BREAKING NEWS: Mgomo wa wanafunzi na walimu Ulayasi sekondari wilayani Ludewa.

Njangula

Senior Member
Oct 20, 2011
179
18
Hivi ninavyoandika kuna migomo mizito miwili hapa shuleni Ulayasi wilayani Ludewa. Walimu wanamkataa msarifu wa shule(bursar) kutokana na ubadhirifu uliopitiliza. Wanafunzi wanadai kutimiziwa kero ambazo hazijaondolewa. Hivi tumeambiwa askari, mkuu wa wilaya na afisa elimu sekondari wanakuja toka makao makuu ya wilaya Ludewa. Walimu hawaingii darasani mpaka mkurugenzi amuondoe mhasibu. Ni mgomo usiyo na kikomo. Shule ina wanafunzi zaidi ya 1500 A-LEVEL na O-LEVEL. Source- mimi mwenyewe ni mwalimu hapa. We seek your help, congrats.
 
Hapa hakuna chama chochote kinachohusika. Ni kero za muda mrefu sana. Walimu walitafakari kwa kina sana majaaliwa ya watoto wa kipangwa(kabila la hapa) na watoto wa A-level kutoka sehemu mbali2 za Tanzania ambao wanafeli sana wakati suluhisho lipo wazi. Tunalenga kuondoa uozo. Polisi wakivamia watakosea hii ni migomo ya amani.
 
CHADEMA hao wanahusika bila ya shaka yoyote. tena kova anajua hili suala. Lazima bursar wenu apelekwe mabwepande na mkenya
 
Hapa hakuna chama chochote kinachohusika. Ni kero za muda mrefu sana. Walimu walitafakari kwa kina sana majaaliwa ya watoto wa kipangwa(kabila la hapa) na watoto wa A-level kutoka sehemu mbali2 za Tanzania ambao wanafeli sana wakati suluhisho lipo wazi. Tunalenga kuondoa uozo. Polisi wakivamia watakosea hii ni migomo ya amani.

Mkuu hiyo nimefanya kama utani tuu si unajua tena
Polisi wetu hawajafundishwa kuwa kuna maandamano ya amani au kuna mgomo ambao watu wanadai haki zaio
Wao wanajua kama ni mgomo ni kwamba sio halali na wala hawana haja ya kuuliza wao ni kutumia nguvu zao walizojifunza huko CCP
 
Hivi ninavyoandika kuna migomo mizito miwili hapa shuleni Ulayasi wilayani Ludewa. Walimu wanamkataa msarifu wa shule(bursar) kutokana na ubadhirifu uliopitiliza. Wanafunzi wanadai kutimiziwa kero ambazo hazijaondolewa. Hivi tumeambiwa askari, mkuu wa wilaya na afisa elimu sekondari wanakuja toka makao makuu ya wilaya Ludewa. Walimu hawaingii darasani mpaka mkurugenzi amuondoe mhasibu. Ni mgomo usiyo na kikomo. Shule ina wanafunzi zaidi ya 1500 A-LEVEL na O-LEVEL. Source- mimi mwenyewe ni mwalimu hapa. We seek your help, congrats.

Ulamwike! Asante mkuu kwa taarifa.
 
Halafu wewe mwalimu badala ushauri wanafunzi warudi madarasani wewe umekimbilia huku kwani bursar ndo mwalimu wa hao wanafunzi acheni kukuza mambo
 
Mapambano ya kudai haki yaendelee, hiyo ndo dawa, kila mtu atajua jinsi ya kudai haki yake maana serikali ya CCM ipo likizo.
 
Naona umekurupuka swahiba kajipange upya. Mbona taarifa za ajali ya meli zimejaa JF badala ya SUMATRA? Nini vision na mission of JF? Umeniuliza nimewashauri mara ngapi hao watoto kabla ya leo? Unajua madhila ya tathnia ya ualimu? If you are politician with naive approach please be informed we are not politicians and we dislike it but we stand for the pedagogy of the oppressed!
Halafu wewe mwalimu badala ushauri wanafunzi warudi madarasani wewe umekimbilia huku kwani bursar ndo mwalimu wa hao wanafunzi acheni kukuza mambo
 
Kweli tumefikia hali mbaya sana, kila kitu kinachotokea hivi sasa vyama vya siasa vinahusishwa badala ya kutatua matatizo yaliyopo.
 
Yeah, uongozi mzito wa wilaya upo kuzungumza na wanafunzi wa A- level on parade ground venue, baadaye wataongea na teaching staff.
 
Walimu wakigoma wataajiriwa wengine toka Malawi, na wanafunzi wataletwa wengine toka Msumbiji!
 
Naona umekurupuka swahiba kajipange upya. Mbona taarifa za ajali ya meli zimejaa JF badala ya SUMATRA? Nini vision na mission of JF? Umeniuliza nimewashauri mara ngapi hao watoto kabla ya leo? Unajua madhila ya tathnia ya ualimu? If you are politician with naive approach please be informed we are not politicians and we dislike it but we stand for the pedagogy of the oppressed!

Usimlaumu mkuu hajui kinachoendelea angekuwa anafahamu mambo yaliyoko huko wala asingekurupuka. Dah! Nimepamisi sana Mlangali
 
Back
Top Bottom