Bungeni: Shibuda aongelea hatma yake ndani ya CHADEMA!

May be ni uchanga wa siasa zetu ndio maana tunalikuza sana hili jambo.
USA wabunge wa Obama wanampinga live bungeni, lakini kwa bongo ni usaliti lol...

Mkuu tukienda kwa namna hiyo, basi everything sucks in Bongoland.
 
Chadema hakiwezi kuwa na watakatifu pekee. Ni jambo lisilowezekana. Wakitaka kumtimua kila msema ovyo watashangaa 2015 hiyo. Hata katika ccm wapo watu wema

Unamaanisha nini kwa kusema watu wema? Wema kwa yapi? Anyway ebu nitajie hao watu wema wa CCM pengine nitaelewa wema huo upo on what grounds.
 
Ningekuwa sehemu ya viongozi wa Chadema mtu kama Shibuda anayejulikana Tanzania nzima kwamba mropokaji ningemuacha tuu ajikaange mwenyewe labda kama anakisaliti cham katika ngazi ya wilaya na mkoa manake kitaifa sidhani kama wanamuhesabu kama mwanachama hana nyimbo kwa sababu tuhuma zake hakuna hata moja mpya ambayo hatujaisikia hapo zamani kwa hiyo hana nyimbo
 
na mimi ndicho nangojea nione kama atakuwa na nguvu ya kurudi magambani. maana asipoangalia yeye ndiye atakaye poteza kwa sababu CDM ilishafika pale bila yeye, hivyo inaweza songa mbele bila yeye.
Shibuda ndiye atakaye loose more ukilinganisha na Chama. I would fully support kumfukuza Shibuda ili awe mfano . Yeye (Shibuda) atapoteza ubunge (income) na itakuwa siyo rahisi kuhamia chama kingine kwenye uwezo wa kumfanya ashinde uchaguzi.
 
Kuhusu suala la lake la kuenguliwa kasema hamuogopi mtu kachaguliwa na wana Maswa.
Na yuko sahihi sana. Tangu 1992 CHADEMA ipo lakini watu wa Maswa hawakuichagua. Na hata CCM walipomwengua, bado watu wa Maswa waliendelea kumchagua hata alipokuwa nje ya CCM. kwa hiyo pale Maswa anayependwa ni Shibuda, siyo CCM wala CHADEMA. Ni kama Mrema wa Vunjo, wanamchagua tu bila kujali chama gani yuko.
 
Mzee wa mipasho wakati anachangia wizara ya maliasili kasema yeye utalii kwake ni utawala bora kwa hiyo anaona aongelee mustakabali wake ndani ya CDM kwani kila siku wabunge wanaamuuliza kama CDM wameshamfukuza.

Amewaonya wahariri wanukuu vizuri kwani wanapotosha, kutokukubaliana kwa hoja na viongozi sio kuonyesha ni muasi, kwahiyo amewaambia wanaomuuliza atafukuzwa lini wamkome yeye anatekeleza maagizo ya CC.
 
Last edited by a moderator:
Unamaanisha nini kwa kusema watu wema? Wema kwa yapi? Anyway ebu nitajie hao watu wema wa CCM pengine nitaelewa wema huo upo on what grounds.

1-dr alieshindwa upadre mwizi wa wake za wa2 ndio mwema no 1
 
Shibuda hamna kitu kabisa ila siyo kosa lake,nahisi hajitambui kabisa kwamba yuko cdm au ccm au PO2 kazi kweli kweli usimfuatilie sana usije pata pressure ya ubongo.
 
siasa za ukweli , hazina nafasi kwa baadhi ya wana CDM ukitaka ufagiliwe toa porojo za kukandia serikali au CCM. SHIBUDA DAIMA husimama kwenye kile anachokiamini, jadiliana naye kwa hoja sio vitisho.
 
hivi CDM wanangoja nini kufukuza hili pandikizi??au mnasubiri 2015 aje alete vurugu na machafuko ndani ya chama wakati wa kupata mgombea? chinjia mbali hili gamba kunako mapema!
 
Watu watakaotaka Shibuda aondolewe chadema watakuwa hawaelewi lengo lake. Shibuda yuko KAZINI, anatamani sana afukuzwe ili malengo yake yatimie. Sasa badala ya kumfukuza, unamwacha ajikaange(kisiasa) kwa mafuta yake mwenyewe.

Tutamfanya kama CCM tu, kutoshwa wakati wa mchakato! Akimbilie UDP!
 
tatizo sio shibuda bali mfumo mzima wa utawala cdm ni wa mashaka na unatia shaka! Kuna harufu ya ukabila na udini!!

wewe mjinga acheni sera za udini zitawafanya rwanda na burundi-mmekosa cha kuongea?chekechea wewe in mind
 
hivi ni mbunge wa chama gani?
Kama ni wa Chadema namshangaa kwa kukinyea kitanda chake mwenyewe.

Kweli kabisa, maana haingii akilini kuwa yeye siku zote wapinzani wake ni chama chake mwenyewe. Sikumbuki kumsikia akikosoa vyama vingine hasa ccm
 
Tatizo sio shibuda bali mfumo mzima wa utawala CDM ni wa mashaka na unatia shaka! kuna harufu ya ukabila na udini!!

Hivi nyie magamba mbona mnahangaika sana kuidhoofisha Chadema kwa propaganda yenu ya udini na ukabila,hamjui hata nchi mmeiharibu kwa propaganda hiyo,Acheni utoto wenu.
 
Back
Top Bottom