BREAKING NEWS: Mgomo wa wanafunzi na walimu Ulayasi sekondari wilayani Ludewa.

Staff tumemaliza kikao na DC. Tunasubiri uamuzi mzito muda mfupi ujao ila walimu tumepewa kinga. All we need is diplomacy in solving problems. Unfortunately two strikes have occured co-incidental.
 
Hivi ninavyoandika kuna migomo mizito miwili hapa shuleni Ulayasi wilayani Ludewa. Walimu wanamkataa msarifu wa shule(bursar) kutokana na ubadhirifu uliopitiliza. Wanafunzi wanadai kutimiziwa kero ambazo hazijaondolewa. Hivi tumeambiwa askari, mkuu wa wilaya na afisa elimu sekondari wanakuja toka makao makuu ya wilaya Ludewa. Walimu hawaingii darasani mpaka mkurugenzi amuondoe mhasibu. Ni mgomo usiyo na kikomo. Shule ina wanafunzi zaidi ya 1500 A-LEVEL na O-LEVEL. Source- mimi mwenyewe ni mwalimu hapa. We seek your help, congrats.

serikali haijapeleza swala hilo mahakamani kweli?!, hebu nitajie jina la viongozi wa mgomo ili ni mtume Hemed Msangi am-limboke.
 
We, thubutuu! Nani akutajie.
serikali haijapeleza swala hilo mahakamani kweli?!, hebu nitajie jina la viongozi wa mgomo ili ni mtume Hemed Msangi am-limboke.

we, thubutuu! Nani akupe jina.
 
CHADEMA hao wanahusika bila ya shaka yoyote. tena kova anajua hili suala. Lazima bursar wenu apelekwe mabwepande na mkenya

Kwa fikra hizi za kimtindio wa ubongo nchi haiwezi kuendelea. Maana itakuwa hata timu ya mpira ikifungwa bao 5-0, CDM inahusika! mtu kaugua malaria sugu, CDM inahusika! umekojoa kitandani, CDM inahusika! mwanao kafukuzwa shule sababu hujalipa karo, CDM inahusika! wavuvi wakose samaki, CDM inahusika, buchani umeuziwa mifupa tupu, CDM inahusika!!!...mnastahili maombi ya mkesha
 
du! Cdm imekukoroga sana,yaani kwa kuanza tu umeanza kuihusisha

Mkuu Comi i was just joking maana kila kitu kwa sasa kinahusishwa na CDM hata mafuriko yakitokea wanasema yameletwa na CDM kwa kuwa hawataki nchi itawalike
 
Last edited by a moderator:
Walimu wakigoma wataajiriwa wengine toka Malawi, na wanafunzi wataletwa wengine toka Msumbiji!
na fungu lipo la kuwalipa hao walimu kutoka nje,zitatengwa bilions of dola just for paying dat tichaz,mabwepande bana...hamnazo kabisi.
 
Kila kitu almost kishasuluhishwa na tumeambiwa jamaa atahamishwa kituoni muda ujao taratibu tu zinaenda kufuatwa wilayani. Amekaa kituoni miaka zaidi ya 22 akijilimbikizia utajiri mkubwa sana akitamba kuwa hamna degree au diploma yoyote itakayomfikia kwa utajiri labda ahame au afe na maheadmaster waliojaribu kumgusa ama walipewa demotion au walihamishwa vituo. Kwa nguvu ya kipesa alipanch kila uhamisho aliopewa. Wanakijiji pia walitaka ahame lakini wameshindwa kwa muda mrefu sana. Mkuu wa shule amepigwa upofu kwa pesa kidogo aliokuwa akipewa. Sasa mkuu akionekana mpotofu pasipo mhasibu kuwepo basi tunaanzisha kunji la kumtoa yeye sasa. Wadau sisi hatuna politics ila tuna uchungu na watoto wa Ludewa ambao wazazi wao waliporwa ardhi kwa fidia ya kizushi ili kujenga shule lakini pia kwa viboko na fines walilazimishwa kufanya kazi lakini watoto wanafeli mno! Sisi walimu tunajua chanzo. Si hapa tu bali hata shule mbili tatu zilifanya mgomo kushinikiza wakuu wa shule kutoka. Leo tunaingia darasani kwa matumaini mapya kabisa. Wanafunzi pia wamemaliza mgomo baada ya baadhi ya kero zao kushughulikiwa na wilaya hasa mashine ya umeme na madishi ya vyakula. Nashukuru wadau kwa michango yenu mizuri sana tena wengine inaonekana wanatoka huku2. Hii ni eneo la mbunge Deo Filikunjombe ambae pia tumemtumia nakala maana ktk ufisadi uliofanyika ni pamoja na mifuko ya sementi100 na mabati 130 alivyotoa kukarabati nyumba za walimu. "Aluta kontinua"
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom