya wahusika. Ikiwa watafanya hivyo basi uwezekano wa wao kurejesha nguvu yao ya awali ya kisiasa ni 98% kama sio 100%. Kinyume cha hapo ni anguko tu iwe in ndani ya muda mfupi au baada ya muda mrefu. Matibabu ya juu juu kama wanayoyafanya hivi sasa hayatasaidia sana maana kila siku wapinzani watakuwa na sababu ya kuwanyooshea kidole. Huwezi kutibu saratani kwa kupaka dawa na kufunga bandeji. Ni lazima kiungo kilichoathirika kikatwe hata kama hiyo inauma. Ninaishauri CCM kufanya kulingana na Ushauri huu vinginevyo wataanguka, na kishindo cha anguko lao kitasikika mpaka nje ya mipaka ya Tanzania.:angry:
 
S.Liondo.

Umewahi kusikia msemo wa,"Kumpigia mbuzi gitaa?"
That is CCM.
 
Kwa jinsi move ya kamati mpya teule ilivyo ni dhairi shairi ccm inasombwa na mvua zijazo za Elnino ...historia yao tutaipeleka jumba la makumbusho ili vizazi vijavyo vipate kujua kilichohisibu nchi yao
 
"............CCM kinakufa" hii ni nukuu ya sehemu ya makala ya Ansbert Ngurumo. Watanzania tujiulize, je CCM ikifa vyama vya upinzani kwa ujumla wake vitaweza kuziba pengo lake?. Ni wazi kwamba wao wenyewe wataishia kutoana macho. Si tumeshuhudia jinsi walivyovutana katika kuunda kambi rasmi ya upinzani Bungeni. Pia si wapo wengine ndani ya CDM walioanza kuropoka baada ya kukosa uwaziri kivuli? Je wataweza kuunda serikali kweli?

Nawasilisha kwenu.
 
Mkuu ele episode ya MBOWE na ZITTO nani awe Chairman iliisha vizuri kweli au ni viginga vya moto ndivyo vimerudihwa nyuma muda ukufika vitachochewa tena? Thehe thehe thehe, mie nimeuliza tu. Ila nasikia sasa hivi bifu ni kati ya bwana mkubwa MBOWE na SLAA
 
Matokeo yake ndiyo hayo mwingine amefanyiwa upasuaji India, lakini pia niwakumbushe ile ajali ya aliyekuwa Mbunge wa Tarime Chacha Zakayo Wangwe ambaye naye alitaka kuwa Kiongozi wa juu CDM.
 
Mbatia apewa siku 21 kujieleza NCCR

Na Muhibu Said
6th November 2011

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia

HalmashauriI Kuu(NEC) ya Chama cha NCCR-Mageuzi, imempa Mwenyekiti wake, James Mbatia, siku 21 kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na baadhi ya wanachama kwamba, ni pandikizi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndani ya chama hicho.
Agizo hilo ni miongoni mwa maazimio kadhaa ya NEC yaliyofikiwa kwa kauli moja na idadi kubwa ya wajumbe wa halmashauri hiyo, katika kikao chake kilichofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe 50, lakini kinyume cha kawaida, waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuhudhuria.
Azimio hilo dhidi ya Mbatia lilisomwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Samuel Ruhuza katika kikao hicho na limezingatia kanuni za chama zinazotoa fursa kwa mwanachama mtuhumiwa kujitetea.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zinaeleza kuwa hoja kuhusu tuhuma hizo, iliwasilishwa katika kikao hicho na Mjumbe wa NEC kutoka Tanga, Mbwana Hassan.
Hoja hiyo imesainiwa na wajumbe 28 wa halmashauri hiyo, ambao kwa kauli moja wanataka Mbatia ajiuzulu uenyekiti wa chama hicho kutokana na tuhuma zinazomkabili.
Kwa mujibu wa habari hizo, kati ya wajumbe waliohudhuria kikao cha jana, ni wajumbe 10 tu ndio wanaodaiwa kumuunga mkono Mbatia kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho, huku wengine waliosalia wakiwa hawana upande.
Kutokana na agizo hilo, Mbatia sasa anatakiwa kujibu tuhuma hizo na kuwasilisha majibu hayo kwa Katibu Mkuu. Katibu Mkuu baada ya kuyapokea, atawasilisha kwa Kamati ya Maadili ya Chama na kisha kupelekwa katika kikao cha NEC kitakachofanyika Februari, mwakani kwa ajili ya maamuzi.
Habari hizo zinasema kuwa baada ya azimio hilo kupitishwa na NEC, Mbatia aliomba kutendewa haki kwa kupewa muda wa kutosha kujibu tuhuma zinazomkabili.
Imeelezwa kuwa awali, viongozi waliokuwa wamekaa meza kuu walijaribu kuzuia hoja inayohusu tuhuma dhidi ya Mbatia kujadiliwa katika kikao hicho. Hata hivyo, idadi kubwa ya wajumbe walipinga hatua hiyo na kushinikiza ijadiliwe.
Mvutano kuhusu suala hilo uliendelea baada ya Mbatia kugoma kujibu tuhuma zinazomkabili.
Jambo lingine lililotaka kulipua kikao hicho, ni madai kwamba, kulikuwa na mabaunsa waliokuwa wamekodiwa na baadhi ya wanachama kwa lengo la kutisha wajumbe na kuleta vurugu.
Hali hiyo ilimfanya Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali, kutishia kuwasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, ili alete askari kwa ajili ya kuwashughulikia mabaunsa hao.
Mkosamali, ambaye ni mjumbe wa NEC, alifikia hatua hiyo baada ya baadhi ya wajumbe kutaka mabaunsa hao waondolewe, huku baadhi ya viongozi wakipinga suala hilo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Mambo yenyewe ndiyo hayo harafu wapewe nchi hawa???
 
