CHADEMA mmepoteza mwelekeo, msimamo, hamna sera, mmekuwa wababaishaji

Almalik mokiwa

Senior Member
Jun 5, 2020
147
157
Hivi nyie CHADEMA ni nani aliye waroga?

Anaandika Almaliki Mokiwa.

Katika nchi yetu ya amani (Tanzania) tumebarikiwa kuwa na vyama vingi vya siasa, wakati ACT, CHAUMA, CUF na vyama vingine kama CHADEMA vikiwa vyama pinzani, na CCM kuwa chama tawala, CHADEMA imejitanabaisha kuwa chama kikuu cha upinzani.

Hapo nyuma tumeshuhudia mtifuano mkali nyakati za uchaguzi, ambapo CCM imekuwa ikikinzana vikali na Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Hali ya kisiasa kwa sasa ni tofauti na hapo nyuma, ambapo kwasasa Chadema imeonekana kupoteza ushawishi na kukosa radha kwa wananchi. Ni wazi kuwa epepo umebadilika hasa baada ya Mwenyekiti CHADEMA (Mh. Mbowe) kuachiwa huru na mahakama baada ya kubambikiwa kesi ya ugaidi na kukamilika kwa mpango wa maridhiano baina ya CHADEMA na Serikali iliyoundwa na CCM.

Nawaandikia CHADEMA ukweli mchungu ili mje mtukane kwasababu, mkikosa hoja matusi ndio silaha yenu kubwa.

CHADEMA kwasasa wameishiwa sera, hawana mikakati tena ya kuishawishi jamii ili iwaamini kuwa, CHADEMA hii ya sasa itatupeleka katika nchi ya kanaani yenye mito ya maziwa na miti ya mitende.

CHADEMA imekosa misimamo na kuwa babaifu, tuliwaamini, wameamua kuungana na watasha kwa jina la maridhiano, na sasa wanafanya siasa za mapambio kuwasifu watawala.

Katika andiko hili, nitaelekeza hoja zangu kuonyesha ni namna gani CHADEMA wamegeuka na kuamua kuonyesha hadharani ngozi yao halisi waliyokuwa wakiificha miaka yote kwa maneno matamu na ahadi zilizojaa sukari nyingi.

Pesa za michango ya wananchi kwa CHADEMA

CHADEMA imekuwa ikikusanya michango kutoka kwa wananchi, ikiwemo mkakati wa ukusanyaji fedha uliopewa jina la "Join the chain" katika mpango ule, wananchi hatukurudishiwa mrejesho juu ya kiasi cha fedha kilicho kusanywa, na mtiririko wa matumizi yake.

Suala hili lilisababisha watu wengi kuhoji katika mitandao ya kijamii bila kupata majibu.

20230327_111559.jpg

Tarehe 23 katika medani za siasa, Edwin Odemba alifanikiwa kumhoji Mh Tundu Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, katika moja ya maswali aliyo uliza na kukosekana kwa majibu thabiti ni kuhusu kiasi cha pesa kilichokusanywa kwenye operation ya "join the chain" na matumizi yake.

Kitu ambacho hatukukitarajia ni majibu aliyojibu mh Tundu Lissu, alidai kuwa (nanukuu) "Sijui ni kiasi gani ilikusanywa kwenye Join the Chain” baada ya majibu haya, tulijiuliza swali la msingi sana, inakuwaje makamu mwenyekiti wa chama hafahamu kiasi cha pesa kilicho kusanywa kutoka kwa wananchi wakati anaingia kamati kuu?

Kamati inayo pokea ripoti ya fedha na kuijadili, inawezekana vipi yeye asifahamu, afahamu katibu mkuu wa chama pekee?

Hii inaonyesha kuwa, kuna ubabaifu umefanyika. Kama mmeanza ubabaishaji kabla hatujawapa mchi, tukiwapa nchi si mtakula mpaka miti nyie?

Mvutano kati ya CHADEMA na ACT kuhusu maridhiano

Miaka miwili iliyopita hapo nyuma, wakati mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, mh Zitto Rumayangwa Kabwe akitafuta maridhiano na serikali, alikutana na pingamizi kali kutoka kwa CHADEMA. Wanachama na viongozi wa CHADEMA walimshambulia vilivyo kwa maneno makali.

Lakini sasa tunashuhudia CHADEMA wakiwa meza moja na serikali kujadili mustakabali na mwenendo wa nchi yetu kwa kivuli cha maridhiano, hii inatafsirika kama CHADEMA kufata nyayo za ACT Wazalendo Licha ya kwamba CHADEMA ndiyo ilikuwa ya kwanza kutaka maridhiano na serikali ya JPM na kukutana na pingamizi kutoka kwa CCM, lakini ni lazima itafsirike kuwa wao ndio wamefata nyayo kwasababu, ACT wamekuwa wakwanza kufanikisha suala la maridhiano.

20230326_174119.jpg

Swali la msingi la kujiuliza, ni kuwa CHADEMA wao wana haki zaidi ya kufanya maridhiano na Serikali, kuliko vyama vingine vya siasa kama ACT? au tuendelee kwenda na methali ya kiafrika isemayo "kunya anye kuku, akinya bata kaharisha?" Haya hapa (kwenye video) mahojiano ya Peter Msigwa kuhusu maridhiano, ni full kujin'gata. Hakuna majibu ya kueleweka.

CHADEMA, hamna haki zaidi kuliko wengine.

Kukataa kwa Uchaguzi Mkuu 2020 na kuendelea kuchukua ruzuku

Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya mwaka 1992 ya Tanzania, vyama vya siasa vinaweza kupata ruzuku kutoka Serikalini kama yatakidhi vigezo vilivyowekwa, kigezo kimojawapo ni Kuwa na angalau asilimia tano ya kura za jumla zilizopigwa katika uchaguzi wa Rais, Wabunge, au Udiwani.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, CHADEMA walitangaza wazi kuwa hawautambui uchaguzi ule na kuupa jina la "UCHAFUZI WA MWAKA 2020". Kufanya hivyo ni kujitoa moja kwa moja katika haki ya kupokea Ruzuku ya vyama vya siasa vilivyo shinda uchaguzi.

Sasa kama CHADEMA hawautambui uchaguzi, kwanini wanaendelea kupokea Ruzuku kutoka serikalini? Si waliweka msimamo wa kususia ruzuku wakati wa JPM, Kwanini sasa wamen'gatuka na kuendelea kupokea Ruzuku? Msimamo wao ni upi?

Edwin Odemba alipofanikiwa kumuhoji Mh. Tundu Lissu, aliuliza swali lifuatalo;
Screenshot_20230327-122118.png

Baada ya swali hilo, alijibu kuwa “Msimamo wa chama cha siasa siyo sheria za Dini kiasi kwamba haibadiliki, Tumechukua Ruzuku kwa sababu kuna mambo yamebadilika” video ya maelezo yake hii hapa;

Mh. Tundu Lissu baada ya kuulizwa kuhusu ubunge wa Aidan khenani aliendelea kusema kuwa hawautambui ubunge wake, lakini hili haliwazuii wao kuchukua Ruzuku, nanukuu “Hatutambui Ubunge wa Aidan Khenani kama ambavyo hatutambui Ubunge wa wale Wabunge 19 lakini Ruzuku tutachukua”
Video hii hapa chini.

Swali; kwanini wachukue ruzuku ya wabunge wasio wao? Majibu anayojibu Mh Tundu Lissu hayatoshi.

Kuhusu mapenzi ya jinsia moja
Juzi alipokuwa anahojiwa mh Lema, kuhusu mtazamo wake juu ya masuala ya ushoga, alipata kigugumizi na kuanza kutafuna maneno, mh Lema ni mtu mwenye ushawishi mkubwa katika jamii, tulitegemea kusikia jibu la moja kwa moja kuhusu kupinga utamaduni wa ndoa za jinsia moja, alipo hojiwa alijibu kuwa yeye anaamini katika biblia, na kusema kuwa, imeandikwa mpende jirani yako, hivyo mashoga wana haki ya kuishi. Pia alidai kuwa, hakuna haki ya kuuawa kwa mashoga kwasababu nao ni wanadamu.

Nilijiuliza maswali mengi, kuwa, ni biblia gani inalinda haki za mashoga? Yeye anasoma biblia ipi? Ilinibidi nirudi kwenye biblia kutazama Mungu amesemaje kuhusu ndoa za jinsia moja. Hebu turudi kwenye biblia tupitie mistari ifuatayo.

- Mambo ya Walawi 18:22 "Usilale na mwanamume kama na mwanamke; ni machukizo."

- Mambo ya Walawi 20:13 "Ikiwa mtu mume akilala na mwanamume kama na mwanamke, wote wawili wamefanya machukizo; watauawa; damu yao itakuwa juu yao."

- Warumi 1:26-27 : "Kwa ajili hiyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao zisizo na adabu, wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa yale yasiyo ya asili, na wanaume vivyo hivyo wakaacha jinsi ya asili pamoja na wanawake, wakawa na tamaa mbaya. wao kwa wao, wakifanya mambo ya aibu pamoja na wanaume, na kujipatia nafsini mwao adhabu iliyostahili kwa ajili ya upotevu wao.”

Hii pia imeonyesha ni kwa namna gani Lema ametumia kichwa kama kifuniko cha shingo, kujibu swali linalogusa jamii kwa kujificha chini ya kivuli cha biblia ambayo haijui.

Kuhusu demokrasia wanayoipigania CHADEMA

Title ya chama na vitendo ni kama mtenganiko wa mbingu na ardhi, CHADEMA wanahamasisha demokrasia ikiwa wao wenyewe hawajifungamanishi nayo.

Tangu Mbowe awe mwenyekiti CHADEMA ni muda mrefu sasa, kwanini asin'gatuke na kuwaachia kiti wengine? Hii inaonyesha kuwa, wanahamasisha demokrasia ya makaratasi. Utawala wa kidemokrasia hauhusishi uongozi wa milele, kwanini Mbowe yuko kitini kama mwenyekiti zaidi ya miaka 10?

Alipo hojiwa Mh. Makamu Mwenyekiti CHADEMA, Tundu Lissu, alikutwa na kigugumizi na kujibu kuwa, Mbowe hatukuwa mwenyekiti milele, ila uenyekiti wake utakoma pale ambapo watu watasema wanataka mabadiliko. Chama chenye katiba dhaifu (ambayo haionyeshi muda wa ukomo wa kiti cha mwenyekiti), kinawezaje kutuongoza kudai katiba mpya itakayo tenganisha mamlaka ya mihimili ya utawala?

CHADEMA, rekebisheni kwanza katiba yenu ndipo mtuongoze kufikia upatikanaji wa katiba mpya.

Bodaboda kuwa kazi ya laana

Mh. Godbless Lema alipokuwa anahutubia umma, alidai kuwa bodaboda ni kazi ya laana. Wakatokea wanaharakati kuunga mkono kauli ya Lema huku wimbi kubwa la watu wakipinga kauli hii.

Kuna bodaboda wanalea familia zao, wanasomesha na kulipa kodi ya pango, kazi hii sio laana bali ni mpango wa vijana kutaka kujinasua kwenye tatizo la ajira, bodaboda zimekuja kupunguza idadi ya vijana wanaoshinda vijiweni, wezi na hata vibaka.

Sasa wamejiajiri wanatengeneza pesa mpaka 50000 kwa siku, pesa ambayo hata mwalimu halipwi kwa mwezi. Leo itakuwaje kazi ya laana? Serikali haiwezi kuajiri kila mtu na ndo maana duniani hakuna nchi iliyofanikiwa kutatua tatizo la ajira kwa 100%
Screenshot_20230327-131229.png

Hata leo hii CHADEMA wakipewa nchi, hawataweza kutatua tatizo la ajira bali kurahisisha upatikanaji wa ajira na kuweka mazingira mazuri ya watu kujiajiri. Vijana wamejiajiri, waacheni wapige kazi, wakiacha kazi ya boda boda kwa tafsiri ya "kazi ya laana" utawaruhusu waje kula kwako?

Hata kule USA nchi imeimarika kiuchumi lakini hawajafanikiwa kutatua tatizo la ajira, watu zaidi ya milioni hawana ajira. Na bado kuna asilimia kubwa ya watu walio jiajiri.
Screenshot_20230327-132842.png

US ni role model wa nchi nyingi kiuchumi, lakini bado tatizo la ajira limekuwa kizungumkuti.
Screenshot_20230327-131336.png

Mh. Godbles Lema, kudai bodaboda kuwa kazi ya laana kwasababu ya kupigwa na upepo siku nzima na kuambulia 7000 ni sawa na kuzilaani na kazi zingine kama saidia fundi (fundi ujenzi) ambao wanashinda juani na kukimbia na vipande vya tofali mabegani huku vumbi la cement likiwa limewajaa mpaka kwenye kope huku wakiambulia ujira wa shilingi 7000 tu kwa siku.

Ulipaswa kuilaumu serikali ya CCM kushindwa kuwawekea bodaboda mazingira mazuri ya kufanya kazi yao na sio kuwatwisha laana. Umewakosea sana bodaboda.

