Bodi ya Mikopo(HESLB) waachia majina ya wadaiwa sugu kuanzia mwaka 1994 hadi 2014

Ivi miaka yote hiyo Board ya mikopo walikuwa wapi kuwatafuta wadaiwa? tatizo sio wadeni sugu tatizo ni board.Kufanya kazi kwa mazoea
 
Hili nenno wadaiwa sugu limetumika kama kivuli cha baadhi ya watu waliopewa dhamana ya kusimamia kanuni na miongozo ya zaserikali kukwepa lawama za kutowajibika kwao kwa uzembe wa kushindwa kusimama imara katika nafasi zao. Mpaka wadaiwa wanakuwa sugu wahusika mlikuwa wapi mpaka watu wanakaa na pesa ya serikali mpaka zaidi ya miaka 20 bila kulipa hata senti na nyie mpo tu!
Hapa watu wanakurupuka ili kuficha madhambi yao!
Lakini, mi bado ninaamini ukweli na haki havitafichika siku zote.
Ni suala la muda tu kila mtu kuubeba mzigo wake kwa nafasi yake.
 
HESLB

Inasikitisha sana kuona HESLB haikuwa imejipanaga ktk hili hakukuwa na mikataba yakueleweka hapo awali walipoanza kutoa tu hiyo mikopo. Kama ilivyomikopo mingine tulitegemea strategic plan ziwepo pamoja na kuwatengeneza mangira ya wahitimu wa vyuo kupata kazi. Mambo ya kuzingatia ni pamoja na:
1- Career development centers katika kila chuo ilikuwakutanisha waajili na wahitimu.
2. Bima mikopo; lazima kuwepo na bima ya mikopo inayotolewa kwa wanafunzi ili endapo wanafunzi wakishindwa kulipa tutokana na kufariki au kutokuwa na kazi waweze kurecover kutoka ktk Bima.
3. Uwepo wa debt collectors kwa zoezi zima la kukusanya marejesho kwa wakati muafaka.
4. Muda wamalipo ulitakiwa kwa SMART kulingana na hali halisi ya uchumi wa nchi.

Inasikitisha kwa staili hii watafungua kesi nyingi na gharama itakuwa kubwa sana kwa serikali na pengine jela hazitatosha, kwa vile watanzania wengi wapo mitaaani hawana kazi. Isitoshe wapo watanzania wengine wameanza kulipa kwaintalments wamewekwa katika list ya wadaiwa SUGU ambao ni udhalilishaji – (Credit defaulter) wanaweza kuathiri nafasi zao za kazi kwa sasa pia kupata mikopo sehemu nyingine, Watu wanamna hii wanaweza kufungua kesi mahakamani kuishitaki HESLB. Nashauri HESLB inafanye proper screening ya watu wanao wadai ambao hawajaanza kulipa madeni kabla ya kukimbilia mahakamani. Kufikilia swala la BIMA na debt collectors kabla ya maamuzi mengine.
Lasivyo hata wakiwapeleka watu mahakamani inaweza kuwa ni kazi ya bure ikiwa baazi ya wadaiwa SUGU ni wafu au hawana kazi wapo mitaani na wazamini wao ni maskini, Kumbuka kuwa kigezo cha umaskini kilitumika ktk kutoa mikopo na maskini huyu sana hajapata kazi. To be honesty let’s think Tanzania ni ya kwetu sote tuijenge pamoja.
 
Unasemaje gharama za kesi zitalipwa na mdaiwa wakati kesi haijaamuliwa? Gharama za kesi hulipwa na anayeshindwa.
Kweli kabisa inaonyesha jinsi gani watu walivyo vilaza..............TUTAISOMA NAMBA - 2020.........Sijui JK aliwezaje kuongoza katika kipindi chake pesa zilitoka wapi.. watu walisoma na kupata mikopo bila matatizo... Mungu atusaidie kwa style hii ni kazi sana kuendelea... we need strategic thinker with high reasoning Capacity...
 
Natafuta mwanasheria niwashtaki Bodi haiwezekani wawe wanakata pesa yao takribani 90k kwa mwezi na bado wametoa jina langu huku wakiniita mdaaiwa sugu? Mdaiwa sugu huku mwakata pesa yenu???

