Bring back Wema

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
7,484
5,142
Washabiki wenye mapenzi ya dhati na Wema Sepetu wamekwazwa na tabia za Wema na maisha yake yasiyokuwa na muelekeo hivyo kuamua kuzindua kampeni ya bring back our Wema Sepetu.

Kampeni hii imezinduliwa rasimi ikiwa na lengo LA kumrudisha Wema kwenye mstari na kumkumbusha juu ya wajibu wake katika kuitengeneza future yake baada ya kufulia kusiko mfano.

Pia mashabiki hao wamesema wamechoshwa na tabia ya watu kumtumia Wema kutimiza malengo yao.

Ameshauriwa afungue mradi wowote wa kumuingizia kipato, aachane na mashoga n.k.

Mashabiki hao wamedai kampeni hii haitakoma hadi Wema abadilike na kuonesha muelekeo.

My take: Wema amezungukwa na team njaa na mbulula unadhani kuna kitu hapo?
Kama kwa jirani yako kumeandi ‘Mbwa Mkali' na unasikia huwawanaibiwa, usimpuuze mbwa yule kuwa hafanyi kazi yake au sio mkali kama wanavyosema. Ukitaka kujua ukweli ingia kwao bila hodi.
Hii inaweza kukusaidia sana kumuamsha kwa haraka ili ajitambue na afanye kazi yake kama mlinzi.

Matokeo yake naamini utayapenda pia na utafikiria tena sababu iliyopelekea wezi kupenya eneo hilo.
Nakujengea picha hii na kile kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kampeni iliyoanzishwa na baadhi ya mashabiki wa Wema Sepetu wanaomtaka Diamond amuache
afanye kazi kama ilivyokuwa zamani kwa kuwa wanaamini ujio wa mwimbaji huyo kwenye maisha yake umebadili utendaji wake wa kazi na kubase kwenye mapenzi huku akimsapoti yeye bila kupata sapoti kutoka kwake.

Mashabiki hao wamesample hash tag maarufu iliyoanzishwa na raia wa Nigeria baada ya kundi la Boko Haram kuwateka wasichana wa shule
#BringBackOurGirls , wakaja na
#bringbackourwema ikimnyooshea
kidole moja kwa moja mwimbaji huyo
ambaye wanaamini kamteka star wao
wa filamu.

Kampeni hii ilianzishwa Instagram na mtu anaetumia jina la Mrekebishatabia ambaye alimtumia ujumbe mrefu Diamond.
"Mambo vipi? Sisi mashabiki wa
wemasepetu tunakuomba umsaidie
Wema kama yeye anavyokusaidia.
Labda niseme kwa uwazi bila woga kwamba mahali ulipo kimziki umefika sababu ya Wema. Wengine hatukuwa mashabiki wako lkn sababu ya mapenzi kwa Wema tukajilazimisha kukupenda tu... so unajua vema bila wema we mziki huna! Tunakuteteaga tu lkn huwezi kujilinganisha na wanamuziki wengine tunaowajua wanafanya vema kuliko wewe....leo sitawataja majina! nije kwa point yangu sasa wewe si mwanaume? Tuoneshe sasa! "Umetembea tembea nchi mbali mbali" umekutana na watu wa aina
mbali...hujamtambulisha wema huko kibiashara, unaishia kusema maneno maneno ya sifa lkn unamwacha wema anapotea. Angekuwa wema she's always proud of you kukutaja popote hata angepata ile nafasi ya kuongea na karuache angekutaja, umeonana na kina davido+iyana bila kutaja waigizaji wakubwa Nigeria...Wema ni brand tunamlinganisha na top stars Africa!! We una nafasi kubwa sana kumfanya wema aonekane.. but what your doing unampoteza kwa makusudi.Unamchezesha viduku, Ulipomwacha alikuwa na maendeleo makubwa alikua ameshatengeneza wanamuziki wake, nyumba yake, kipindi chake cha in my shoes kilianza bila mkono wako...ukaona hapa atakuzidi na unajua jinsi
anavokupenda ukamtumia..hujawahi kusema hadharan feelings zako kwake zaidi ya mafumbo mafumbo...hujawahi kukanusha ile interview ya spora uliyomdiss vibaya wema....Je tueleweje sasa? Si lazima kuanika kila kitu mambo yenu binafsi. Wema haoni kwa sasa
sababu ya mapenzi yake kwako...tunakuambia leo kama hauna nia nzuri na wema tunakuomba umuache. Maana
unajua tu akimpigia promo mwanamuziki wake mirror utapotea
kwa game. She has all this power tunaomba usimtumie kwa maslahi yako binafsi.
#bringbackourwema "


Ujumbe huu kwa Diamond ulipokelewa vizuri na mashabiki wengi ambao waliiendeleza kwa kuisapoti kwa nguvu kampeni hiyo na ndani ya siku moja ikawa maarufu.
Umaarufu wa kampeni hii ukageuka kuwa mfano wa kile nilichosema kwenye aya ya kwanza. Diamond alishindwa kuvumilia, akaamka haraka na kutupa jiwe ambalo halikuwapata tu mashabiki waliouliza bali lilimpiga vyema Wema Sepetu na kutaka aamke afanye kazi na sio kumtegemea yeye.

Majibu ya Diamond yalionesha wazi kuwa kinachompoteza mpenzi wake huyo ni kujikita zaidi katika maisha ya anasa na kuendekeza marafiki wanaopenda starehe huku pesa yake
nyingi akiielekeza katika kuwapigisha bata mashoga zake na kusahau kuwekeza katika vitu vya msingi na kufanya kazi.

"Nafikiri ningewaona kweli mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa wasanii wenu….kama mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe."

Jiwe hilo limeupiga upande mwingine wa Wema Sepetu na kuonesha kuwa kinachomponza ni uvivu na kubase katika mapenzi na starehe akisahau kuhusu tasnia.
Inaonekana pia Wema amebadilika na kuwa tegemezi kwa Diamond ambaye amekiri kuwa anahakikisha anacheza nafasi yake kama mwanaume.

"Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. Waswahili wanasema Mchungaji bora
anatakiwa aamue kunywa maji!!!!!
Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie????
Alichokiandika Diamond kinaweza kuwa mwiba kwa mashabiki wake au hata kwa Wema Sepetu. Lakini ukiisoma post yake kwa jicho la tatu na kuyafikiria mapenzi ya sasa. Utagundua kuwa jibu hilo linatakiwa kuwafungua macho wasichana wengi katika tasnia ya sanaa na wote wanaofanya kazi zao
binafsi na baadae kuingia katika mapenzi.

Unapokuwa katika uhusiano na mtu fulani, ni muhimu kucheza nafasi yako huku ukichukua tahadhari kwa uangalifu kila wakati kama dereva anaeikaribia kona kali ili mapenzi yasiharibu kabisa career yako.
Wapo wasichana wengi ambao wameweza kufanya vizuri ingawa wamezama kwenye mapenzi na wanaendelea kuwahudumia mashabiki wao.
Lakini wapo wengi ambao mapenzi yamechukua nafasi ya kazi yao na wamepoteza kile walichokuwa nacho awali au wamezama kwenye anasa na starehe zaidi ambao naamini jiwe hili la Diamond litakuwa limewagusa.

Mapenzi yasiwe sehemu ya wewe kujivunia tu alichonacho mpenzi wako au unavyomkubali na kusahau kikubwa ulichonacho. Kitu ambacho mashabiki wa Wema wanakiri kuwa kila wakati yeye humtangaza Diamond na kumuweka mbele.
Nadhani sio vibaya, lakini anatakiwa pia kutosahau kuweka mbele kipaji chake na kazi yake. Mashabiki hao wameeleza kuwa Wema amemuongezea sana Diamond mashabiki. Kama hii ni kweli nadhani ni vyema Wema asisahau kuwatumia mashabiki hao ambao ni wake, aendelee kuwapa kile kilichofanya wamshabikiea la sivyo watakuwa wa Diamond na sio wake.
Lakini pia tumewahi kusikia habari za Diamond kumkutanisha Wema Sepetu na waigizaji wakubwa wa Afrika ili kufanya nao kazi. Kama story hizo zilipita kama upepo basi inawezekana zimekwamishwa na jitihada binafsi za Wema katika kuzifanikisha na ndio maana Diamond anamrushia mpira wa
lawama.

"Ni juhudi zako kwanza!...leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!" Ameandika Diamond.

Mwisho, naweza kusema inawezekana
kabisa kuwa Wema Sepetu alikuwa hajui ni kwa kiasi gani Diamond anayachukulia maisha yake na kuwa anachukizwa na aina ya marafiki alionao, ukiacha maongezi yao sasa atakuwa anajua zaidi.
Naamini ataichukulia positive na kupigana zaidi kwa kuwa bado ana ushawishi mkubwa kwenye jamii na ana uwezo mkubwa ambao mashabiki
wanaumiss kwa kutomuona tu kwenye runinga akifanya yake.


Kwa mtazamo wangu nadhani badala ya kumuomba Diamond amrudishe Wema Sepetu, mashabiki wangeanzisha kampeni ya kumwambia Wema moja kwa moja arudi kwa nguvu aliyokuwa nayo awali kwa kuwa wanamhitaji.

 
Ujaweka sawa hebu funguka kwani a yupo wqpi sasa na alikuwq wapi ili arudi unaposema wewe
 
Hahahaaa kizazi cha wahongaji kimekwisha wao wanakumbuka shuka asubuhi,madam kigodoro ndio mpango mzima kinamuweka mjini yeye na mganga wke aunt,mana hata akienda choo mganga yupo nyuma cjui sauz mara mwz yupo nyuma,au domo anagegeda wote
 
Hivi kuna mwanaume aliyetulia na mwenye future anaweza kuingiza dushe kwenye kitu ya huyo dada, waliompitia wote hata kwenye google unawapata, nafikiri kigodoro ni saizi yake, hongera angela damas,unakula kipupwe tu
 
angela damas yuko wap cku hz???

Hivi kuna mwanaume aliyetulia na mwenye future anaweza kuingiza dushe kwenye kitu ya huyo dada, waliompitia wote hata kwenye google unawapata, nafikiri kigodoro ni saizi yake, hongera angela damas,unakula kipupwe tu
 
Back
Top Bottom