BUNGENI: Waziri Ghasia awasilisha Bajeti yake; mishahara yapanda

Mshahara utapanda kila mtu atafurahi na kukubali kuwa CCM ni chama bora kuliko vyote TZ watumishi msisikilize porojo za hao mavuvuzela mwisho wa mwezi mtashangaa nyongeza mtakayoikuta

Huu ndio mwisho wako wa kufikiri mkuu??
 
Ukweli sio kwamba mshahara unapanda bali hiyo ni malipo stahiki kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha ukilinganisha na mwaka jana au wenzetu huita CPI yaani CONSUMER PRICE INDEX...
Nimekukubali mchumi! Hope kila kitu kitakwenda sawa! Umeeleweka vyema!
 
mshahara umepanda kwa kiasi gani nyie, mbona hamnijibu?? sina redio hapa nilipo
 
mshahara umepanda kwa kiasi gani nyie, mbona hamnijibu?? sina redio hapa nilipo
Mkuu swali lako bado ni fumbo. Kilichopo nikwamba bajeti ya utumishi imeongezeka mpaka kufikia kiasi cha shiling trilion 3.2 ambayo ni sawa na ongezeko la 40.2%, kuhusu mshahara specificaly bado kujua. Punguza presha!
 
kwani si mliambiwa mshahara utapanda kwa 40% na kilichokuwa kinasubiriwa ni waziri wa utumishi kutangaza hilo. Hili limeandikwa sana hapa, hata kama kuna ajira mpya ishu inabaki palepale mshahara umeongezeka kwa hiyo asilimia arobaini. Ni common sense tu au mlitaka waseme 25% kama walivyosema zanzibar?
 
Taarifa ya habari saa 7 mchana Radio One imetangazwa kuwa serikali itapindisha mishahara ya wafanyakazi lakini kiwango cha nyongeza bado hakijajulikana. Hata hivyo serikali imesema (according to Radio one) nyongeza hiyo ya mshahara itazingatia mfumuko wa bei (inflation), gharama za maisha etc. Kwa tafsiiri nyingine ni kuwa Mhe Hawa Ghasia amesimama mbele ya bunge la Jamhuri akiomba ridhaa ya wawakilishi wa wananchi katika chombo hicho muhimu waidhinishe matumizi ya kado zao (wananchi) kwenye mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuoengeza mishahara kwa wafanyakazi katika idara/taasisi mbalimbli. Sasa;

1. Kama Mh. Ghasia HAJUI nyongeza itakuwa ni kiasi gani anataka bunge liidhinishe nini? na kwa misingi ipi?

2. Ni kwa nini Wizara hii imeshindwa kusema categorically mishahara itaongezeka kwa kiasi fulani i.e 1%, 3%, 6%, etc etc? Hawajui inflation?hawajui GDP rate? hawajui idadi ya watumishi? Muda wa kuandaa bajeti ulikuwa mfupi? au hana wataalam wa kukokotoa numbers? what is it that Mh. Ghasia amekosa na ndio sababu ameshindwa kusema kiasi cha nyongeza?

3.Wizara ya Utumishi wa umma imekuwa na tatizo sugu la wafanyakazi hewa, na hata Mh Ghasia alikiri hilo mbele ya Rais Kikwete mapema mwaka huu, je kama ameshindwa kutatua hilo tatizo wabunge wataidhinishaje matumizi ya hela kwa wizara inayolipa watumishi hewa?

4. Bajeti nzima ya Wizara hii inaonekana kuongezeka kwa zaidi ya theluthi moja ya bajeti ya mwaka uliopita. Nyongeza hiyo inajumuuisha pia malipo kwa watumishi hewa?

Kubwa zaidi:
Miongoni mwa wabunge wa 'viti maalum-ccm' wamo wabunge walao wawili wanaowakilisha vyama vya wafanyakazi. Mmoja ni Binti Kawawa na mwingine ni Angela Kairuki. Ni vizuri tufuatilie kwa karibu mchango wa wabunge hawa wawili ili kubaini aina ya 'uwakilishi' wao bungeni. Je watasimama kutetea maslahi ya wafanyakazi? Watatumia nguvu yao (kuzuia mshahara wa waziri, shilingi) hadi hapo Serikali itakaposema kiasi cha nyongeza? tukumbuke kama serikali haikusema kiasi, na bunge likapotisha serikali inaweza kuongeza mishahara kwa Tsh 200 na bado wakashinda argument maana hakuna mahali popote waliposema ni kiasi gani!

Naamini humu jamvini wapo watu walio kwenye vyama vya wafanyakazi au wako karibu na viongozi wa TUCTA. Wawabane hawa waheshimiwa maana majimbo yao ni vyama vya wafanyakazi.
 
Nyongeza ya mshahara ni ndoto wakuu hiyo imekula upande wetu!!

Tuomboleze sisi na familia zetu!!

Na sisi acha tukome tunakiherehere mno! Watu wanachakachua na sisi tunaangalia tuuuu (Maana asilimia kubwa ya wasimamizi wa uchaguzi ni hao hao wafanyakazi wa umma)!!

Lakini kama hawataongeza nina mashaka na utendaji utakavyokuwa huko maofisini. Si hapo raia ndo wataumia jamani? Yaani asije mtu kunijua kabisaaaa!! Itabidi watusamehe kwa kweli.

Yetu macho na hii sirikali ya Mkwer'e
 
Nyongeza ya mshahara ni ndoto wakuu hiyo imekula upande wetu!!Tuomboleze sisi na familia zetu!!Na sisi acha tukome tunakiherehere mno! Watu wanachakachua na sisi tunaangalia tuuuu (Maana asilimia kubwa ya wasimamizi wa uchaguzi ni hao hao wafanyakazi wa umma)!!Lakini kama hawataongeza nina mashaka na utendaji utakavyokuwa huko maofisini. Si hapo raia ndo wataumia jamani? Yaani asije mtu kunijua kabisaaaa!! Itabidi watusamehe kwa kweli.Yetu macho na hii sirikali ya Mkwer'e
Mkuu hii mambo inakuwaje? Hawa waheshimiwa wanataka iwaje?
 
Mkuu swali lako bado ni fumbo. Kilichopo nikwamba bajeti ya utumishi imeongezeka mpaka kufikia kiasi cha shiling trilion 3.2 ambayo ni sawa na ongezeko la 40.2%, kuhusu mshahara specificaly bado kujua. Punguza presha!

Vipi kuhusu ajira mpya?
Maana kuna walimu na watumishi waafya wengi tu wanatakiwa kuajiriwa!
 
kwani si mliambiwa mshahara utapanda kwa 40% na kilichokuwa kinasubiriwa ni waziri wa utumishi kutangaza hilo. Hili limeandikwa sana hapa, hata kama kuna ajira mpya ishu inabaki palepale mshahara umeongezeka kwa hiyo asilimia arobaini. Ni common sense tu au mlitaka waseme 25% kama walivyosema zanzibar?
Hapa unataka kuforce.Bado haijatamkwa wazi na authorized source kuwa mshahara umepanda kwa hizo asilimia 40.2!Kilichowazi mpaka sasa ni kuwa kwa mwaka huu wa fedha bajeti ya mishahara kwa watumishi wa uma imepanda kwa hizo asilimia 40.2.Hizo zingine ni speculation zako mkuu.
 
[Kubwa zaidi:
Miongoni mwa wabunge wa 'viti maalum-ccm' wamo wabunge walao wawili wanaowakilisha vyama vya wafanyakazi. Mmoja ni Binti Kawawa na mwingine ni Angela Kairuki. Ni vizuri tufuatilie kwa karibu mchango wa wabunge hawa wawili ili kubaini aina ya 'uwakilishi' wao bungeni. Je watasimama kutetea maslahi ya wafanyakazi? Watatumia nguvu yao (kuzuia mshahara wa waziri, shilingi) hadi hapo Serikali itakaposema kiasi cha nyongeza? tukumbuke kama serikali haikusema kiasi, na bunge likapotisha serikali inaweza kuongeza mishahara kwa Tsh 200 na bado wakashinda argument maana hakuna mahali popote waliposema ni kiasi gani!

Naamini humu jamvini wapo watu walio kwenye vyama vya wafanyakazi au wako karibu na viongozi wa TUCTA. Wawabane hawa waheshimiwa maana majimbo yao ni vyama vya wafanyakazi.[/QUOTE]

hawa wabunge wa viti maalum mtawalaumu bure hawakujui kama wanawakilisha kundi fulani, hawa wanajua kazi yao kubwa ni kutoa uburudisho kwa waheshimiwa wa bunge i.e filikanjombe, mkulo, masele,titus, wasira, waziri mdogo, etc. wabunge wa ccm wakichoka kuropoka bungeni na wengine kusinzia muda wate wanajua wakitoka wanaviburudisho vyao (viti malaam)
 
anasema ktk bajeti hii mazingira ya utumishi wa umma yataboreshwa kimafunzo na kiujuzi zaidi!

