Askari Wanawake Mbeya watoa zawadi ya taulo za kike, sabuni na vifaa vingine kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Msingi

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Mwenyekiti wa Mtandao wa Askari Polisi Wanawake Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Afisa Mnadhimu namba moja Mkoa wa Mbeya ACP Christina Musyani, Machi 06, 2023 amewaongoza Askari Polisi Wanawake Mkoa wa Mbeya kuwatembelea na kutoa zawadi kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Msingi zilizopo katika mamlaka ya Mji Mdogo - Makongolosi Wilayani Chunya.

Akizungumza wakati wa utoaji wa taulo za kike, sabuni na vifaa vingine kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Kipoka, Nyerere na Makongolosi na Shule ya Sekondari Kipoka, ACP Musyani amewataka wanafunzi hao kuhakikisha wanajitunza kwa kutoruhusu miili yao kushikwashikwa mtu yeyote yule ili kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vinaweza kutowesha ndoto zao za kimaisha.

1.JPG

2.JPG

Aidha, ACP Musyani amewataka wanafunzi hao kutokaa kimya pindi waonapo vitendo vya ukatili wa kijinsia au uhalifu wa aina yoyote, amewataka kutoa taarifa kwa wazazi, walezi au walimu wao kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Sambamba na hilo, ACP Musyani kwa niaba ya mtandao wa Askari Polisi wanawake Mkoa wa Mbeya ameushukuru uongozi wa mamlaka ya Mji Mdogo wa Makongolosi kwa jitihada za makusudi za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Naye Diwani wa Kata ya Bwawani, Sairon Mbalawata Pashila amelishukuru kipekee Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kuwakumbuka wanafunzi wa Shule za Sekondari na Msingi zilizopo katika mamlaka ya Mji Mdogo wa Makongolosi. Pia amewahakikisha kuwa zawadi walizotoa zitakwenda kupunguza changamoto ya utoro kwa wanafunzi pindi wawapo hedhi.
3.JPG

Kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke dunia uadhimishwa Machi 08 kila mwaka ambapo uambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea wahitaji, utoaji wa zawadi, misaada kwa makundi maalum pamoja na kutoa elimu kwa jamii.
 
"A wise woman wishes to be no one's enemy; a wise woman refuses to be anyone's victim."

Happy Women's Day to strong, intelligent, talented and simply wonderful women! Don't ever forget that you are loved and appreciated.
 
Back
Top Bottom