Boss Bima ya Taifa ya Afya (NHIF) jiandae kusimamishwa kazi!

bima ya taifa ni taasisi safi kiutendaji wanachama wanafurahia huduma zetu 100%


Hakuna huduma mbaya kama za NHIF yaani ni majizi kazi ni kutafuna pesa. Ingekuwa na option ningejitoa kabisa. Hospital huduma mbaya tena unaangaliwa vibaya kama unatibiwa bure au umepotea njia. Kwa nchi nyingine bima ya afya ni first class service ila hapa ni vice versa. Wanachoweza ni kujilipa mishahara na posho kubwa. Tena sijui ni kwa nini Magufuli hakuanzia. Dhuluma ya kuhujumu afya ni kubwa kuliko ile ya kuhujumu pesa.
 
Ni kweli kuwa huduma mbovu...
1. Lakini je, huduma mbovu inasababishwa na uwepo wa viyoyozi maofisini..??
2. Haiwezekani kuwa na huduma nzuri na bado kukawa na magari ya kifahari na viyoyozi maofisini..??
3. Tunalalamikia huduma au viyoyozi..??
4. Kwamba viyoyozi vikiondoka huduma zitakuwa bora..??

Jamani, HIVI KUNA ANY DIRECT RELATIONSHIP KATI YA HUDUMA NA CONTENT ZA OFISI..??


Wewe hukumwelewa kaonyesha uhusiano tena uliopo kati ya NHIF na huduma zinazotolewa. Kimsingi huduma ni mbovu, dawa hakuna hata viofisi vya NHIF mahospital vipo maeneo ya kiajabuajabu, dawa hakuna etc. Lakini wakati huo mabosi wa mfuko huo wanatanua mjini na mashangingi na kujilipa mishahara ya kufa mtu.
 
Nakuelewa mkuu, lakini my point ni kuwa kuna watu wanalalamikia vitu ambavyo wamevisaini.... Hizo dawa zinazozuiliwa si kwamba mtu tu anakurupuka... FROM day one list unaijua halafu uje ulalamike huku...


Wewe inaonekana ni ubishi tu tena wa kutokujua. NHIF ni mfuko wa lazima hivyo kusema watu wanakuletea karatasi hii ni hoja mfu. Hata kama ukijua ndo ufanye nini, na zaidi makato yanafanyika hata bila kushirikishwa.
 
Nchi hii ingekua ni mwili wa binadamu basi una majipu hadi matakoni....
 
Hata hizo BIMA haziruhusu extended family members. Tatizo watu hawaelewi maana ya BIMA. Bima siyo akiba. Ndiyo maana unakuwa na gari unakata BIMA, siyo lazima upate ajali, ila ikitokea umepata utanufaika kupitia hela uliyoitoa wewe na wenzako wengine ambao wametoa lakini hawakupata ajali. Kama wewe huna wategemezi 4, basi michango yako inasaidia kuhudumia wenzako wenye wategemezi wanne.

Hii inanikumbusha habari niliyowahi kusimuliwa na Mamangu kuwa kuna mtu alikuwa mvivu, alikuwa akikumbwa na njaa kila mwaka, alipokuwa akiulizwa kuwa inakuwaje kila mwaka familia yake inakuwa na njaa, alijibu kwa kusema kuwa familia nyingine wanakuwa na chakula cha kutosha kwa sababu wanachangiwa chakula wanapokuwa na misiba.

Mwaka huo huo akafiwa na mtoto wake, alipokuwa akilia, akaambiwa usilie maana nawe mwaka huu utachangiwa chakula!

Bima ya afya ni jipu. Hakuna ubunifu,hakuna nia ya kuwawezesha watanzania wengi kuwa wanachama. Ni ukiritimba mwingi unaolenga kuwanyima huduma hii watanzania hasa masikini kwa kuweka masharti mengi kwenye wategemezi 4. OMBI: Boss wa NHIF atumbuliwe. Hili ni jipu. Wao wanajilipa mashahara mikubwa, maisha ya fahari. Wakati huohuo huduma zao ni hovyo kabisa. Boss wa NHIF ang'olewe. Liwalo na liwe. Hapa lazima kusema wazi kwaajili ya masilahi ya watanzania wengi wanaonyimwa haki ya bima afya kwasababu ya mizengwe iliyowekwa kwa makusudi na utawala wa NHIF.
 
Katika Taasisi ya umma ambayo utendaji wake ni wa mashaka sana ni hii NHIF huduma mbovu pamoja na makato makubwa (kuchangia Huduma) kwa wafanyakazi wa umma.

NHIF wao wanajilipa vizuri sana, safari kila kukicha na Magari ya Kifahari, ofisi nzuri na yenye nafasi (spacious) pamoja na kiyoyozi pale Kurasini.