Vyama vyote vya upinzani ni watoto wa CCM kwa sababu vimeanzishwa kutokana na uongozi bora wa ccm; na vinafanya kazi kutokana na makosa ya ccm kwa hiyo bado havijakomaa kuweza kuziba pengo la chama kilichoishi kwa miaka 50.
 
"............CCM kinakufa" hii ni nukuu ya sehemu ya makala ya Ansbert Ngurumo. Watanzania tujiulize, je CCM ikifa vyama vya upinzani kwa ujumla wake vitaweza kuziba pengo lake?. Ni wazi kwamba wao wenyewe wataishia kutoana macho. Si tumeshuhudia jinsi walivyovutana katika kuunda kambi rasmi ya upinzani Bungeni. Pia si wapo wengine ndani ya CDM walioanza kuropoka baada ya kukosa uwaziri kivuli? Je wataweza kuunda serikali kweli?

Nawasilisha kwenu.
Mkuu kwa hali iliyopo na vyama vya upinzani tulivyonavyo sioni pengo likizibwa! Sijaona chama ambacho kimejiandaa kutwaa madaraka na kuongoza nchi bali tuna pressure groups (au activists) ambazo zinafanya kazi zao vizuri anyway.
 
Hakika napenda sikuniione CCM mpya,CCM iliyojikita katika misingi yake ya kutetea wanyonge,CCM ya wakulima na wafanyakazi,CCM yenye sera za kweli za kumkomboa Mtanzania kutoka katika lindi la umaskini uliokithiri.Njia moja wapo ya kufikia haponi kurudia miiko na misingi iliyounda chama chetu,kuwatosa makupe (mafisadie),kuwawajibisha wavivu,na kuweka viongozi wenye nia thabiti na uwezo na kuonyesha njia kule tunakotaka kwenda.Tukifanya hivyo hakikia Tanzania yenye maendeleo,amani na utulivu tutaiona.Kamwe sitavaa gwanda na kamwe sitatetea mafisadi.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mfa maji haishi kutapatapa.
La kuvunda halina ubani.

Sikio la kufa halisikii dawa.
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza.
Kila chenye mwanzo hakikosi mwisho.
 
ccm ndo yenye dola kama yaliwezekana mngefanya,kama yanawezekana fanyeni.

huenda nia ipo uwezo haupo au uwezo mnao ila nia haipo.

leteni vitendo sio maneno.
 
Hakika napenda sikuniione CCM mpya,CCM iliyojikita katika misingi yake ya kutetea wanyonge,CCM ya wakulima na wafanyakazi,CCM yenye sera za kweli za kumkomboa Mtanzania kutoka katika lindi la umaskini uliokithiri.Njia moja wapo ya kufikia haponi kurudia miiko na misingi iliyounda chama chetu,kuwatosa makupe (mafisadie),kuwawajibisha wavivu,na kuweka viongozi wenye nia thabiti na uwezo na kuonyesha njia kule tunakotaka kwenda.Tukifanya hivyo hakikia Tanzania yenye maendeleo,amani na utulivu tutaiona.Kamwe sitavaa gwanda na kamwe sitatetea mafisadi.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Nakapanya kumbe na wwe nimwa sisiem?wwe nimtoto wakigogo yupi?sisiem niya matariji,vigogo,watoto wao,wake zao.ssa wwe upo kundi lipi?wakati mnaendelea namchakato wakukijenga upya chama chenu,inabdi mbadirishe nembo yachama.toa jembe na nyundo weka kisu na kijiko mpaka mkimaliza ujenzi.
 
chenge hajashtakiwa kwenye sakata la rada na hana hatia ila anamiliki utajiri usio wa kawaida.

by hoshea.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom