Boss Bima ya Taifa ya Afya (NHIF) jiandae kusimamishwa kazi!

NHIF ni taasisi makini kunakodhihirishwa na kupata tuzo za kimataifa. Tatizo watanzania wengi mmezoea kufoji so mnafikiri NHIF itavumilia upuuzi wenu huo.
Mnajipambanua tu bure...niambie kwanini tuna changia hela kibao ambayo ningetibiwa vizuri tu Agha Khan lakini siruhusiwi.
 
Nashauri NHIF irudishe mfumo wa zamani wa kuweka wategemezi 4 bila kujali ni mtoto wako au ni Jirani yako kwani sisi waafrika tunalelewa na ndugu kaka dada mjomba shangazi na hata rafiki tu, anakusomesha mpaka chuo kikuu kwa kutumia jembe lake la mkono. Leo hii nisimpe kadi ya Bima eti kisa siyo mzazi Wangu kibiologia ! Jipu!
 
Mkuu bima za afya binafsi, zimezuia dawa chache sana. Bima ya afya ya Taifa, inakupa option ndogo, wao ni vigumu sana kupata dawa brand kubwa maana wanaogopa gharama, ingawa zinaweza kuwa bora hata mara 20 ya brands cheap.
Nakuelewa mkuu, lakini my point ni kuwa kuna watu wanalalamikia vitu ambavyo wamevisaini.... Hizo dawa zinazozuiliwa si kwamba mtu tu anakurupuka... FROM day one list unaijua halafu uje ulalamike huku...
 
Yap, connection ipo mkuu.
Kukiwa na grades kubwa za mishahara lazima kuwe na reflection kwenye service delivery,
Sasa mishahara mikubwa, facilities nzuri then huduma mbovu??
Huu ndio use...ngerema sasa
Kaka sijauliza just connections... NIMESEMA DIRECT CONNECTION..... kwa maneno mengine... they do not have direct proportionality..... kwa sababu kuna other factors zinazoangaliwa pia....
 
bima ya taifa ni taasisi safi kiutendaji wanachama wanafurahia huduma zetu 100%
ndiyo naona mnajikongoja sasa tena baada ya awamu hii ya tano..... nilitakiwa kufanyiwa CT-scanning pale regency nilikuwa mgonjwa eti naambiwa hiyo bima haiwezi nilipia mpaka nikachukue barua ofisi za mwenge kama kibali ,,, nikajiuliza kila mwezi mnanikata hela leo hii mnaniambia nikachukue barua kwas sababu zipi.... bora hizi bima za private aiseee
 
katika hili kwa kweli bosi wa NHIF anapaswa kutumbuliwa jipu kwa kuwa alikubali kuchota tsh trilion 3 na kuipa serikali kwa ajili ya kujengea barabara na upuuzi mwingine kama huo kana kwamba NHIF ni ROAD FUND. atumbuliwe tu!
huku afya zetu zikidumaa ....
 
NHIF ni taasisi makini kunakodhihirishwa na kupata tuzo za kimataifa. Tatizo watanzania wengi mmezoea kufoji so mnafikiri NHIF itavumilia upuuzi wenu huo.
Nikiwa mimi ni mtu nimejiajiri nikitaka kujiunga na hiyo NHIF ni vitu gani natakiwa kuwa navyo including gharama n.k
 
Naomba ufafanuzi, hawa NHIF wanajitangaza sana, lakini hawa elekezi ni jinsi gani wasio ajiriwa na walio jiajiri wenyewe ni jinsi gani wanaweza wanafaidika na huu mfuko.
Kaka imelenga pale nilipokuwa napahitaji, nyie NHIF tunaomba ufafanuzi kwenye hili
 
Jipu la NHIF likitumbuliwa itakuwa safi kabisa. Watu tunakatwa hela kubwa ila tuko restricted kuweka wategemezi. Mfano mimi nakatwa laki moja kila mwezi hapo bado mke wangu na bado za mwajiri. Lakini wazazi wangu wakienda hospitali huko mikoani waliko madaktari wanawaangalia shingo upande hawapewi huduma sawa na wenye kesi. Kimsingi NHIF haijawaelimisha Madaktari namna ya kuhudumia wateja wake na wanalalamikia usumbufu wanaopata kuhudumia mgonjwa wa NHIF ikiwa ni pamoja na kutolipwa consultation fee. Wahusika warekebishe hili maana nalo ni jipu
 
ATUMBULIWEEEEEEEEEEEEEEEEEEE WANANTUTESA SAANA HAWA MTU WAKATWA MSHAHARA HALAFU HUDUMA HAZIPO UNAPIGWA FOLENI BALLAA HALAFU HATA PANADOL HUPATI WEZI WAKUBWA WACHA WATUMBULIWE
 
ndiyo naona mnajikongoja sasa tena baada ya awamu hii ya tano..... nilitakiwa kufanyiwa CT-scanning pale regency nilikuwa mgonjwa eti naambiwa hiyo bima haiwezi nilipia mpaka nikachukue barua ofisi za mwenge kama kibali ,,, nikajiuliza kila mwezi mnanikata hela leo hii mnaniambia nikachukue barua kwas sababu zipi.... bora hizi bima za private aiseee
Mgonjwa ameenda hospital anaumwa anaambiwa haiwezekani aende akachukue barua mwenge ndiyo aje?

Ukitoka Regency mpaka ufike msenge unakuta ofisi imefungwa, jipu tayari!
 
