Bungeni: Mbowe aweka msimamo wa posho

Nchi hii.
1. Viongozi wana safiri business class kwenda nje ya nchi huku wanao tupa misada wakipanda econimic class
2. Posho inabidi wabunge wachukue uamuzi mgumu sana
3. Viongozi wanatumia magari mapya ya serikali, je ni wangapi wakistafuu wana uwezo wa kuyanunua mapya wakisha stafu?

Kwa kifupi mkuu ameongoe sana na makinda ilibidi aongeze mda makusudi

Ha ha ha Alijishau ile ni Sindano ya Ganzi nadhani Katibu wa Bunge ilibidi amkumbushe Mh Anapitisha Muda ha ha a
 
Anasema ni viongoz leo hii wanatembelea magari ya kifahari lakin wakistaaf wananunua Mark II, vitara nk. Leo hii wanatumia magari ya kifahari sababu wanajua pesa ipo serikalin na leo hii wakisafiri kwa ndege hutaka Kusafiria First clas je ni wangap wakistaaf hupanda ndege kwa safari za ndan na hata wakipanda ndege wangapi husafiria First class?.
 
Watu wagumu kweli kuziachia hizi PESA... pesa mbele mauti nyuma.... pesa mbele uzalendo nyuma.....

Duh hata Marijani Rajabu aliliona hilo miaka mingi iliyopita:

Pesa pesa eeeeee
pesa ndiyo sabuni ya rohoo, mwenye pesa eeeee
mwenye pesa siyo mwenzio nasemaaaa.........

mwenye pesa akifikaaa, watu husimaa aaaaa
pesa pesa eeee......
 
Kama huwezi kuweka taarifa kamili ni bora ukachangia za wengine.sasa unataka tukueleweje?uoneshe ukomavu wa fikra mkubwa kama mwanajamii mwenye malengo ya kuelimisha jamii sio kukurupuka tu,so unataka tukuulize kasema nini ndo utueleze sio?haya kasema nini kuhusu posho?
 
Mbowe ni mzalendo wa kweli! Watanzania lazima tubadilike, wakati wa kuachana na viongozi wasioweka maslahi ya taifa mbele umepita, 2015 ni wakati wa kuitupilia mbali CCM!!
 
hii inakera sana watu kuweka tittles hapa badala ya kuweka information sasa hapo unataka sisi tuchngie nini ningekuwa na uwezo ningedelete hiki ki uzi.....
 
Wanakera sana hawa waanzisha thread kwani sie wote tunaangalia bunge? uh!!
 
Anasema ni viongoz leo hii wanatembelea magari ya kifahari lakin wakistaaf wananunua Mark II, vitara nk. Leo hii wanatumia magari ya kifahari sababu wanajua pesa ipo serikalin na leo hii wakisafiri kwa ndege hutaka Kusafiria First clas je ni wangap wakistaaf hupanda ndege kwa safari za ndan na hata wakipanda ndege wangapi husafiria First class?.

Aliyekuwa waziri kwenye serikali ya Mkapa, Kilontsi Mpologomi, nimemkuta anakopa spare za kufunga kwenye gari lake pale mtaa wa Libya, baada ya kuondoka yule mwenye duka akawa analalamika sana kwamba huyu bwana anapenda kukopa halafu kulipa kwa mbinde, kumbe walishazoea vya dezo serikalini.
Na hiyo ndio siri ya wastaafu wengi kufa mapema mara baada ya kustaafu. Haya maisha ya kitaa watuachie wenyewe wabishi wa mjini.
 
Hadi spika mwenyewe alikuwa mpole hakuna cha mtu kuomba muongozo wala taarifa,hakuna cha lukuvi wala olesendeka maana hawa wawili ndio wanakiherere cha kuomba muongozo na taarifa.

Huyo Sendeka ni ***** wa mwisho. Madini ya Tanzanite yanapatikana katika Jimbo lake tu hakuna sehemu yeyote hapa Dunian utayapata. Lakini cha kushangaza Jimbo lake ndo la kwanza kwa Umaskini hapa Tanzania limepitwa na jimbo analotokea Mh Zitto kabwe ambao wao wanalima tu mihogo
 
Amewapa vidonge vyao, ni ngumu kumeza ila lazima kieleweke tumechoka na hao wanafiki magamba!
 
Hii ni nchi ambayo huwezi hata kujieleza kwa wengine jinsi tulivyo. Hatuwezi kupata mtu makini kuwa Rais, waziri mkuu na hata kupata 1st 11 ya timu ya mpira.

Pinda alipoongea kuteteta posho sikuweza kuelewa kama ana kichwa au ni kifuu cha nazi. Tatizo kubwa ilikuwa kujidai kutumia lugha ya upole ili aonekane ni mwema au muungwana kama zilivyo sifa za watu wa CCM. Baadaye eti anasema posho zinatumiwa na wabunge kuwagawia wapiga kura wao nje ya Bunge!! Nonsense!!

Kwa ujumla lazima tukubali kama kweli hicho ndo kizazi kinachostahili kuwa cha wanasiasa wanaofaa kutuongoza, basi hatuna haja ya kuwa na nchi.
 
isije kuwa kisebusubu na kiroho papo.

Hongera chadema kama mu wasema kweli na mkatekeleza
 
Hii ni nchi ambayo huwezi hata kujieleza kwa wengine jinsi tulivyo. Hatuwezi kupata mtu makini kuwa Rais, waziri mkuu na hata kupata 1st 11 ya timu ya mpira.

Pinda alipoongea kuteteta posho sikuweza kuelewa kama ana kichwa au ni kifuu cha nazi. Tatizo kubwa ilikuwa kujidai kutumia lugha ya upole ili aonekane ni mwema au muungwana kama zilivyo sifa za watu wa CCM. Baadaye eti anasema posho zinatumiwa na wabunge kuwagawia wapiga kura wao nje ya Bunge!! Nonsense!!

Kwa ujumla lazima tukubali kama kweli hicho ndo kizazi kinachostahili kuwa cha wanasiasa wanaofaa kutuongoza, basi hatuna haja ya kuwa na nchi.

Kwa hiyo akiwa kama Waziri mkuu anatuambia wananchi twende bungeni tukawe ombaomba kwa wabunge?
 
Huwez amin kwa mara ya kwanza leo ameongea mpinzani ukumbi mzima ulikua kimyaaa!. Hadi niliona kama muda wamempa mchache vile? Maana mpaka ye mwenyewe akatingisha kichwa alipoambiwa muda umekwisha.
 
Back
Top Bottom