Bungeni: Mbowe aweka msimamo wa posho

Haihitaji sayansi ya rocket kujua kuwa kinachopingwa na CHADEMA ni "mfumo" wa kulipa posho hizo. Kila mmoja anayepinga anaweza kuchukua hatua zake mwenyewe. Ndio Zitto akachukua hatua alizochukua. Hata huko CCM kuna watu waliwahi na wako na msimamo tofauti wa kichama. Walichukua hatua zao na kila mtu anajua walichokipata. Marehemu Kolimba ni mmoja wao.

Mfumo ni zaidi ya mtu mmoja mmoja!! Inatosha kabisa kupinga mfumo. Hata Mbowe akigomea hizi pesa, bila shaka utahoji kwanini Lissu na wengine hawajafanya hilo. Ili hao nao wasistahili, kubadilisha mfumo au sera hiyo ni muhimu zaidi kuliko Zitto na Makamba!

Mkuu naona kama unaenda kusiko. Kwanza ujue CDM ni CDM na inaipinga CCM hivyo basi si busara kujipima kwa CCM kwa makosa iliyofanya/waliyofanya na CDM iyafanye!
Hapo kwenye wekundu: Suala la posho siyo la mtu binafsi kwa CDM; hii ni sera ya CHAMA inatakiwa kuchukua hatua za kichama siyo kila mtu achukue hatua zake mwenyewe. Ingekuwa siyo sera ya Chama bali ni utashi wa mtu binafsi ingekuwa sawa kwa Zitto kufanya alichofanya. Lakini hapa tunaonelea sera na kiranja mkuu wa CDM ni Mbowe akiwa ndani ya Bunge na nje kama mwenyekiti hivyo basi alitakiwa kuonyesha mfano wa utekelezaji wa sera ya chama.
 
Unapotunga uongo kama huu hakikisha unakuwa mwangalifu, mbona posho za wabunge hazitolewi dirishani kwa mhasibu kama unavyoeleze wewe! wacha majungu yasiyo na maana wewe! mtu mzima ovyooo!

unatafsiri neno kwa neno,utapa sana shida,hilo limetumika tu kuonyesha watu wamekua wakisaini hizo posho mzee,acha kukimbilia vitu vyepesi nenda hoja kwa hoja
 
Mkuu naona kama unaenda kusiko. Kwanza ujue CDM ni CDM na inaipinga CCM hivyo basi si busara kujipima kwa CCM kwa makosa iliyofanya/waliyofanya na CDM iyafanye!
Hapo kwenye wekundu: Suala la posho siyo la mtu binafsi kwa CDM; hii ni sera ya CHAMA inatakiwa kuchukua hatua za kichama siyo kila mtu achukue hatua zake mwenyewe. Ingekuwa siyo sera ya Chama bali ni utashi wa mtu binafsi ingekuwa sawa kwa Zitto kufanya alichofanya. Lakini hapa tunaonelea sera na kiranja mkuu wa CDM ni Mbowe akiwa ndani ya Bunge na nje kama mwenyekiti hivyo basi alitakiwa kuonyesha mfano wa utekelezaji wa sera ya chama.

strong point...angalau wewe unaonekana kuelewa kinachozungumziwa hapa na maudhui yake hawa jamaa wanakurupuka kutetea tetea tu hata mambo ya ovyo mradi kafanya bwana mkubwa basi yatapakwa mafuta mradi tu udhaifu wa bwana usionekane,wanaleta ile haditi ya mkubwa akombi mboga akikomba wanasema kaipenda eti!amekomba mbogo amekomba tu wala msitafute neno zuri la kuelezea ukombaji wake wa mboga!
 
kamanda kwa hiyo unataka kusema dogo yanaweza kumkuta kama ya chacha wange,maana ya chacha na kolimba ni kama yanalingana lingana hivi.mungu apishie mbali usiwe na maana hiyo kaka.

Unaposema "mfumo"wakati watu wanpokea pesa ambayo tungeweza kuwapa madaktari una maanisha nini?na pia kilichotakiwa sio zitto au yeyote kuachiwa peke yake bali kiongozi awaongoze wabunge wote kugoma na kususia vikao kama kipindi kile aliwaongoza kutoka bungeni siyo yeye anapokea zitto ndio anagoma,wabunge wengine watajali kugoma kwa zitto wakati bosi wanasaini nae kuchukua?

Jitahidi kuandika majina ya watu kwa kuanza na herufi kubwa, Mungu huanza kwa herufi kubwa.

Wanpokea ni kitu gani?

chacha wange ni yupi huyo ?

Bange ni mbaya sana hasa kama hujala
 
strong point...angalau wewe unaonekana kuelewa kinachozungumziwa hapa na maudhui yake hawa jamaa wanakurupuka kutetea tetea tu hata mambo ya ovyo mradi kafanya bwana mkubwa basi yatapakwa mafuta mradi tu udhaifu wa bwana usionekane,wanaleta ile haditi ya mkubwa akombi mboga akikomba wanasema kaipenda eti!amekomba mbogo amekomba tu wala msitafute neno zuri la kuelezea ukombaji wake wa mboga!

Jifunze kuandika, zingatia matumizi ya herufi kubwa, sidhani kama kuna great thinker wa kukuelewa kwa uandishi huu!
 
Jitahidi kuandika majina ya watu kwa kuanza na herufi kubwa, Mungu huanza kwa herufi kubwa.

Wanpokea ni kitu gani?

chacha wange ni yupi huyo ?

Bange ni mbaya sana hasa kama hujala

Huyo alikuwa anakurupuka kuandika awahi posho yake ya siku
 
MwanaJF, Kim Kadrash,

Kama ungefuatilia mijadala Bungeni mwaka uliopita, ungeona kwamba Mwenyekiti wa CDM ndiye aliyeibua mjadala kuwa posho na marupurupu kwa wabunge haviendani na hali halisi ya umaskini wa nchi yetu Tanzania. Aliendelea zaidi na kusema anarudisha gari shangingi la Serikali alilopewa kutumia binafsi kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni.

Baada ya hapo ndipo Zitto Kabwe alipoingia katika mkakati wa kuto-saini orodha ya Mahudhurio katika Kamati za Bunge, ambayo hutumiwa na maafisa wa Bunge kuwalipa posho Wabunge wanao hudhuria vikao vya Kamati za Bunge. (Nifafanue kwamba Wabunge wote wanalipwa mshahara kila mwezi kama watumishi wengine wa umma. Lakini wanapohudhuria vikao vya Kamati za Bunge wanalipwa posho, yaani sitting allowance. Wakati huo posho ilikuwa ni Sh. 70,000 kwa siku).

Wakati wa enzi za Nyerere, watumishi Serikalini tulilipwa posho kama tulisafiri nje ya miji ya makazi yetu. Inaonekana kwamba kwa vile viongozi wengi sasa hawaishi Dodoma, mtindo wa kulipwa posho umeingizwa ili kuboresha mapato ya wabunge. Mimi naona huu ni upotoshaji, kwa vile kazi ya wabunge ni kujadili miswada na sera za Serikali, ama ukumbini mwa Bunge au nje katika kamati za Bunge.

Maoni yangu kuhusu maslahi ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ni kwamba apatiwe gari na Serikali kama mawaziri, lakini sio lazima liwe shangingi linalogharimu mamilioni mengi. Liwe tu ni gari linalomudu hali halisi ya barabara zetu Tanzania. Of course, kama MwanaCDM nakubaliana na msimamo kuwa posho ya Sh. 200,000 katika mazingira ya umaskini wa Tz is outrageous. Hata hivyo ni vizuri kupigania general review of salaries ya watumishi wote wa umma.
 
Nimekua nikijiuliza kila siku bila kupata majibu sababu za wabunge hususan wa chadema wakiongozwa na mbowe kutoonesha dhana ya uwajibikaji wa pamoja kwa vitendo;....

Wakati mbunge kijana ZITTO KABWE alipogomea kupokea posho ya kukaa kitako kwa vitendo licha ya vitisho vya spika kwamba atapoteza ubunge wake kwa kutoweka saini ya kupokea pesa hizo haramu wabunge wengine wa chama cha ZITTO wakiongozwa na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni wamekua wakionekana kwenye dirisha la mhasibu wa bunge wakipanga foleni dirishani hapo kuchukua fedha hizo haramu.

Je ni kwanini mbowe hakuitumia kofia yake ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kumuunga mkono Zitto na kushawishi kambi nzima ya upinzani kugomea posho hiyo haramu na badala yake kusisitiza pesa hiyo kama ipo na haina kazi ipelekwe kwenye sekta ya afya inakohitajika sana?

Nawasalisha.

Pesa sabuni ya roho kaka
 
Mkuu kumbukumbu zinanionyesha kwamba suala la Posho lilianzia kwenye Budget ya Wizara ya Fedha (Kivuli) chini ya ZZK, baada ya hapo ZZK akaandika kuzisusa posho za vikao akasema zipelekwe kwenye mfuko gani sijui. Kelele zikapigwa akaamua tena kwamba hata huko zisiende na hazitaki na akaamua kutosaini daftari la mahudhurio.
Ikaja wakati KUB anachangia hotuba ya PM ndio naye kaongelea mambo ya posho; akapinga posho kama ulivyosema. Baadaye akarudisha gari ya KUB. Hapa nina maana kwamba KUB alirudisha gari baada ya ZZK kuwa amezikataa posho (kama si sahihi nitarekebishwa tu). Suala la posho ni sera ya CDM na hilo suala lipo kwenye budget mbadala (kivuli). Baadaye tukaambiwa ilitokea sokomoko wakati wabunge wa CDM wakijadili kuhusu kuzikataa posho (kumuunga mkono ZZK); wengi waliiipinga hii sera ya kujiondelea posho (japokuwa hawajaifuta) na ikawa hivyo ndio maana ZZK akabaki peke yake akizikataa (kwa upande wa CDM). Wengi ndani ya CDM wameishia tu kusema posho hazifaoi lakini wanazichukua.

Kuhusu KUB: Kwa mujibu wa sheria ana hadhi kama ya Naibu Waziri wa Serikali. Hivyo anastahili kila kitu ambacho Naibu Waziri anastahili. Hivi sasa KUB ana V8.
 
kwa hiyo mnataka kila siku tuwe tunaiongolea ccm na watu wake tu,chadema hapana,kwanini lakini hamtaki chadema ipate publicity?
Maralia Sugu, hata ujibadili kama kinyonga ni kazi bure tu. Tuambie chama chako ni cha kifalme? Mbona mnarithishana nyazifa bila aibu!!!! Nauye na mwanawe, Makamba na mwanae, Marehemu Sumari na mwanae, Sitashangaa kuona Maralia Sugu Junior humu JF.
 
Kwa habari nilizonazo na za uhakika posho hailipwi dirishani bali kwenye bank account. Ila, ni lazime attendance isainiwe na ni the same attendance hutumika kwa mahudhurio na ni mandatory kuijaza. Kwa hiyo ukijaza ile ni lazima ulipwe utake usitake. Usipoijaza hujaja kazini. Ni sawa na ukitema nakupiga panga ukimeza nakuchoma kisu. Wafanyeje hawa wasiozitaka posho?
 
Nimekua nikijiuliza kila siku bila kupata majibu sababu za wabunge hususan wa chadema wakiongozwa na mbowe kutoonesha dhana ya uwajibikaji wa pamoja kwa vitendo;....

