lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,159
- 33,397
Freeman Mbowe sio mtu wa Kawaida, amini nakuambia.
Huyu mwamba amezaliwa kwenye familia ya kitajiri, Baba yake alikua ni tahiti na alimwezesha Mwlm Nyerere kifedha kwenda NY Marekani kudai uhuru. Hakukulia kwenye Manisha ya shida, Amezaliwa ama amekulia katikati ya jiji la Dar es salaam, Sea view Upanga.
Pamoja na utajiri wao mwingine lakini ndio waliokua wamiliki wa Mbowe hotel na baadae club bilicanas, club iliyokua maarufu sana hapa jiji Kabla ya kubomolewa na mwendazake.
Kwa kifupi Mbowe ni tahiti Hadi leo. Mbowe ndie mwenyekiti wa Chadema alieijenga chadema kwa jasho na damu binafsi. Amepitia mateso, machungu na magumu Sana katika kuijenga chadema kuliko mwanasiasa yoyote wa Tanzania kuliko hata mwalimu Nyerere alivyokua akidai uhuru wa Tanganyika.
Alishuhudia tukio baya kabisa la kushambulia kwa mbunge na mwanachama wa chama anachokiongoza, Mbunge Lissu,
Wanachama machachari na mabwege aliowatafuta na kuwafanya wakapata majina makubwa nchini walimsaliti na wakaondoka huku wakimkashifu,lakini hakuwajibu kitu, Aliwakaribisha kiungwana baadhi ya wanasiasa kuja chadema na kupata haki sawa lakini baadae wakarudi waalikotoka huku wakimtukana. Hawa wote Mbowe hakujibizana nao.
Mbowe kila alipopata nafasi ya kuongea na taifa hakusita kuomba maridhiano ya kitaifa. Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais Marehemu Magufuli katika sherehe za uhuru huko CCM Kirumba Mwanza alipompa Mbowe nafasi ya kusema machache, Mbowe aliomba Maridhiano ya kitaifa.
Mbowe leo hii Yuko ndani kwa kesi ya Ugaidi lakini sio mara ya kwanza kuwekwa ndani, Mbowe aliwekwa ndani miezi Bila kufikishwa mahakama na mara nyingine aliwekwa yeye na viongozi wenzake wa Chadema. Mbowe na wenzake walitoka kwa kulipiwa faini iliyochangishwa nchi mzima na wananchi wenye mapenzi mema.
Unaweza kukuuliza Kwa nini Mbowe amekubali kumpigia haya wakati hana shida yoyote, ni tajiri kama kama majajiri wengine walioamua kujiegemeza CCM ili wapate Kinga za utajiri wao?
Lowoasa alihamia chadema akatikiswa kidogo tu akarejea CCM, Halikadharika Sumaye, Nyalandu na wengi kama hao.
Tazama wabunge wa Ndugai akina Mdee, kuona tu hawatakua wabunge wote wakatimkia Bungeni kinyume na Sheria I'll wapate posho.
Mbowe ni Mzalendo wa kweli, ni mtaka mabadiliko wa kweli ni mpenda haki wa kweli.Mbowe hayupo kwenye siasa kwa sababu ya njaa,Mbowe kweli ni mtetezi wa wanyonge na ndio kazi ya chadema na chama makini cha siasa. Mbowe kwa sasa anashitakiwa kwq kosa la hatari na kubwa Sana kosa la Ugaidi. Angekua mtu mwingine angeshanyoosha mikono na kurudi kufanya biashara. Siku zote ukimuona Mtu huyu huonesha sura ya Tanasamu hata akiwa mahakama. Sikuwahi kujua kama Mbowe ana kaka Mwanajeshi, tena Major General wa JWTZ Marehemu. Ukisikia kuna watu wakweli Dunia I Mbowe ni mmoja wao.
Mbowe alaiondokewa na wanasiasa mahili kama Zito, Slaa, Mwigamba, Arfi, Mashinji, Mdee, Bulaya, Shonza, Safari, Katambi, Mwambe, kutoka na wengine wengi, lakini Mbowe hajateteleka na Chadema Bado inapendwa.
Pamoja na jitihada zote za kumtoa Mbowe kwenye mstari na ndani ya misimamo yake, jitihada za kutaka kuiua chadema lakini chadema bado ni tishio kubwa Sana na Bado inaaminika na wananchi wengi Sana.
Chadema imeimarika zaidi na Mbowe amekuwa imara zaidi kuliko wakati wowote ule.
Mbowe hana shida za kiuchumi lakini anapigania haki za kisiasa katika Taifa hilo.
Kumbuka siasa ndio kila kitu.
Unapozungumzua siasa unazungumzia bei za umeme, maji, cementi, mafuta,chakula, elimu,usalama, katiba, amani, haki, furaha, sayasi, imani, utamaduni, mali biashara na Kila kitu, kwani vitu hivyo hupangwa na kuamuliawa na wanasiasa.
Mbowe anakosa nini?
Mbowe sio Gaidi.

- Mbowe amebomolewa club bilicanas,
- Ameharibiwa mashamba yake ya mbogamboga,
- Alinusurika kupigwa risasi siku ya Akwilina,
- Alipigwa na watu wasiojulikana akiwa Dodoma.