CCM/CUF washambulia Wanaharakati- CDM wapinga kupitisha Mswada wa Mapitio ya Katiba

Hamadi Rashid alikuwa anachangia huo mswada huku akichanganya na hasira za kutoshirikishwa kwenye kambi ya upinzani.

huyu mama/mbibi anayeongea sasa hivi anaongea pumba tu hajui impact ansahau kuwa hata hao cdm wanawakilisha wananchi.
kilaza tu
 
Wanahistoria wanaamini 'History is Spiral' yaani historia hujirudia, wala hakuna jambo jipya kabisa juu ya ardhi. Mjadala wa Katiba huu wa sasa si mpya hata kidogo, pengine kizazi kinachoujadili ndicho kipya chenye upofu wa historia. Napenda kuanza kwa kumnukuu Mwalimu Nyerere katika hotuba yake kuhusu Katiba aliyoitoa mwaka 1962


"The point must be made that ultimately the safeguard of a people's right, the people's freedom and those things which they value, ultimately the safeguard is the ethic of the nation. When the nation does not have the ethic which will enable the Goverment to say: ' We cannot do this, that is un- Tanganyikan'. Or the people to say: ' That we cannot tolerate, that is un-Tanganyikan'. If the people do not have that kind of ethic, it does not matter what kind of constitution you frame. They can always be victims of tyranny....... What we must continue to do all the time, is to build an ethic of the nation, which makes the Heads of State whoever he is to say, ' I have the power to do this under the Constitution, but I cannot do it, it is un- Tanganyikan'. Or for the people of Tanganyika, if they have made a mistake and elected an insane individual as their Heads of State, who has the power under the Constitution to do XYZ if he tried to do it, the people of Tanganyika would say, 'We won't have it from anybody, President or President squared, we won't have it'.

I believe, sir, that is the way we ought to look at this constitution. We have got to have a little amount of faith, although I know that some Members have been questioning the idea of faith. But, sir, democracy is a declaration of faith in human nature, the very thing which we are struggling to safeguard here, the very idea of democracy is a declaration of faith in mankind. And every enemy of democracy is some person who somewhere has no faith in human beings. He doubts. He think he is all right, but other human beings are not all right.

28 June 1962 Hansard, 1st Session
Goverment Motion- Proposal for a Republic"

Naamini kwa dhati kabisa kuwa Katiba sio mwarobaini wa matatizo yetu kama taifa kwa sasa. Tunalo tatizo la kimaadili na kiuongozi kuanzia ngazi ya familia, Serikali, Chama Tawala na Vyama vya Upinzani. Tatizo hili tiba yake sio Katiba, bali ni kurudi katika misingi(Soul searching) ya Taifa hili. Tupitie upya na kuboresha yale mambo ya yaliyotuunganisha kama Taifa likiwemo Azimio la Arusha na kuliboresha kuweza kujibu changamoto za sasa. Pale ndipo kwenye agano la Taifa na zindiko la Tafa hili na si Katiba mpya.

Afrika Kusini ni nchi ambayo imepata Katiba mpya katika miaka ya karibuni. Katiba ambayo imesifiwa kuwa ilikuwa na mchakato wa wazi zaidi na ushirikishwaji wa hali ya juu. Katiba ile imeruhusu hadi haki za mashoga kwa mantiki ya kuheshimu haki za binadamu. Lakini maisha ya wazalendo wa Afrika Kusini bado yangali ni magumu na yaliyopoteza matumaini. Afrika Kusini ni nchi yenye mpasuko mkubwa pamoja na kuwa na uchumi imara.

Gharama tunazoingia katika kutafuta kile kinachoitwa Katiba mpya ni kubwa kuliko manufaa au matokeo yake kwa Mtanzania. Tutasimamisha uzalishaji na maendeleo na kuelekeza rasilimali zetu kwenye Katiba. Tutakuwa na Tume ambayo itazunguka na kufanya mikutano kwa miaka 2 na kutumia rasilimali; tutakuwa na Bunge la Katiba, Wabunge wale karibia 600 watalipwa posho na watachukua muda kufikia muafaka katika kujadili na Kamati kubishana sentensi zikaaje. Kisha tutakuwa na kura ya maoni nchi nzima ambayo ni sawa na uchaguzi mkuu, na mwaka mmoja baadae tutakuwa na uchaguzi mkuu. Gharama zote hizi zitabebwa na wananchi kwa gharama ya kuaihirisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mwisho tutakuwa na document inaitwa Katiba mpya! ambayo haitabadilisha hali ya wananchi kwa kuwa tutakuwa hatujapatia jawabu tatizo letu la msingi.

Huwezi kujua kama kuiba ni kosa bila neno usiibe, Mafisadi tumewajua baada ya sheria ya mikataba. Kwa hiyo makosa yote yanajulikana kwa sababu ya sheria zilizopo na sheria hizo zina msingi wake ambao ni KATIBA.Katiba ni lazima na ni suluhisho ya matatizo yanayohusu uongozi wa nchi yakiwemo na maadili ya viongozi.
 
Hamad Rashid atakuwa na wakati mgumu sana kule Zanzibar. Maoni yake kuhusu huu muswada ni tofauti na baraza la wawakilishi. Sidhani kama atarudi bungeni 2015 (labda apewe ubunge wa mezani - kuteuliwa).

CCM na wapambe wao wanaonekana kutojua nini wanatakiwa wafanye. Kama kweli wanajadili muswada inakuwaje wajadili CHADEMA na wanaharakati? Nilidhani wangekuwa wanajadili vifungu vilivyo kwenye huo muswada lakini wao wanaongelea CHADEMA. Ni vizuri CHADEMA wametoka nje maana hakuna la maana wanaaongea zaidi ya mipasho.
 
Ninapofuatilia mjadala wa bunge nasikia kichefuchefu. Hadi nafikia kujiuliza, hivi ccm inawabunge kweli huku tanzania bara? Kweli kwa wabunge walio wazalendo na wakweli watakubali upendeleo wa wazi kwenye mswada huu. Kwa nini wazanzibar wapewe nafasi kuamua tena kwa kura ya turufu hata mambo ya bara? It is phenomenon!
 
mfungwa rage yaani sikutegemea kuwa ni boya kiasi hiki khaaaa! wish asingetoka angeendelea kunyea debe keko!
 
sasa mnamlaumu nini?
awe na uchungu na katiba mpya ya nini wakati hii iliyopo inawezesha hata wasio raia na wahalifu kuwa wabunge kama yeye!
 
Huyu jamaa ni limbukeni sana.
I wonder inakuwaje kuna chama cha siasa kinaweza kumuona anaweza kuwakilisha jimbo, na watu nao wanampa kura!!
Rage hawezi kuwa hata katibu tarafa!!......empty head.
 
Nashangaa sana wananchi wa Tabora kutuletea Wasomali Bungeni....nadhani hili kosa watani wangu hawatalirudia mwaka 2015. Ni aibu sana huyu Msomali kututukana hadharani. Kama vp aende akagombee ubunge kwao Mogadishu
 
Angekuwa ameongea Mtanzania ningekuwa na lakuchangia, lakini huyu Al Shabaab hilo ni zigo la wana wa Tabora mjini wanaopiga kura kama vipofu.
 
Yule ni mfadhili wa alshabaab tangu zamani, ndiye anaingiza wasomali kwa malori wanamlipa.
 
Back
Top Bottom