Wakati mbunge kijana ZITTO KABWE alipogomea kupokea posho ya kukaa kitako kwa vitendo licha ya vitisho vya spika kwamba atapoteza ubunge wake kwa kutoweka saini ya kupokea pesa hizo haramu wabunge wengine wa chama cha ZITTO wakiongozwa na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni wamekua wakionekana kwenye dirisha la mhasibu wa bunge wakipanga foleni dirishani hapo kuchukua fedha hizo haramu.

Je ni kwanini mbowe hakuitumia kofia yake ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kumuunga mkono Zitto na kushawishi kambi nzima ya upinzani kugomea posho hiyo haramu na badala yake kusisitiza pesa hiyo kama ipo na haina kazi ipelekwe kwenye sekta ya afya inakohitajika sana?

Nawasalisha.

Lengo lako hasa ni kumchafua Mbowe na kutaka kuwaaminisha wana CHADEMA kuwa kiko segregated kama serekali ilivyo segregated. Utashindwa tuuu
 
Kwa habari nilizonazo na za uhakika posho hailipwi dirishani bali kwenye bank account. Ila, ni lazime attendance isainiwe na ni the same attendance hutumika kwa mahudhurio na ni mandatory kuijaza. Kwa hiyo ukijaza ile ni lazima ulipwe utake usitake. Usipoijaza hujaja kazini. Ni sawa na ukitema nakupiga panga ukimeza nakuchoma kisu. Wafanyeje hawa wasiozitaka posho?
Tata nyangomboli hili suala naona hujalifuatilia kwa makini. Zitto alitishiwa katika misingi hiyohiyo baada y kusema kwamba hasaini. Hakusaini. Wakasema watamfukuza kwa kuwa atakuwa anaonekana hajahudhuria vikao, Zitto akasema kuna ushahidi mwingi tu wa kuonyesha kuwa anahudhuria ikiwa ni pamoja na kuchangia na kurekodiwa kwenye hansard. Kama CDM wote watazikataa hakuna mtu wa kuwafukuza.
 
zito ni mnafiki anapinga posho huku anataka wabunge walipwe milioni 12 na laki tano kwa mwezi.kwa kutumia sheria ya utawala wa bunge(the national assembely administration act) ya mwaka 1988.kabwe aliwataka wabunge ktk kikao cha utangulizi kikao cha 6,alitaka itumike njia raisi kuongeza mishahara kuliko posha ili wananchi wasijuwe,jambo lilipingwa sana na wabunge wengi ata wa ccm na kudai anakataa posho huku akizitaka kwa mlango wa nyuma.ni fisadi tu huyo walisema wabunge wenzaka ana bilioni 3 bank kapata wapi?
 
Vichwa vingine vina mdomo, macho, pua na masikio tu, ndani ni shimo la panya buku.
 
zito ni mnafiki anapinga posho huku anataka wabunge walipwe milioni 12 na laki tano kwa mwezi.kwa kutumia sheria ya utawala wa bunge(the national assembely administration act) ya mwaka 1988.kabwe aliwataka wabunge ktk kikao cha utangulizi kikao cha 6,alitaka itumike njia raisi kuongeza mishahara kuliko posha ili wananchi wasijuwe,jambo lilipingwa sana na wabunge wengi ata wa ccm na kudai anakataa posho huku akizitaka kwa mlango wa nyuma.ni fisadi tu huyo walisema wabunge wenzaka ana bilioni 3 bank kapata wapi?

Mnafiki utakuwa wewe ndugu!
Swala la kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa idara zote na ngazi zote lipo very clear, anachopinga zitto ni mfumo wa kulipana posho katika kazi abazo ni wajibu wako wa kila siku.
 
Najua vyakuchangia hapa ni vingi sana, ila mimi labda niulize kitu. kama sisi wananchi ndo 2naowaweka hawa wala posho madarakani, tatizo lipo wapi hadi 2nalalamika kiasi chote hiki? si tumetoka kwenye uchaguzi hivi juzi tu, tulishindwa nini?
 
Back
Top Bottom