Kukosa sera na kufanya siasa za mapambio

Baada ya kuondolewa kwa zuio haramu la mikutano ya hadhara, tarehe 21 CHADEMA walikuwa mwanza wakizindua mikutano ya hadhara. Walikuwepo wajumbe wa kamati kuu na baadhi ya waandamizi wakiongozwa na mh Freeman Aikel Mbowe.

Siku kama hiyo tumekuwa tukiisubiri kwa muda mrefu, tukitegemea makubwa kutoka CHADEMA ila mambo yamekuwa tofauti baada ya mwenyekiti kupanda jukwaani. Mwenyekiti aliingia kufanya siasa za mapambio za kusifu watawala. Kutoa shukrani sio dhambi, ila hakukuwa na ulazima wa kushukuru kwa kupamba na kutoa onyo kali kwa wanachama wake, tena jukwaani.

Huu sio wakati wa kusifu watawala, ajenda za msingi ni nyingi, ingependeza kama msisitizo ungeelekezwa huko. Umakini na utashi unahitajika zaidi kuungana na CCM chini ya kivuli cha maridhiano hakutaifanya Chadema kushinda uchaguzi mwaka 2025. CCM ina mizizi, imekomaa na imewekeza kwenye chama. Kwa siasa hizi, hakuna mahali mtaenda wanaChadema.

Namalizia kusema kuwa, Chadema mnapaswa kufanya siasa zilizoshiba na sio hizi siasa mfu za kujitengenezea maadui watatu (JPM, ACT na CCM).

Mbadala wa kupanda jukwani na kumsema JPM kwa mabaya, mzungumze sera na mikakati yenu namna mtakavyoweza kuivusha nchi yetu kutoka kwenye kupanda kwa gharama za maisha, kuboresha elimu, kupunguzwa kwa gharama za mitandao, kuboresha sekta ya afya, kuboresha sekta ya kilimo, madini, utalii, usafirishaji na hata uvuvi.

Tuelezeni namna ambavyo mtatuwekea vijana mazingira mazuri ya ajira, iwe ni kuajiriwa au kujiajiri, elezeni namna mtakavyo tuhakikishia utatikanaji wa umeme na maji mara tu baada ya kuitoa nchi yetu kwenye mikono dhwalim ya hawa CCM.

Acheni kupambana na JPM, hamtafanikiwa kumchafua kwasababu bado anaishi katika mioyo ya watu. Hata hivyo ameshaa pumzika na hayupo tena. Acheni kuwafanya ACT kama maadui zenu, kaeni mezani msuke sera na mipango itakayo ibadilisha nchi yetu kuwa Ulaya.

Mwisho.

almalikmokiwa@gmail.com
 
Umejitahidj kuandika ila sijasoma.

Ila tambua kuwa kila mwenye nia na jambo lake lazima ajifunze kula na kipofu na kuwazuga maboya.

Chadema ingekuwa haina upinzani wa kweli ungeshanunuliwa yote na kufa mda tu. Kumbuka jiwe alitumia kila njama kuiua CHADEMA na hakufanikiwa, so propaganda zako hazina maana kwa tunaofahamu.

This is deep, lakini kwa uzoefu wetu wa miaka kadhaa tunawajua hao jamaa ni wabishi na wajuaji kwelikweli.

Hata siku wakishika madaraka (God forbid) watakuwa mdikteta zaidi ya Iddi Amini.

Ndio maana wanasema Tanzania tunacho chama kimoja tu cha siasa, nacho ni CCM. Hao wengine ni mkusanyiko wa wanaharakati, wafanyabishara wa siasa, madalali n.k
 
Ni furaha kwako. Kula shiba lala, si kuvuja kwa pakacha bwana.
 
This is deep, lakini kwa uzoefu wetu wa miaka kadhaa tunawajua hao jamaa ni wabishi na wajuaji kwelikweli.

Hata siku wakishika madaraka (God forbid) watakuwa mdikteta zaidi ya Iddi Amini.

Ndio maana wanasema Tanzania tunacho chama kimoja tu cha siasa, nacho ni CCM. Hao wengine ni mkusanyiko wa wanaharakati, wafanyabishara wa siasa, madalali n.k
kwamba kuna mtu angetegemea wewe bwabwa la sukuma gang na nguruwe wa uvccm useme kuwa ccm sio chama, hovyo kabisa
 
Umeandika uharo mtupuuuu , unataka ujue mahesabu ya kitu ambacho hukuchangia ?¿ Ina kuuma nn chadema kupoteza mwelekeo ??? Si ndo furaha yenu chadema ikifa ??? ccm inachangishaga mabilion ya pesa kwa matajiri, ni lini waliwahi kukutangazia ??? Alafu njoo ujibu hili swali, ccm kwa mwezi wanapata ruzuku kutoka serikalini sh ngp???
 
akikujibu hilo swali la mwisho natoka jf.
 
Hivi nyie CHADEMA ni nani aliye waroga?

Anaandika Almaliki Mokiwa.

Katika nchi yetu ya amani (Tanzania) tumebarikiwa kuwa na vyama vingi vya siasa, wakati ACT, CHAUMA, CUF na vyama vingine kama CHADEMA vikiwa vyama pinzani, na CCM kuwa chama tawala, CHADEMA imejitanabaisha kuwa chama kikuu cha upinzani.

Hapo nyuma tumeshuhudia mtifuano mkali nyakati za uchaguzi, ambapo CCM imekuwa ikikinzana vikali na Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Hali ya kisiasa kwa sasa ni tofauti na hapo nyuma, ambapo kwasasa Chadema imeonekana kupoteza ushawishi na kukosa radha kwa wananchi. Ni wazi kuwa epepo umebadilika hasa baada ya Mwenyekiti CHADEMA (Mh. Mbowe) kuachiwa huru na mahakama baada ya kubambikiwa kesi ya ugaidi na kukamilika kwa mpango wa maridhiano baina ya CHADEMA na Serikali iliyoundwa na CCM.

Nawaandikia CHADEMA ukweli mchungu ili mje mtukane kwasababu, mkikosa hoja matusi ndio silaha yenu kubwa.

CHADEMA kwasasa wameishiwa sera, hawana mikakati tena ya kuishawishi jamii ili iwaamini kuwa, CHADEMA hii ya sasa itatupeleka katika nchi ya kanaani yenye mito ya maziwa na miti ya mitende.

CHADEMA imekosa misimamo na kuwa babaifu, tuliwaamini, wameamua kuungana na watasha kwa jina la maridhiano, na sasa wanafanya siasa za mapambio kuwasifu watawala.

Katika andiko hili, nitaelekeza hoja zangu kuonyesha ni namna gani CHADEMA wamegeuka na kuamua kuonyesha hadharani ngozi yao halisi waliyokuwa wakiificha miaka yote kwa maneno matamu na ahadi zilizojaa sukari nyingi.

Pesa za michango ya wananchi kwa CHADEMA

CHADEMA imekuwa ikikusanya michango kutoka kwa wananchi, ikiwemo mkakati wa ukusanyaji fedha uliopewa jina la "Join the chain" katika mpango ule, wananchi hatukurudishiwa mrejesho juu ya kiasi cha fedha kilicho kusanywa, na mtiririko wa matumizi yake.

Suala hili lilisababisha watu wengi kuhoji katika mitandao ya kijamii bila kupata majibu.

View attachment 2567381

Tarehe 23 katika medani za siasa, Edwin Odemba alifanikiwa kumhoji Mh Tundu Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, katika moja ya maswali aliyo uliza na kukosekana kwa majibu thabiti ni kuhusu kiasi cha pesa kilichokusanywa kwenye operation ya "join the chain" na matumizi yake.

Kitu ambacho hatukukitarajia ni majibu aliyojibu mh Tundu Lissu, alidai kuwa (nanukuu) "Sijui ni kiasi gani ilikusanywa kwenye Join the Chain” baada ya majibu haya, tulijiuliza swali la msingi sana, inakuwaje makamu mwenyekiti wa chama hafahamu kiasi cha pesa kilicho kusanywa kutoka kwa wananchi wakati anaingia kamati kuu?

Kamati inayo pokea ripoti ya fedha na kuijadili, inawezekana vipi yeye asifahamu, afahamu katibu mkuu wa chama pekee?

View attachment 2567402
Hii inaonyesha kuwa, kuna ubabaifu umefanyika. Kama mmeanza ubabaishaji kabla hatujawapa mchi, tukiwapa nchi si mtakula mpaka miti nyie?

Mvutano kati ya CHADEMA na ACT kuhusu maridhiano

Miaka miwili iliyopita hapo nyuma, wakati mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, mh Zitto Rumayangwa Kabwe akitafuta maridhiano na serikali, alikutana na pingamizi kali kutoka kwa CHADEMA. Wanachama na viongozi wa CHADEMA walimshambulia vilivyo kwa maneno makali.

Lakini sasa tunashuhudia CHADEMA wakiwa meza moja na serikali kujadili mustakabali na mwenendo wa nchi yetu kwa kivuli cha maridhiano, hii inatafsirika kama CHADEMA kufata nyayo za ACT Wazalendo Licha ya kwamba CHADEMA ndiyo ilikuwa ya kwanza kutaka maridhiano na serikali ya JPM na kukutana na pingamizi kutoka kwa CCM, lakini ni lazima itafsirike kuwa wao ndio wamefata nyayo kwasababu, ACT wamekuwa wakwanza kufanikisha suala la maridhiano.

View attachment 2567420

Swali la msingi la kujiuliza, ni kuwa CHADEMA wao wana haki zaidi ya kufanya maridhiano na Serikali, kuliko vyama vingine vya siasa kama ACT? au tuendelee kwenda na methali ya kiafrika isemayo "kunya anye kuku, akinya bata kaharisha?" Haya hapa (kwenye video) mahojiano ya Peter Msigwa kuhusu maridhiano, ni full kujin'gata. Hakuna majibu ya kueleweka.

View attachment 2567424
CHADEMA, hamna haki zaidi kuliko wengine.

Kukataa kwa Uchaguzi Mkuu 2020 na kuendelea kuchukua ruzuku

Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya mwaka 1992 ya Tanzania, vyama vya siasa vinaweza kupata ruzuku kutoka Serikalini kama yatakidhi vigezo vilivyowekwa, kigezo kimojawapo ni Kuwa na angalau asilimia tano ya kura za jumla zilizopigwa katika uchaguzi wa Rais, Wabunge, au Udiwani.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, CHADEMA walitangaza wazi kuwa hawautambui uchaguzi ule na kuupa jina la "UCHAFUZI WA MWAKA 2020". Kufanya hivyo ni kujitoa moja kwa moja katika haki ya kupokea Ruzuku ya vyama vya siasa vilivyo shinda uchaguzi.

Sasa kama CHADEMA hawautambui uchaguzi, kwanini wanaendelea kupokea Ruzuku kutoka serikalini? Si waliweka msimamo wa kususia ruzuku wakati wa JPM, Kwanini sasa wamen'gatuka na kuendelea kupokea Ruzuku? Msimamo wao ni upi?

Edwin Odemba alipofanikiwa kumuhoji Mh. Tundu Lissu, aliuliza swali lifuatalo;View attachment 2567463
Baada ya swali hilo, alijibu kuwa “Msimamo wa chama cha siasa siyo sheria za Dini kiasi kwamba haibadiliki, Tumechukua Ruzuku kwa sababu kuna mambo yamebadilika” video ya maelezo yake hii hapa;
View attachment 2567468

Mh. Tundu Lissu baada ya kuulizwa kuhusu ubunge wa Aidan khenani aliendelea kusema kuwa hawautambui ubunge wake, lakini hili haliwazuii wao kuchukua Ruzuku, nanukuu “Hatutambui Ubunge wa Aidan Khenani kama ambavyo hatutambui Ubunge wa wale Wabunge 19 lakini Ruzuku tutachukua”
Video hii hapa chini.

View attachment 2567476
Swali; kwanini wachukue ruzuku ya wabunge wasio wao? Majibu anayojibu Mh Tundu Lissu hayatoshi.

Kuhusu mapenzi ya jinsia moja
Juzi alipokuwa anahojiwa mh Lema, kuhusu mtazamo wake juu ya masuala ya ushoga, alipata kigugumizi na kuanza kutafuna maneno, mh Lema ni mtu mwenye ushawishi mkubwa katika jamii, tulitegemea kusikia jibu la moja kwa moja kuhusu kupinga utamaduni wa ndoa za jinsia moja, alipo hojiwa alijibu kuwa yeye anaamini katika biblia, na kusema kuwa, imeandikwa mpende jirani yako, hivyo mashoga wana haki ya kuishi. Pia alidai kuwa, hakuna haki ya kuuawa kwa mashoga kwasababu nao ni wanadamu.

View attachment 2567483
Nilijiuliza maswali mengi, kuwa, ni biblia gani inalinda haki za mashoga? Yeye anasoma biblia ipi? Ilinibidi nirudi kwenye biblia kutazama Mungu amesemaje kuhusu ndoa za jinsia moja. Hebu turudi kwenye biblia tupitie mistari ifuatayo.

- Mambo ya Walawi 18:22 "Usilale na mwanamume kama na mwanamke; ni machukizo."

- Mambo ya Walawi 20:13 "Ikiwa mtu mume akilala na mwanamume kama na mwanamke, wote wawili wamefanya machukizo; watauawa; damu yao itakuwa juu yao."

- Warumi 1:26-27 : "Kwa ajili hiyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao zisizo na adabu, wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa yale yasiyo ya asili, na wanaume vivyo hivyo wakaacha jinsi ya asili pamoja na wanawake, wakawa na tamaa mbaya. wao kwa wao, wakifanya mambo ya aibu pamoja na wanaume, na kujipatia nafsini mwao adhabu iliyostahili kwa ajili ya upotevu wao.”

Hii pia imeonyesha ni kwa namna gani Lema ametumia kichwa kama kifuniko cha shingo, kujibu swali linalogusa jamii kwa kujificha chini ya kivuli cha biblia ambayo haijui.

Kuhusu demokrasia wanayoipigania CHADEMA

Title ya chama na vitendo ni kama mtenganiko wa mbingu na ardhi, CHADEMA wanahamasisha demokrasia ikiwa wao wenyewe hawajifungamanishi nayo.

Tangu Mbowe awe mwenyekiti CHADEMA ni muda mrefu sasa, kwanini asin'gatuke na kuwaachia kiti wengine? Hii inaonyesha kuwa, wanahamasisha demokrasia ya makaratasi. Utawala wa kidemokrasia hauhusishi uongozi wa milele, kwanini Mbowe yuko kitini kama mwenyekiti zaidi ya miaka 10?

Alipo hojiwa Mh. Makamu Mwenyekiti CHADEMA, Tundu Lissu, alikutwa na kigugumizi na kujibu kuwa, Mbowe hatukuwa mwenyekiti milele, ila uenyekiti wake utakoma pale ambapo watu watasema wanataka mabadiliko. Chama chenye katiba dhaifu (ambayo haionyeshi muda wa ukomo wa kiti cha mwenyekiti), kinawezaje kutuongoza kudai katiba mpya itakayo tenganisha mamlaka ya mihimili ya utawala?

View attachment 2567511
CHADEMA, rekebisheni kwanza katiba yenu ndipo mtuongoze kufikia upatikanaji wa katiba mpya.

Bodaboda kuwa kazi ya laana

Mh. Godbless Lema alipokuwa anahutubia umma, alidai kuwa bodaboda ni kazi ya laana. Wakatokea wanaharakati kuunga mkono kauli ya Lema huku wimbi kubwa la watu wakipinga kauli hii.

Kuna bodaboda wanalea familia zao, wanasomesha na kulipa kodi ya pango, kazi hii sio laana bali ni mpango wa vijana kutaka kujinasua kwenye tatizo la ajira, bodaboda zimekuja kupunguza idadi ya vijana wanaoshinda vijiweni, wezi na hata vibaka.

Sasa wamejiajiri wanatengeneza pesa mpaka 50000 kwa siku, pesa ambayo hata mwalimu halipwi kwa mwezi. Leo itakuwaje kazi ya laana? Serikali haiwezi kuajiri kila mtu na ndo maana duniani hakuna nchi iliyofanikiwa kutatua tatizo la ajira kwa 100%View attachment 2567523
Hata leo hii CHADEMA wakipewa nchi, hawataweza kutatua tatizo la ajira bali kurahisisha upatikanaji wa ajira na kuweka mazingira mazuri ya watu kujiajiri. Vijana wamejiajiri, waacheni wapige kazi, wakiacha kazi ya boda boda kwa tafsiri ya "kazi ya laana" utawaruhusu waje kula kwako?

Hata kule USA nchi imeimarika kiuchumi lakini hawajafanikiwa kutatua tatizo la ajira, watu zaidi ya milioni hawana ajira. Na bado kuna asilimia kubwa ya watu walio jiajiri.View attachment 2567531
US ni role model wa nchi nyingi kiuchumi, lakini bado tatizo la ajira limekuwa kizungumkuti.View attachment 2567537
Mh. Godbles Lema, kudai bodaboda kuwa kazi ya laana kwasababu ya kupigwa na upepo siku nzima na kuambulia 7000 ni sawa na kuzilaani na kazi zingine kama saidia fundi (fundi ujenzi) ambao wanashinda juani na kukimbia na vipande vya tofali mabegani huku vumbi la cement likiwa limewajaa mpaka kwenye kope huku wakiambulia ujira wa shilingi 7000 tu kwa siku.

View attachment 2567539
Ulipaswa kuilaumu serikali ya CCM kushindwa kuwawekea bodaboda mazingira mazuri ya kufanya kazi yao na sio kuwatwisha laana. Umewakosea sana bodaboda.

Kukosa sera na kufanya siasa za mapambio

Baada ya kuondolewa kwa zuio haramu la mikutano ya hadhara, tarehe 21 CHADEMA walikuwa mwanza wakizindua mikutano ya hadhara. Walikuwepo wajumbe wa kamati kuu na baadhi ya waandamizi wakiongozwa na mh Freeman Aikel Mbowe.

Siku kama hiyo tumekuwa tukiisubiri kwa muda mrefu, tukitegemea makubwa kutoka CHADEMA ila mambo yamekuwa tofauti baada ya mwenyekiti kupanda jukwaani. Mwenyekiti aliingia kufanya siasa za mapambio za kusifu watawala. Kutoa shukrani sio dhambi, ila hakukuwa na ulazima wa kushukuru kwa kupamba na kutoa onyo kali kwa wanachama wake, tena jukwaani.
View attachment 2567547

Huu sio wakati wa kusifu watawala, ajenda za msingi ni nyingi, ingependeza kama msisitizo ungeelekezwa huko. Umakini na utashi unahitajika zaidi kuungana na CCM chini ya kivuli cha maridhiano hakutaifanya Chadema kushinda uchaguzi mwaka 2025. CCM ina mizizi, imekomaa na imewekeza kwenye chama. Kwa siasa hizi, hakuna mahali mtaenda wanaChadema.

Namalizia kusema kuwa, Chadema mnapaswa kufanya siasa zilizoshiba na sio hizi siasa mfu za kujitengenezea maadui watatu (JPM, ACT na CCM).

Mbadala wa kupanda jukwani na kumsema JPM kwa mabaya, mzungumze sera na mikakati yenu namna mtakavyoweza kuivusha nchi yetu kutoka kwenye kupanda kwa gharama za maisha, kuboresha elimu, kupunguzwa kwa gharama za mitandao, kuboresha sekta ya afya, kuboresha sekta ya kilimo, madini, utalii, usafirishaji na hata uvuvi.

Tuelezeni namna ambavyo mtatuwekea vijana mazingira mazuri ya ajira, iwe ni kuajiriwa au kujiajiri, elezeni namna mtakavyo tuhakikishia utatikanaji wa umeme na maji mara tu baada ya kuitoa nchi yetu kwenye mikono dhwalim ya hawa CCM.

Acheni kupambana na JPM, hamtafanikiwa kumchafua kwasababu bado anaishi katika mioyo ya watu. Hata hivyo ameshaa pumzika na hayupo tena. Acheni kuwafanya ACT kama maadui zenu, kaeni mezani msuke sera na mipango itakayo ibadilisha nchi yetu kuwa Ulaya.

Mwisho.

almalikmokiwa@gmail.com
WAJINGA MNAZIDI KUONGEZEKA ULIYOYAANDIKA HAYA ZINGEKUWA NI NOTES KWA WATOTO WAKO WANGEFAULI MITIHANI CHADEMA IPO IMARA NDIO MAANA HATA RAIS ANAFANYA NAYO MARIDHIANO PUNGUZA UJINGA
 
CHADEMA imekuwa ikikusanya michango kutoka kwa wananchi, ikiwemo mkakati wa ukusanyaji fedha uliopewa jina la "Join the chain" katika mpango ule, wananchi hatukurudishiwa mrejesho juu ya kiasi cha fedha kilicho kusanywa, na mtiririko wa matumizi yake.

Suala hili lilisababisha watu wengi kuhoji katika mitandao ya kijamii bila kupata majibu.
Aisee..

Dogo, acha porojo za vijiweni.

Ni lini ccm walitoa mrejesho wa mchanganuo wa makusanyo na matumizi ya michango kama hiyo hapo chini wanayokusanya nchi nzima kila mwaka?!
👇👇

Kama una mchanganuo tuwekee hapa..
 
kwamba kuna mtu angetegemea wewe bwabwa la sukuma gang na nguruwe wa uvccm useme kuwa ccm sio chama, hovyo kabisa
What happened to "no hate no fear"? 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣, You are spewing a lot of hate.

Wait....... 🤔, It has been updated to 'No honey 🍯 no fear 😋'
 
Back
Top Bottom