BUNGENI: Waziri Ghasia awasilisha Bajeti yake; mishahara yapanda

Naongea kwa uzoefu kama mfanyakazi. Hebu rejea bajeti ya mwaka jana (nanukuu: "43. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2010/2011 Serikali inatarajiakutumia shilingi trilioni 2.332 kugharamia malipo ya mishahara kwa watumishiwaliopo Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, ajira mpya, upandishwaji vyeo na kulipiamadai ya malimbikizo na mapunjo ya mishahara ya watumishi. Kiasi hiki ni sawa naasilimia 38.84 ya Mapato ya Ndani. Aidha, kiasi hiki kimeongezeka kwa shilingibilioni 558 ambayo ni sawa na asilimia 31.5 ya fedha zilizotengwa kwa ajili hiyokatika mwaka wa fedha 2009/2010". mwisho wa kunukuu.

Mshahara uliongezeka kwa 31.5% kwa kima cha chini mwaka jana ingawa wenye kipato cha juu zaidi ilikuwa chini ya hiyo lakini haikupungua 25%. Fuatilia bajeti zilizopita utagundua hilo.

Naomba nikukuhakikishie Mnyakatari hapo juu kuwa kima cha chini kitapanda kwa 40%. Kadri mshahara unavyokuwa mkubwa na hiyo 40% inapungua lakini haiwezi kupungua zaidi ya 35%.
 
Mbunge wa Dodoma mjini mh. David malole anawasilisha hoja, mmh salamu zimekua nyingi kweli, hadi mjukuu kapewa duh!
 
kwani si mliambiwa mshahara utapanda kwa 40% na kilichokuwa kinasubiriwa ni waziri wa utumishi kutangaza hilo. Hili limeandikwa sana hapa, hata kama kuna ajira mpya ishu inabaki palepale mshahara umeongezeka kwa hiyo asilimia arobaini. Ni common sense tu au mlitaka waseme 25% kama walivyosema zanzibar?
Kwani wewe ulitakaje? wengi wetu tulihitaji wataje kiasi chenyewe!
 
Dr. Titus Kamani, Mbunge wa Busega anazungumza sasa, Yani anayoyasema sijui yanahusianaje na mjadala huu wa bajeti ya utumishi wa umma! Hayaoan kabisa!
 
Mh. Joseph Selasin Mbunge wa Rombo sasa Anazungumza. Anatoa tahadhari juu ya ishu ya Udini, anadeclare interest yake kwamba yeye ni kiongozi ktk kanisa katoliki!
 
anasema kwa nin viongoz hawachukui hatua juu ya hao wenye udini! Kukaa kimya kwaweza kubomboa ustaarabu wetu!
 
Analalamika kuwa swala la udini halishughurikiwi kwa ukamilifu!
 
mh. Selasin analaumu kuhusu rushwa, katoa mfano kua polisi huko himo wanasindikiza magari ya mahindi kenya!
 
Anaitaka takukuru kupambana na rushwa kuepuka migogoro huko mbeleni!
 
anamtaka waziri aje na mkakati wa kudhibiti mishahara hewa! Anawataka watanzania wafanyao kazi ktk maofisi wawajibike, waache kupiga kidomo domo WAFANYE KAZI!
 
Mh. David Silinde Mb. Mbozi Magharibi anazunguza, nae kama kawa anapondo TAKUKURU! anasema tumeendelea kuzuia rushwa pasipo chombo mbadala!
 
Anasema kushindwa kwa TAKUKURU ndio chanzo cha kifo cha Gavana japo kwa utata!
 
Anataka serikali iboreshe Maslah ya Wafanyakazi wa Umma! Anataka maslah yaambatane na Makazi ya watumishi kama motisha!
 
Anazungumzia Ajira za kada ya chini kwa mfumo wa decentralization kuwa unaingiliwa na central government!
 
Anasema uongozi ni kizazi kwa kizani, waliokuwa machaguo ya mungu 2005 wamefanya madudu Mungu kawatema, mwaka 2010 wakaibuka wengine waliopendwa na mungu, wale wa 2005 wakaanza kuwazushia wale wa 2010 Kuwa ni wadini. Amesema huu mchezo wa kutangaza udini wa kizushi!
 
Mustafa Akunaay Mb. wa Mbulu sasa anaongea, KAMA KWAWAIDA ANAPONDA UDINI..
 
Back
Top Bottom