Bungeni: Shibuda aongelea hatma yake ndani ya CHADEMA!

Mzee wa mipasho wakati anachangia wizara ya maliasili kasema yeye utalii kwake ni utawala bora kwa hiyo anaona aongelee mustakabali wake ndani ya CDM kwani kila siku wabunge wanaamuuliza kama CDM wameshamfukuza.

Amewaonya wahariri wanukuu vizuri kwani wanapotosha, kutokukubaliana kwa hoja na viongozi sio kuonyesha ni muasi, kwahiyo amewaambia wanaomuuliza atafukuzwa lini wamkome yeye anatekeleza maagizo ya CC.
 
Akichangia hoja ya Maliasili na Utalii bungeni leo,amerudia kauli yake ya malipo ya Muha iliyopingana na msimamo wa Cdm. Amesema kuna viongoz maslahi na yeye hatishwi na mavuvuzela.Mimi sio tundapoli hata wanamaswa wanajua. Ameichana cdm kwa mafumbo makalimakali na kusema haogopi chochote.Msije kutuletea viongoz Idd Amin kwa kuelekezwa na siasa za chuki na kutumia vyombo vya habari.
 
Five star Modern Taarabu bado nafasi zipo wazi, Jamaa anaweza chuana na Mzee Yusufu duh mwanaume maneno yamemtoka vuvuzela yeye
 
leo ktk kuchangia bajeti ya mali asili na utalii Mh Shibuda amesema hajawai kukiuka tamko na maagizo ya kamati kuu ya chadema ila wanatofautiana ktk mtazamo baina ya mtu na mtu so kamwe hataogopa mtu ktk kutoa mtazamo na mawazo yake. Pia ameonya magazeti kwa kuandika habari zenye uzushi pia ametoa angalizo magazeti hayo yatatuletea kiongozi kama Iddy Amini wa Uganda.

My take:

Shibuda ameongea mengi tena kwa mafumbo ambayo upande wa pili wa ccm walikuwa wakicheka uku chadema wakiwa kimya na kumsikiliza kwa makini.

Wana JF amesema Yeye ni Tunda la Maswa so hatatokea mtu aje na kulichukua tu pia ametolea mfano kwa kujifananisha kwa kuteswa na kusulubiwa kwa Yesu kama yeye.

Nawasilisha.
 
Mbunge wa Maswa John Magale Shibuda ametumia nafasi aliyopewa kuchangia hotuba ya Mali Asili na Utalii kuwaponda viongozi wake wa Chadema na kwamba wananchi wa jimbo lake wapo nyuma yake.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwaponda waandishi na wahariri wanaobeba ajenda za viongozi wa kisiasa akiwalenga hasa wa Chama chake wanaoendelea udhalimu na maslahi binafsi.

Maneno kama kamati kuu ya Chadema, viongozi dhalimu, kukosekana kwa demokrasia yamejirudia sana kwenye hotuba yake. Wakati akisema hayo wabunge wengi wa Chadema kama Msigwa, Lucy Owenya na Christina Lissu wameonekana wanyonge sana.
 
Napita tu wakuu nitarejea baadae ngoja nisubiri wenye chama watakuja sasa hivi.
 
Akichangia hoja ya Maliasili na Utalii bungeni leo,amerudia kauli yake ya malipo ya Muha iliyopingana na msimamo wa Cdm. Amesema kuna viongoz maslahi na yeye hatishwi na mavuvuzela.Mimi sio tundapoli hata wanamaswa wanajua. Ameichana cdm kwa mafumbo makalimakali na kusema haogopi chochote.Msije kutuletea viongoz Idd Amin kwa kuelekezwa na siasa za chuki na kutumia vyombo vya habari.

Hapo kwenye red ni MWIA(MWIHA) if spelling not mistaken, ni kweli amewaponda sana viongozi wa cdm hasa wanaopenda kutumia vyombo vya habari kumchafua yeye.

Anasema haogopi mtu na yupo tayari kwa lolote kwani watu wake wa Maswa nao wanasubiri maamuzi ya cdm ili wamuunge mkono.Pia amesema Maswa si tunda ambalo kila mtu anaweza kulichuma bali lina wenyewe ambao ni wana Maswa.
 
Watu watakaotaka Shibuda aondolewe chadema watakuwa hawaelewi lengo lake. Shibuda yuko KAZINI, anatamani sana afukuzwe ili malengo yake yatimie. Sasa badala ya kumfukuza, unamwacha ajikaange(kisiasa) kwa mafuta yake mwenyewe.
 
Akichangia hoja ya Maliasili na Utalii bungeni leo,amerudia kauli yake ya malipo ya Muha iliyopingana na msimamo wa Cdm. Amesema kuna viongoz maslahi na yeye hatishwi na mavuvuzela.Mimi sio tundapoli hata wanamaswa wanajua. Ameichana cdm kwa mafumbo makalimakali na kusema haogopi chochote.Msije kutuletea viongoz Idd Amin kwa kuelekezwa na siasa za chuki na kutumia vyombo vya habari.

Aisee huyu jamaa simpendi kuliko wabunge wote wa magamba.
 
hivi shibuda hana bendi ya taarab? mbona hajasifia idea ya kubana posho iliyopelekea kuchangia kwenye mpango dharura wa megawati?
 
Watu watakaotaka Shibuda aondolewe chadema watakuwa hawaelewi lengo lake. Shibuda yuko KAZINI, anatamani sana afukuzwe ili malengo yake yatimie. Sasa badala ya kumfukuza, unamwacha ajikaange(kisiasa) kwa mafuta yake mwenyewe.

Hili ni gamba kwa chadema endapo watamfukuza itabidi waingie gharama kubwa kusafisha hali ya hewa kwani alichoongea leo bungeni ambako sio sehemu yake pia ameacha maswali mengi yasio na majibu mfano huyo kiongozi kama Iddy Amini ni nani?
 
Kuhusu suala la lake la kuenguliwa kasema hamuogopi mtu kachaguliwa na wana Maswa.
Mkuu unaweka habari nusu nusu.... ameponda viongozi wa kisiasa hasa wa Chadema kwa udhalimu, na maslahi binafsi.Amesema yeye hatishwi na Kamati Kuu na amewaonya waandishi wa habari wanaobeba maslahi binafsi ndani ya Chama. Wakati anaongea wabunge wa CDM walionekana wanyonge sana
 
Nimemsikiliza sana Shibuda tena kwa makini sana. Hili ni jambo linaloweza kuletwa kwenye vikao ambavyo mimi ni mjumbe. No comment for the time being.
 
hata wale madiwani wa Arusha walijitapa hivyo hivyo mwisho wa siku wakaishia kuzomewa. Nafikiri ni wakati mzuri kwa CHADEMA kuchukua maamuzi makini dhidi ya huyu jamaa. Tayari wananchi wa Arusha walishauliza juu ya hatua zinazochukuliwa dhidi ya huyu jamaa. Ni dhahiri kwamba hata wananchi wa kawaida wamemchoka. Its high time for him to go now.
 
Huyu mtu hastahili kuendelea kubaki ndani ya chama...Wembe uliotumika kuwaondoa wale wasaliti kule Arusha,utumike pia kwa huyu.
 
Niliwaambia CHADEMA kuwa hakuna haja ya kumpa siku 90 Shibuda (kama magamba), just damp him and move on...

Kwa kweli CDM wameshaniudhi sasa. Ishu ya madiwani wa Arusha iliibuka nyuma kabisa ya upuuzi wa Shibuda, lakini ikashughulikiwa fastafasta. Wanamuogopea nini huyu? Bora hilo jimbo lipotee? Kwani CHADEMA haijiamini?
 
Back
Top Bottom