Abdul-Aziz Carter
Member
- Sep 27, 2023
- 7
- 23
Naitwa Abdul-Aziz Carter Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM):
Octoba 20,2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya mikopo (HESLB) Abdul-Razaq Badru aliishukuru serikali kwa kutenga Bilioni 731 kwa ajili mikopo ya wanafunzi 220,376 wa Elimu ya juu, lakini pia alitangaza awamu ya kwanza ya wanufaika wa mkopo (first batch) ambapo alisema Bilioni 159.7 zimetumika kuwanufaisha wanafunzi 56,132.
Taarifa hii inatia mashaka kwa sababu ukiangalia akaunti za wanafunzi (students individual permanent account) maarufu kama SIPA wanafunzi wengi wa mwaka wa 1 wamepata chini ya 20% .
Kiwango cha pesa kilichotengwa (Bilioni 159.7) hakiendani na 20% ambayo wanafunzi wengi wamepewa.
TAHLISO wanapaswa kusimama na kupigania haki za Wanafunzi kwani ndio lengo la kuundwa kwake, Bodi ya mikopo inapaswa kutoa ufafanuzi kwa kuwa Kuna wanafunzi walikua na sifa na vigezo vilivyoainishwa na bodi ya mikopo,licha ya kuweka viambatanisho katika maombi yao bado wamepata chini ya 20% na mwisho serikali kupitia wizara ya Elimu wanapaswa kufanya uchunguzi ili kubaini na kuitafutia suluhu changamoto hii.
=============
UFAFANUZI WA BODI YA MIKOPO: MKOPO UNATEGEMEA NA UHITAJI WA MUOMBAJI KWA ALIVYOOMBA
Mkuu wa Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania (HESLB), Omega Ngole anafafanua:
“Upangaji wa viwango vya mikopo kwa Wanafunzi wanufaika unatokana na uhitaji wa muombaji kulingana na nyaraka alizowasilisha HESLB wakati wa maombi yake, mfano muombaji akisema ana ulemavu, yatima, historia yake kimasomo n.k inaweza kuchangia kiwango anachotakiwa kukipata.
“Hali hiyo inafanya viwango vitofautiane, kuna makundi yanayopewa kipaumbele mfano yatima, wenye ulemavu au waliofanya vizuri zaidi katika mitihani n.k
"Hao wanaolalamika wanatakiwa kujua kiwango cha mkopo kinatokana na nyaraka zao wenyewe.
"Kiwango cha mkopo hakiwezi kulingana kwa kila Mwanafunzi na ndio maana kila mmoja anaingiziwa fedha kwenye akaunti yake binafsi, hilo ni suala la mtu mmoja mmoja kulingana na mahitaji na ndio maana wapo ambao wamepata mkopo kwa kiwango cha 100%."