Anaweza wakawa wana nia nzuri. Wajiulize je Huko wanakopeleka Fungu la Mafunzo linatumika ipasavyo. Kuna fununu kwamba pesa za mafunzo huwa zinatolewa kwa kujuana. Wanaoenda mafunzo hasa short courses kila mwaka ni wale wale.
 
Naongea kwa uzoefu kama mfanyakazi. Hebu rejea bajeti ya mwaka jana (nanukuu: "43. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2010/2011 Serikali inatarajiakutumia shilingi trilioni 2.332 kugharamia malipo ya mishahara kwa watumishiwaliopo Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, ajira mpya, upandishwaji vyeo na kulipiamadai ya malimbikizo na mapunjo ya mishahara ya watumishi. Kiasi hiki ni sawa naasilimia 38.84 ya Mapato ya Ndani. Aidha, kiasi hiki kimeongezeka kwa shilingibilioni 558 ambayo ni sawa na asilimia 31.5 ya fedha zilizotengwa kwa ajili hiyokatika mwaka wa fedha 2009/2010". mwisho wa kunukuu.

Mshahara uliongezeka kwa 31.5% kwa kima cha chini mwaka jana ingawa wenye kipato cha juu zaidi ilikuwa chini ya hiyo lakini haikupungua 25%. Fuatilia bajeti zilizopita utagundua hilo.

Naomba nikukuhakikishie Mnyakatari hapo juu kuwa kima cha chini kitapanda kwa 40%. Kadri mshahara unavyokuwa mkubwa na hiyo 40% inapungua lakini haiwezi kupungua zaidi ya 35%.
 
Kwa kuzingatia nyongeza (5,000-20,000/-) ambayo waalimu na askari wamekuwa wakipata kila mara serikali inapotangaza kuongeza mshahara, kamwe mshahara hautaweza kuongezwa kwa 40% na naweza kusema haijawahi kutokea. Kama kuna nyongeza za namna hiyo, basi ni kwa nafasi za juu kama rais,waziri mkuu, waziri. Ongezeko la bajeti ya mishahara kwa 40%, bila shaka linaenda sambamba na tarajio la kuajiri wafanyakazi wapya.

Kama kungekuwa na nyongeza ya 40% kwa kila mfanyakazi wa serikali, hiyo nyongeza ingekuwa wimbo-CCM wangeuimba toka mwezi wa 5 bajeti ilipokuwa inaandaliwa. Yaani kuwe na nyongeza kubwa hivyo, halafu W/Mkuu na Waziri huska wasiitangaze? Kwa kifupi, hata nchi zenye uwezo kiuchumi, haziwezi kumudu ingezeko hilo la mshahara. Tujikumbushe mvutano kati ya COSATU na Serikali ya SA mwaka 2008, ambao walikuwa wanataka mshahara uendane na mfumuko wa bei, ndo tutaelewa ugumu wa kupandisha mshahara kwa asilimia zote hizo. Naweza kusema, hakuna nchi(ndani ya miaka 10 iliyopita) ambayo imeweza kuongeza mshahara wa wafanyakazi wake japo kwa 20%
 
Hakuna anayefanya Analyisis yoyote kweli jamani,ni Majungu na Vijembe kurusha tu,kweli Hii ni Forum ya Majungu?kama huna Facts hapa sio sehemu yake,fanya uchambuzi na utuambie kwamba kwanini?Vinginevyo unatuambia Majungu tu hapa....
 
Fungu zima ndo limepanda kwa 40.2%,nadhani inajumuisa mishahara ya ajira mpya zaidi ya elfu 64!

kima cha chini 135,000/= ktk ongezeko la 40.2% ni sawa na 189,000/=

Mshahara ukipanda wakati nchi haina umeme, Serikali itakusanya kodi toka vyanzo vipi ili hiyo mishahara ilipwe?

Mkuu hiyo % ni ya fungu zima la mishahara. Kumbuka hapo kuna ajira mpya haswa upande wa walimu na madaktari, annual increments na malimbikizo ya nyongeza za nyuma ambazo hazikuwahi kulipwa. Ni juzi tu tumesikia walimu wanatishia kugoma sababu wanadai malimbikizo!!!!!

Hata hivyo usishangae kesho kwenye magazeti wanatoka na vichwa JK aongeza mshahara 40%!!!!!!

Serikali wanatumia lugha ya kujificha wanaposema fungu limeongezeka ni kwa misingi ipi?
kulipia ajira mpya? au mabosi kula zaidi?
wangetangaza vimo kama tulivyozoea hapo hakuna kilichopata ni uhuni wao kuwapoteza watu,
wakija kushituka bajeti ya 2012/2013 itakuwa inasomwa mjengoni
 
Back
Top Bottom