Bungeni: Mbowe aweka msimamo wa posho

Mbowe amezungumza ukweli mtupu. Nawakubali Chadema sasa wanakuwa chama kinachokamilika na 2015 kuna dalili watashinda uchaguzi hata kama CCM watachakachua. Viongozi wa serikalini wamejisahau sana na CCM pia.

Wabunge wa CCM wakikubali posho ziendeleee Chadema nendeni mkawaumize majimboni mwao maana vijijini sasa hivi watu wanaelewa nini kinaendelea nchi na ukame huu wa hela na chakula msumari wa posho unawatosha kuwamaliza wabunge walafi. Hii nchi yetu sote na kodi tunalipa sote kwanini keki iliwe na watu wachache?
 
Nahisi JK na watu wake kila siku wanawaota kona Zitto, Mbowe, Mnyika na makamanda wengine wa CDM akipanga mikakati ya kuwamaliza....ulieni CDM linchi lenu hili sasa hivi mtakabidhiwa.
 
Mboooooooooooooooooooooooweeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!BIG UP KWAKUWATOLEA UVIVU HAO WALAFI WA HELA ZA UMMA KWA STAREHE ZAO
 
basi yaishe mkuu, sote tu askari wa kupambana na adui, tusimpe adui nafasi. nimekuelewa.

Huo ndio uungwana. Tunapingana kisha tunashikana mikono siyo kushikania mapanga. Tupo jahazi moja likitoboka tuanzama wote na najua hujui kuogelea kwa kuwa unatoka nkuhungu!!! teh teh
 
To be honest jamaa amelomga, Big up bro freeman! Lakini wapo watakoibuka na kuanza yale yale ili tu waendelee kumeza mihela
 
Nimesikiliza aliyosema mbowe,nakiri kwamba wafanyakazi wote tulio ngazi ya chini na wananchi kwa ujumla tunatakiwa kulikemea hili. Posho ni malipo yanayo nyanyasa nafasi za watu, taaluma za watu, na kujenga matabaka ya wale wanaosema naweza ni kala na nikavaa au nikafanya kitu chochote wakati wowote kwa sababu ninazo ngawila.

Posho inavunja ari ya wafanyakazi, inaongeza msongo wa akili, inaongeza zinaa na dhuluma, lazima kuwe na maamuzi magumu, zifutwee tena hatua hiyo isingoje iwe sasa.

Wabunge kutoka chama cha magamba lazima hili walione kwamba Posho ni Janga la kitaifa na lazima tiba yake ipatikane sasa na sio kesho.
 
Huo ndio uungwana. Tunapingana kisha tunashikana mikono siyo kushikania mapanga. Tupo jahazi moja likitoboka tuanzama wote na najua hujui kuogelea kwa kuwa unatoka nkuhungu!!! teh teh


hahahahahahaha!! mkuu najua kuogelea, mkuu LUSHOTO tuna vijito kibao na kutokana na milima huwa vinatengeneza mabwawa (swimming pool za kiswahili) huko ndo nimejifunzia kuogelea, hata hivyo tusiwakatishe tamaa wasiojua kuogelea maana hatutazama na 2015 tutafika ng'ambo ya pili.
 
Nimesikiliza aliyosema mbowe,nakiri kwamba wafanyakazi wote tuliongazi ya chini na wananchi kwa ujumla tunatakiwa kulikemea hili,Posho ni malipo yanayo nynyasa nafasi za watu,taaluma za watu,na kujenga matabaka ya wale wanaosema naweza ni kala na nikavaa au nikafanya kitu chochote wakati wowote kwa sababu ninazo ngawila,Posho inavunja ari ya wafanyakazi,inaongeza msongo wa akili,inaongeza zinaa na dhuluma,lazima kuwe namaamuzi magumu,zifutwee tena hatua hiyo isingoje iwe sasa,Wabunge kutoka chama cha magamba lazima hili walione kwamba ni Posho ni Janga la kitaifa na lazima tiba yake ipatikane sasa na sio kesho