Wanachama wanadhalilika sana kwa watoa huduma (hospitalini & Maduka ya dawa) huonekana kama wanatibiwa bure. Mbona Bima za Afya za Binafsi (AAR, Metropolitan n.k.) zinawashinda nyie NHIF? mmekosa nini wandugu?

Eti wategemezi wanne tena wawe ndugu Biological (sio extended).

NB: Kwa ninavyowajua Mawaziri wa afya Mhe. Ummy & Dr. Kigwangallah walivyo makini na kazi zao, wewe ndio unafuata baada ya wale jamaa zako wa MSD, Stuka sasa!!!

Umeongea ukweli 100% Sijui huyu mkurugenzi wa nhif anakitengo cha monitoring and evaluation ikiwemo yeye mwenyewe ajipime. Ukiwa na NHIF ni sawa na kuwa mwanafunzi kwenye daladala hospitalini mnabaguliwa,dharauliwa kama vile huduma ni ya bure. Kwa kweli waajiri mtu competent na asiye na longolongo la kulipa hospitali bill za wagonjwa zinapotumwa kwao. Nimetumia Strategis,medex,aar kwa hapa tz lakini nhif ni worst. Inahitajika kufumua mfumo uliopo hapo.
 
Acha kudanganya umma.

NHIF wanachangisha pesa nyingi, halafu huduma zao ni za hovyo zenye masharti mengi.

Wale wategemezi 4 wamewekewa masharti mengi ambayo yanalenga kuondoa uwepo wa wategemezi hao.

Bima ya afya lazima masharti yao yaendane na hali halisi ya wakati husika. Wafanyakazi wengi siku hizi ni singles.

Hivo inasababisha ndugu wenhine extended wasinufaike hata kama walichangia huyu mwanachama kupata elimu. Huu ni ukiritimba usio na tija.

Masharti ya wategemezi yarekebishwe ili mwanachama awe huru kuingiza ndugu zake 4 anavyoona inafaa.

Utaratibu huo ungesaidia kuwaingiza watanzania wengi kwenye bima ya afya.

Naunga mkono hapo kwenye wategemezi,
 
loooh! WAMULIKWE MAJIPU hawa NHIF.TABIA YA KUNIPANGIA WATU WA KUFAIDIKA NA MAKATO YA HUDUMA YAANGALIWE.PIA KAMA MWAJIRIWA KAMA HAJAJIUNGA NA HUDUMA KWANINI AKATWE? NAPELEKA MAJINA YA NDUGU WANAOPASWA KUFAIDIKA NA BIMA YANAKATA NA KUSEMA HAYA TOA AFU MWAKA MZIMA NAKATWA ILIHALI SIJAPELEKA TAARIFA HUSIKA.
 
Ila hizi za kutumbua majipu zisiharibu hata baadhi ya vitengo vyenye ufanisi...NHIF naona wanajitahidi kwa huduma zao
 
Mie nalia nao upande wa wategemezi....


Uuuuuwwwwiiiii.... Sasa ndio ukute wazazi wote wa pande mbili walishafariki, na wewe ndio kwanza hujapata mtoto. Inakulaje kwako mazimaaa!!!
 
Hawa jamaa ni waajabu kweli,eti mtegemezi lazima awe mke,mtoto,mzazi.Sasa kama hukubahatika watoto wanakula fedha za bure.Hili JIPU LIMEIVA KABISA KUPIISHA NCHA YA KIPINI
 
Wewe inaonekana ni ubishi tu tena wa kutokujua. NHIF ni mfuko wa lazima hivyo kusema watu wanakuletea karatasi hii ni hoja mfu. Hata kama ukijua ndo ufanye nini, na zaidi makato yanafanyika hata bila kushirikishwa.
Naona umefika wakati kila mtu ajichagulie kampuni ya bima ya afya anayoitaka, kama ilivyo kwenye mifuko ya jamii mingine. Kitendo cha kuingizwa kwenye mfuko wa NHIF kwa lazima ni KUVUNJA KATIBA ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Ibara ya 20 juu ya haki ya kujiunga. Hapo NHIF itashika adabu kwa kukosa clients.
 
bima ya taifa ni taasisi safi kiutendaji wanachama wanafurahia huduma zetu 100%
Wanachama wenu wa wapi? wa Tanzania hii au Uganda na Kenya. Kama unamaanisha Tanzania hii usidhani sisi ni vipofu au mazuzu. Kaweeleze maneno hayo mazuzu na wala siyo watu makini.....
 
zamani kufungua fail ilikuwa bima inatumika nowdays unatoa pesa yako na uku unabima ya afya wizi mtupu
 
Back
Top Bottom