Bungeni: Shibuda aongelea hatma yake ndani ya CHADEMA!

39-Jay-Z-Ehhh.gif
 
Shibuda alipuka bungeni
MBUNGE wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda jana alilishangaza Bunge baada ya kutumia sehemu ya dakika zake za kuchangia Hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuzungumzia zaidi hatma yake kisiasa na chama chake. Akizungumza wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2011/12, Shibuda alisema hata siku moja hakuwahi kuvunja msimamo wa kikao cha Kamati Kuu(CC) ya chama hicho, bali anatofautiana na viongozi wa Chadema kwa dhamana zao binafsi huku akisisitiza, “Ni haki katika hili”. Shibuda amewahi kuhojiwa baada ya kupingana na msimamo wa chama hicho wa kumsusia Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizindua Bunge Desemba mwaka jana kwa kuhudhuria dhifa katika Ikulu ya Chamwino huku akiweka bayana kupingana na msimamo huo.

Lakini, jana akizungumza kwa msisitizo na kutoa mifano mingi ya maneno ya Kiswahili, Shibuda alisema, “Ninaulizwa maswali mengi juu ya hatma yangu ndani ya Chadema na hili vilevile nimeona ni bora kulizungumza,”.
Kauli hiyo ya Shibuda ilimshtua Spika wa Bunge, Anna Makinda ambaye aliuliza iwapo suala hilo linahusu masuala ya Utalii, “Hilo nalo ni utalii,”

Baada ya kujibu kuwa suala hilo pia linahusu masuala ya maliasili na utalii, Shibuda alisema “Maliasili ya nchi yetu ni siasa bora na utawala bora, nimeona hilo nilizungumze”.Alisema viongozi wa dini kazi yao kubwa ni kumng’arisha binadamu ili aweze kwenda ahera na viongozi wa siasa kazi yao ni kuwa madobi wa kuing’arisha Serikali. “Nimeamua kulisema kwa kuwa kila mtu (hata wabunge) wananiuliza kama kamati kuu ya Chadema imeniita na kwamba, nitafukuzwa,” alisema Shibuda.

Atuhumu baadhi ya vyombo vya habari
Licha ya kutotaja majina ya magazeti aliyoyatuhumu, Shibuda alisema kwamba kauli zinazoandikwa na kunukuliwa na baadhi ya magazeti ni kauli hatarishi , huku akisisitiza kuwa kauli hizo za vyombo vya habari zinaacha vikwazo kwa wanasiasa. Alisema kuwa hata Jukwaa la vyombo vya habari nchini lina mazuri na mabaya yake na kwamba apendaye kutumia jukwaa la siasa ni sawa na mtu mpenda fitina. “Maneno yaliyonukuliwa na viongozi wa Chadema katika vyombo vya habari kwamba mimi ni msaliti si kweli na wala sijavunja msimamo wa uongozi wa kikao cha kamati, nimetofautiana na watu kwa dhamana zao binafsi,” alisema Shibuda.Alisema kuwa hawezi kugandishwa na kukosa demokrasia ya kikatiba ya kutoa maoni yake, na kwamba yoyote anayegeuza au kutumia cheo chake kwa maslahi binafsi hatakuwa na tofauti na Pius Msekwa.

Msekwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara anatuhumiwa kuingilia watendaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), kwa kujihusisha na utoaji wa ofa kwa wafanyabiashara wanaotaka kujenga hoteli za kitalii. “Mazuri huwa ya baba na mabaya huwa ya mama…, bahari ikichafuka nahodha hupimwa kwa ujasiri wake, nakiri kuchafua hali ya hewa ila napenda kuwaambia kuwa Shibuda ni jasiri,” alisema.

Aliongeza, “Maswa sio Pundapori ina wenyewe na wananchi wa Maswa wamekataa kuporwa mbunge wao kama wanyamapori, CCM ni demokrasia pana na Chadema ni kwa maslahi ya jamii, lakini kila kizuri hakikosi kasoro heshima na busara ndio itatuongoza kufika salama,”. “Vyama vya siasa vipo kama 12 hivi, vipo vyama maslahi binafsi, jamii, ushirika na Saccos…, mimi kudhalilishwa na kupuuzwa sijali sana kwa kuwa ninaongozwa na ukweli na siwezi kusema uongo,” alisema Shibuda.

Mwananchi
 
Mimi nina mtizamo tofauti, nazani Shibuda hana msimamo wa pamoja, na alikwenda CDM kwa ajili kutafuta ubunge tu, hata km kuna uhuru wa kujieleza na uhuru wa kusikilizwa ambazo ni haki za msingi kikatiba lakini huwezi kusema kila kitu mahala popote, km ulimsikilza Shibuda jana bungeni, utagundua hilo, kwa mtizamo wangu mimi pale hapakuwa mahali pa kuelezea mambo ya chama, ni kweli anaweza kuwa resource, na kansa ya baadaye. CDM watch out
 
nadhani wamwache tu kwani ktk chama chenye watu wengi kama CDM watu yeye hawkosekani nao wana nafasi yao, mbona watu kama akina Kolimba walima Chama chao kimepoteza dira wakiwa bado wanachama
 
MBUNGE wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda jana alilishangaza Bunge baada ya kutumia sehemu ya dakika zake za kuchangia Hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuzungumzia zaidi hatma yake kisiasa na chama chake.