Froida wasifute posho zenye umuhimu kama usafiri na matibabu na nyenginezo kama ni umuhimu wa posho kuwapo. Lakini zijumuishwe katika kodi ili zikatwe kodi. Hilo litaongeza mapato ya nchi na kukuza ustawi wa jamii wa mfanyakazi Tanzania. Posho nyenginezo ifanyike kama nchi zilizoendelea kwamba kama ni vikao wateuliwe watu maalumu walipwe ndani ya mishahara yao posho za vikao (ambayo itakatwa kodi). Ikisha kila mwaka wazitoe taarifa katika jamii tufahamu wanalipwa kiasi gani ili tujue kodi tunazowalipa wamefanya kazi kiasi gani ili wakizembea tuwatimue ofisini.

Kama ni chakula na malazi warudishiwe kiasi walichotumia hotelini na hivyo kama mtu amekaa hoteli bei mbaya atajijua mwenyewe kwani ofisi itaamua ni mwisho kiasi gani walipwe na hivyo ukitumia zaidi ya hapo utajilipia mwenyewe. Vile vile tiketi ya ndege mfano wakiweka afisa au mkurugenzi mwisho wa tiketi kulipiwa ni $1300 na hivyo mkurugenzi akipanda business class shauri yake ajue anafidiwa $1300 tu nyenginezo analipia mwenyewe.

Mfumo wa sasa haufai na ni janga kwani mpaka wasomi kama maprofessa wameona hailipi kuwa mhadhiri na hivyo wanakimbilia kugombea ubunge kwani hakuna anayependa kuteseka maisha haya.
 
UMASIKINI SIO BABA YETU ILA UNALETWA NA KUKUZWA NA ccm TUKIAMUA TUTAWAONDOA CCM NA KUUTOKOMEZA UMASIKINI,TUUNGANE TUAMUE SASA
 
Safi sana!

There are currently 209 users browsing this thread. (75 members and 134 guests)
 
Kwa kweli CDM imejidhihirisha kwamba wao ni wazalendo na wana umia sana kuona pesa za sisi wananchi masikini zinatumika hovyo hovyo badala ya kuwasaidia wananchi. Mabadaliko ya kweli yataletwa na CDM na sisi tunaochukuzwa na chama cha magamba kuihujumu nchi yetu bila huruma. Muda umefika sasa wa kuwatoa hawa CCM na sababu tunazo, nia tunayo na uwezo tunao 2015. Tunataka viongozi wenye uwezo wa kufikiri sawa sawa na siyo wavivu wa kufikiri kama walivyo ccm! Tunataka kiongozi akiongea watu wananyamaza kimya- mfano mzuri Mbowe leo bungeni! Tunataka vichwa vyenye uwezo wa kuchambua mada mbalimbali na kuleta mawazo mbadala, tunataka viongozi wenyewe ujasiri kama mbowe, zito na wenzake wa CDM! Siyo viongozi wa kusinzia bingeni kama wa ccm, wakishtuka wanapiga kofi meza hata bila ya kujua nini kinachoendelea, hatutaki viongozi wanasifia kwa unafiki, waongo, wazinzi, walafi, waliojaa tamaa ya kujilimbikizia mali, na wavivi wa kusoma na kufikiri kama wa ccm! Yani kama hawa ccm hata kusoma alama za nyakati zinawashinda, kwanini tuendelee nao? Tunataka mabadiliko hata kama hayo mabadiliko yatakuwa mabaya, tunabadilisha kila baada ya miaka mitano hadi tuwapate wenye uzalendo ila siyo ccm kwa sasa.
 
Hili la posho ni janga na kwa sisi tulio huku ngazi za kijiji, kata na halmashauri tunaona kila siku kazi za maendeleo zinavyokwamishwa na kitu posho. Mkurugenzi au DC anaalikwa kwenye jambo nyeti la wilaya anakacha anaenda kwenye semina ya kikundi ili mradi kuna posho.

