Wikiliki
JF-Expert Member
- Dec 20, 2010
- 528
- 139
Tangu Chama tukufu cha Demokrasia na Maendeleo -(CHADEMA) kitangaze na hatimaye kianze maandamano na mikutano ya hadhara humu jf kumejitokeza kundi linalopinga hatua hiyo kwa nguvu zote,limekuwa likitumia lugha mbalimbali za chuki,mara dakika tisini za michezo zimeisha,mara mikutano na maandamano hayana mshiko,mara wao wahamashishe maendeleo(kana kwamba tayari serikali walioichagua ya ccm imekufa!) ninataka niwaambie wanachofanya CDM ni kitu cha msingi sana kwa chama hai cha siasa cha kuendelea kuboresha mahusiano yao na wananchi.