Akizungumza wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2011/12, Shibuda alisema hata siku moja hakuwahi kuvunja msimamo wa kikao cha Kamati Kuu(CC) ya chama hicho, bali anatofautiana na viongozi wa Chadema kwa dhamana zao binafsi huku akisisitiza, “Ni haki katika hili”.Shibuda amewahi kuhojiwa baada ya kupingana na msimamo wa chama hicho wa kumsusia Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizindua Bunge Desemba mwaka jana kwa kuhudhuria dhifa katika Ikulu ya Chamwino huku akiweka bayana kupingana na msimamo huo.Lakini, jana akizungumza kwa msisitizo na kutoa mifano mingi ya maneno ya Kiswahili, Shibuda alisema, “Ninaulizwa maswali mengi juu ya hatma yangu ndani ya Chadema na hili vilevile nimeona ni bora kulizungumza,”.

Kauli hiyo ya Shibuda ilimshtua Spika wa Bunge, Anna Makinda ambaye aliuliza iwapo suala hilo linahusu masuala ya Utalii, “Hilo nalo ni utalii,”

Baada ya kujibu kuwa suala hilo pia linahusu masuala ya maliasili na utalii, Shibuda alisema “Maliasili ya nchi yetu ni siasa bora na utawala bora, nimeona hilo nilizungumze”.Alisema viongozi wa dini kazi yao kubwa ni kumng’arisha binadamu ili aweze kwenda ahera na viongozi wa siasa kazi yao ni kuwa madobi wa kuing’arisha Serikali.

“Nimeamua kulisema kwa kuwa kila mtu (hata wabunge) wananiuliza kama kamati kuu ya Chadema imeniita na kwamba, nitafukuzwa,” alisema Shibuda.

Atuhumu baadhi ya vyombo vya habari
Licha ya kutotaja majina ya magazeti aliyoyatuhumu, Shibuda alisema kwamba kauli zinazoandikwa na kunukuliwa na baadhi ya magazeti ni kauli hatarishi , huku akisisitiza kuwa kauli hizo za vyombo vya habari zinaacha vikwazo kwa wanasiasa.
Alisema kuwa hata Jukwaa la vyombo vya habari nchini lina mazuri na mabaya yake na kwamba apendaye kutumia jukwaa la siasa ni sawa na mtu mpenda fitina.

“Maneno yaliyonukuliwa na viongozi wa Chadema katika vyombo vya habari kwamba mimi ni msaliti si kweli na wala sijavunja msimamo wa uongozi wa kikao cha kamati, nimetofautiana na watu kwa dhamana zao binafsi,” alisema Shibuda.Alisema kuwa hawezi kugandishwa na kukosa demokrasia ya kikatiba ya kutoa maoni yake, na kwamba yoyote anayegeuza au kutumia cheo chake kwa maslahi binafsi hatakuwa na tofauti na Pius Msekwa.

Msekwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara anatuhumiwa kuingilia watendaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), kwa kujihusisha na utoaji wa ofa kwa wafanyabiashara wanaotaka kujenga hoteli za kitalii.

“Mazuri huwa ya baba na mabaya huwa ya mama…, bahari ikichafuka nahodha hupimwa kwa ujasiri wake, nakiri kuchafua hali ya hewa ila napenda kuwaambia kuwa Shibuda ni jasiri,” alisema.

Aliongeza, “Maswa sio Pundapori ina wenyewe na wananchi wa Maswa wamekataa kuporwa mbunge wao kama wanyamapori, CCM ni demokrasia pana na Chadema ni kwa maslahi ya jamii, lakini kila kizuri hakikosi kasoro heshima na busara ndio itatuongoza kufika salama,”.

“Vyama vya siasa vipo kama 12 hivi, vipo vyama maslahi binafsi, jamii, ushirika na Saccos…, mimi kudhalilishwa na kupuuzwa sijali sana kwa kuwa ninaongozwa na ukweli na siwezi kusema uongo,” alisema Shibuda.

Source:Mwananchi
 
Chadema hakiwezi kuwa na watakatifu pekee. Ni jambo lisilowezekana. Wakitaka kumtimua kila msema ovyo watashangaa 2015 hiyo. Hata katika ccm wapo watu wema
 
ni vizuri chadema wakatafakari kwa kina kabla ya kumchukulia hatua,kinachoonekana kwa mh Shibuda ni kutofautiana kimtazamo na wenzake na ndio tabia yake tokea akiwa magamba akitaka ashindane kinang'anyiro cha urais na m..kwere.Kinachotakiwa apewe onyo na apige kimya kwa maendeleo yake ya baadae kisiasa.Apunguze kujiamini sana na atumie busara katika kauli zake.
 
This i would perceive as peak of democracy to the democrats like Dr. Slaa....as secretary gen.of the party he should watch keenly on ths politcal advancement. Its a change we have to admit,he should consider it a strength withn the party extreme. We all knw and aware that such politcal difference are nt common in Tz but we should learn as they happen n c hw we go about them. All mutual success in any political arena demamd political tolerance,an aspect that should be observed frm time to time if true change is a necessity in tz.
 
Mkuu unaweka habari nusu nusu.... ameponda viongozi wa kisiasa hasa wa Chadema kwa udhalimu, na maslahi binafsi.Amesema yeye hatishwi na Kamati Kuu na amewaonya waandishi wa habari wanaobeba maslahi binafsi ndani ya Chama. Wakati anaongea wabunge wa CDM walionekana wanyonge sana
<br />
<br />


Unaposema "Wabunge wa Chadema" walionekana wanyonge sana unataka kutuambia nini?
 
Ndugu zangu nami nimemsikiliza vizuri sana Mheshimiwa Shibuda, ninamheshimu kaongea ukweli. mimi naona viongozi wa Chadema au wanachadema sisi siyo Mungu. Hatuwezi kulazimisha wote tuwaze sawa, Shibuda anauhuru wa kuchangia kile anacho ona sawa.

Mbona shibuda alikuwa hivi hivi hata alipokuwa CCM, ni mara ngapi alikuwa amemtisha JK wakati anataka kugombea Urais kupitia CCM. Tumpe uhuru wake naye
ni hayo tuu
 
CDM hawamuwezi huyo kamanda wa Maswa. Kwanini anaongea bila wasiwasi na viongozi wanakosa majibu. Ujanja wa Mbowe na Slaa umekwama hapo. Huo ni mwiba mkali na mchungu kama mgao wa umeme Mwanza.
 
Nimemsikiliza sana Shibuda tena kwa makini sana. Hili ni jambo linaloweza kuletwa kwenye vikao ambavyo mimi ni mjumbe. No comment for the time being.

Inaonyesha nijinsi gani Shibuda alivyo mtovu wa nidhamu kwani unashindwa kwenda katika vikao vya chama na kuliongelea hilo? au kuitisha waandishi wa habari na kuwaambia na kuwapa onyo ila nafikiri pia na uwezo wa spika wetu au yule aliyekuwa anaongoza hicho kikao anamapungufu makubwa sana.

Hivi kama kuna mada ya kujadili mbele yake yeye analeta story nyingine ina maana gani hii inashangaza sana na spika au aliyekuwa anasimamia kikao alikuwa anamwangalia tu achangie au atoe dukuduku lake moyoni kwa kuwa alikuwa anawapaka viongozi wake na si serikali au chama cha magamba ina sikitisha sana hili.

hivi angekuwa anatoa mipasho kumwelekezea rahisi au mwenyekiti wa ccm angekuwa anamwangalia au angemwambia hiyo mada hapa haipo UDHAIFU MKUBWA SANA HUU JAMANI SIO WA KUUANGALIA NA KUUSHABIKIA
 
shibuda kashaijua hatima yake ndani ya CDM kuwa atafukuzwa tu,..ndio maana anaendelea kuropoka,.ameshalikoroga atulie asubiri hukumu yake..huyu si alishinda kwa kura moja?
 
Viongozi wa CHADEMA jifunzeni kuwa wavumilivu. Mhe. Shibuda ana haki ya kutoa maoni yake na kusikilizwa hata kama anayoyasema hamuyapendi. Uamuzi wowote wa kumfukuza Mhe. Shibuda utakuwa pigo kwa CDM kama ilivyo kwa Arusha! Na kama CDM watashindwa kurudisha kata hizo, basi Mhe. Godbless Lema aanze kuliaga Bunge mapema.....!

Kwenye siasa za vyama vingi, watu kama akina Mhe. Shibuda wapo tu...na wataendelea kuwepo.......Cha msingi ni kupima athari za matamshi na matendo yake kwa chama.

CCM japo inamekumbwa na misukosuko mikubwa ya magamba n.k, lakini bado ni chama chenye viongozi wavumilivu na katika maamuzi yao hawakurupuki......NI MAONI TU!
 
Inasikitisha kama spika alikuwa anamwachia tuuuu asemeutumbo wake hapo bungeni badala ya kuchangia mada iliyokuwa mezani.
 
ile imani ya wengi kuwa ccm imepanda magamba yake kwa chadema inaanza kupenya kwenye upeo wangu shibuda john magale ni mtu wa kutumiwa hana maslahi na machungu na nji hii ni mmoja kati ya vibaraka wa siasa za ufisadi na rushwa si mpambanaji ni jamii za kina mrema na tambwe hizza waroho waroho sana hata hao wana maswa si majahazi wapelekwepelekwe na upepo usio na malengo au dira shibuda unawachosha wana maswa kama ujijui si tuna mapambano ya kweli na tuna uwezo wa kutambua mavi na makande. Kama unawapelekesha wana maswa ni hkhk umekuja kuivuruga cdm. TUMEKUSTKIA HATUNA IMANI NA WW TUNAHITAJI TZ YA UHURU
 
Back
Top Bottom