Ningekuwa najua jinsi ya kuattach hapa jamvini ningewapa maandiko ya siku za nyuma kuhusu kansa ya posho- help plz!!
 
Hili la posho ni janga na kwa sisi tulio huku ngazi za kijiji, kata na halmashauri tunaona kila siku kazi za maendeleo zinavyokwamishwa na kitu posho. Mkurugenzi au DC anaalikwa kwenye jambo nyeti la wilaya anakacha anaenda kwenye semina ya kikundi ili mradi kuna posho.

Ningekuwa najua jinsi ya kuattach hapa jamvini ningewapa maandiko ya siku za nyuma kuhusu kansa ya posho- help plz!!

Mkuu hata huko kijijini ukiomba ardhi watu wakikaa kwenye mkutano wa kijiji unatakiwa utoe posho!! Kama kuna mtu anabisha ajitokeze hapa. Posho imejikita kuanzia chini kabisa. Posho posho posho!!
 
TAFADHALI VYOMBO VYOTE VYA HABARI!

Kwa kuzingatia uzalendo na maslahi ya umma, kwa kumwogopa Mungu na kutumia vipawa na previleges zenu kama wanahabari, tunaomba muitawanye, muandike kwa mapana na kuhakikisha kuwa kila mtanzania, wakuangalia TV, Radio, magazeti, blogs nk, wanapata hotuba ya Mh Mbowe. Watawala watapata joto ya jiwe na kujisikia aibu, toka ndani wakati dhamira zao zinawasuta, maana ukweli ni ukweli tu hata kama utaupaka matope au kuukanusha.

Tunataka Serikali ikate matumizi, posho ni kiashiria tu, tunasema tumechoka kutumika na kunyonywa na watu tuliowakasimu madaraka.

Kama alivyozoea kusema Mtikila miaka ya 90, saa ya ukombozi ni sasa! This is your corporate social responsibility, tutawakumbuka kwenye historia ya kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye ukoloni wa ndani, tulionao sasa!
 
Mwenye masikio ya kusikia asikie, na wale wote watakaojifanya hawajaelewa, baso waanze kufunga virago 2015.

Pamoja na hayo yote, kuna yale sasa ambayo yanafanyika nyuma ya pazia ambayo watanzania waliowengi si rahisi kuyajua. Mfano mmoja ni huu; mara baada ya kutangazwa baraza jipya la mawaziri, Naibu Waziri mmoja (jina kapuni kwa sasa) aliyepangiwa nyumba ya serikali kule maeneo ya Masaki, alikataa kuingia ktk Nyumba hiyo hadi anunuliwe furniture mpya. Baadhi ya vitu alivyovitaka ni kufungiwa DSTV na kununuliwa flat Screen (3) kubwa za nchi 52. Kitanda alichochagua ni cha sh. mil 15. In summary, furniture tu ziligharimu zaidi ya shi millioni 140,000. Huyu ni just naibu Waziri, ukizidisha kwa baraza zima unapata Sh. Ngapi? Hizo ni mabilioni mengine ambayo yanapotea bila kuwekwa wazi.

Pendekezo, hembu CAG tufanyie audit kisha utuhabarishe, na yeyote aliye na network serikalini, jaribu kufuatilia utaambiwa ukweli.

Source: from a private supplies company which usually do furnish furniture to Gvt houses and offices.
 
Nimeipenda hiyo wanajf, ufike wakati viongozi waonyenshe uzalendo kwa vitendo badala ya kuuimba majukwaani huku moyoni hawamanishi hicho. haiwezekani mtu kwenye inchi masikin kama tanzania asafiri kwa bussiness class badala ya econmy class. ni muda mwafaka watu wa magamba kujiweka pepembeni kama kazi imewashinda na kuwapa wengine wafanye kazi.
 
Back
Top Bottom