CCM/CUF washambulia Wanaharakati- CDM wapinga kupitisha Mswada wa Mapitio ya Katiba

hivi kwa nini tunawanyenyekea hawa wa Zanzibar kiasi hiki? kuna faida gani tunapata kutokana na huu muungano wa kijinga?
 
Kisaikolojia, mtu akishafungwa jela unaathirika kutokana na mazingira yaliyoko huko jela na makosa aliyofanya.

Rage aliiiba pesa za TFF enzi hizo akafungwa, akatolewa kwa madai ya ugonjwa wa Kisukari! Sasa ni mbunge......amezoea siasa za vijiweni za posta..habari maelezo na foodworld....mtu kama huyo unategemea atasema nini? Hawezi kukubali katiba makini ambayo itazuia harakati zake za wizi.....Hata huko simba ni yaleyale.
 
Hilo ndo tatizo la viongozi wa CCM.

Sasa tuseme anataka kutwambia raisi aliyepata kura zisizozidi milion 6 kati ya Watanzania milioni 42 ndiye amechaguliwa na wananchi?

Kwanza hata neno Wanaharakati sijui kama anajua maana yake, Rage nenda darasani bwana! Inawezekana leo kama angekuwa anarudi nyumbani, mwanae anayesoma chekechea leo angekataa kumsalia kwa sababu ya maneno aliyoyasema leo, maana dogo angeshindwa kutofautisha hizo busara kati ya baba yake na hao wenzake anaocheza nao akiwa shule, angeona bora hiyo shikamoo awape wale wenzie maana wanafikiri sana kabla ya michezo yao ya kombolela na kujificha kuliko baba yake ambaye hata neno wanaharakati hajui maana yake hadi anadai eti wapigiwe kura (wachaguliwe)!
 
Katika muendelezo wa kujadili mchakato wa katiba mpya katika vikao vya bunge linaloendelea muheshimiwa na mbunge wa Singida bwana Tundu Lisu wabunge wa CCM wamemdhalilisha sana, haya ndio matamshi ambayo yametawala bungeni kwenda kwa muheshimiwa huyu:
  1. Hajui sheria
  2. Aje tumfundishe sheria tena tutamlipia.
  3. Amesomea sheria chini ya mti.
  4. Mwanaharakati feki.
  5. Eti anajifanya ni msomi aliyebobea.
  6. Anawadanganya wapiga kura wake.
  7. Anajifanya mwanasheria je kasomea wapi sheria?
Jamani bunge hili mbona kama naona ni bunge lenye majungu? wenzangu naomba kuwasilisha.
 
Hii ndio bongo bwana lisu anawakimbiza ndo maana wanalia

hawana la maana hawa jamaa kila kukicha wanasema
hovyo badala ya kutoa hoja za msingi
 
wabunge wa bara ndo hao akina simbachawene, prof maji marefu, kibajaji na wengine, unategemea nini kutoka kwao. mungu ibariki tanzania.
 
Acha kukariri kama kasuku, katiba ndiyo sheria mama ya nchi. Kama utakuwa na katiba
mbovu, hao viongozi wazuri utawapata je? Mafisadi utawadhibiti vipi? Wachakachuaji (NEC)
wa kura zetu? utawala wa sheria na haki? etc.

Kwahiyo unasema tuwe na katiba mbovu eti kwasababu katiba inayokidhi matakwa ya
wananchi sio mworobani? You're an obtuse person.
 
Kwa kusema JUKWAA LA KATIBA ni wahuni, alipaswa kueleza umma alichokusudia, lakini pia kufuta kauli kwa kusema ana uchungu, anapaswa kuweka wazi ni uchungu gani. Maana labda ni uchungu wa kutamani kuona Machafuko au umwagaji wa damu kama ailvyozoea kuleee.... Sooomaaaa......
 
Alshabab live ndani ya bunge, na bado tutatukanwa sana hadi tutaingiziwa kidole kwenye jicho tunawaangalia tu, nchi ya amani!

Hebu mie, lunch time saa hizi nikakae chini ya mti nipunge upepo saa nane nirudi mzigoni
 
hahaaa haaaa hawana haya, miezi miwili iliyopita katunukiwa Cheti Cha Heshima kwa kuwa wanautambua mchango kama mwanaharakati wa kweli kutoka Chuo kikuu jina la chuo limenitoka
 
Nimeshindwa kuamini kuwa wabunge wetu wamefikia wakati wa kutukana watanzania na kuona wao wako juu ya katiba na hakuna wa kuzuia kufanya lolote,

Nimesikitishwa pia kwa wabunge kuona wao wanajua sheria zaidi ya magwiji wa sheria na kuanza kumtukana prof shivji kuwa yeye ni muhuni na ana lolote kwenye sheria na wao wanajua kuliko watu wengine


je jeuri hii ya wabunge wa CCM wameipata wapi?
 
Asante sana kwa maoni yako. Kama unaamni kuwa katiba ndio jibu, je, mbona ungereza haina written document na inayo maadili yake? China je?
ukitazama hizi nchi mbili ulizozitolea mfano uwajobikaji wao katika majukumu ya kitaifa ni tofauti na tz, wale wenzetu waziri akijikoroga kidogo tu anajiwajibisha mwenyewe na kuwaachia wengine lakini si tanzania ambapo licha ya kuwajibika mwenyewe hata mkubwa wake hawezi kumuwajibisha hivyo basi tunataka katiba itakayokuwa na vipengele vitakavyowabana hawa viongizi wetu na wa kuwahoji kwa kila kitu ambacho tunaona hawakwenda sawa
 
CCM chama cha matarumbeta, msishangae yao mipasho siasa washa shindwa hao
 
Huwezi hata siku moja kumfanisha Hamad rashid na Tindu lissu. Kwani hakuna cha japo kushabihiana wala kukaribiana kwani Hamad yupo juu kwa kila kitu.

Labda Lissu unaweza kumfananisha na Ismail Jussa na hata huyo hamuwezi. Lissu ni hasira na jazba tu lakini hawezi lolote.
 
Asante sana kwa maoni yako. Kama unaamni kuwa katiba ndio jibu, je, mbona ungereza haina written document na inayo maadili yake? China je?

constitution can either be written or unwritten, Kutokuwa na written constitution haimaanishi kuwa huwezi kufanya kitu uncostituional, so paper work isikuchanganye, UK wanayo katiba yao, iko damuni kiasi kwamba everybody knows nchi inaendeshwaje, haki na stahili zao wanazijua toka katika katiba yao.
 
Wabunge wa CCM wamepotoka wanatakiwa wajadili muswaada kama wanaunga mkono lakini sio kuhamisha mjadala kwa waziri kivuli wa sheria kwa sababu wanamfanya wanachi wamuamini zaidi
watu wengi watafikiria kuwa wabunge wanatetea serikali ya chama chao
 
Back
Top Bottom