Bodi ya Mikopo(HESLB) waachia majina ya wadaiwa sugu kuanzia mwaka 1994 hadi 2014

Kumbukeni mtaala ulibadilishwa 2005 kuwa competency based, ina maana unapewa maarifa baada ya hao upaje ujuzi na ubunifu wa kujiajiri, wanategemea tuwe tumejiongeza na kupata kipata cha kurudisha pesa ya watu
umemaliza chuo mwaka gani mkuu maana haya waweza kuwa wayaongea ki-mtaala ila hali halisi huijui
 
Kuna vitu vya kujua kuhusu haya madeni wakati serikali inawatafuta hawa wadaiwa:
  • Nasikia HESLB wanadai jumla ya shilingi Bilioni 2 kutoka hawa wadaiwa.
  • Jumla ya wadaiwa wote (ukijumlisha majina katika orodha zote 5) ni 142,462.
  • Ukigawanya hili deni kwa jumla ya wadaiwa unapata wastani wa shilingi 14,039. Yes, kila mmoja anadaiwa wastani wa shilingi elfu 14.
Mimi ningekuwa serikali ingeniwia vigumu kufanya maamuzi ya kuzisaka hizi bilioni 2. Wewe ungefanyaje?
  1. Ungewasamehe wote kwa sababu gharama za kuwatafuta zitakuwa kubwa kuliko deni lenyewe?
  2. Ungewaambia kila anaejitokeza kwa hiari atapunguziwa alipe nusu tu? Hii itapunguza wadaiwa sugu wa kuwafuatilia.
  3. Utakaza uzi wa kuwasaka hata kama itagharimu trilioni 1?
 
Utadhani list ya kamati ya harusi?
Waweke jina, jinsi, chuo, program uliosoma, mwaka uliomaliza, kiasi unachodaiwa.
Shame!
Eti mimi nadaiwa uku nilisoma kadiproma kwa kuunga unga, sijui haya majina wanayatoa wapi
 
Matarajio yao bodi nikukusanya hicho kias kwalazima, lakini sidhani kama wameangalia hivi vtu
Katika hili kundi kuna watu ni
Marehemu
Vichaa
Vilema wakudumu
Wagonjwa wa muda mrefu
Majambazi
Waliozamia nchi za mbali.

Katika makundi yote yawezeka idadi yao ikawa kubwa kulingana na maisha yavokwenda kasi namajanga ya kila siku, yawezekana katika hao wadaiwa sugu wenye uwezo wakuweza kurudisha hcho kiasi hata 10%hawafiki.
Wakurupukaji sana nyie bodi

Ongeza na
Jobless
 
Kuna vitu vya kujua kuhusu haya madeni wakati serikali inawatafuta hawa wadaiwa:
  • Nasikia HESLB wanadai jumla ya shilingi Bilioni 2 kutoka hawa wadaiwa.
  • Jumla ya wadaiwa wote (ukijumlisha majina katika orodha zote 5) ni 142,462.
  • Ukigawanya hili deni kwa jumla ya wadaiwa unapata wastani wa shilingi 14,039. Yes, kila mmoja anadaiwa wastani wa shilingi elfu 14.
Mimi ningekuwa serikali ingeniwia vigumu kufanya maamuzi ya kuzisaka hizi bilioni 2. Wewe ungefanyaje?
  1. Ungewasamehe wote kwa sababu gharama za kuwatafuta zitakuwa kubwa kuliko deni lenyewe?
  2. Ungewaambia kila anaejitokeza kwa hiari atapunguziwa alipe nusu tu? Hii itapunguza wadaiwa sugu wa kuwafuatilia.
  3. Utakaza uzi wa kuwasaka hata kama itagharimu trilioni 1?

Walizogawana wabunge wa CCM juzi 2.1b zingetosha kabisa kutulipia hilo deni
 
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inatangaza orodha ya majina ya Wadaiwa Sugu ambao wamehitimu katika Vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu kuanzia mwaka wa masomo 1994/1995.

Wasugu hao wanapewa siku 30 kulipa madeni yao ndani ya muda huo kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa na wahusika kulazimika kulipia gharama za kuwasaka na kuendesha kesi.

Chanzo: Tovuti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
Hahahahaah wataisoma
 
Nilijaribu sana kufuatilia kama kuna njia ya mtu kulipia kulipia mkopo wake kwa njia ya mobile money au benki ila sikukuta eneo lolote hawa bodi walipo weka "UTARATIBU WA KUTAKA KUREJESHA MKOPO". Usikute hii ndio changamoto ambayo wengi wanaikuta kutokujua jinsi gani ya kurejesha hii mikopo. Nadhani wao pia wangeweka mambo hadharani katika tovuti yao ili mtu ujue mkopo huo unaanzaje kurejesha hata kwa kutuma pesa kidogo kidogo hadi iishe.
 
Mwanzoni wakati watu mtaani wakisema kuwa Bodi hawana takwimu sahihi za watu wanao wadai mimi hilo sikuliamini kabisa. Ila kwa orodha hii, napata shaka sana juu ya uwezo wa bodi. Kama kuna watu hawakukopa na wanadaiwa, wamelipa na bado inaonyesha wanadaiwa, watu mliopata asilimia sawa ya mkopo kuonekana mna deni tofauti mmoja kubwa mwingine dogo haya ni maajabu ya sayari ya mars. Mwezi ulopita kuna mfanyakazi mwenzangu ameanza kukatwa na Bodi ilihali hata chuo kikuu hakuwahi soma.

Mi nadhani Bodi inatakiwa iombe ushauri kwa wadau namna ya kuwapata wadaiwa sugu waliokopa muda mrefu na hawakatwi marejesho ya mikopo yao, wasione aibu kwa uzembe huu.
Pia ikumbukwe kuwa Hawa maofisa wa Bodi miaka hiyo ndio walikuwa wap[igaji wakubwa wa hizi hela za mikopo. Uhakiki wanyaraka ufanyike na wahusika katika ofisi za Boodi wapo na hatua zichukuliwe dhidi yao badala ya kuwabambikiza madeni watu wengine wasio kuwa na hatia.
Mimi ninaamini wakati sasa unakuja tutajua mbivu na mbichi bila kuoneana haya wala aibu maana hakuna mtanzania atakaye kubali kuonewa kwa maslahi ya wachache. Waliokula pesa za mikopo na kufanya uzembe kaatika kukopesha na kushindwa kufuatilia marejesho kwa kusimamia sheria lazima wawajibishwe pia maama wamelitia taifa hasara kwa kutotanguliza maslahi ya nchi badala yake wakatanguliza matumbo yao mbele.
Naishauri bodi ipitie tena hiyo orodha badala ya kukurupuka kiasi cha kujidhihirisha madhaifu.
Bodi ijipange kisayansi zaidi na kuanzisha mfumo shirikishi wa kuwapata wadaiwa sugu na ukusanyaji wa marejesho ili pesa ipatikane na wadogo zetu.wapate kunufaika.
 
maajabu haya utayaona Tanzania pekee...
mtu alishindwa kulipa ada ya chuo, akamaliza, hajaajiliwa, kamaliza hajakaa hata miaka miwili eti ni mdaiwa sugu!!
kamaliza 2013/2014 anakuaje sugu, huo usugu maana yake ni nini sasa??
haa haa kwel noma sana...
Kuna kubambikizana madeni hapa,, na ikithibitika kuwa nilibambikiwa deni ntaenda Mahakamani o_O:eek::oops::mad:
 
Back
Top Bottom