Nahitaji msaada wa kisheria hawa watu lazima wanilipe fidia ya uzalilishaji!!!! naona wamekurupukwa wacha tukaweke kijiwe mahakamani kwanza!!
 
Mmm,hii ni ngoma nzito.Niko sarari kidogo simu niliyonayo haina capacity kubwa kwa hiyo sijayaona majina.Hata hivyo nadhani ni ngoma nzito.Ni mtafaruku mkubwa kwa kweli.Wenye waajiri wazuri waombe mikopo hakuna jinsi.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inatangaza orodha ya majina ya Wadaiwa Sugu ambao wamehitimu katika Vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu kuanzia mwaka wa masomo 1994/1995.

Wasugu hao wanapewa siku 30 kulipa madeni yao ndani ya muda huo kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa na wahusika kulazimika kulipia gharama za kuwasaka na kuendesha kesi.


Chanzo: Tovuti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu..

 
Sure. Ama wagawe mashamba kwa wadaiwa na kuwatafutia masoko yanazao halafu waone kama hawatalipa. Maana kazi hakuna
Of course! Isijekuwa wanang'ang'ana na "majoblesi", wakaishia kutupiwa mawe bure!
 
Niliomba mkopo 100% wakanipa 40% nimeishi maisha magumu sana chuo,nimemaliza 2010/2011 na sikatwi,SILIPI NG'OOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO HADI AKINA WALIOBA,LOWASA,N.K WALIPE
 
Kwakuwa mmeamua kudai marejesho yenu kisheria, mnapaswa kuwa makini. Kwakuwa mnalenga kupata marejesho yenu yote ya mikopo kisheria, hampaswi kufanya makosa ya wazi kuanzia mwanzo wa mchakato wenu.

Kuanzia jina la mdaiwa, kiasi anachodaiwa, kozi aliyoisomea na mwaka aliomaliza, vyote vinapaswa kuwa sahihi. Mnaweza kukumbana na changamoto,kwa njia ya mapingamizi ya kisheria, huko mahakamani mnakopanga kwenda ikiwa kutakuwa na jambo litakwenda mrama. Epukeni makosa kama haya:

DEFAULTERS LIST STUDIED UDSM


S.No Full Name Institution Graduation Year

25649

"NYANG""ANYI. ALEX M" "UDSM UDSM(CASS)"

25650 "NG""HAMBI. LAZARO WILSON" "UDSM UDSM(CASS)"

25651 "MOH""D. MOH""D SALUM" "UDSM UDSM(CASS)"

25652 "MNG""ONG""O. STANLEY " "UDSM(UDSE) UDSM"

25653 "MKING""I. FARIJI " "UDSM UDSM(CASS)"

25654 "MINGA. ING""E VENANCE" "UDSM UDSM(CASS)"

25655 "MANGULA. ANG""EMELYE GERSON" "UDSM(UDBS) UDSM

25656 "LEVOYO. NESERIAN OJUNG""U" "UDSM UDSM(CASS)"

25657 "LENG""OKO. ANDERSON MOJELWA" "UDSM UDSM(CASS)"

25658 "KING""UNZA. DENIS R" "UDSM UDSM(CASS)"

25659 "KING""ETI. YAKOBO E" "UDSM(IKS) UDSM"

25660 "CHANG""A. SHAHA " "UDSM UDSM(CASS)"

25661 """MOH""""D"". KHADIJA N" UDSM 2000/2001

25662 """MOH""""D"". JUMA K" UDSM 2002/2003

Ndiyo nini hichi mlichoandika hapo juu?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
  • Thanks
Reactions: SMU
While kimsingi nakubaliana na dhana ya watu waliochukua mikopo kuirejesha ili wengine nao wanufaike, ningeomba ili zoezi liendeshwe kiumakini kidogo. Nimepitia hii list naona jina langu limo ingawa nilishalipa na kumalizana nao kabisa.pia watu wangu wa karibu nnaowafahamu kuwa wamemaliza na wengine walipewa certificates majina pia yamo.Mnaohusika na utoaji wa haya majina tafadhali hakikini tena kwa kupitia vyema vyanzo vya kumbukumbu/taarifa zenu..
 
Back
Top Bottom