Jipu la NHIF likitumbuliwa itakuwa safi kabisa. Watu tunakatwa hela kubwa ila tuko restricted kuweka wategemezi. Mfano mimi nakatwa laki moja kila mwezi hapo bado mke wangu na bado za mwajiri. Lakini wazazi wangu wakienda hospitali huko mikoani waliko madaktari wanawaangalia shingo upande hawapewi huduma sawa na wenye kesi. Kimsingi NHIF haijawaelimisha Madaktari namna ya kuhudumia wateja wake na wanalalamikia usumbufu wanaopata kuhudumia mgonjwa wa NHIF ikiwa ni pamoja na kutolipwa consultation fee. Wahusika warekebishe hili maana nalo ni jipu
nadhani NHIF hawatoi malipo kwa wakati ndiyo maana wateja wanadharauliwa
 
Mgonjwa ameenda hospital anaumwa anaambiwa haiwezekani aende akachukue barua mwenge ndiyo aje?

Ukitoka Regency mpaka ufike ****** unakuta ofisi imefungwa, jipu tayari!
huwezi kuamini nilienda na barua ikatoka baada ya siku mbili .. mkuu usiombe yakukute wanakera sana
 
Ni kweli kuwa huduma mbovu...
1. Lakini je, huduma mbovu inasababishwa na uwepo wa viyoyozi maofisini..??
2. Haiwezekani kuwa na huduma nzuri na bado kukawa na magari ya kifahari na viyoyozi maofisini..??
3. Tunalalamikia huduma au viyoyozi..??
4. Kwamba viyoyozi vikiondoka huduma zitakuwa bora..??

Jamani, HIVI KUNA ANY DIRECT RELATIONSHIP KATI YA HUDUMA NA CONTENT ZA OFISI..??

Relation ipo ya moja kwa moja.
Inaonekana shirika limewekeza kwenye anasa kuliko kuhudumia wateja.
Michango inatumika vibaya
 
NHIF ni taasisi makini kunakodhihirishwa na kupata tuzo za kimataifa. Tatizo watanzania wengi mmezoea kufoji so mnafikiri NHIF itavumilia upuuzi wenu huo.
Mbona hamtaki kusajiri ndugu au nako ni kufoji mfaano MTU hajazaa ana ndugu tu
 
NHIF wanakupa bima ya afya halau unaandikiwa baadhi ya dawa wanakwambia hizi hazipo kwenye bima sasa nini maana ya kuchangia bima halafu wanatoa matumizi mengine ambayo hayahusiani na bima ya afya kama walimvyomnunulia waziri wa afya gari

Kama ingekuwa amri yangu huu mfuko ungefutwa kabisa na kuundiwa utaratibu mwingine wa uchangiaji na utoaji huduma,

  • Mara kadhaa ukienda kupata huduma ya matibabu ni nadra sana kupata dawa zote
  • Imagine mtu anachangia Tshs 21,480.00+ kwa mwezi, ambayo ni sawa na Tshs 257,760.00 kwa mwaka, anakwenda hospitali anakosa dawa yenye thamani ya Tshs 20,000.00 ati hazimo kwenye bima kwakuwa zina gharama kubwa, miwani nayo anatakiwa kuongezea fedha kwakuwa ni gharama kubwa,
  • Mtu anayeweza kupona malaria kwa dawa kama duocotexine analazimishwa kupokea alu ati kwakuwa hizo ndizo zinalingana na kiasi anachochangia member
  • Hali kadhalika ukienda kwenye baadhi ya vituo vya afya wanakwambia kupima typhoid ni Tshs 3,000.00+ ukisema nina bima ya afya wanakataa na kukwambia hailipiwi
  • Viongozi wa mfuko huu muda wote wamejifungia maofisini hawapiti kwenye vituo na kusikiliza changamoto zinazowakabili wanachama na wala ukipeleka malalamiko hawawezi kuyashughulikia,
  • Nafasi ya mwenza hairuhusiwi kujazwa na ndugu mwingine ikiwa mwenza naye ni mtumishi wa umma na ni mchangiaji
  • Ikiwa mchangiaji hana mtoto, basi hana uhuru wa kuweka mtoto wa ndugu au jamaa, kwa maana hiyo uchangiaji unakuwa haumnufaishi member nadhani fedha za wanachama wa aina hiyo ndizo hutumiwa vibaya na watumishi wa nhif
Niliwahi kupendekeza kuwa mfuko huu ufutwe, badala yake, zifunguliwe akaunti maalumu kwenye mabank ya serikali, ambako zitatolewa kadi maalumu ambazo hazitamruhusu mchangiaji kutoa pesa badala yake zitatumika tu pale anapopata huduma ya matibabu kwa kuzipitisha kwenye mashine maalumu zitakazokuwepo kwenye vituo vitakavysajiliwa kutoa huduma hizo

Vinginevyo michango yetu itabaki kuwaneemesha watu fulanifualani tu huku wachangiaji tukiendelea kuteseka
 
Ni kweli kuwa huduma mbovu...
1. Lakini je, huduma mbovu inasababishwa na uwepo wa viyoyozi maofisini..??
2. Haiwezekani kuwa na huduma nzuri na bado kukawa na magari ya kifahari na viyoyozi maofisini..??
3. Tunalalamikia huduma au viyoyozi..??
4. Kwamba viyoyozi vikiondoka huduma zitakuwa bora..??

Jamani, HIVI KUNA ANY DIRECT RELATIONSHIP KATI YA HUDUMA NA CONTENT ZA OFISI..??
Hapo sasa...
Na walitegemea wajilipe vibaya...wakae ofisi mbovu???
 
Back
Top Bottom