Wazazi na Walezi Wilayani Ludewa Tuwapeleke Watoto Mashuleni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944

WAZAZI NA WALEZI WILAYANI LUDEWA TUWAPELEKE WATOTO MASHULENI

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa- Victoria Mwanziva ametoa rai kwa wazazi wote kuhakikisha Watoto ambao wamefikia umri wa kuanza masomo ya Awali, Darasa la Kwanza na wanaoanza Kidato cha Kwanza- kwa mwaka wa masomo 2024 kufanya hima kuwaandikisha watoto
mashuleni waanze masomo.

Aliasa na kutoa rai hizi kwa Wana-Ludewa alipozungumza na wananchi kupitia kituo cha redio Rafiki Fm kilichopo mjini Ludewa, lengo likiwa ni kuhimiza wazazi kuwaandikisha watoto mashuleni na kuhakikisha wanawasimamia Wanafunzi kuwa na bidii katika masomo yao;

"Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada kubwa kuandaa na kuboresha miundombinu ya elimu wilayani Ludewa, yakiwemo madarasa bora na kuongeza walimu wa kufundisha, wazazi tuhakikishe tunapeleka watoto wetu wote mashuleni," amesema Mwanziva

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa amewaelekeza wasimamizi wa Shule na wote wanaohusika kuwapokea wanafunzi wanaokwenda kuripoti mashuleni, kuhakikisha kuwa wanapokea wanafunzi wote hata kama mahitaji yao hayajakamilika ili kuwapa wazazi nafasi ya kukamilisha hayo mahitaji kabla ya mwisho wa Mwezi wa Januari.

Sambamba na hilo, amewaomba viongozi wa Kidini, Kimila, Kijamii na wadau wote kusaidia kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa watoto kupata elimu kwa manufaa ya jamii na taifa kiujumla- hivyo viongozi wote wazidi kulihimiza jambo hilo na kulifuatilia hatua kwa hatua Wilayani Ludewa.

WhatsApp Image 2024-01-18 at 00.38.20.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-18 at 00.38.21.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-18 at 00.38.21(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-18 at 00.39.01.jpeg
 
Back
Top Bottom