Bodi ya Mikopo(HESLB) waachia majina ya wadaiwa sugu kuanzia mwaka 1994 hadi 2014

Kwa kweli nimepitia orodha yao nimeona ina mapungufu mengi tu. Wanahitaji kufanya house cleaning ya kutosha kabla ya kutoka hadharani na kutoa vitisho. Kuna hata mkanganyiko wa vyuo pia.

Hata uwezo wa kufungua mmashauri kwa maelfu wanao kweli? Most likely tukaona demos (zenye milengo ya kisiasa) kama zile za NHC.
 
Yaani Taifa lilikuamini sasa Leo kijinga kabisa unajibu eti hulipi Ng'ooo akili za kilevi kabisa
 
Hawa jamaa kwenye Mikutano ya kampeni za Uchaguzi wa 2010 watapata shida ni kujilipua aks kujitoa mhanga maana najua watapita tu hata tufanyeje
 
mfa maji hakosi kutapatapa..wanaleta porojo za list ya vikao vya sendoff..shame on u!!!
 
While kimsingi nakubaliana na dhana ya watu waliochukua mikopo kuirejesha ili wengine nao wanufaike, ningeomba ili zoezi liendeshwe kiumakini kidogo. Nimepitia hii list naona jina langu limo ingawa nilishalipa na

kumalizana nao kabisa.pia watu wangu wa karibu nnaowafahamu kuwa wamemaliza na wengine walipewa certificates majina pia

yamo.Mnaohusika na utoaji wa haya majina tafadhali hakikini tena kwa kupitia vyema vyanzo vya kumbukumbu/taarifa zenu..
Bodi hawana kumbukumbu za baadhi ya wadaiwa! Hivyo wanaweja yu majina almradi mbele kwa mbele mtajuana huko. Hawana basis yoyote ya kumpeleka mtu mahakamani kwa sababu kumbukumbu na hata ile mikataba ya miaka ya 2005 mpaka 2012 hawana! Sijui iliungua au ilikuwaje!
 
Inabidi wajipange na kufanya kwa weledi na kisasa zaidi kwa kweli...
 
Bodi ya mikopo hii tabia ya kurupuka kwa taasisi kubwa kama hii ni hatari sana nilikua private na mpaka leo nina receipts zote nilizoliipia ada na accomodation..lkn jina langu liko kwenye orodha kama mdaiwa sugu they have to apologize kwa public if at all kama hawana data sahihi wakawaombe wadai sugu watawapatia,hawa loan board wana kichaa They want to solve political pressure siasa za maji taka zitawaua bongo Duplicates kibao za majina
 
Utakuwa uliapply lkn pia kulikuwa uozo sana huko,kuna mambo mengi sana huko loanbd
 
Kumbukeni mtaala ulibadilishwa 2005 kuwa competency based, ina maana unapewa maarifa baada ya hao upaje ujuzi na ubunifu wa kujiajiri, wanategemea tuwe tumejiongeza na kupata kipata cha kurudisha pesa ya watu
Wawe na SUBIRA hadi nivune mbao zangu...waanze kuwakata waliowaajiri kwanza
 
Je wote walio kopa wana Ajira za kuwawezesha kulipa hayo madeni au ndo hawa mamalishe na wauza mitumba huku mtaani?
Wao waliomba mikopo wasome au wapate ajiraa???
Walipe mikopo ndani ya muda huo.
 
Hili povu kabisa la HESLB jamani., then unajua kuna watu watatakiwa kulipa hizo pesa though hawajawahi soma katika hicho chuo flani either ulichaguliwa chuo flank then ukachkua transfer ya chuo kingine au ukachkua kozi nyingine then majina yote yakawa yanatokea katika vyuo vyote na pesa inaingia katika.a/c zako zote .Au kuna mtindo hivi vyuo vyetu huwa vinapeleka majina ya wanafunzi loans board hata ya wale ambao hawaja ripoti vyuoni so board inatoa cheque kulingana na namba ya wanafunzi waliopo na wasio kuwepo hapo sasa chuo kinakuwa kina idadai tofauti ya wanafunzi na ile ya loans board chuo ulishahamaga muda but pesa inaingia , so jamani tuangalie vizuri katika hilo hivi vyuo navyo jipu tena la kooni
 
Hawa jamaa (loan board) wa ajabu sana kuna ndugu mmoja yeye alijipeleka mwenyewe kuomba aanze kulipa baada ya kuona hawajaanza kumkata baada ya miaka miwili kwisha tangu apate kazi. Basi walimpa bili yake yenye faini juu ya kuchelewa kulipa baada ya mwaka mmoja kwa mujibu wa mkataba. Akakubali bili hiyo na wakaanza kumkata. Anasema mwakani mwezi wa saba ndiyo anamaliza deni hilo. Sasa anashangaa eti naye ni mdaiwa sugu...!!!
Hivi mtu ukiitwa mdaiwa sugu si ni udhalilishaji? Je. Hakuna uwezekano wa huyu ndugu kuwafungulia mashtaka hawa jamaa na kashinda Kesi hii kweli na wakamlipa fidia ya kumdhalilisha?
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom